Masasi kata ya Jida namba ya simu siwezi weka hapa kwa sababu hii sio ishu binafsi suala la msingi wewe ndo uwasiliane na Tanesco Masasi uulizie Nini tatizo uje na majibu yanayo eleweka hapa.Mimi namba siweki hapa.
Swala hili hatuwezi kulijibu moja kwa moja mpaka kupata taarifa kamili kutoka ofisi ya eneo lako tafadhali tupatie namba ya mita na namba ya simu. AIDH mteja anawajibika kulinda miundombinu ya umeme iliyotumika kumpatia umeme
Sent using Jamii Forums mobile app
Tunaomba namba yako ya simu tafadhaliApa ninavyotoa haya malalamiko umeme umekatika tokea jana haujarudi na hiyo ni kawaida ya umeme wa huku yani unakatika masaa 12 unawaka masaa 2 au nusu saa unakatika tena wenyeji wa hapa wanasema tatizo hili lilianza mara baada ya kubadili chanzo cha umeme kutoka wa mafuta na kuanza kutumia umeme wa gesi kuna jamaa yangu yupo UTP(hawa ni km wanawasaidia TISS) anasema aliwahi kwenda ktk ofisi za tanesco kufanya uchunguzi akaniambia pale kuna tatizo sio tu suala la umeme wa gesi lkn hakunieleza kwa undani,
TANESCO Liwale tunaomba mtupe majibu yanayoeleweka kwnn umeme haueleweki huku Liwale kama tatizo ni gesi kwnn msiturudishe kwenye umeme wetu wa uhakika kwnn muingie ktk biashara msiyoiweza ya kutumia gesi ilihali mnajua kuwa hamuuwezi km tatzo ni wafanyakazi au mabosi tunaomba mkuu wa wilaya uliangalie hili kwa umakini kwani tunateseka sn wakazi tunapata hasara mno vitu vimekua vikiungua kutokana na waka zima hii.
Nawasilisha
Sent using Jamii Forums mobile app
Tunashukuru kwa taarifa tunaifanyia kaziHabari
Mi mkazi wa mshangano manispaa ya songea tatizo langu ni kuhusu kuingiziwa umeme process zote nimeshamaliza ambapo mpaka wapimaji washapima inahitajika nguzo moja.
Swali langu je Mimi nitahudumiwa lini maana naona muda unapita tu ila naona majirani wanaingiziwa umeme( wa ndani ya mita 30)
Hela ya kuingiza umeme ninayo mnanisaidiaje na Mimi nikae mwenye umemee
Tafadhari sana.
0767309201
wakunyumba@gmail.com
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kuna jinsi ya ku disable alarm za luku zinazolia kila saa kama umeme unaisha ..?? Inaleta usumbufu, mbona zingine hua ni mara moja tu zinalia
Tukikupeni namba za simu mnaanza kututolea kauli zenye kutia shaka mm nadhani huo utaratibu wa kuomba namba za simu muubadilishe TANESCO