Habari!! Inachukua muda gani kukabidhiwa miradi iliyokuwa ya REA? Maana tunaohitaji kuunganushiwa kwa kuweka nguzo ni zaidi ya mwaka sasa tunaambiwa mradi haujakabidhiwa. Maeneo jirani na shule za Nkilizya zilizopo kata ya nkilizya wilayani Ukerewe mkoa wa mwanza
 
Tanesco wananchi wa Tabata Kisiwani tunaomba mturejeshee umeme tafadhali
 
TANESCO KIGAMBONI
Kuna Mradi wa Viwanja Vipya zaidi ya 200 Eneo la Mkorea Mtaa wa kisiwani vilivyopimwa na Kampuni ya GOMBO ujenzi wake Umeanza kwa kasi na baadhi ya wahusika Wamehamia.Changamoto iliyopo ni UMEME .Kuna baadhi ya nyumba zimepata umeme uliotokea KISOTA na nyingine Ungindoni.
Ushauri kwa Uongozi wa TANESCO KIGAMBONI
Wateja wapo wanawasubiri nyinyi ili wapatiwe Umeme.
Ni wakati sahihi kwa Shirika kuanza kutandaza nguzo ili Wananchi walipie na kupatiwa Umeme.Wateja sio Tatizo bali Tatizo ni Tanesco.
Mimi ni miongoni mwa wananchi ninayesubiri HUDUMA yenu.

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
TANESCO.
Kuna jambo linanishangaza. Tanzania ina misimu miwili ya mvua. Vuli na masika. Mabwawa yanaweza kujaa au yasijae.

Sasa kwanini TANESCO hawaoni umuhimu wa KUVUNA MAJI YANAYOTIRIRIKA BAADA YA KUFUA UMEME NA KUYAPUMP BACK KWENYE BWAWA NA KUACHA YALE TU YA ZIADA HASWA WAKATI WA MASIKA. UMEME NI WENU. UNACHOHITAJI NI KUYAKUSANYA NA KUYARUDISHA NA SIO KUYAACHA YA POTEE BAADAE UNAANZA KULALAMA.

AMKENI.

BWAWA LA MWALIMU NYERERE HILO LIFIKIRIWE MAPEMA.

HIVI KUKIWA NA UKAME MIAKA 3 NCHI HAITAKUWA NA UMEME?
 
Washenzi kabisa ivi na mvua yote hii na.mafurikko bado mnakata umeme kuanzia saa 12 asubuh mpaka saa sita usiku??sioni kama kuna nia ya dhati ya kumaliza tatizo la umeme.TANESCO Ingebinafsishwa hata kabla ya bandari
Yamekata umeme juzi jioni, yakarudisha usiku wa manane, umeme haujakaa hata masaa mawili yakakata, tukashinda bila umeme ukarudi jana usiku, tukasema kwa kuwa yalikata bila mpangilio kuanzia juzi, basi leo tungeshinda nao tufanye kazi zetu zilizokwama. Yameshakata tayari asubuhi asubuhi hii 😡😤
 
Tanesco mnachofanya mnashusha elimu yenu ya mambo ya umeme ,hivi mnakata kata umeme bila taarifa na bila kutuandaa hii SI kuua uchumi wa Taifa letu?

Kumbuka watu wamewekeza Kila Kona ya Nchi wakijua umeme ni wauhakika sasa Kila wakati mnakatakata umeme Kwa elimu Gani mliyosoma? Mfike mahali muone heshima ya ujuzi wenu mliyosoma acheni kukata umeme.

Ushauri wangu ni huu tengeni eneo maalum basi ambalo mtafunga umeme usiokatika Ili liwe eneo la viwanda vikubwa na vidogo TU Ili hapo Nchi akusanye Kodi kwingine basi chezeeni mnavyotaka. Asante Kwa kunielewa
 
HABARI TANESCO LINI MTATUFUNGIA TRANSFORMER WANANCHI TUNAOISHI CHANIKA WILAYA YA ILALA MTAA WA NZASA DARAJANI NJIA YA KWENDA KWA MPANGO NGUZO ZA HTT ZIMESHAPITA NA NGUZO NDOGO PIA ZISHAPITA LAKINI TRANSFOMER BADO KUFUNGIWA UNAENDA MWEZI WA 2

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
TANESCO.
Kuna jambo linanishangaza. Tanzania ina misimu miwili ya mvua. Vuli na masika. Mabwawa yanaweza kujaa au yasijae.

Sasa kwanini TANESCO hawaoni umuhimu wa KUVUNA MAJI YANAYOTIRIRIKA BAADA YA KUFUA UMEME NA KUYAPUMP BACK KWENYE BWAWA NA KUACHA YALE TU YA ZIADA HASWA WAKATI WA MASIKA. UMEME NI WENU. UNACHOHITAJI NI KUYAKUSANYA NA KUYARUDISHA NA SIO KUYAACHA YA POTEE BAADAE UNAANZA KULALAMA.

AMKENI.

BWAWA LA MWALIMU NYERERE HILO LIFIKIRIWE MAPEMA.

HIVI KUKIWA NA UKAME MIAKA 3 NCHI HAITAKUWA NA UMEME?
Habari ndugu mteja, ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu, tumepokea mapendekezo yako kwa ajili ya utekelezaji ^JM
 
HABARI TANESCO LINI MTATUFUNGIA TRANSFORMER WANANCHI TUNAOISHI CHANIKA WILAYA YA ILALA MTAA WA NZASA DARAJANI NJIA YA KWENDA KWA MPANGO NGUZO ZA HTT ZIMESHAPITA NA NGUZO NDOGO PIA ZISHAPITA LAKINI TRANSFOMER BADO KUFUNGIWA UNAENDA MWEZI WA 2

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Habari Efendi, tunafurahi kukuhudumia kupitia ukurasa wetu huu na poleni sana kwa adha mnayoipitia, tumepokea taarifa zako kwa ajili ya ufuatiliaji na utekelezaji ^JM
 
Tanesco mnachofanya mnashusha elimu yenu ya mambo ya umeme ,hivi mnakata kata umeme bila taarifa na bila kutuandaa hii SI kuua uchumi wa Taifa letu?

Kumbuka watu wamewekeza Kila Kona ya Nchi wakijua umeme ni wauhakika sasa Kila wakati mnakatakata umeme Kwa elimu Gani mliyosoma? Mfike mahali muone heshima ya ujuzi wenu mliyosoma acheni kukata umeme.

Ushauri wangu ni huu tengeni eneo maalum basi ambalo mtafunga umeme usiokatika Ili liwe eneo la viwanda vikubwa na vidogo TU Ili hapo Nchi akusanye Kodi kwingine basi chezeeni mnavyotaka. Asante Kwa kunielewa
Mpendwa mteja, habari za wakati huu, ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa wetu na tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, tafadhali tufahamishe mkoa, wilaya na eneo ulilopo kwa msaada zaidi ^JM
 
TANESCO ni siku ya tatu leo sina umeme. Napiga simu kila baada ya masaa 2 napewa ahadi mafundi watakuja lakini sijaona hata fundi kuja.

Kwapost hii napenda kuwataarifu msijihangaishe kuja kwani ninatafuta kishoka aje kurekebisha tatizo nililoripoti
 
Tanesco,kitengo Cha kununulia lulu,mmenidhulumu Hela yangu nimenunua luku ya 5000/elfu tano mmeniletea ujumbe na token hamjanipa mpaka Leo na nilinunua luku tarehe 15 october.hii so haki ni dhuluma kubwa kumdhuluku mtejaznimesha apigia simu sana,mnadai mnashughulikia maple Leo,kumbe longolongo tu.
 
Habari ndugu mteja, ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu, tumepokea mapendekezo yako kwa ajili ya utekelezaji ^JM
Mpendwa mteja, habari za wakati huu, ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa wetu na tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, tafadhali tufahamishe mkoa, wilaya na eneo ulilopo kwa msaada zaidi ^JM
Asante Kwa kufuatilia maoni yetu wananchi,lakin tatizo la umeme Kwa sasa ni la Nchi nzima kukatika Kwa umeme imekuwa ni kama kawaida kiangazi Hadi masika sababu za kutukatia umeme zimekuwa rukuki.

shirika la Tanesco tuliamini baada ya serikali kulifanyia maboresho tulitegemea mtaona hasara kukata umeme kwani hata nyie mnalikosesha shirika lenu pesa.
 
Back
Top Bottom