Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Hakuna cha utawala bora wala ushuzi......Waziri Simba alitakiwa kuonyesha mfano. Kama alijua kuwa Malecela kalamba m200 kutoka kwa fisadi, walishindwa nini kufanya uchunguzi tokea mwanzo...badala yake wanakuja na DOUBLE POSHO kwa wabunge.

This time mtasema yote, nafikiri ni wakati muafaka muanze kuungama.
 
Matusi mengine haya jamaa mmh haya.

By the way Da Sophy sio mndengestan ni mluguru! au na waluguru nao hawako serious pia?

Huyu ni mchanganyiko wa mluguru na mzaramo, hata hivyo kabila😕 linakujaje kwenye issue ya Ufisadi?
 
Who is Sofia Simba anyway? And why is she defending the rotten ones in CCM?
What it shows is that all apples in the CCM cart are rotten to the core. Yeyote anayesema kuwa Chenge alishasafishwa anahitaji kupelekwa Mirembe.
 
Mi nadhani wanatumia Mndegestan kwa sababu ya kuushonga kumbe kweli wnaa maana ya kudharau kabila hilo...Duh! haya makubwa tena wakati wa Mkapa watu walisema nchi imeongozwa na Machinga!..Kaazi kweli kweli!
 
Waache waubuane na kutajana wenyewe kwa wenyewe kwanza ndipo mambo mengi yata toka kigazi.
 
sidhani kama ntakuwa nimekosea nikisema hii nchi imepoteza muelekeo..sawa watu watamlaumu mama Sofia Simba ,but at least amebwatuka na kumbe tumejua leo kuwa Mzee malecela alichukuwa 200m kwa Jeatu Patel...hahaaa na harusi yake ilikuwa funded na Jeatu..these are very good news to me..na ule usemi wa mama Anna Kilango kuwa patachimbika bungeni ndo tunangoja pachimbike katika kujibu haya
Huyo mama Simba hana lolote nani msafii mtu anaemkemea rafiki yake baada ya kugundua ya kua ni mwizi au fisadi au yule anaendelea kukaa kimya na kumuacha rafiki yake aendeleze ufisadi kwa vile alimfadhili?!!!!!! Ama kweli CCM hawana la kufanya SIKIO LA KUFA ALISIKII DAWA.MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
vita vya panzi furaha kwa kunguru. acha waendelee kuanika uozo wao, wanazidi kutufumbua macho
 
Wote wachafu...ingawa wanatofautiana kwa wingi wa uchafu walio nao, kundi la mama Simba na wenzake wao wanatetea uchafu kwa nguvu zote, kundi la kina mama Kilango wanauma na kupulizia na ni ndumilakuwili....lakini kwa ujumla wote wachafu....WIZI MTUPU.

😀..........wacha mie nipalilie kiunga changu cha minazi....😀

Sofia anajua anachokifanya, kumbuka sofia kikwete,lowasa na rostam ni kundi moja hilo.
Sofia ni opportunists,njia zake za kusurvive huwa ni kujipendekeza,Sofia kama unasoma huu ujumbe hukumbuki kwamba ni wewe ulikuwa tayari kuhonga ngono kwa mzee Malechela wakati ni waziri mkuu ili upate madaraka,Rafiki yako wa karibu sana akakukemea kwamba huyo ni sawa na baba yako(wengine hili hamwezi kulijua).
Nadhani ni wakati mwafaka wa kuanza kuwaweka wazi hawa wanaotuona watanzania ni mabwege.
 
mwanakijiji... Huyu mama si ndie uliyemfagilia kipindi akitwaa uchaiewomeni wa uwt, na ukasahau kabisa kama alishawatetea akina mkapa na wenzake? Kulikoni


kibunango kwenye signature yangu mkandara kashakuelezea kila kitu isome tafadahali then tafakari.
 
Lakini kama waziri wa utawala bora anadiriki kuhalalisha rushwa? Kwamba kwa kuwa kina malecela walifadhiliwa na fisadi basi wakae kimya wakiona wengine wanajihusisha na ufisadi. huu ndio utawala bora kweli?

niliposema ajiuzulu watu bado hawajaelewa kwa nini.
 
Kila kukicha naombea kikao hiki cha CCM kiendelee vyema.. NAOMBEA HATIMA YAKE IWE ni Kuvunjika kwa CCM....... Na vitokee vyama vi2 vyenye nguvu sawa... Natamani chama kimojawapo kiitwe Chama Cha Mafisadi na Kingine kiitwe Chama Cha Wazalendo....... Mungu yupo na watanzania.
 
sidhani kama ntakuwa nimekosea nikisema hii nchi imepoteza muelekeo..
Nchi haijapoteza mwelekeo, iliyopoteza ni CCM na kwa kweli ilpoteza mwelekeo siku nyingi, ila sasa ndipo mambo yanaanikwa hadharani.
 
Hilo la harusi niliwahi kusikia kwamba ilifadhiliwa na wafanyabiashara ingawaje sikumbuki ni wapi nilisikia. Wakati huo niliamini ni majungu tu.

Vita vya ufisadi lazima vianzie nyumbani kwetu, kwa kila mtu kujisafisha yeye kwanza kabla hata ya kumgusa mwingine.

Kuna baadhi ya hao wanaojiita wapiganaji wa ufisadi, huwezi kuwaachia hata mbuzi wako wakutunzie, watamla.

Watanzania tunadanganya sana kwa hizi ngojera za kisiasa huku matendo yetu ni mabaya mno.

Njia pekee ya kupigana na ufisadi ni kwa bunge kutunga sheria ambazo haziangalii sura ya mkosaji. Sheria zenye msumeno na kwa ajili ya kila mtu, kuanzia muuza nyanya mtaani mpaka rais wa nchi.

Pia vyombo kama PCCB, mahakama na police viwe huru bila kuingiliwa na wanasiasa. Kazi ya wanasiasa iwe kutunga sheria safi za kuvisaidia vyombo vya ulinzi na usalama kutimiza majukumu yao.

Kwa mwendo wa sasa, sahau kuhusu vita vya ufisadi na hata viendelee miaka 100, hakuna ushindi.

Poti

Wewe mwenyewe una tuhuma

1. Kupewa milioni 400 na mafisadi
2. Kuiba mtihani SUA na kukamatwa ukisoma majibu uliyoandika ******
3. Kutoroka kesi uliyofunguliwa na SUA ukitumia landcruiser ya dada mmoja jina namwihifadhi.
4. Kuidanganya Serikali ya poland kwa kutosema ukweli kuhusu history yako

Kabla ya kuanza kumshabikia Sophia Simba jibu kwanza tuhuma zako. By the way faili lako la Sua limeshapatikana.

Ona utakavyokuja kwa jazba wakati umeyaanzisha mwenyewe!
 
Huyu mama nae ni mnafiki kama alichukua hizo 200m kwa nini asimshughulikie pale pale ukizingatia ndie anae shughulika na Utawala bora sasa kwa nini anaficha maovu ya watu basi nae ana maovu yake makubwa zaidi ha hili la 200m.
 
Poti

Wewe mwenyewe una tuhuma

1. Kupewa milioni 400 na mafisadi
2. Kuiba mtihani SUA na kukamatwa ukisoma majibu uliyoandika ******
3. Kutoroka kesi uliyofunguliwa na SUA ukitumia landcruiser ya dada mmoja jina namwihifadhi.
4. Kuidanganya Serikali ya poland kwa kutosema ukweli kuhusu history yako

Kabla ya kuanza kumshabikia Sophia Simba jibu kwanza tuhuma zako. By the way fail lako la Sua limeshapatikana.

Ona utakavyokuja kwa jazba wakati umeyaanzisha mwenyewe!

Hahahahaha dah hii tunaita uswazi Titi fo tati unakong'oli nawe wanakukong'oli hehehe kwa Mtanzania nae ana shutuma juu ya shutuma kha! kweli usikimbilie kutoa bolt kwa mwenzako toa kwanza yako hahaha
 
- Wewe na Sophia simba mngekwua na ushahidi ndio ingependeza, maana mimi ninao wa majina ya wote waliochangia ile harusi, aliyechangia nyingi ni Mzee Mengi tu, na hazikufika hizo amount na besides Mzee hana uhusiano wa karibu na Jeetu, lakini anao uhusiano wa karibu sana na Shabibu ambaye ni mkazi wa Dodoma na ndiye mmiliki wa New Africa Hotel ya Dar, sasa huyu ni fisadi then ni kweli hizo ngonjera.

- Halafu kwa nini unahnagika na kujaza thread na ma-ID kibao, si utumie moja tu useme unachotaka ksuema maana nimekuona muda sasa ukihangaika, wewe is mtumzima mke na na watoto mbona unakuwa tena kama Auntie Sophia! Ha! ha! ha! ha! Nilijua mkuu it won't take long kabla hujaonyesha rangi yako ya kweli, lakini muhimu ni ushahidi ambao Sophia hana!

Ahsante



Hivi Bill unaweza kutuambia zile hela walizompora majambazi Mama Killango wakati ule wanajiandaa kwa kampeni alizitoa wapi?
 
FM.. siyo kuhusu kile alichosema ni kuhusu kile asichosema vile vile. Huwezi kusimamia utawala bora kwa kuufafanua ufisadi wa kundi moja kwa kuelezea ufisadi wa kundi jingine. Kwa hiyo, tuhuma alizotoa nyingine zinahusu uhalifu wa viongozi wenzake na madai ya mambo kadha ambayo yanapakana na uhalifu. Badala ya kuwaambia kuwa sheria itawafuatia mkondo yeye anaapa kuwa hata hawa wengine nao watasafishwa tu kwa sababu wote ni wachafu. Waziri wa Utawala bora anayetetea ufisadi kwa kuonesha ufisadi mwingine siyo tu hafai anatufanya tujiulize huyo aliyemteua na chama chake wana lengo gani na Watanzania?

do we have any principles au kila kitu kinaangaliwa in terms of nani anaathirika au anafaidika?

MKJJ,

I believe only few understand, ukiona mke analipizia kwa yale mabaya alofanya mume hapo hakuna familia tena.

I would say Tanzania tulioizoea haipo tena,
 
Hivi Bill unaweza kutuambia zile hela walizompora majambazi Mama Killango wakati ule wanajiandaa kwa kampeni alizitoa wapi?
Sasa wewe umegusa pabaya mkuuu, acha kabisa kaka. hapo pabayaa mkuu.
 
kwa sasa Tanzania hamna lolote, program za maendeleo hakuna service delivery hakuna, watu wanazidi kuwa masikini...na kila siku ni mambo hayahaya..CCM bana Mnakera sana.
 
Back
Top Bottom