Tunashukuru sana mpendwa.mteja wetu.tunaomba maswala.yanayohusu TANESCO yaje kwetu moja kwa moja kwa ufafanuzi aidha wateja wanaruhusiwa kutoa maoniMaelezo yenu yana double standards, angalia Tariff 1 na Tariff 4, wewe unasema mtumiaji wa kiwango cha chini anakuwa tariff 1 Na wa Juu anakuwa Tariff 4 ,which is which
HIZI NDIO SABABU ZINAZOKUFANYA ULIPIE UMEME KWA GHARAMA KUBWA.
Unaweza kushangaa kuona wengine wakinunua Umeme wa 9,150 Wanapata Unit 75 wew ukinunua Umeme wa 10,000 unapata Unit 28.1
Iko hivi Watumiaji wadogo wa Umeme ambao kwa mwezi Matumizi yao hayazidi Unit 75 Wapo Tarrif D1(4) Na wanauziwa Unit moja kwa Sh.122,
Wakati watumiaji waliowengi wako Tarrif T1 hawa Unit moja wanauziwa Sh.kati ya sh.356.45 Kama sikosei
Maana yake mtumiaji aliyeko Tarrif D1(4) Ananunua Unit 41 Kwa sh 5,000
Wakati walioko Tarrif T1 Wananunua Unit 14 kwa sh.5000
NAWEZAJE KUA MIONGONI MWA WATUMIAJI WADOGO WA UMEME YAANI (TARIFF D1)
Kama ni nyumba yakupanga na mko wengi ni ngumu kidogo. Kwanza unatakiwa Kupunguza Matumizi Ya Umeme Yasiyo ya Lazima
Pili nunua Vifaa vyenye Wats ndogo vitu kama taa,Tv,Friji,Pasi n.k
Tuchukulie mfano wa Taa zenye Wats 40 nje zikiwa nne na za Wats 18 kwa ndani zikawa Taa 8 nyumba yako nzima itakua na jumla ya Taa 12 Ambazo zitakua na Jumla ya Wats 304
Lakini ukinunua Taa zenye Wats ndogo (Energy Saver) Japo bei yake iko juu ukilinganisha na Taa zenye Wats kubwa Kwa mfano huu huu ukanunua Taa zenye Wats 5 kila moja za nje Nne na taa 8 za ndani zenye Wats 3 kila moja
Jumla ya taa 12 zitakua na Jumla ya Wats 44 tu.
Maana yake utakua umepunguza jumla ya Wats 250 upande wa Taa tu lakini idadi ya Taa imeendelea kua ni ile ile. Mtu mwenye taa moja ya Wats 40 akiwasha nawew ukawa taa zote 12 Matumizi yenu yatakua hayana tofauti kubwa
Mwisho kabisha matumizi yako ya Umeme yakiwa chini ya Unit 75 kwa miezi mitatu mpaka Sita Mfululizo unatakiwa kuandika Barua unaiadress kwa Meneja wa TANESCO wa Ofisi uliyoko Karibu nayo Kuomba kubadilishiwa Kutoka Tarrif 1 kwenda Tarrif 4.
Siku ukitumia Zaidi ya Unit 75 kwa mwezi utarudishwa Tariff 1.
Kwa swali lolote ushauri kuhusu matumizi bora ya umeme
Usisite kuwasiliana nami
MR ELETRIC
0674656694
allanshaolin12@gmail.com
Kwa maelezo yako mpo kundi sahihi la matumizi ya nyumbani cha msingi kila mmoja asimamie vizuri matumizi yake kwani sehemu za wapangaji huwa zina matatizo ya kila mmoja kujifanya hana matumizi makubwa lakini ukweli anaujua mwenyewewakubwa hii nyumba nnayoishi tupo kwenye system ya matumizi makubwa.....bas kila week tunanunua umeme was elfu tano tano (unit 15)......yani inatucost tunashindwa hata kunyoosha nguo....
Nisaidie utaratibu kwa mtaalam yeyote aliepo humu ndani jamn.....hili swala ni mzigo
@TANESCOHuu ni mkanganyiko, kama matumizi yangu ya mwanzo nimeyaeleza 7500 nilikua napata 61.5units saivi kwa hiyo hiyo bei ni unit 21.1 nashindwa kuelewa kwamba hili kundi ndio sahihi? Sipingi huo uhakiki wenu ila mseme zoezi litachukua muda gani kurudi hali ya awali
Tunaomba namba yako ya simu mpendwa.mteja wetuTanga eneo la Kange Kasera kwanini hamtaki kutuwekea nguzo za umeme eneo la chini ya msikiti ile hali tupo wateja xaidi ya 40 na ambao tumeshafanya wiring na kuleta barua ofisi za Meneja mkoa zaid ya mara tatu tangu mwaka jana mwezi wa pili?
Sababu za kibajet mnazotupa haturidhiki nazo kwa kuwa maeneo mengiine mapya kabisa mnaweka nguzo na maombi wameleta nyuma yetu. Kamma ni kuchangia gharama za hizo nguzo basi tuweken sawa sisi wananchi tupo tayari tuchangishane mtuwekee nguzo ili tupeleke maombi ya kuingiziwa umeme
Nasubiri jibu la hapaHuu ni mkanganyiko, kama matumizi yangu ya mwanzo nimeyaeleza 7500 nilikua napata 61.5units saivi kwa hiyo hiyo bei ni unit 21.1 nashindwa kuelewa kwamba hili kundi ndio sahihi? Sipingi huo uhakiki wenu ila mseme zoezi litachukua muda gani kurudi hali ya awali
Mtanifungia umeme lini jamani mbona imekua ni kero sana!!!I? Nina miezi 3 tangu nilipie na muda kusubiri umekwisha kila siku hakuna sababu za msingi. Wengine wamefungiwa kwa haraka na tulikuwa pamoja kwenye malipo mpaka ufuatiliaji nimuone nani; na mimi nitoe kidogo nipate huduma. Maana haya ni mazingira ya RUSHWA. TANESCO Makao Makuu nimeomba namba zenu hamtaki kunipa shida Ni nini jamani. Tanesco Kigamboni wanatesa wao huwajali wenye uwezo kipesa na mamlaka. Sisi walala hoi kila siku huambiwa nguzo, mara mita na waya hamna. Wakiona wamezidiwa hukimbilia magari mabovu ya kusambaza nguzo. Nifanye nini jamani.Tutakufungia umeme hauna haja ya kuwa na hofu wala kudhani tunahitaji chochote.hii ni haki yako na sisi ni wajibu wetu.upo kwenye orodha yetu