TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Tanesco Nyamagana mnatuumiza wateja wenu tumelipia kuvuta umeme tangu mwezi wa kumi mwaka jana hadi leo ni chenga tu za hapa na pale....ohh nguzo hamna, nguzo hazijaja huku wengine wanafungiwa tabia mbaya.
 
Tanesco Kisarawe, sie wakazi wa Chanika zingiziwa tunahitaji umeme tulitafuta surveyor kaja kuhesabu nguzo zinazohitajika zimefika 15 amesema idadi hyo yapasa tupate mradi, awamu zote za Rea wametupita kama hawatuoni na nguzo zetu zikahamishwa kupelekwa Mvuti cc CCM tunawasubiri kwa hamu maana mliahidi tumchague Waitara mlete umeme .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo Tabora vijijini.Nimewapigia Tanesco mikoani (Regional Manager) siku ya 5 sasa hatuna umeme.Namba zangu 0787938347.Vitu vinaharibika kwenye Frizer jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco Kisarawe, sie wakazi wa Chanika zingiziwa tunahitaji umeme tulitafuta surveyor kaja kuhesabu nguzo zinazohitajika zimefika 15 amesema idadi hyo yapasa tupate mradi, awamu zote za Rea wametupita kama hawatuoni na nguzo zetu zikahamishwa kupelekwa Mvuti cc CCM tunawasubiri kwa hamu maana mliahidi tumchague Waitara mlete umeme .

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunaomba namba yako ya simu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mrad wa rea morogoro ifakara kata ya mbasa kuna baadh ya maeneo yamechimbwa mashimo hawajaweka nguzo ili hal sehem nyingine wanasambaza nyaya na kila tukimuuliza mkandaras anasema nguzo zimeisha na hana matumain ya kuleta hii imekaaje?
Tunaomba namba yako ya simu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO WANAZINGUA SANA UNALIPIA UMEME KUJA KUFUNGUWA HADI KIELEWEKE BAHASHA KWA MAFUNDI NA FUNDI MKUU ANAYEPANGA WATU....guys Mh Kalemani kweli tutafika unayoongea kwenye majukwaa na Bungeni ni tofauti na hali halisi ….haswa DMS...KITUO CHA TEGETA ….RUSHWA RUSHWA...
Tunaomba namba yako ya simu tufatilie tuhuma zako na kuchukua hatua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moshi eneo la mjohoroni Shia hakuna umeme wiki sana. Simu ikipigwa majibu 'mafundi wanakuja sasa hivi' wiki sasa,,Kulikoniii
 
Kumekuwa na katika katika ya Umeme kwa muda mrefu bila taarifa. Maeneo mengi ya jiji la Dar Umeme unakatika kuanzia asubuhi hadi jioni.
TANESCO tufahamisheni kama ni matengenezo ya kawaida ni mgawo ili tuwe na ratiba.
Huo Umeme mnaojivunia nao kwamba upo wa kutosha uko wapi? View attachment 1026133

Sent using Jamii Forums mobile app
*FEBRUARI 16, 2019*

*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*

*TAARIFA YA MATENGENEZO YA MASHINE KITUO CHA KUFUA UMEME KWA GESI CHA UBUNGO II PAMOJA NA KITUO CHA SONGAS*

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wa Dar es Salaam na Zanzibar kuwa kutokana na kufanya maboresho makubwa yanayohusisha matengenezo ya mashine 3 za kituo cha ubungo II moja baada ya nyingine, uwekaji wa transfoma kubwa la MVA 300 kwenye kituo cha kupoza umeme cha Ubungo ili kukiongezea uwezo na kwenda sambamba na ukuaji wa mahitaji ya jiji la Dar es Salaam kutakuwa na mapungufu ya upatikanaji wa huduma ya umeme kwa maeneo tajwa.

Aidha, Kampuni ya Songas itafanya matengenezo kinga katika mashine zake. Matengenezo hayo katika vituo vya Ubungo na Songas yataendelea kwa awamu na yanatarajiwa
kukamilika ifikapo mwezi Juni , 2019.

Wataalamu wetu kwa Kushirikiana na Mkandarasi Kampuni ya SIEMENS kutoka nchini Sweden wanaendelea na matengenezo ya mashine na ubadilishaji wa vipuri ili kuongeza ufanisi zaidi katika uendeshaji wa mitambo hii na kuimarisha hali ya upatikanaji umeme kwa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar.

Huduma ya umeme haitakosekana kwa kipindi chote cha matengenezo ila kwa baadhi tu ya siku na nyakati.

Mashine hizo za Ubungo II na Songas zimeungwa katika mfumo wa usambazaji umeme wa msongo wa kilovolti 132 wa Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar na hivyo kusababisha mapungufu katika maeneo tajwa.

Tutaendelea kutoa taarifa zaidi ya hali ya matengenezo inavyoendelea.

Ahsanteni kwa ushirikiano wenu.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100

*Tunaomba radhi kwa usumbufu unakaojitokeza*

Tovuti: www.tanesco.co.tz,

*Mitandao ya kijamii*

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

*IMETOLEWA NA:*

OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imekua kero sasa hasa wakazi wamaeneo ya kwangulelo mpaka tengeru. Kila siku umeme unazimwa kuanzia saa 1 usiku mpaka saa 4 usiku.

mbaya tanesco mkoa haitoi taharifa yeyote kwa wateja wake inafanya mazoea na kukatatu bila kujali athari wanazopata wateja kwa kukosa huduma iyo hasa nyakati mbaya za usiku.

tunaomba taharifa pia mjue sio wananchi wote wanauwezo wakumiliki majenereta kama sisi wenye uwezo mkubwa hivyo muwe mnatoa taharifa kwa wananchi wajiandae kwa mgao uo.
Wilaya

Namba ya simu

Eneo

Tunaomba hizo taarifa kwa hatua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi unit 50 mnazotowa mara baada ya kufungiwa umeme kwa mara ya kwanza ni hisani na kama hisani ni bora muitoe iliijulikane moja haipo

Tangu mwaka Jana mwezi wa 10 hadi leo nasumbukia unit 40 kweli

Kuweni waungwana tu

Namba ya luku ni 54183706958

Jina Rebeca Ruhunde Mahona

Mkoa Shinyanga
Wilaya Kahama
Mtaa MWENDAKULIMA KATI
Siku hizi wanatoa 10 tu ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
86 Reactions
Reply
Back
Top Bottom