Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,007
- 15,248
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, inatarajiwa kuendelea leo, Februari 17, 2026, katika Mahakama Kuu, Masijala Ndogo, Dar es Salaam.
Leo kesi hiyo itaendelea kusikilizwa mfululizo katika hatua ya ushahidi, ambapo tayari mashahidi wanane wa Jamhuri wameshatoa ushahidi wao.
Mahakama ilitoa maelekezo kwa upande wa Jamhuri kuwasilisha mashahidi wasiopungua watatu. Maelekezo hayo yalitolewa baada ya Lissu kueleza kuwa kutokuwepo kwa mashahidi wa kutosha kunasababisha upotevu wa muda mwingi wa mahakama.
--
Majaji nao wanaingia kama kawaida yupo
1. Jaji Dunstan Ndunguru Kiongozi wa Jopo.
2. Jaji James Karayemaha
3. Jaji Ferdinand Kiwonde
Wote watatu wapo wakiwa kwenye majoho yao mekundu na Beib nyeupe.
Renatus Mkude anasimama, yupo na ajuaye, Thawabu Issa, Ignas, Winiwa Kasawa pia.
Anasema leo wako na mashahidi watatu na tuko tayari kuendelea.
Jaji anamuuliza Mshitakiwa nae anamjibu niko tayari.
Majaji wanaandika kidogo.
Ukimfuatilia Mwenyekiti wa Jopo la Majaji, Jaji Ndunguru amekuwa anaonekana ni mtu mstaarabu.
PF 1864 ASP Geofrey Lutufye
Naitwa PF18544 ASP Geofrey Aggrey Lutufye
Umri wa miaka 47.
Naishi Arusha.
Mkristu.
Anaongozwa na Renatus Mkude.
Anaanza Renatus Mkude kumuuliza Maswali.
Wakili: Ikumbushe mahakama majina yako.
ASP Geofrey Lutufye: Anataja majina yake hapa
Wakili: Kazi yako?
ASP Geofrey Lutufye: upelelezi, niko ofisi ya mkuu wa upelelezi Arusha na mimi ni kiongozi wa kikosi cha Anti Robbery
Wakili: Anti Robbery ni nini?
ASP Geofrey Lutufye: Kikosi cha kuzuia uhalifu kama vile uporaji.
Kumbe ndio maana ana hali hii huyu askari. maana kiukweli amekaa hovyo sana kumbe anadeal na mambo ya kupora.
Wakili : Umepata mafunzo gani?
ASP Geofrey Lutufye: Nilipata tarehe 28/04/2003 Chuo cha Polisi Moshi.
Nilijifunza upelelezi na mafunzo mengine mbalimbali, nilimaliza mwezi wa 11, 2003.
Mafunzo mengine nilipata ya nyota ya kwanza, nilisomea Chuo cha Polisi Moshi ilikuwa ni Mwaka 2013 na baadae mafunzo ya cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi. Nililipata chuo Dar es salaam Polisi Academy hapa Dar es salaam nilimaliza mwezi wa 11 mwaka 2023.
Wakili: kingine ni nini?
ASP Geofrey Lutufye: Mengine ni on job training yaani mafunzo kazini.
Wakili: Una uzoefu kazini wa mwaka gani?
ASP Geofrey Lutufye: Miaka 15 ya upelelezi ninayo.
Wakili: Arusha uko tangu lini ofisi ya upelelezi.
ASP Geofrey Lutufye: Tangu mwaka 2023.
Wakili: kabla ya hapo ulikuwa wapi?
ASP Geofrey Lutufye: Nilianzia Polisi Oysterbay Dar es salaam, nilianza kama General Duty na baadae nikapelekwa Geita Ofisi ya Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Geita ndo nikahamia mkoa wa Arusha baada ya huko.
Wakili: Majukumu yako hapo ofisi ya Upelelezi Arusha ni yapi?
ASP Geofrey Lutufye: Kufanya doria mbalimbali, kukamata watuhumiwa, kufanya upelelezi na kuwafikishia watuhumiwa Mahakamani.
Wakili: Tarehe 03/04/2025 kilitokea nini?
ASP Geofrey Lutufye: Nilikuwa na wenzangu tukiwa na section 1 ambayo ni askari 9 hadi na dereva tukiwa kwenye doria.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Tulikuwa tunafanya doria tukiwa tunatumia gari la Polisi aina ya Toyota Landcruiser na nikapata maelekezo kutoka kwa kaimu mkuu wa upelelekezi ASP Bonny Mgogo.
Wakili: kwa njia ulipata maelekezo?
ASP Geofrey Lutufye: Nilipata kwa njia ya radio call ambayo ni kifaa cha mawasiliano. Maelekezo kuwa amepata taarifa kutoka kwa msiri kuwa kwa Mromboo kijiwe cha Bajaji kuna vijana wanahamasishana kuzuia uchaguzi wa mwaka 2025.
Wakili: Baada ya kufika huko kwa Mromboo nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Nilikuta vijana wakila njama za kuzuia uchaguzi Mkuu 2025.
Jaji anasema umesema Walikuwa wanakula nini?
ASP Geofrey Lutufye: Walikuwa wanazungumzia uchaguzi mkuu wa 2025.
Jaji: Kumbe walikuwa wanazungumzia sio kula tena?
Watu wanacheka.😂😂😂
Wakili wa Serikali anaendelea kumuongoza shahidi
Jaji: Endeleeni
Wakili: Eheee, kikaendelea nini?
ASP Geofrey Lutufye: Nilivyowakuta wale vijana waliokuwa wanakula njama nikawaambia wako chini ya Ulinzi.
Jaji: Hiyo MIC ameshikaje mbona hasikiki?
Wakili: ikawaje shahidi?
ASP Geofrey Lutufye: Tuliwakamata P4 na P7 ambao walikuwa wameanza kukimbia baada ya hapo nilitoa maekekezo wapelekwe kituo cha Polisi Murieti, hao askari ni wanne, kituo cha Murieti kipo Mkoa wa Arusha.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Sisi tuliendelea kuwatafuta waliokuwepo pale lakini hatukufanikiwa kuwakamata.
Wakili: Nini kingine kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Waliacha Bajaji zao tukazichukua na kuzipeleka kituo cha Polisi Murieti na mbili zilikuwa za wale watuhumiwa tuliowakamata.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Majira ya saa moja ndio tulizipeleka hizo Bajaji kituo cha Polisi Murieti.
Wakili: Kituo cha Polisi Murieti nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Ulipata maelekezo kutoka kwa kaimu mkuu wa upelelezi Arusha.
Maelekezo hayo yalinitaka niwapeleke ofisi za mkuu wa upelelezi Arusha, tukiwa njiani tunawapeleka P4 na P7 niliwahoji kwamba kwanini mnahusika kula njama kutaka uchaguzi mkuu wa 2025 usifanyike?
Wakili: Ikawaje?
ASP Geofrey Lutufye: Wote walikiri kuwa wanamuunga mkono Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu kutokana na ile kauli yake aliyoitoa kwenye Mtandao kuwa atazuia Uchaguzi, ataleta uchochezi na atakinukisha.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Tuliwafikisha Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha majira ya saa mbili.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Nilipewa maelekezo tena nifungue jalada la uchunguzi. Nilifungua jalada hilo ambalo ni ARS/D/CID/B/40/2025.
Wakili: Kikaendelea nini?
ASP Geofrey Lutufye: Nikapewa maelekezo tena na Kaimu Mkuu wa Upelelezi Arusha yakinitaka niwahoji watuhumiwa hao kwa kuchukuliwa maelezo yao.
Wakili: Nini kiliendelea?
ASP Geofrey Lutufye: Mimi niliwaa asign maaskari wengine wa RCO wawachukue maelezo na mimi nikaendelea na majukumu mengine.
Wakili: Kingine kilichoendleea?
ASP Geofrey Lutufye: Niliandika maelezo yangu Tarehe 18/04/2025.
Renatus Mkude, Wakili wa Serikali. Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji kwa shahidi huyu.
Jaji Ndunguru: Maswali ya Dodoso
Mhe. Lissu anasimama: Shahidi, naomba nikuulize maswali na ujibu maswali yangu kwa kadri nitakavyokuuliza.
Sasa waeleze majaji, Huko Polisi mnakojifunzia hizi kazi huwa mnafundishwa kuwa waongo?
ASP Geofrey Lutufye: Hatufundishwi kuwa waongo.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama huwa mnafundishwa mnapotoa ushahidi mahakamani kuongeza maneno ambayo hayapo?
ASP Geofrey Lutufye: Hatufundishwi.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama huko Polisi mnafundishwa kutokuwa na heshima?
ASP Geofrey Lutufye: Sio kweli
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama huko Polisi mnafundishwa watu wasio na maadili?
ASP Geofrey Lutufye: Sio kweli
Mhe. Lissu: Sio kweli nini sasa?
ASP Geofrey Lutufye: Tunafundishwa kuwa watu wenye maadili.
Mhe. Lissu: Unafahamu kitu kinaitwa PGO?
ASP Geofrey Lutufye: Amekaa kimya kidogo, PGO naifahamu mimi.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama ni sahihi au sio sahihi kwamba PGO inasema askari wanapaswa kuwa weledi kwenye kazi zao?
ASP Geofrey Lutufye: Ni kweli inasema hivyo.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kwa mujibu wa PGO Polisi wanatakiwa kuwa waaminifu. Anamsomea PGO hapa. Wasiwe mafisadi na wawe wakweli
ASP Geofrey Lutufye: Ni kweli.
MheLissu: Hii PGO leo tutacheza nayo sana. Umesema uliandika maelezo yako Polisi?
ASP Geofrey Lutufye: Ni kweli niliandika na naweza kuyatambua.
Mhe. Lissu: Mheshimiwa Jaji naomba apewe maelezo yake.
Anatafutiwa na kupewa hapa.
ASP Geofrey Lutufye: Haya ndio maelezo uliyoandika Tarehe 18/04 mwaka jana.
Mhe. Lissu anaendelea na maswali ya dodoso.
Mhe. Lissu: Nani alikuandikia hayo maelezo?
ASP Geofrey Lutufye: Niliandika mwenyewe.
Mhe. Lissu: Nani alikupa onyo wakati unaandika hayo maelezo?
ASP Geofrey Lutufye: Hakuna aliyenipa onyo.
Mhe. Lissu: Nani aliyekushuhudia?
ASP Geofrey Lutufye: Hakuna aliyenishuhudia.
Mhe. Lissu: Naomba ku impeach credit ya huyu shahidi, anamsomea Maelezo yake.
Nina cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi na majukumu yangu kusimamaia askari walio chini na kufanya upelelezi.
Anasoma maelezo ya shahidi ambayo alijiandika mwenyewe kuhusu alivyokwenda kuwakamata watuhumiwa.
Amemaliza kumsomea hayo maelezo yake, anamtajia maeneo anayotaka kumkanusha.
1. Eneo kuhusu Elimu yake na mafunzo yake.
2. Uzoefu kazini wa miaka 15.
3. Maeneo yote alikopitia kuanzia Oystebay, Geita hadi kufika Arusha
4. Kikosi chako cha watu 9.
5. Ulipigiwa simu ya radio call
Anamsomea maeneo ambayo shahidi ameyaongeza hapa Mahakamani hajayaweka kwenye maelezo yake.
Mhe. Lissu: Sasa wambie Majaji kama ungependa hayo maelezo yako yaingie kama Kielelezo.
ASP Geofrey Lutufye: Ndio nataka yaingie kama kielelezo.
Jaji: Maelezo yatakuwa ni Exbit D8.
Mhe. Lissu: Mh. Jaji apatiwe maelezo.
Mhe. Lissu: Ukishika hayo maelezo uniambie?
ASP Geofrey Lutufye: Ninayo tayari.
Mhe. Lissu: kuhusu mambo ya elimu yako ni muhimu au sio muhimu.
ASP Geofrey Lutufye : ni Muhimu
Mhe. Lissu: Yapo kwenye maelezo uliyotoa Polisi?
ASP Geofrey Lutufye: Kwenye statement sheet siwezi kuandika kila kitu.
Mhe. Lissu: Nimesema yapo au hayapo?
ASP Geofrey Lutufye: Hayapo.
Mhe. Lissu: Uzoefu wa miaka 15 katika upelelezi umesema.
ASP Geofrey Lutufye: kweli
Mhe. Lissu: Umesema hayo ili mahakama ifahamu una utaalamu?
ASP Geofrey Lutufye: ili ujue mimi ni mzoefu?
Mhe. Lissu: Uliona usema hivyo ili mahakama ifahamu kwasababu ni jambo muhimu?
ASP Geofrey Lutufye: Uko sahihi.
Mhe. Lissu: uliandika au hukuandika?
ASP Geofrey Lutufye: Sikuandika.
Mhe. Lissu: Kwasasa uko ofisi ya RCO Arusha lakini uliwahi kuwafanya maeneo mengine ikiwemo Oysterbay na Geita.
ASP Geofrey Lutufye: Ni kweli
Mhe. Lissu: Ulisema ili mahakama ijue wewe ni askari mzoefu wa maeneo mbalimbali.
ASP Geofrey Lutufye: Kweli.
Mhe. Lissu: Umeandika hayo mambo kwenye maelezo yako Polisi?
ASP Geofrey Lutufye: Siwezi kuandika kila kitu.
Mhe. Lissu: Jibu swali langu
ASP Geofrey Lutufye: Sikuandika.
Mhe. Lissu: Tarehe 03/04 ukiwa kwenye patrol ukiwa na wenzako section ya watu 9 pamoja na Dereva.
ASP Geofrey Lutufye: Ni kweli
Mhe. Lissu: yapo kwenye maelezo yako?
ASP Geofrey Lutufye: Hayapo.
Mhe. Lissu: ulisema uliwasiliana na Deputy RCO Mgogo akakupa mawasiliano kwa radio call?
ASP Geofrey Lutufye: Hayapo
Mhe. Lissu: Wakati unawapeleka kwa RCO mkiwa kwenye gari uliwahoji kwanini wanakula njama ili uchaguzi mkuu usifanyike, waeleze majaji kama yapo kwenye maelezo yako?
ASP Geofrey Lutufye: Sikuyaandika.
Mhe. Lissu: Unasema ulitoa maelekezo kuwa watuhumiwa wahojiwe, angalia kwenye maelezo yako kama kuna hayo maneno kwenye maelezo yako?
ASP Geofrey Lutufye: Hayapo.
Mhe. Lissu: Kwahiyo Shahidi ni sahihi nikisema kuna mambo hukuyasema kwenye maelezo yako Polisi ila umeyaongeza hapa Mahakamani?
ASP Geofrey Lutufye: Nilikuwa najaribu kufafanulia Mahakama.
Mhe. Lissu: Umeeleza sababu ya tofauti hizi ambazo nimezionesha.
ASP Geofrey Lutufye: Siwezi kuandika maelezo yote kwenye statament sheet ni maelezo muhimu na yenye uzito.
Mhe. Lissu: Unafahamu masharti ya kazi ya Polisi kwa mujibu wa PGO?
ASP Geofrey Lutufye: Nafahamu
Mhe. Lissu: Order 1 Para 25 ya PGO za 2021 inayosema makosa ni lazima yawe yamesemwa na sheria.
Sasa kwenye kielelezo D8 umesema "nilipata maelekezo kutoka kwa ASP Mgogo kuwa kuna watu wanapanga njama ya kuzuia uchaguzi" hayo ni maelezo yako?
ASP Geofrey Lutufye: Ni kweli yangu.
Mhe. Lissu: Ni sheria gani inayosema ni kosa la jinai?
ASP Geofrey Lutufye: Siwezi kujua.
Mhe. Lissu: Sasa ulienda kukamata watu kwa kosa gani walilofanya wakati hujui kosa lao? Ulienda kuwakamatia nini?
ASP Geofrey Lutufye: Tuliwakamata kwasababu ya Uchochezi.
Mhe. Lissu: ulienda kukamata watu kwa kosa gani?
ASP Geofrey Lutufye: Walikuwa wanakula njama.
Mhe. Lissu: Kula njama ya nini?
Umeshaaingia kwenye 18 zangu.
Mhe. Lissu: Sasa twende kwenye maelezo yako, nani aliyekuruhusu kujiandikia maelezo wewe mwenyewe?
ASP Geofrey Lutufye: Nilikuwepo kwenye ukamataji
Mhe. Lissu: Nani aliyekwambia unaweza kujiandikia maelezo?
ASP Geofrey Lutufye : Amekaa kimya.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa amekaa kimya. Sema nani aliyekwambia unaweza kujipa onyo?
ASP Geofrey Lutufye: Kakaa kimya
Mhe. Lissu: Kwa vile halina swali na hilo jibu swali lingine kuwa nani alikushuhudia.
ASP Geofrey Lutufye : amekaa kimya.
Mhe. Lissu: Sasa ngoja nikupeleke kwenye PGO.
Mhe. Lissu : Hivi PGO imeweka utaratibu ukisoma PGO 236 imeweka utaratibu wa kuandika maelezo ya mashahidi?
ASP Geofrey Lutufye: ni kweli.
Mhe. Lissu: Hiyo PGO 236 inasema investigation statements sasa ni kweli kwa mujibu wa hiyo PGO mtu anayeandika maelezo ya shahidi anakuwa tofauti na huyo anayemuandikia?
ASP Geofrey Lutufye: unaweza jiandika mwenyewe.
Mhe. Lissu: PGO ya ngapi?
ASP Geofrey Lutufye: Sikumbuki
Mhe. Lissu: Ngoja nikupe PGO ujikumbushe.
ASP Geofrey Lutufye: Mi nimesema siwezi kukumbuka.
Mhe. Lissu: apatiwe PGO amepewa.
Mhe. Lissu: Sasa tuonyeshe PGO gani inasema unaweza jiandika mwenyewe.
ASP Geofrey Lutufye: Siwezi kukumbuka.
Mhe. Lissu: Hukumbuki au hujui.
ASP Geofrey Lutufye : Sijui.
Mhe. Lissu: Umesema umeandika maelezo kwa mujibu wa kifungu cha 10(3) cha CPA.
ASP Geofrey Lutufye: Ni kifungu cha 10(3)B
Mhe. Lissu: Hicho kifungu hakipo unajua?
ASP Geofrey Lutufye: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Sasa hicho kifungu cha 10(3) hakina lolote kuhusu kujikanya, kujiandika.
ASP Geofrey Lutufye : Sikumbuki mimi.
Mhe. Lissu: Ni kweli maelezo yako yalipaswa yaandikwe na askari mwingine?
ASP Geofrey Lutufye : Naweza kuandika au anaweza kuniandika.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli maelezo yako yanapaswa yaandikwe na askari mwingine?
ASP Geofrey Lutufye : sijui hapo.
Mhe. Lissu: Ni kweli huyo askari mwingine ndio anapaswa akupe onyo?
ASP Geofrey Lutufye: sina jibu
Mhe. Lissu: PGO 236 para 19, importance of this order.
Anamsomea hapa kwamba kila polisi anapaswa kuijua kuhusu utaratibu wa kuandika maelezo. Je ulichokifanya kinaenda sambamba na masharti haya?
ASP Geofrey Lutufye: Siwezi kujua.
Mhe. Lissu: Turudi kwenye maelezo yako, uliposema mlipofika kwa mromboo mliwakuta vijana wakiwa wanazungumzia masuala ya Uchaguzi mkuu, ni sheria gani inayosema ni kosa la jinai?
ASP Geofrey Lutufye : Sio kosa la jinai.
Mhe. Lissu: Hawakuwa na kosa lakini umewakamata?
ASP Geofrey Lutufye: Walikuwa wanapanga kuzuia uchaguzi
Mhe. Lissu: Unajua hakuna kosa la kuzuia Uchaguzi?
ASP Geofrey Lutufye: Ni kosa.
Mhe. Lissu: kwa sheria gani?
ASP Geofrey Lutufye: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Nyie mmelitoa wapi hilo kosa wakati sheria ya uchaguzi hailitambui hilo kosa?
ASP Geofrey Lutufye : Mi najua ni kosa lakini sheria sijui.
Mhe. Lissu: kwasababu Kingai na Wambura wanasema ni kosa basi ni kosa?
ASP Geofrey Lutufye: Kimya.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama kuna sheria nyingine yoyote inayosema ni kosa?
ASP Geofrey Lutufye: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Je wale vijana mlipowakamata mliwapeleka mahakamani?
ASP Geofrey Lutufye: Mimi sikuaandika mimi maelezo yao.
Mhe. Lissu: Kwahiyo walipelekwa mahakamani au hawakupelekwa?
ASP Geofrey Lutufye : Sijui
Mhe. Lissu: Itakushangaza nikikwambia hawakupelekwa mahakamani?
ASP Geofrey Lutufye: Siwezi kushangaaa.
Mhe. Lissu: Mnajifanya mapolisi mnawasingizia watu vitu vya bure haya itakushangaza hao mliowakamata baada ya kesi yao kuisha ni mashahidi wa kesi hii?
ASP Geofrey Lutufye: Hainishangazi.
Mhe. Lissu: haikushangazi kwasababu huo ndio utaratibu wenu mapolisi wa Tanzania.
Mhe. Lissu: Au unabisha nikufungulie ripoti ya Jaji Mkuu Othman Chande amesema mnawafungulia watu makosa ya uongo.
Sasa nikuulize swali lingine, umewahi kuona video mimi nikiwa nazungumza habari za huo uchaguzi mkuu?
ASP Geofrey Lutufye : amekaa kimya
Mhe. Lissu: Unajua kwanini nimeshitakiwa kwa Uhaini ASP geofrey lutufye? Unajua sababu.
ASP Geofrey Lutufye : Sababu ya ile kauli uliyotoa.
Mhe. Lissu: Ipi hiyo?
ASP Geofrey Lutufye : Ulisema utazuia uchaguzi wa mwaka 2025.
Mhe. Lissu: Ndiyo, nakuuliza, uliiona hiyo video?
ASP Geofrey Lutufye: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Hawa ndio kesho watakuwa ma RPC siku inayofuata utashangaa anakuwa IGP,
Sina maswali mengine, Waheshimiwa majaji.
Anasimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude kwa ajili ya Re-examination
Maelezo yako uliandika kama nani?
ASP Geofrey Lutufye: Kama shahidi.
Wakili: Unalizungumziaje kuhusu kujiandika mwenyewe?
ASP Geofrey Lutufye : Naweza kujiandika mwenyewe au kuandikwa.
Renatus Mkude: Sina swali lingine. Re Examination imeishia hapo.
Jaji anamruhusu Shahidi.
Shahidi anatoka akiwa ameshika kipaza sauti.
Jaji Ndunguru: Unasahau maji yako hapo.
Shahidi: Hapana siyataki tena.
Jaji: Basi turudishie hiyo MIC tafadhali.
Anairudisha na kutoka nje akiwa anatikisa kichwa.
Watu wanacheka.😂😂😂
Kesi inaahirishwa watu wakale.
---
Mahakama imerejea.
Majaji wameingia muda huu saa tisa.
Mhe. Tundu Lissu yupo.
Cha ajabu Mawakili wa Serikali hawapo. Mh. Lissu ameuliza Jamhuri imekimbia.
Watu wanacheka.😂😂😂
Hakuna kinachoendelea muda huu.
Sasa wanaingia baada ya kuwaweka Majaji dakika kama 20 hivi.
Anasimama Renatus Mkude anasema Waheshimiwa Majaji tunaomba radhi kwa kuchelewa kwa niaba ya wenzangu naomba mtusamehe.
Tunae shahidi mwingine tunaomba kuendelea.
Majaji wanaandika kidogo
Shahidi anayefuata ni P4 na ataongozwa na Wakili Winiwa Kasawa.
Huyu ni Shahidi anayelindwa sasa Winiwa anajiandaa kuja kumuhoji P4 ambae ni Shahidi wa 10 wa Jamhuri.
Jaji anamuuliza una miaka mingapi?
Shahidi wa kificho P4: 29
Jaji: Dini yako?
Shahidi wa kificho P4 : Mkristo.
Jaji: Haya muapisheni.
Anaapishwa hapa P4
Wakili: Wewe ni mkazi wa wapi?
Shahidi wa kificho P4 : Arusha.
Wakili: unajishughulisha na nini:
Shahidi wa kificho P4 : Dereva Bajaji.
Wakili: Unafanyia wapi hizo bajaji?
Shahidi wa kificho P4 : Kwa Mrombo.
Wakili: Unakumbuka nini tarehe 03/04/2025
Shahidi wa kificho P4 : Nakumbuka tarehe hiyo majira ya saa sita mchana nikiwa natoka nyumbani nilifika mahali nikasimama mahali kusubiri wateja.
Nikawa naperuzi kwenye simu yangu nikaingia kwenye mtandao wa Youtube. Nikakutana na habari za Mwenyekiti wa Chadema. Anaitwa Tundu Lissu
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho P4 : Akawa anaelezea kuwa amejipanga kuzuia uchaguzi.
Wakili: Kingine nini uliona?
Shahidi wa kificho P4 : Alisema watakinukisha maana hawana imani na Uchaguzi. Kwani hata Majaji ni vibaraka wa CCM.
Wakili: ikawaje?
Shahidi wa kificho P4 : Alisema hawana imani na tume ya Uchaguzi kwani imevuruga uchaguzi mdogo wa 2024 kwahiyo hawana imani na tume.
Wakili: Nini kingine?
Shahidi wa kificho P4 : Hata Polisi wanashiriki kuiba kura.
Wakili: Ikawaje sasa?
Shahidi wa kificho P4: Maneno yale yalini convice kusapoti alichokuwa anakisema.
Wakili: Nini kingine kiliendelea?
Shahidi wa kificho P4 : Abiria wangu walifika niliwapeleka kwa Mrombo na baadae kijiweni.
Wakili: Nini kilikuwa kimeku convice?
Shahidi: Maneno ya kwamba tutafanya uasi, tutakinukisha na hivyo vyombo vyote kuwa hawezi kuviamini.
Wakili: Yalikushawishi nini?
Shahidi wa kificho P4 : Hali ya maisha ni ngumu sana ndio maana nikashawishika.
Wakili: Kingine je?
Shahidi wa kificho P4 : Nikarudi kwa Mrombo pale maana nilikuwa nimeshawapeleka wateja wangu.
Wakili: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P4 : Walikuwa wanasimuliana pale kijiweni kuhusu Mwenyekiti wa Chadema alivyokuwa anazungumza pale kijiwe cha Bajaji.
Wakili: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho P4 : Watu wengi walikuwa wanaunga mkono wanasema bora kinuke ili unafuu wa maisha upatikane.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Wana kasi wawe taratibu.
Wakili: Nilikuuliza akina nani hao?
Shahidi wa kificho P4 : madereva bajaji wenzangu na mwenye kiduka pembeni.
Wakili: ikawaje?
Shahidi wa kificho P4 : Nilishangaa Polisi wametuvamia na kila mtu akakimbia ila nikakamatwa Mimi na Mwenzangu ambae ni P7. Tukapelekwa kituo cha Murieti na Baadae Central Mjini.
Wakili: Ikawaje?
Shahidi wa kificho P4 : Tukaambiwa pale Polisi kuwa tunazuia Uchaguzi. Tukawekwa ndani.
Wakili: Nini kilifuata?
Shahidi wa kificho P4 : Tuliandikwa maelezo tukawekwa ndani.
Wakili: Ikawaje tena?
Shahidi wa kificho P4 : Wakaja mdogo wangu na Dada angu kuniwekea dhamana.
Wakili: Walijuaje?
Shahidi wa kificho P4 : Tulikamatwa watu wakiwa wanatuona. Walituwekea dhamana na Polisi walitupa utaratibu wa kwenda kuripoti kila siku.
Wakili wa Serikali anaendelea kumuongoza shahidi wa kificho P4
Wakili: Nini kingine?
Shahidi wa kificho P4 : Tulivyoenda kuripoti Tarehe 17/04 tuliambiwa tusubiri tuandikwe maelezo, nikaandikwa hayo maelezo.
Wakili: Unamfahamuje huyo Tundu Lissu?
Shahidi wa kificho P4 : Namtambua kama Mwanasiasa Mkubwa kwenye hii Nchi.
Wakili wa Serikali Winiwa Kasawa anasema Waheshimiwa Majaji ni hayo tu.
Jaji Ndunguru: Maswali ya Dodoso Karibu Mshitakiwa.
Mhe. Lissu: Sasa shahidi jibu maswali kama hujui sema hujui sema najua kama unajua na kama umesahau sema nimesahau.
Mhe. Lissu: Umesema unakaa Arusha?
Shahidi wa kificho P4 : Kweli
Mhe. Lissu: Wambie Majaji umekuja Dar es salaam lini?
Shahidi wa kificho P4 : Leo nina siku ya pili.
Mhe. Lissu: kwahiyo umekuja Jumapili ya juzi?
Shahidi wa kificho P4: Ndio.
Mhe. Lissu: Nani alikwambia uje Dar es salaam
Shahidi wa kificho P4 : Hiyo nashindwa kusema hapa.
Mhe. Lissu: Utasema tu. Mimi sikuoni na watu hawakuoni. Wambie majaji ndio wanaokuona pekee kuwa nani alikwambia uje Dar es salaam
Shahidi wa kificho P4 : Nilipigiwa simu.
Mhe. Lissu: Na nani alikupigia simu.
Shahidi wa kificho P4 : Mtu alijitambulisha kuwa ni Wakili wa Serikali.
Mhe. Lissu: Alikwambia jina lake?
Shahidi wa kificho P4 : Ninazo sababu binafsi
Mhe. Lissu: Kwahiyo majaji waandike kuwa umekataa kusema sababu kwanini hutaki kumtaja aliyekuita Dar es salaam sawa muraaaaa
Shahidi wa kificho P4 : Ndio.
Mhe. Lissu: wapo wakurya wenzako humu.
Mhe. Lissu: Ieleze Mahakama kama ulipata summons ya Mahakama?
Shahidi wa kificho P4 : nilipigiwa simu nikaenda kituoni nilipata barua ya Mahakama.
Mhe. Lissu: Nani aliyekulipia nauli ya kutoka Arusha Kuja Dar es salaam?
Shahidi wa kificho P4 : Nilikuja na nauli nililipa mwenyewe maana nilikuja kwenye shughuli nyingine binafsi.
Mhe. Lissu: Una nyumba hapa?
Shahidi wa kificho P4 : Sina.
Mhe. Lissu: Nani anayelipa gharama za kula na kila kitu?
Shahidi wa kificho P4 : Leo nimekuja na gari ya wanasheria
Mhe. Lissu: Tarehe 03/04/2025 ulipelekwa kituo cha Polisi mjini na kabla ulikuwa kituo cha Muriet
Shahidi wa kificho P4 : Ndio
Mhe, Lissu: Hayo maelezo yalikiwa yanahusu kosa gani?
Shahidi wa kificho P4 : Walisema tuna kesi ya kutaka kuzuia Uchaguzi.
Mhe. Lissu: Umewahi kupelekwa Arusha kwa hilo kosa ulilokamatwa nalo?
Shahidi wa kificho P4: Sikuwahi kupelekwa Mahakamani.
Mhe. Lissu: Hiyo kesi iliishia wapi?
Shahidi wa kificho P4 : Mimi sijui.
Mhe. Lissu: Hayo maelezo ya Tarehe 03/04 yako wapi?
Shahidi wa kificho P4 : Sijui.
Mhe. Lissu: Nilikwambia kwamba ulikamatwa bure tu hukuwa na kosa lolote we utasemaje?
Shahidi wa kificho P4 : Sijui mimi.
Mhe. Lissu: Siku hiyo ya Tarehe 03/04 wewe na wenzako mlikuwa mnazungumza juu ya maneno mlioyaona kwenye mtandao na wengi mliyaunga mkono
Shahidi wa kificho P4 : Ndio.
Mhe. Lissu: Je, hilo lilikuwa kosa nyie kuunga mkono na kuzungumza kauli hizo.
Shahidi wa kificho P4 : Sijui
Mhe. Lissu: Maelezo yako ya 17/04 ukioneshwa unaweza kuyatambua?
Shahidi wa kificho P4 : Naweza
Shahidi wa kificho P4 ameyatambua maelezo yake na Mh. Lissu anamsomea Maelezo ambayo shahidi aliyaandika pale Polisi.
Mhe. Lissu: Niliyosoma hapa ni sawa na maelezo uliyonayo hapo.
Shahidi wa kificho P4 : Ndio
Mhe. Lissu: Sasa shahidi nataka kukuhoji kuhusu hayo maelezo.
Shahidi wa kificho P4 : Sawa.
Mhe. Lissu: Maeneo hayo ni
1. Uliperuzi kwa simu yako
2. Nilisema tutakinukisha
Anamtajia maeneo kama 8 hivi ambayo atamuuliza maswali.
Mhe. Lissu: Je ungependa yawe sehemu ya ushahidi?
Shahidi wa kificho P4 : ndio.
Jaji: Jamhuri mnasemaje?
Wakili Renatus: Sina pingamizi.
Jaji: Hiyo itakuwa ni D9 upande wa utetezi.
Mhe. Lissu anaendelea na kumfanyia cross examination Shahidi wa kificho P4
Mhe. Lissu: Ulisema ulikuwa unaperuzi kwa simu yako majira ya Mchana, waeleze kwenye hayo maelezo, maneno hayo yapo?
Shahidi wa kificho P4: yuko kimya.
Shahidi wa kificho P4: anajibu sasa: Haipo.
Mhe. Lissu: Pia leo umesema wakati ninahutubia mkutano nilisema tutakinukisha. Onyesha hayo nayo yapo wapi kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P4 : Hayapo kabisa.
Mhe. Lissu: umesema kuwa nitafanya fujo kuzuia uchaguzi, hayo maneno umeyasema au hujasema?
Shahidi wa kificho P4 : nimesema na hayapo kwenye maelezo yangu.
Mhe. Lissu: Unasema mlihojiwa halafu mkawekwa ndani tuoneshe kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P4 : Hapa hayapo.
Mhe. Lissu: Tarehe 04/04/2025 ulisema walikuja Dada yako na mdogo wako. Hayo nayo yapo kwenye maelezo?
Shahidi wa kificho P4 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Siku hiyo wakati unahojiwa na Polisi hawakukuuliza kama unamfahamu Tundu Lissu?
Shahidi wa kificho P4 : Niliwaambia namfahamu ni mwanasiasa mkubwa.
Lissu : Sasa tuoneshe ni wapi umeyaandika kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P4 : hayapo.
Lissu: Je ulitumia Computer?
Shahidi: Siwezi kumiliki computer nilitumia simu
Lissu: Wengi wenu mlikuwa mnaunga mkono bora kinuke. Je kusema hivyo ni kosa la jinai?
Shahidi: Mimi sio msimamizi wa sheria siwezi kujua.
Lissu: Kuhamasika na maneno kwamba Uchaguzi unaibiwa na wagombea wa Chadema wanafutwa ni kosa la jinai?
Shahidi: Sijui.
Lissu: Majaji ni vibaraka wa CCM ni kosa la jinai?
Shahidi: Sijui
Lissu: Na polisi kuwa ni wezi wa kura wanashiriki kuiba uchaguzi nalo ni kosa?
Shahidi: Sijui
Lissu: Umesema sana maneno kukinukisha. Je unajua maana ya neno kunuka?
Shahidi: Kitu kinachotoa harufu mbaya.
Lissu: unajua maana ya neno kunukia?
Shahidi: Kutoa harufu nzuri.
Lissu: Mtu akisema atakinukisha anaweza kuwa anaamisha atafanya harufu iwe mbaya?
Shahidi: Inategemea na maana ipi?
Lissu: Na kunikia vizuri pia inaweza kuwa ni kukinukisha.
Shahidi: hiyo ni lugha ya mtaani.
Lissu: Mtaa upi? Mimi mtaani kwangu hakuna hiyo lugha.
Shahidi: Tunakoishi hayo maneno tunayasikia.
Lissu: Unajua kwenye uchaguzi wa mitaa wa 2024 CCM ilishinda asilimia 100 na wapinzani walifutwa wote?
Shahidi: Ndio CCM ilishinda.
Lissu: Wagombea wa Chadema walifanywa nini?
Shahidi: Hawakuwepo kwenye uchaguzi
Lissu: Ninaposema wasimamizi wa uchaguzi wanafanya mambo ya ovyo ninaposema tuwaondoe nakosea hapa
Shahidi: Sijui
Mhe. Lissu: Unajua Tume ya Uchaguzi ilisema wagombea wa Chadema hawaruhusiwi kugombea uchaguzi wa mwaka jana na wa miaka mingine mitano
Shahidi: Sijui
Lissu: Je, umewahi kuwasiliana na Polisi tena baada ya kuandika maelezo.
Shahidi: Juzi Tarehe 15 waliniita Polisi.
Mhe. Lissu: Kwahiyo waliokwambia kuna wito wa Mahakama ni Polisi?
Shahidi wa kificho P4 : Ndio.
Mhe. Lissu: Kwahiyo kuanzia tarehe 17/04 hadi hiyo juzi hukuwahi wasiliana na Polisi?
Shahidi wa kificho P4 : Sikuwasiliana nao.
Mhe. Lissu: Je ulitishiwa na mtu yeyote?
Shahidi wa kificho: hapana
Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kwanini umejificha kwenye hizo mbao?
Shahidi wa kificho : Nahofia maisha yangu.
Mhe. Lissu: Nani aliyekufundisha hayo maneno wakati umesema hakuna aliyekutisha?
Shahidi wa kificho : Sijasema kama nimefundishwa.
Mhe. Lissu: Unajua polisi wamekuja mahakamani na kuomba amri ufichwe kuwa unatishiwa?
Shahidi wa kificho: Sijui.
Mhe. Lissu: Video uliyoiona Youtube umeiwasilisha Mahakamani
Shahidi wa kificho : Hapana.
Mhe. Lissu: Je umesema kokote hiyo video uliangalia kupitia wapi?
Shahidi wa kificho : Habari24 ndio niliangalia.
Mhe. Lissu: Umeweka hayo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho : Hapana.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji nimemaliza kwa Shahidi huyu.
Jaji Ndunguru anawaita upande wa Serikali kwa ajili ya Re-Examination
Wakili wa Serikali anasema hawatakuwa na maswali.
Jaji Ndunguru : Shahidi sasa uende tumemalizana.
Shahidi anasepa.
Renatus Mkude: Tunae shahidi P7 tunaomba yeye aendeleee kesho asubuhi.
Majaji wanaandika kidogo pale juu.
Kesi inaahirishwa hadi kesho asubuhi maana muda umeisha inakaribia saa 11 jioni.
So tutaendelea kesho, Mungu akitujalia uzima.
Soma Pia:

- Shahidi wa Kesi ya Lissu (P7): Nauli ya kuja mahakamani leo nimepewa na mwanamke wangu. Ndiye ananiweka mjini
- Kesi ya Tundu Lissu kuendelea leo Februari 17, 2026, mashahidi wa Jamhuri wasiopungua watatu wangojewa
- Kesi ya uhaini dhidi ya Lissu: Shahidi wa saba kati ya 30 wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi
- Kesi ya Lissu | Shahidi wa Siri (P6): Lissu alisema tunakwenda kuvuruga uchaguzi na kukinukisha
- Kesi ya Lissu: Hiki ndicho Kizimba cha mashahidi wa kificho, kilichosababisha Kesi kuahirishwa
- Baada ya takribani miezi mitatu, kesi ya Tundu Lissu kuendelea leo Februari 9, 2026
- Kesi ya Lissu: Mahakama yaagiza Kizimba cha Mashahidi wa siri kirekebishwe Majaji wawaone. Kesi kuendelea Feb 12, 2026
- Kesi ya uhaini ya Lissu, mahakama kutoa uamuzi wa mapingamizi leo Feb 11, 2026
- Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu kuendelea Februari 9 hadi Machi 6, 2026
- Shahidi wa kesi ya Lissu (P7) anasema alikamatwa mara tu baada ya kuangalia video ya Lissu iliyokuwa Jambo TV
- Kesi ya Lissu | Shahidi wa siri (P5): Niliona video ya Lissu akisema atakinukisha, uchaguzi mkuu hautafanyika
- Mama wa CHADEMA azimia mahakamani baada ya Lissu kudai kunyimwa chakula
- Mahakama kuu, Kanda ya Dar es salaam Tarehe 11 Februari, 2026 kutoa uamuzi mdogo katika kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu