Renegade
JF-Expert Member
- Mar 18, 2009
- 7,126
- 6,764
Mimi kuna kitu kimoja kina nitatiza kuhusu Mkapa. Mimi naamini Nyerere hakua mtu wa kukurupuka. Kama alimchagua Mkapa naamini kabisa Nyerere alidhani anafaa. Je Mkapa ni alikua anaficha makucha yake au kweli alikuwa "Clean" akaja kubadilika baadae?
Mwalimu alimfahamu Mkapa toka siku nyingi, toka Mkapa akiwa Mwanafunzi wa Pugu sekondari,Na Nyerere alikuwa Mwalimu wake na alimpenda pia. Wakati Nyerere akiwa Rais Mkapa amewahi ku-serve kama Waziri wa Mambo ya Nje, na unapokuwa Waziri wa mambo ya nje enzi ya mwalimu siyo kitu kidogo.
Nimewahi kuongea na Mzee Ibrahim Kaduma ambaye pia aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Nyerere, kwa kweli anasema ilikuwa kazi kubwa kwa Muhusika, Mwalimu anaweza kumuita mtu wakati wowote na kutaka taarifa zozote, kwa hiyo ni kazi amabayo ilikuwa inataka muhusika awe na Taarifa nyingi, lakini inahitaji mtu amabye ni HARD WORKING, na Mkapa ni Hardworking, Tofauti na JK Ambaye kwake vitu vingi vinafanyika ki kawaida sana, JK ni mvivu wa kufikiri, kila kitu kwake ni rahisi sana, hata vitu vinavyohitaji umakini uvirahisisha.