Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 28,749
- 91,814
Hii Miili kwa Mujibu wa Mtoa taarifa, ilikua inatoa harufu Kali sanaaaa , maana yake Kama imefukiwa na Serikali, ni kwamba sehemu ilipokua miili hiii, Serikali haikua na uwezo wa kuihifadhi , Je Serikali inakoswa uwezo wa kuhifadhi miili ???
TAHARUKI YAZUKA BAADA YA MIILI MINGI ILIYOHARIBIKA KUFUKIWA MSAE, KIBAHA
Baba Askofu Mwamakula!
Jana, 22 Februari 2026, tukio la ajabu liltokea Kibaha Mkoani katika Mtaa wa Uhuru. Ilikuwa hivi: Ilipita pikipiki ya miguu mitatu na ilibeba viroba vyeusi vingi kama uchafu vikitoa harufu kali. Kuifuatilia ile Toyo, ikasimama katika eneo la Makaburi ya Msae. Na palikuwa na takribani makaburi ishirini yamechimbwa. Ghafla wale watu wachache wakaanza kuvirusha vifurushi kwenye makaburi hayo na kuanza kuvifukia.
Hakukuwa na Mwenyekiti wa Mtaa, mjumbe wala askari; bali waliokuwepo ni wachimbaji na gari suzuki yenye namba SM. Taharuki ilikuwa kubwa kwamba hizo maiti zilitoka wapi? Kama ni hospitali kwa nini zizikwe hivyo asubuhi? Na kama ni zilizokosa ndugu, utaratibu uko hivyo?
Kwa kweli fuatilieni mtagundua hayo makaburi bado ni mabichi na ufafanuzi sahihi upatikane kutoka kwa wahusika ili kuondoa sintofahamu. Nimetuma picha hizo hapo.
S. M.,
Mwananchi kutoka Kibaha, 23 Februari 2026.
Ndugu Watanzania!
Hii ni habari ya kutisha sana, ilihitaji ujasiri kwa mtoa taarifa hii kuifikisha. Lakini ilihitaji ujasiri wa hali ya juu kwetu kuiweka hapa. Kwa hiyo, hii inabaki kuwa tuhuma dhidi ya watu ambao hawajulikani kuwa walifanya mauaji ya watu hao ni kwenda kuwafukia kule Kibaha.
Kwa kuwa mtoa taarifa anaeleza kuwa 'mizigo' au miili iliyowekwa katika viroba vile ilikuwa pia inatoa harufu kali sana inawezekana kuwa miili hiyo ilikuwa imekaa muda mrefu huko ilikotoka.
Kwa kuwa eneo lililotajwa linajulikana, ushauri wetu ni huu: wanakijiji wote wafike mahali pale kesho au keshokutwa na kuudai uongozi wao wa Mtaa uite viongozi wa juu kujadili juu ya hilo tukio. Lakini pia hata vyombo vya habari vifike mahali pale kuona kama kweli kuna mazingira ya kuzika miili mahali pale.
Watu wema waanze kufuatilia nyendo za watu kuanzia usiku huu. Wapige picha kwa siri hata kurekodi video kuhusu jambo lolote linalotokea kuanzia sasa. Kama ni kweli hilo tukio lilitukia, wahusika watatafuta namna ya kufukua mahali pale ili kuiondoa kuipeleka sehemu nyingine!
Kwa maelezo ya mtoa taarifa hapo juu, huenda miili hiyo kuna mahali ilikuwa imewekwa kwa muda mrefu ndio maana pia ikawa imeharibika kiasi cha kutoa harufu kali sana. Je, wewe ni mwenyeji wa Kibaha? Je, kuna eneo linaloitwa Makaburi ya Msae? Je, umesikia taarifa hizo?
Je, kuna makaburi au majimbo mengi mabichi?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 23 Februari 2026; Saa 5:45 usiku