Tanzania: Ni yapi yaliyojiri 1995?

The Boss,

..mtandao ni wa Lowassa na Rostam.

..kwa mtizamo wangu JK alidandia tu humo na bahati ya mtende ikamuangukia.

..kuna jamaa ameandika ushuhuda wake kwamba hata 2005 ilikuwa Lowassa agombee ila akaachiwe JK kutokana na ushawishi wa Rostam.

..pia kuna mwandishi amewahi kuandika kwamba Mzee Mwinyi ndiye aliyemwambia JK agombee tena alimwita Ikulu wakati JK ni waziri wa fedha.
 
Mh walimuambia nini Lowassa mpaka akakubali? Maana 1995 JK alimpiku Lowassa, 2005 amuachie tena? Ningependa kujua alishawishiwaje amuachie nafasi JK.
 
mawazo yako yamekuwa drived na chuki zaidi kuliko facts. We want facts na sio blabla humu.

Mkuu Heshima Mbele,
Kwamba JK si mchapa kazi? ni blabla?Muulize juu ya Tatizo la umeme, Kama alivyohojiwa na BBC, alisema kuwa yeye hawezi kujaza maji kwenye mabwawa!! Kwake yeye umeme ni Mabwawa kujaa tu.

Kwamba JK ni Mvivu wa kufikiri? JK Ni rahisi ambaye hajui matatizo ya Watanzania,Hajui kwanini Watanzania Masikini, Hajui Richmond ni nini na hamjui mmiliki wake. Hajui, Hajui , Hajui!!!!!
 
Mh walimuambia nini Lowassa mpaka akakubali? Maana 1995 JK alimpiku Lowassa, 2005 amuachie tena? Ningependa kujua alishawishiwaje amuachie nafasi JK.

mkuu take it from me
ndani ya ccm kuna unwritten rules
ambazo hazipo kwenye maandishi but ndio zinaongoza kumpata mgombea

1.rais asitoke kwenye mikoa au makabila ambayo tayari yamesha toa rais
victims wa hii rule.msekwa,warioba n.k

2.rule no 2.urais utabadilishana kati ya waislam na wakristo kila baada ya miaka kumi
1995 waislamu wawili tu,walichukua fomu,
3.2005 wengi mno
 
So ni the classic blame it on the wife mkuu? Maana Kitine nae walisema mke wake alimuingiza mkenge. Kibaki walisema mke wake alimforce ahakikishe haachii madaraka. Gbagbo nao Ivory Coast inasemekana alikua tayari kuachia ngazi mke akamuambia asi thubutu. Mwinyi nae walidai anaendeshwa na mkewe. Inaelekea hawa mamama wana influence kubwa sana.
So his father went down unto the woman: and Samson made there a feast; for so used the young men to do. 11 And it came to pass, when they saw him, that they brought thirty companions to be with him. 12 And Samson said unto them, I will now put forth a riddle unto you: if ye can certainly declare it me within the seven days of the feast, and find it out, then I will give you thirty sheets [2] and thirty change of garments: 13 But if ye cannot declare it me, then shall ye give me thirty sheets [3] and thirty change of garments. And they said unto him, Put forth thy riddle, that we may hear it. 14 And he said unto them, Out of the eater came forth meat, and out of the strong came forth sweetness. And they could not in three days expound the riddle. 15 And it came to pass on the seventh day, that they said unto Samson's wife, [Entice thy husband, that he may declare unto us the riddle, lest we burn thee and thy father's house with fire: have ye called us to take that we have? is it not so? 16 And Samson's wife wept before him, and said, Thou dost but hate me, and lovest me not: thou hast put forth a riddle unto the children of my people, and hast not told it me. And he said unto her, Behold, I have not told it my father nor my mother, and shall I tell it thee? 17 And she wept before him the seven [4] days, while their feast lasted: and it came to pass on the seventh day, that he told her, because she lay sore upon him: and she told the riddle to the children of her people. 18 And the men of the city said unto him on the seventh day before the sun went down, What is sweeter than honey? and what is stronger than a lion? And he said unto them, If ye had not plowed with my heifer, ye had not found out my riddle.

Do not under-estimate the power of a woman
 
Mada ni nzuri japo ina ukweli na story za Mitaani nyingi ila wenye akili wanaweza pambanua

pia nafurai jinsi mtoamada (MwanaFalsafa1) anavyoiendesha Kama MAKWAIA WA KUENGA
 
Mind that nafasi za elimu kwa nchi yeyote hazitakiwi kutolewa kwa uwiano bali kwa uwezo. Degeree hazigawiwi kama vitumbua au vyakula vya msaada. Ndiyo sababu walimpuuza. Shule zilikuwa za serikali na kusoma bure halafu anakuja na ripoti ya uchonganishi. No wonder alipigwa kikumbo mpaka akapata pressure iliyomuua.

Kama waziri wa elimu alitakiwa kuja na mkakati wa kuwahamasisha waislamu wasome siyo kugawiwa nafasi za kusoma hata kama hawakuwa na uwezo. Si unajuwa panga la chuo (DISCO...) lilivyokuwa linafagia wazamiaji??
Mkuu pengine neno nilotumia ndilo halipaswi lakini ingekuwa vizuri kwanza ukaelewa nini yalikuwa madai ya Malima. Na at least ungeweka hapa report yenyewe na ukaitoa makosa kuliko kutunga njia ya Mkato kutokana na imani yako ya dini.

Ni report ipi ya Uchonganishi ambayo wewe umeisoma na una hakika sio kweli?.. maanake tunapenda sana kutumia neno kuchonganisha badala ya kutazama ukweli kisha upatiwe ufumbuzi.. Ndio maana tunapewa majibu rahisi kktk matatizo yetu. hakuna Umeme unaambiwa mvua hazijanyesha na mnaamini hivyo wakati IPTL imepewa mafuta mgao umepungua au ondoka bila hizo mvua kunyesha!

Shule zilikuwa za serikali YES! na Malima aliilaumu serikali na sio vyombo vya dini kwa kuwepo gap kubwa ya maendeleo ya watoto kielimu..Leo wewe unamtaka waziri wa elimu awaambie waislaam waende shule? kwani yeye ni waziri wa waislaam au wananchi wote..Hal;afu unadasi waislaam waende shule nakuomba nipe data za mahudhulio ya wananzi kwa dini zao darasa la kwanza saba wakati wa Mwinyi kuonyesha waislaam walikuwa hawaendi shule!..

Haya ni mawazo ya kujazwa ujinga, ni mawazo ambayo hata wazunfgu wa South Affrika walifikiria hivyo kwamba watu weusi hawataki kwenda shule, wajinga nusu Binadamu na kwa mazungumzo yako sioni tofauti kabisa na kaburu ambaye haoni makalio yake.. Utanisamehe lakini hata siku moja usiseme waislaam hawakuwa na uwezo haki unachoandika hapa ni kuonyesha Udini wako..

Pengine wewe huwezi hata kuelewa mathlan, Chadema wanapopiga kelele kupanda kwa maisha, kuwepo kwa gap kubwa baina ya maskini na Matajiri..kwa fikra zako unaona au kufikiri dawa ni kuwaambia maskini wafanye kazi zaidi na kwamba Chadema wanataka kuchonganisha wananchi baina ya maskini na matajiri?.
 
MwanaFalsafa1,

..muongoza mada!!

..haya kuna kitu hiki hapa chini hebu kitazame kidogo.

..source ni gazeti la Mwanahalisi ambalo wengine hawaliamini kidogo.

..labda mnaweza kuchambua pumba ni zipi na mchele ni upi.
HUYU ANAJUA "MACHUNGU" YA ROSTAM.

HATIMAYE Rostam Adulrasul Aziz ameandika historia. Ni kwa kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hii ni baada ya miezi mitatu ya malumbano kati yake na baadhi ya wajumbe wapya wa sekretarieti ya CCM.

Kwa wale tuliobahatika kuwa ndani ya sakata zima la kupanda na kushuka kwa Rostam, hatutakuwa tumetenda haki tusipoeleza kilichojiri mpaka kuanguka kwake. Ni vema tukaeleza haya ili kuipa historia nafasi yake; lengo likiwa kufanya umma uelewe nini kilijiri.

Rostam alikuwa rafiki wa muda mrefu wa Edward Lowassa. Ni wazi pia alikuwa rafiki wa Rais Jakaya Kikwete. Sina uhakika ni nini kilimfanya Rostam awe karibu na Kikwete kuliko Lowassa katika miaka ya 2002 hadi 2005.

Rostam alikuwa na mapenzi ya kweli na Kikwete; alidhihirisha mapenzi yake hayo mwaka 2002 pale palipotokea mivutano ndani ya mtandao iliyohusu nani hasa awanie nafasi ya urais kati ya Kikwete na Lowassa.

Wakati huo ilikuwa ikinong'onwa na kuripotiwa kuwa Lowassa alikuwa na nguvu kubwa ndani ya chama kuliko Kikwete.
Wengi walimuona Kikwete kuwa mtu wa matukio mepesi kama vile kukaa na wazee na kula nao, ili kujionyesha kuwa yeye ni "mtu wa watu" mwenye uwezo wa kuishi maisha kama yao.

Hatimaye baada ya ushawishi mkubwa wa Rostam, wakati wa mkutano wa bunge la bajeti mwaka 2003, ndipo Lowasa alipokubaliana na matakwa la Rostam.

Aliwaita wazee nyumbani kwake, wakuu wa mikoa 14 na watu wengine maarufu waliokuwa wanamuunga mkono na kuwatangazia rasmi kuwa hatogombea tena urais. Aliekeza wafuasi wake kuhamishia nguvu zao kwa Kikwete. Hili halikuwa jambo rahisi. Baadhi ya wafuasi wake waligoma hadi kufikia wengine kuamua kukaa pembeni.

Miongoni mwa waliokaa pembeni ni Anne Makinda na Abdulrahman Kinana. Ila Kinana inadaiwa alijiondoa baada ya kuona wenzake ndani ya mtandao wanachafua wagombea urais wengine.

Kilichofuata ikawa kutafuta uungwaji mkono ndani ya chama. Kwa nguvu ya Rostam na Lowassa hili lilifanikiwa, huku Umoja wa Vijana (UV-CCM) ukiwa ndiyo nguzo kuu ya kusimamia kampeni za Kikwete. Vijana waliotapakaa nchi nzima walianza kazi ya kumwita Kikwete kwenye matamasha mbalimbali kwa lengo la kumjenga kisiasa.

Baada ya hilo kukamilika, likaingia zoezi Na. 2 ambalo ni Rostam kutafuta njia ya kujipenyeza katika maeneo nyeti ya dola ili kuwaaminisha kuwa Kikwete anafaa. Hilo lilifuatiwa na kampeni ya chinichini na wazi na upikaji taarifa, nyingine za "kiintelijensia" ili kuonyesha Kikwete ana nguvu isiyoweza kuzuilika.

Hatimaye, hata Rais Benjamin Mkapa akashawishika kumuunga mkono Kikwete. Rostam alipiga hesabu za haraka na kugundua kitendo cha kupiga kura tatu kwa mgombea mmoja kilikuwa hatari kwa Kikwete. Ni baada ya kubaini Frederick Sumaye, Profesa Mark Mwandosya, Dk. Abdallah Kigoda na Dk. Salim Ahmed Salim kuungana ili wafuasi wao wapigiane kura.

Kitendo cha wafuasi wa Kikwete kumpigia kura yeyote kwa kupitia utaratibu wa kura tatu, kama ulivyoelezwa kwenye kanuni za uchaguzi za CCM, kilikuwa kinakamilisha safari ya kushindwa kwake maana angekuwa anaongezea wenzake ushindi, huku yeye akibaki na kura chache.
Katika uchaguzi huo, kati ya kura zaidi ya 215 zilizopigwa, Kikwete alipata kura 76 tu.

Kwa maana nyingine, ilibidi kumshawishi Mkapa kupindisha kanuni za uchaguzi. Ghafla Mkapa akatangaza mtu "mmoja kura moja."
Huu ukawa ushindi mwingine wa Kikwete uliotengenezwa, kurabatiwa na kuandaliwa na au kwa msaada wa Rostam.
Uchaguzi mkuu ulikuwa mwepesi kwa kuwa kazi zote za chini zilifanywa na Rostam ambaye aliongoza timu kubwa ya wapiga kampeni waliotapakaa nchi nzima.

Mathalani, mimi nilikuwa nikiongoza kundi la watu tuliokuwa tukipokea maelekezo kutoka kwa Rostam moja kwa moja.
Baada ya ushindi wa Kikwete ndipo hasa tatizo la umoja ndani ya kundi kubwa la wanamtandao lilipojitokeza.
Katika kuhakikisha kila mwanamtandao anapata stahiki yake, Rostam akajikuta anatengeneza uadui na "vyombo" vya dola na viongozi wa chama, jambo lililochangia anguko lake la juzi.

Kosa la kwanza lilikuwa ni kusimamia Lowassa kupewa uwaziri mkuu. Baadaye "akamuumba" Samwel Sitta kwa kumpa nafasi ya spika – mtu ambaye alikuwa na matumaini makubwa ya kuwa waziri mkuu.

Katika kuhakikisha mpango wake wa kumweka Sitta katika kiti cha uspika unafanikiwa, Rostam aliwaomba wagombea wengine walioonekana wenye nguvu, akiwamo Philip Marmo kujitoa katika kinyang'anyiro hicho.
Inaaminika Rostam alifanya yote haya kwa baraka za Kikwete mwenyewe. Bali hapa ndiko ilikuwa tamati ya ndoa ya wanamtandao….
Mtandao uliobaki ukawa ule wa wote walioamini kuwa ni marafiki wa Kikwete, wakati ukweli ulikuwa Kikwete hakuwa tena na upande, bali aliunga mkono upande ulioonekana kushinda.

Kwa upande wa pili, ilianza kuonekana kuwa Kikwete amepoteza hamu na Rostam na ushawishi wake. Ghafla Kikwete alimteua Pius Msekwa kuwa makamu mwenyekiti wa CCM, ilhali akijua Msekwa ni mhanga wa uspika uliochukuliwa na Sitta chini ya maelekezo thabiti ya Rostam.
Shughuli zote za kuendesha chama sasa zikawa chini ya Msekwa huku yeye akiwa nyuma akitazama minyukano yao.

Kama vile haitoshi, Kikwete akamteua George Mkuchika kuwa naibu katibu mkuu wa CCM, Tanzania Bara. Mkuchika alikuwa mhanga wa Rostam katika kinyang'anyiro cha nafasi ya katibu wa wabunge wa CCM. Alipambana na Ali Ameir Mohammed. Ushindi wake huu haukuja hivihivi. Ilikuwa kama kumlipizia kisasi hasa baada ya Mkuchika, aliyekuwa rafiki wa Kikwete, kumgeuka wakati wa kampeni. Mkuchika alimuunga mkono Mwandosya.

Matokeo yake, Rostam akawa tayari amezungukwa na maadui wa kisiasa ndani ya chama, ndani ya bunge na ndani ya serikali.
Ripoti ya Bunge ya Richmond ilikuwa eneo mojawapo ambalo bunge chini ya Spika Sitta, CCM na serikali viliungana kuwashambulia Rostam na Lowassa, jambo lililobadili mwelekeo kutoka kilichoitwa na Kikwete, "ajali ya kisiasa" na kuwa tuhuma na hatimaye kuachia ngazi.
Bado wale viongozi waliokuwa wakituambia ubaya wake wamenyamaza kimya.

Ni wazi kabisa kumfanya Dk. Harisson Mwakyembe kuwa mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond hakukuwa kwa bahati mbaya.Huyu alikuwa meneja wa kampeni wa Mkuchika katika kinyang'anyiro cha ukatibu wa wabunge wa CCM.
Matokeo ya uchaguzi uliopita ndiyo yaliyoleta taharuki ndani ya CCM, huku yakitafutwa majibu mepesi ya kufanya vibaya kwa chama hicho.

Mathalani hakuna aliyetayari kusema chama kiliwekwa pembeni katika uchaguzi mkuu uliopita na hata mwenyekiti wa kampeni, Kinana, alikuwa hajui kinachofanyika zaidi ya kuongea na vyombo vya habari. Kazi zote za Umoja wa Wanawake (UWT) zilihamishwa kwenye chama zikakabidhiwa kwa mke wa rais, Mama Salma, huku zile za UV-CCM zikikabidiwa kwa watoto wa rais, Ridhiwani na Miraji Kikwete.

Kuna taarifa kuwa baadhi ya maeneo kama Iringa, msafara wa Ridhiwani ulikuwa na magari mengi zaidi kuliko aliyokuwa nayo mgombea mwenza, Dk. Mohammed Gharib Bilal. Akiwa Iringa, Ridhiwani alivishwa uchifu, huku Dk. Bilal akiachwa bila kufanyiwa chochote, jambo lililosababisha chuki kwa wananchi, serikali na katika chama. Wenye chama walijitenga na shughuli za kampeni na kuiacha familia na marafiki zao.

Rostam hajajiuzulu kwa kuogopa matambo ya Nape Nnauye na wapambe wake. La hasha. Ni kwa kujua kwa dhati kuwa siyo kwamba Nape anawakilisha maazimio ya NEC, ukweli anawakilisha mawazo na maelekezo ya Kikwete.

Kwa kutambua hawezi kupambana na Kikwete anayepigana naye chini kwa chini, akaamua kufanya uamuzi wa busara wa kujiuzulu.
Rostam ameondoka. Lakini bado ana machungu na kinyongo.
 
Mkandara said:
Mkuu pengine neno nilotumia ndilo halipaswi lakini ingekuwa vizuri kwanza ukaelewa nini yalikuwa madai ya Malima. Na at least ungeweka hapa report yenyewe na ukaitoa makosa kuliko kutunga njia ya Mkato kutokana na imani yako ya dini.

Ni report ipi ya Uchonganishi ambayo wewe umeisoma na una hakika sio kweli?.. maanake tunapenda sana kutumia neno kuchonganisha badala ya kutazama ukweli kisha upatiwe ufumbuzi.. Ndio maana tunapewa majibu rahisi kktk matatizo yetu. hakuna Umeme unaambiwa mvua hazijanyesha na mnaamini hivyo wakati IPTL imepewa mafuta mgao umepungua au ondoka bila hizo mvua kunyesha!

Shule zilikuwa za serikali YES! na Malima aliilaumu serikali na sio vyombo vya dini kwa kuwepo gap kubwa ya maendeleo ya watoto kielimu..Leo wewe unamtaka waziri wa elimu awaambie waislaam waende shule? kwani yeye ni waziri wa waislaam au wananchi wote..Hal;afu unadasi waislaam waende shule nakuomba nipe data za mahudhulio ya wananzi kwa dini zao darasa la kwanza saba wakati wa Mwinyi kuonyesha waislaam walikuwa hawaendi shule!..

Haya ni mawazo ya kujazwa ujinga, ni mawazo ambayo hata wazunfgu wa South Affrika walifikiria hivyo kwamba watu weusi hawataki kwenda shule, wajinga nusu Binadamu na kwa mazungumzo yako sioni tofauti kabisa na kaburu ambaye haoni makalio yake.. Utanisamehe lakini hata siku moja usiseme waislaam hawakuwa na uwezo haki unachoandika hapa ni kuonyesha Udini wako..

Pengine wewe huwezi hata kuelewa mathlan, Chadema wanapopiga kelele kupanda kwa maisha, kuwepo kwa gap kubwa baina ya maskini na Matajiri..kwa fikra zako unaona au kufikiri dawa ni kuwaambia maskini wafanye kazi zaidi na kwamba Chadema wanataka kuchonganisha wananchi baina ya maskini na matajiri?.

Mkandara,

..Prof.Malima alishapata kuandika waraka mwingine wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere akiwatuhumu mawaziri waliokuwa wakipendekeza marekebisho ya uchumi kuwa ni wasaliti wa taifa.

..nadhani Prof alimsoma Mzee Ruksa na ktk kujaribu kuingia ktk inner circle akatoka na huu waraka wa kudai Waislamu wananyimwa nafasi za elimu.

..Prof.Malima alikwenda mbali na kudai kwamba ameanzisha utaratibu wa namba za watahiniwa ambao ndiyo utakuwa muarubaini wa kusitisha hujuma za Wakrito dhidi ya Waislamu ktk kupata nafasi za elimu.

..sisi wengine tumesoma na kufanya mitihani kabla Prof.Malima hajateuliwa Waziri wa Elimu na tulifanya mitihani ya kitaifa kwa kutumia namba za mtihani. pia kama utaratibu aliouanzisha Prof.Malima ulikuwa ni dawa ya kweli kukomesha dhuluma anazodai zilikuwepo basi leo hii kusingekuwa na malalamiko ya imbalance ktk wanafunzi wanaopata nafasi za kwenda sekondari za serikali na vyuoni.

..lakini pia tujiulize yeye Prof.Malima kama mbunge ameacha legacy gani ktk sekta ya elimu jimboni kwake Kisarawe?

..kuna mambo mengi yanayosababisha wananchi wakakosa elimu ktk nchi hii. kuna suala la UMASIKINI. yapo maeneo ambapo wazazi wanaona shule ni kero kubwa kutokana na kukosa fedha za michango ya shule. lipo suala la kuwa na uduni wa maendeleo ktk maeneo fulani fulani. ukiangalia mikoa kama ya kusini kumekuwa na tatizo sugu la huduma duni za afya,elimu,barabara, etc ktk mazingira yale si rahisi kuwa na watu wenye muamko wa elimu.
 
Mh binafsi naamini kwamba kama kweli JK kawatenga kiujanja watu waliomsaidia kuupata uraisi hilo ni jambo la hatari sana huko mbeleni. Hata sasa tunaona jinsi Lowassa bado alivyo na nguvu na ushahidi ni mkutano wa CC (kama sikosei) uliopita ambapo Lowassa aligoma kujiuzulu na kupewa support ya majority ya wajumbe.

Tatizo kwa JK halitakua kwa sasa akishikilia uraisi kwa vile vyombo vyote vya dola vipo chini yake. Hatari itakua pale JK akiondoka madarakani na haswa kama maadui zake watafanikiwa "kumteua" mgombea wao na akashinda. Hivi visasi vina weza kuja kumhunt JK baadae. Siamini kama ni jambo la busara kuwatupa hawa watu especially kwa style hii. Mheshimiwa akumbuke kuwa uraisi siyo milele.

Pia hata sasa tunaona maadui aliojijengea JK jinsi wanavyo mpa wakati mgumu. Sina uhakika ila inaelekea sasa hao maadui wamefanikiwa kumfanya JK aonekane raisi hovyo kuliko wote na kwa kiasi kikubwa wanachangia kuharibu legacy ya JK. Nina uhakika 2015 uchaguzi wa CCM kumpata mgombea utakua mkali sana kwani haya makundi yanajua yasipo toa wao mgombea basi kundi lao limekwisha.

Anyway ni mtazamo wangu tu.
 
Mkandara,

..Prof.Malima alishapata kuandika waraka mwingine wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere akiwatuhumu mawaziri waliokuwa wakipendekeza marekebisho ya uchumi kuwa ni wasaliti wa taifa.

..nadhani Prof alimsoma Mzee Ruksa na ktk kujaribu kuingia ktk inner circle akatoka na huu waraka wa kudai Waislamu wananyimwa nafasi za elimu.

..Prof.Malima alikwenda mbali na kudai kwamba ameanzisha utaratibu wa namba za watahiniwa ambao ndiyo utakuwa muarubaini wa kusitisha hujuma za Wakrito dhidi ya Waislamu ktk kupata nafasi za elimu.

..sisi wengine tumesoma na kufanya mitihani kabla Prof.Malima hajateuliwa Waziri wa Elimu na tulifanya mitihani ya kitaifa kwa kutumia namba za mtihani. pia kama utaratibu aliouanzisha Prof.Malima ulikuwa ni dawa ya kweli kukomesha dhuluma anazodai zilikuwepo basi leo hii kusingekuwa na malalamiko ya imbalance ktk wanafunzi wanaopata nafasi za kwenda sekondari za serikali na vyuoni.

..lakini pia tujiulize yeye Prof.Malima kama mbunge ameacha legacy gani ktk sekta ya elimu jimboni kwake Kisarawe?

..kuna mambo mengi yanayosababisha wananchi wakakosa elimu ktk nchi hii. kuna suala la UMASIKINI. yapo maeneo ambapo wazazi wanaona shule ni kero kubwa kutokana na kukosa fedha za michango ya shule. lipo suala la kuwa na uduni wa maendeleo ktk maeneo fulani fulani. ukiangalia mikoa kama ya kusini kumekuwa na tatizo sugu la huduma duni za afya,elimu,barabara, etc ktk mazingira yale si rahisi kuwa na watu wenye muamko wa elimu.
Mkuu nakusikia sana na labda tujaribu kutenganisha unachofikiria wewe na ukweli uliokuwepo. Tanzania leo hatuna Umeme na tunalaumu zaidi Ufiosadi, sasa kwa kila njia tunapotumia njia na mifano ya kuupata lakini bado imeshindikana haina maana kwamba hakuna Ufisadi ktk tatizo la Umeme..

Habari yako ktk swla la elimu lazima ufahamu kwamba Malima alimwandikia barua Mwinyi kumwelezea hali ya elimu nchini. Ndiyo ilikuwa kazi yake kama waziri na yanapokuwepo matatizo sidhani kama kiongozi mzuri angekubali kuyaficha ili mradi kupendezesha. Mwinyi hakupendezewa na report ile na kuiepeleka kwa Mwalimu na Warioba wote hawa waliipata..

Na unaposema kama kutumia namba haikuwa Muarobaini, imekuwaje ziliondolewa na matumizi ya majina (kama sikosei yalirudishwa). Kwa nini ukatize program fulani kwa visingizio vya udini. Jokakuu, wewe na mimi tumesoma kabla kabisa ya matatizo haya ya namba na kadhalika. Na muda wote tunajua Nyerere alifikia asilimia 90 ya wanafunzi wenye umri wa kwenda shule kujiunga na shule za primary lakini ONLY 5% ndio wali advance!

Sisi tumesoma wakati wa Nyerere ambapo shule nzima ya watoto zaidi ya 200 (darasa la saba) hushinda mtoto mmoja au wawili tu.. Kilichofuatia miaka ya 80's mkuu wangu watu walikuwa wakinunua majibu ya mitihani kuweza kushinda na kuendelea form 4. Amini maneno yangu ndio mission town zilikuwa kwa sababu demand kubwa, supply ya shule ndogo..again Scarcity as the mother of Corruption ndipo tulipoanzia lawama hizi..Sasa sema Malima hakufanya utafiti zaidi ya kutazama namba alizoletewa mezani na ku panic.. was it not true? - No katika shule yenye waislaam/wanawake asilimia 50, less than 1% will advance ktk report ya mwaka hadi mwaka.

Tuseme watoto 20 wamechaguliwa kuendelea na masomo sekondary - Muislaam alikuwa mmoja na mwanamke mmoja vile vile. Lakini ukirudi ktk masomo yao ya kawaida na maksi shuleni utakuta walikuwa wakienda sambamba Wanawake, Waislaam na Wakristu..Ndivyo report ilivyoonyesha na sii kuonyesha umaskini wa wanafunzi kwenda form 4 wakati serikali ilikuiwa ikilipia kila kitu, na shule nyingi zilikuwa za kulala. halafu kwa nini swala hili lisiwe pia la wanawake bali waislaam against wakristu?..

Na ndio maana I concluded kwamba Malima alichoshindwa kuelewa ni kwamba wanafunzi walikuwa wakinunua mitihani na ununuzi ulianza kwanza kwa watoto wa wakubwa, na mitaa ya fridge open (who happened to be Christians - A fact!)..Kwa hiyo haikuwa mpango wa serikali wala kanisa bali Ufisadi kama tunavyoshindwa kukomesha RUSHWA leo hii na wapo viongozi na wananchi wanaomini kuwa Ufisadi wahusika wake wakubwa ni Wahindi na waarabu..

Hata hivyo mkuu wangu kubishana nadhani haiwezi kutusaidia kitu tena haswa vitu ambavyo vilikwisha pita. Yote haya ni hearsay na kaa nilivyosema hakuna Mtanzania yeyote anadiriki kuchukua taarifa ya Malima na kuipitia upya kwa sababu tunaona aibu wenyewe kwa yale tutakayo yakuta, hivyo tunachoweza kufanya ni kutafuta mchawi.
 
..niliwahi kuisoma hiyo barua ya Prof.Malima kwenda kwa Raisi Mwinyi.

..so far hakuna taarifa yoyote ile ya utafiti ulioambatana na barua ile.

..alichopeleka kwa Raisi kilikuwa barua siyo ripoti ya utafiti.

..Waislamu wa Kagera wana maendeleo ya elimu kuliko Wakristo wa Sumbawanga.

..pia watoto wa kike Uchagani wanasonga mbele kielimu kuliko wavulana wa mikoa hata ktk baadhi ya maeneo yenye Wakristo.

..Prof angekuwa amefanya utafiti unaoheshimika asingeweza kukurupuka na conclusion kwamba kuna hujuma ya Wakristo dhidi ya Waislamu.

..pia kama unasema tatizo lilikuwa watoto wa wakubwa kuiba mitihani basi walipaswa kuchukuliwa hatua kama wahalifu wengine, lakini siyo "Wakristo-Wahalifu" kama unavyotaka kuonyesha.

..kitu kingine kilichosababisha lawama kubwa zielekezwe kwa Prof.Malima ni wakati na mazingira alipotoa tuhuma zile. kipindi hicho hicho ndipo kulikuwa kumeibuka vikundi vya mihadhara ya kukashifu Biblia.

NB:

..katika kusoma kwangu na kufanya mitihani sijawahi kuona miujiza yoyote ile ambapo mwanafunzi aliyekuwa akifanya vibaya akafaulu na kuacha wale waliokuwa wakifanya vizuri.

..nimesoma na wasichana na wavulana Waislamu. Waliokuwa wakifanya vizuri darasani walifaulu ktk mitihani ya kitaifa, waliokuwa wakizembea hawakufaulu. hata waalimu wetu hawakututenga kwa dini zetu hata siku moja.
 
Je hiyo report Mh. Malima aliipataje? Kwa maana kama report imetolewa ina maana uchunguzi ulifanyika. Swali langu ni je huo uchunguzi ulifanywa na nani? Naamini kama kulikuwa na report basi ina maana kuna watu Malima aliwaagiza kufanya uchuguzi. Je hiyp report ilikua matokeo ya any official investigation au? Ni maswali tu najiuliza.
 
Jokakuu, Unaweza kunionyesha ni wapi nilipoandika na kuonyesha Wakristu walikuwa na makosa hayo!
Mkuu usiwe nawe unashindwa kunielewa kama ilivyokuwa kwa Malima.. wapi nimesema kuna hujuma ya wakristu dhidi ya waislaam.

Kuna tofauti kubwa baina ya kusihi kwako na matukio halisi. kifupi sijaona Ufisadi ukipita machoni mwangu, watoto wa wakubwa tuna struggle pamoja lakini haina maana hakuna Ufisadi mkuu wangu kwa sababu wapo watoto wa viongozi wana pata shida kama sisi.

Swala ni kuwatafuta wanaofanya Ufisadi huo na kuzama zaidi umetokana na kina nani, sasa tunaposema ni viongozi wa CCM mnachukia kwa sababu they belong to a party uliyopo na niliyesema natoka Chadema.

Lakini ukweli unabakia hatuwezi kukihukumu chama kizima kwa matendo ya Lowassa na Rostam na wala haina maana huku Chadema hakuna mtu ambaye ni fisadi.. Sijui kama unanielewa! tunazungumzia case ya waislaam/wakristu kutopewa nafasi ya kuendelea na masomo form 4..

Na hoja yako mkuu wangu haina mshiko kwa sababui inachukua case ya mtu mmoja mmoja. Hesabu za kitaifa ni ktk maelfu, wanatazama waislaam/wanawake wangapi wanaendelea na masomo toka darasa la saba kwenda sekondary.. Na ajabu ni kwamba nyote mnaamini kwamba waislaam na wanawake hawakusoma!.. Mkiulizwa sababu ati waislaam hawakutaka kusoma, wakati huo huo mnadai mlikuwa nao mashuleni!

Mkuu wangu zipo shule Tanzania zilikuwa zikitoa wanafunzi 20 kwenda sekondary na shule nyingine mtoto moja au hakuna hata mtoto mmoja aliyeshinda, unayajua haya?.. Hivyo huwezi kutumia experience ya shule hizi mbili tofauti kuzungumzia swala la elimu kitaifa. Kagera ilikuwa na shule nyingi na kuliko Sumbawanga hivyo tunapozungumzia kuboresha elimu Sumbawanga tutaweza kutumia mfano wa Kagera haina maana Sumbawanga wana jenga Umajimbo dhidi ya Kagera.

Kwa hivyo mfano wa Muislaam na Mkristu au mwanamke hauna mshiko ikiwa Kitaifa kulionekana kuna hitilafu. Na hakuna mtu alotaka ku deal na hitilafu hizo isipokuwa kumtafutia dawa ya kumwondoa. Ndio yale yale ya Malecela na serikali tatu.

Aliondolewa madarakani kwa sababu tulishindwa kuukubali ukweli na itaendelea kusemekana kuwa ni njama ya Wabara kuwanyanyasa Wazanzibar. Mkuu nimechoka sana kuendelea na ubishi hivyo wewe amini unachoamini nami nitaamini nachoamini maadam hatuvunjiani heshima, wadhungumkuti wanasema - Tukubaliane kutokubaliana..
 
Je hiyo report Mh. Malima aliipataje? Kwa maana kama report imetolewa ina maana uchunguzi ulifanyika. Swali langu ni je huo uchunguzi ulifanywa na nani? Naamini kama kulikuwa na report basi ina maana kuna watu Malima aliwaagiza kufanya uchuguzi. Je hiyp report ilikua matokeo ya any official investigation au? Ni maswali tu najiuliza.

Mkuu hapo sasa haya ndiyo maswali ambayo yalitakiwa kufanywa wakati ule. badala yake tuliyachukulia kama ile scandal ya Richmond na hivyo kuongeza mashaka zaidi kwa viongozi wetu. Kama serikali ya Mwinyi ingechukua utaratibu wa kuchukua barua ile kisha kuomba report nzima na kuiwakilisha tuseme bungeni ingekuwa wazi zaidi kwa wananchi wote. Hakuna barua ambayo unaweza kumwandikia rais na usiwe na ushahidi unao back up maelezo yako..

Nimesoma mahala fulani humu kuna mada inayomzungumzia barua ya Mkapa kuwapa jibu Maimam wa Kiislaam na ukimsoma utaona akieleza jinsi majukumu ya waziri, waziri mkuu na hadi rais.

Lakini kwa sababu Mwinyi alikuwa anatakua Urahisi na kujikosha akichukua maamuzi yasiyokuwa na hekima kabisa sawa na siku alomgeuka Sheikh Kassim Bin Juma kwa sababu tu aliyetaka kuiua Bakwata na kuunda Balukta..

Why is it so hard for the government kuiondoa Bakwata ikiwa waislaam wenyewe hawaitaki?, hili ni swali dogo sana. waislaam wengi hawaitambui Bakwata why inaendelea kuwa chombo cha waislaam hali hawakitaki?
 
msiharibu uzi,kama vipi Malima bora afunguliwe thread yake tu,maana ishakuwa ligi tayari na mwisho tutarudi kulekule yaani Waislam wanaonewa,Nyerere kawabana na bla bla kama hizo
 
Nina maswali kuhusu Dr.Salim:Hivi amesha deliver nini hasa kwa taifa hili mpaka kuonekana anafaa sana kuwa Rais,mpaka Nyerere kumbembeleza mara kibao as if hakuna wengine capable kumshinda?

Kama Dr.Salim angeukwaa huo Urais tuseme 1985 au 1995 ama 2005,je bongo sasa tungekuwa tunacheza na GDP per capita ya Botswana,Namibia au hata Kenya ama tungekuwa kama Wasomali tu?

Inaelekea Dr.Salim ni arrogant na alijihisi kuwa yuko overqualified kwa nafasi ya Urais wa Tanzania au alikuwa hataki au hana nia hasa ya kuwa Rais wa Tanzania.

Kama alikuwa anajua kuwa Wazanzibari wenzake hawamtaki, iweje akatae Urais wa 'kupewa mezani' na Nyerere,kisha ghafla tu autake Urais huohuo 2005,wakati Nyerere ambaye angeweza kumbeba hakuwepo?
 
Back
Top Bottom