Yamekata umeme juzi jioni, yakarudisha usiku wa manane, umeme haujakaa hata masaa mawili yakakata, tukashinda bila umeme ukarudi jana usiku, tukasema kwa kuwa yalikata bila mpangilio kuanzia juzi, basi leo tungeshinda nao tufanye kazi zetu zilizokwama. Yameshakata tayari asubuhi asubuhi hii 😡😤Washenzi kabisa ivi na mvua yote hii na.mafurikko bado mnakata umeme kuanzia saa 12 asubuh mpaka saa sita usiku??sioni kama kuna nia ya dhati ya kumaliza tatizo la umeme.TANESCO Ingebinafsishwa hata kabla ya bandari
Habari ndugu mteja, ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu, tumepokea mapendekezo yako kwa ajili ya utekelezaji ^JMTANESCO.
Kuna jambo linanishangaza. Tanzania ina misimu miwili ya mvua. Vuli na masika. Mabwawa yanaweza kujaa au yasijae.
Sasa kwanini TANESCO hawaoni umuhimu wa KUVUNA MAJI YANAYOTIRIRIKA BAADA YA KUFUA UMEME NA KUYAPUMP BACK KWENYE BWAWA NA KUACHA YALE TU YA ZIADA HASWA WAKATI WA MASIKA. UMEME NI WENU. UNACHOHITAJI NI KUYAKUSANYA NA KUYARUDISHA NA SIO KUYAACHA YA POTEE BAADAE UNAANZA KULALAMA.
AMKENI.
BWAWA LA MWALIMU NYERERE HILO LIFIKIRIWE MAPEMA.
HIVI KUKIWA NA UKAME MIAKA 3 NCHI HAITAKUWA NA UMEME?
Habari Efendi, tunafurahi kukuhudumia kupitia ukurasa wetu huu na poleni sana kwa adha mnayoipitia, tumepokea taarifa zako kwa ajili ya ufuatiliaji na utekelezaji ^JMHABARI TANESCO LINI MTATUFUNGIA TRANSFORMER WANANCHI TUNAOISHI CHANIKA WILAYA YA ILALA MTAA WA NZASA DARAJANI NJIA YA KWENDA KWA MPANGO NGUZO ZA HTT ZIMESHAPITA NA NGUZO NDOGO PIA ZISHAPITA LAKINI TRANSFOMER BADO KUFUNGIWA UNAENDA MWEZI WA 2
Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Mpendwa mteja, habari za wakati huu, ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa wetu na tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, tafadhali tufahamishe mkoa, wilaya na eneo ulilopo kwa msaada zaidi ^JMTanesco mnachofanya mnashusha elimu yenu ya mambo ya umeme ,hivi mnakata kata umeme bila taarifa na bila kutuandaa hii SI kuua uchumi wa Taifa letu?
Kumbuka watu wamewekeza Kila Kona ya Nchi wakijua umeme ni wauhakika sasa Kila wakati mnakatakata umeme Kwa elimu Gani mliyosoma? Mfike mahali muone heshima ya ujuzi wenu mliyosoma acheni kukata umeme.
Ushauri wangu ni huu tengeni eneo maalum basi ambalo mtafunga umeme usiokatika Ili liwe eneo la viwanda vikubwa na vidogo TU Ili hapo Nchi akusanye Kodi kwingine basi chezeeni mnavyotaka. Asante Kwa kunielewa
Hiyo hela ya kulipia nguzo mbona imerudi mbona enzi za magufuli ilikuwa hamnaNahitaji umeme nyumbani kwangu lakin tanesco tanga wamekua na bla bla nyingi. Mtanksaidiaje nipo tanga mjini
Habari ndugu mteja, ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu, tumepokea mapendekezo yako kwa ajili ya utekelezaji ^JM
Asante Kwa kufuatilia maoni yetu wananchi,lakin tatizo la umeme Kwa sasa ni la Nchi nzima kukatika Kwa umeme imekuwa ni kama kawaida kiangazi Hadi masika sababu za kutukatia umeme zimekuwa rukuki.Mpendwa mteja, habari za wakati huu, ahsante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa wetu na tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, tafadhali tufahamishe mkoa, wilaya na eneo ulilopo kwa msaada zaidi ^JM
Mvua zinanyesha mpaka mafuriko bado mnakata umeme? Mna roho mbaya sana kuliko kiumbe chochote hapa duniani.