Tanesco Kimara mna matatizo gani wiki hizi mbili?Kwanini umeme unasumbua hivi?Usiniulize namba ya simu nimeshakupa location ni kote kuanzia Ubungo,Kimara hadi Mbezi umeme unakatika mno.
Hivi Tanesco hili suala lina siri gani,kwanini inapofika miezi kuanzia October hadi February huwa huduma zenu za umeme ni mashaka sana?Nawafuatilia miaka mingi iko hivi yaani ikishafika miezi hii ya October,November,December huwa kuna umeme kukatika mno.Sijui siri ya hii ni nini.Tumeenda mwaka vizuri sana huu ila tayari saa hizi ni full matatizo.Mnaua uchumi wa mtu mmoja mmoja jamani.
Mm napata hasara kila siku yani?
Wanakata bila hata taarifa kazi zinadolola ,
Unaenda kazini kung'aa sharubu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu nilikuwa ninanunua umeme kupitia simu Vodacom kwa bahati mbaya mita ile sio yenyewe, sijui jinsi ya kuurudisha tafadhali kama kuna mzoefu wa haya masuala yaani kiukweli hapa nilikuwa na akiba hiyo hiyo jana tu nimetoka kufanya manunuzi ya sikukuu.

Tafadhali nawaomba sana jinsi ya kurudisha ninunue namba genuine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kofia ya plastiki,
Kusema kweli muamala huo ukishafanyika huwezi ku"reverse". Hiyo ndio imetoka. Kuna jirani yangu alinunua umeme wa sh 50000 badala ya 5000 na hakuwa na akiba nyingine ya pesa ya matumizi alipoenda TANESCO wamsaidie walisema haiwezekani kwa hiyo aende akautumie kwa amani. Ikabidi aangalie tv huku njaa inauma.

Sijajua kama ulikosea kuingiza namba ya mita au ulifanya selection kimakosa.Kama ni selection yaani huenda kuna mita nyingine uliwahi kununulia umeme kwa simu yako ikajisajili Mpesa kama uliyemnunulia unamfahamu mnaweza kuyajenga.
Iliwahi kunitokea nilikuwa nimemnunulia mtu umeme kwa simu yangu mara kadhaa kwa hiyo namba yake ya mita bado ipo Mpesa hadi leo. Siku hiyo nikakosea selection.

Nikachagua yake badala ya kuchagua yangu. Niliwasiliana naye nikamtumia token akaingiza tulipoonana akanirudishia hela.

Sijajua kama wewe kama tatizo lako ni kama hilo langu.
 
Kusema kweli muamala huo ukishafanyika huwezi ku"reverse". Hiyo ndio imetoka. Kuna jirani yangu alinunua umeme wa sh 50000 badala ya 5000 na hakuwa na akiba nyingine ya pesa ya matumizi alipoenda TANESCO wamsaidie walisema haiwezekani kwa hiyo aende akautumie kwa amani.Ikabidi aangalie tv huku njaa inauma.
Sijajua kama ulikosea kuingiza namba ya mita au ulifanya selection kimakosa.Kama ni selection yaani huenda kuna mita nyingine uliwahi kununulia umeme kwa simu yako ikajisajili Mpesa kama uliyemnunulia unamfahamu mnaweza kuyajenga.
Iliwahi kunitokea nilikuwa nimemnunulia mtu umeme kwa simu yangu mara kadhaa kwa hiyo namba yake ya mita bado ipo Mpesa hadi leo. Siku hiyo nikakosea selection. Nikachagua yake badala ya kuchagua yangu. Niliwasiliana naye nikamtumia token akaingiza tulipoonana akanirudishia hela. Sijajua kama wewe kama tatizo lako ni kama hilo langu.
Kuna mita mbili mkuu moja ni mbovu sasa hapa inachofanyika unanunua nyingine unaingizia nyingine sasa nikakosea kutumia namba ya mita ya zamani hapo ndo yaliponiiiva macho mkuu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Subiri tarehe 27 uende ofisini tanesco ujieleze watakusaidia maana hizi namba ni token wala siyo halisi kama haijaingizwa kwenye luku. Labda mkuu kama hutajali tukupige tafu tu usilale gizani! Nitumie pm namba zako za luku nikushike mkono!
 
Back
Top Bottom