Kumekuwa na katika katika ya Umeme kwa muda mrefu bila taarifa. Maeneo mengi ya jiji la Dar Umeme unakatika kuanzia asubuhi hadi jioni.
TANESCO tufahamisheni kama ni matengenezo ya kawaida ni mgawo ili tuwe na ratiba.
Huo Umeme mnaojivunia nao kwamba upo wa kutosha uko wapi?
View attachment 1026133
Sent using
Jamii Forums mobile app
*FEBRUARI 16, 2019*
*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*
*TAARIFA YA MATENGENEZO YA MASHINE KITUO CHA KUFUA UMEME KWA GESI CHA UBUNGO II PAMOJA NA KITUO CHA SONGAS*
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wa Dar es Salaam na Zanzibar kuwa kutokana na kufanya maboresho makubwa yanayohusisha matengenezo ya mashine 3 za kituo cha ubungo II moja baada ya nyingine, uwekaji wa transfoma kubwa la MVA 300 kwenye kituo cha kupoza umeme cha Ubungo ili kukiongezea uwezo na kwenda sambamba na ukuaji wa mahitaji ya jiji la Dar es Salaam kutakuwa na mapungufu ya upatikanaji wa huduma ya umeme kwa maeneo tajwa.
Aidha, Kampuni ya Songas itafanya matengenezo kinga katika mashine zake. Matengenezo hayo katika vituo vya Ubungo na Songas yataendelea kwa awamu na yanatarajiwa
kukamilika ifikapo mwezi Juni , 2019.
Wataalamu wetu kwa Kushirikiana na Mkandarasi Kampuni ya SIEMENS kutoka nchini Sweden wanaendelea na matengenezo ya mashine na ubadilishaji wa vipuri ili kuongeza ufanisi zaidi katika uendeshaji wa mitambo hii na kuimarisha hali ya upatikanaji umeme kwa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar.
Huduma ya umeme haitakosekana kwa kipindi chote cha matengenezo ila kwa baadhi tu ya siku na nyakati.
Mashine hizo za Ubungo II na Songas zimeungwa katika mfumo wa usambazaji umeme wa msongo wa kilovolti 132 wa Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar na hivyo kusababisha mapungufu katika maeneo tajwa.
Tutaendelea kutoa taarifa zaidi ya hali ya matengenezo inavyoendelea.
Ahsanteni kwa ushirikiano wenu.
Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.
Kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100
*Tunaomba radhi kwa usumbufu unakaojitokeza*
Tovuti:
www.tanesco.co.tz,
*Mitandao ya kijamii*
Twitter,
www.twitter.com/tanescoyetu,
Facebook
https://www.facebook.com/tanescoyetultd/
*IMETOLEWA NA:*
OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
Sent using
Jamii Forums mobile app