Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sophia Simba anatekeleza matakwa ya mteuajii....

hana chakupotezaa..wanamwihitaji sana kwa michezo yao ya kufikia ushindii..
Kama kweli anatetea matakwa ya mteuaji, tumekwisha.
 
- Ninamfahamu sana huyu waziri tena kwa karibu sana, na kwa yoyote anayemfahamu vizuri anajua kwamba haya ni maneno yake binafsi kwa sababu ndio kawaida yake kuzungumza maneno low na out of sense.

William.
Ndio maana nikasema tangu jana,utampaje Wizara Nyeti kama hiyo mtu muhudhuriaji mzuri wa Travertien Hotel kwenye mipasho ya akina Yusuph Mzee! No wonder ipo siku atawanyooshea vidole juu mpaka Bungeni akidhani yupo Tandale kwa mtogole!
 
Kila kukicha naombea kikao hiki cha CCM kiendelee vyema.. NAOMBEA HATIMA YAKE IWE ni Kuvunjika kwa CCM....... Na vitokee vyama vi2 vyenye nguvu sawa... Natamani chama kimojawapo kiitwe Chama Cha Mafisadi na Kingine kiitwe Chama Cha Wazalendo....... Mungu yupo na watanzania.
Naungana na wewe mkuu. Tena acha watukanwe sana maana kama kweli unachukia ufisadi hauwezi kukaa ndani ya CCM. Ona sasa wanakumbushiana viporo vya miaka hiyoooo. Tokeni mkapambane kivyenuuu.
 
Naona kinachotokea hapa Tanzania kinatia kichefu chefu na kutudhalilisha Watanzania wote kana kwamba wote tuna vichwa vya kuku! Very sad in deed😕
DC,vichwa vya kuku vina afadhali,tungekuwa tunaruka mara moja tukishitukia deal,mimi nadhani tunadhalilishwa kama vile tuna Vichwa vya Kondoo! Kila kitu kwetu ni hewala Bwana.
 
Hivi Bill unaweza kutuambia zile hela walizompora majambazi Mama Killango wakati ule wanajiandaa kwa kampeni alizitoa wapi?

- Zile Shillingi Laki mbili walizompora na masanduku yake ya biashara toka US, au una maana zingine?

- It is about time sasa ukajibu swali la msingi Baba yako mdogo Mboma alikupa hela ngapi za Kiwira kumsomeshea mtoto wake uliyekuwa unaishi naye? kuwa mkweli ndugu yangu!

BILL COOL DOWN YOUR TEMPER MZEE, PARA ONE ILITOSHA KWA MAJIBU YA HUYO NDG MBOMA Jr.
 
Sasa wewe umegusa pabaya mkuuu, acha kabisa kaka. hapo pabayaa mkuu.

Unajua Semenya wakati mwingine unashangaa watu wanapoamua kuwatetea watu ambao wanatia shaka. CCM ni mafisadi na wananchi wengi wanalalamika tatizo labda hawajapata mbadala. Hili kundi la wanaojiita wapiganaji waliichukua issue ya ufisadi ambayo CHADEMA walikuwa wanapigana nayo vizuri ili kupunguza nguvu za Chadema. Sasa wamejikuta wanapambana wao kwa wao. Kama wangekuwa wasafi si wangehamia CHADEMA ili waendeleze mapambano? (ushauri wangu kwa CHADEMA endeleeni kuwasha moto hata hawa wanaojiita wapambanaji kama wana uchafu wao usemeni).

Kuna issue kibao za ufisadi hawaziongelei wao wanafanya selective fighting. Posho mbili wamezitetea, kuna issue ya NICOL watu wameliwa wao wamenyuti. Lakini kila siku tunasumbuliwa na mpambano wa RA na EL vs Six na Mengi. Inakera na inaudhi sana. Kama mtu anataka kupambana na ufisadi apambane lakini kama anataka kufanya unafiki lazima tumnyamazishe milele.
 
- Zile Shillingi Laki mbili walizompora na masanduku yake ya biashara toka US, au una maana zingine?

- It is about time sasa ukajibu swali la msingi Baba yako mdogo Mboma alikupa hela ngapi za Kiwira kumsomeshea mtoto wake uliyekuwa unaishi naye? kuwa mkweli ndugu yangu!

William.

Bill acha hasira,
Mnaweza kuwa mnajuana na Mama Sophia au Mama Sophia alishawahi kuwa rafiki wa Mama Anna Killango na hivyo mnaona kama amesaliti usuhuba wenu. Lakini hapa tunajadili matendo yao na kauli zao kama viongozi. Mimi ukiniuliza Mama Sophia namweka kundi gani kwangu ni rahisi kuwa kwa kuwa yeye ni kiongozi wa CCM na wamekuwa wakitumia pesa kushinda chaguzi nitasema ni fisadi. Na pia nitakwambia kuwa hata yeye hafichi yuko kundi gani, maana siku zote hulisemea kundi la mafisadi. Nadhani hata kwake yeye inakuwa rahisi. Tatizo ni Mama Anna Killango, wakati anataka tumwamini kuwa yeye ni msafi bali anabanwa na mafisadi historia yake na ushirika wake na watu fulani unatia mashaka. Na hapo ndipo tatizo linapkuja, kwani mtu akimnyooshea kidole tu nyie mnakuja hapa na kuanza kutukana wengine na kusema kuwa wamepewa pesa. Siyo nzuri kwa majadiliano yenye siha.

Swali langu halikuwa ni shilingi ngapi nilikuuliza alizitoa wapi? Umuhimu wa hili ni kuwa katika maelezo yako umekuwa ukionyesha kama vile unajua vyanzo vyote vya mapato vya muheshimiwa kitu ambacho nina wasiwasi nacho. Kwa mfano unaweza kusema alifadhiliwa na nani katika kupigania ubunge kule kwao (hapa nasema siyo kwa sababu ni Anna Killango ni kwa sababu najua wabunge wengi walihonga vitu vingi ili wachaguliwe-kama uko Tanzania pitia lile Tangazo la Watanzania tusidanganyike lililotolewa nadhani na TAMWA kama sikosei)
 
Hakika Mwaka huu tutashuhudia mengi na waswahili wana msemo wao "UKITAKA KUIJUA TABIA YA MTU MPE HELA" Na Wengine wanasema ilikumfahamu mtu ustarabu wake mpe kileo anapoanza kunywa akitaka kujisaidia atakwenda ******,taratibu kileo kinapochukua mkondo wake hata choo hukiona kipo mbali then atajisaidia pembeni tu nje ya choo mwisho hata kusimama ataona uvivu na kumaliza haja zake hapo hapa na ndipo tutajua tabia ya mnywaji wetu. kwa msemo huo nakubali kabisa Sasa hii ni nafasi yetu kujua Nani ni nani ,na nani yupo kwa ajili ya nani?

Kabla sijaendelea kuchangia zaidi naomba wale wanao mfahamu Sofia Simba watueleze who is Sofia Simba and where she come from i mean political isije kuwa tuna umiza vichwa humu kumbe ni type ya "NDIO MZEE TYPE".
 
Unajua Semenya wakati mwingine unashangaa watu wanapoamua kuwatetea watu ambao wanatia shaka. CCM ni mafisadi na wananchi wengi wanalalamika tatizo labda hawajapata mbadala. Hili kundi la wanaojiita wapiganaji waliichukua issue ya ufisadi ambayo CHADEMA walikuwa wanapigana nayo vizuri ili kupunguza nguvu za Chadema. Sasa wamejikuta wanapambana wao kwa wao. Kama wangekuwa wasafi si wangehamia CHADEMA ili waendeleze mapambano? (ushauri wangu kwa CHADEMA endeleeni kuwasha moto hata hawa wanaojiita wapambanaji kama wana uchafu wao usemeni).
.

Sikubaliani na wewe,

Unasema CCM wote ni mafisadi je unao ushahidi? waache wapambane humohumo unataka wakimbie chama wamwachie RA na Chenge!! jamani mwenye ushahidi wa hawa wapambanaji apeleke mahakamani ndo sisi wananchi tutamwelewa huyo Simba. Na kwanini hii yote itokee wakati huu, mara Hosea huyo Bungeni, mara Sophia hii yote ni kutapatapa.
 
K4,

Una haki ya kutokubaliana na mimi kabisa.

Nilichosema ni kwamba CCM ni mafisadi sasa kama unatafsiri kuwa hapo ina maana ni wote hicho ni kitu kingine. Lakini nikisema CCM ni mafisadi ina maana kuwa maamuzi ya CCM yamejaa agenda za kifisadi. Hao wapiganaji wakiondoka ni kwamba hawamwachii Chenge CCM bali wanakiacha chama chenye ajenda za kuifisadi nchi. Suala ni nchi siyo chama. Sasa wewe unapambana na ufisadi halafu unawasaidia viongozi wanaofisadi nchi tutakuweka kundi gani kama siyo fisadi. Kitu cha muhimu jamani ni nchi wala siyo chama.

Vyama vinaweza kufa na kuzaliwa vingine lakini nchi itakuwepo hivyo kwa watu wenye mapanzi mema lazima waiangalie nchi kwanza badala ya kuwaza eti hatuwezi kukimbia chama.
 
Mama Simba anaelekea kutumia vibaya taarifa anazozipata kutoka vyombo vya DOLA vilivyo chini ya wizara yake. Watampotosha jamaa wa UwT na TAKUKURU. Yeye ni outsider kama sisi wengine. Watamwangusha tu. Anasema NDOA takatifu ya JSM na Mama Kilango ilifadhiliwa na JEETU PATEL?!
 
Tunayoyaona sasa hivi yalishasemwa siku nyingi na Marehemu Kolimba(RIP) kuhusu CCM. Ilikuwa mapema sana kama maneno yake wangeyafanyia kazi wakati ule ndani ya chama lakini wao wakamweka kiti moto kama vile mtu aliyefanya kitendo cha kihaini. Wajumbe wa Kikao kile cha kumsulubu Kolimba KAMA WANA AKILI na MAPENZI NA CHAMA CHAO huu ndio wakati wa kujuta na kuomba radhi kwa marehemu na wanachama wa chama chao
 
Kinachosikitisha ni kwamba huyu ni Waziri wa wizara muhimu kama aliyonayo na pia ni Mwenyekiti wa Umaoja wa Wanawake wa Tanzania.

William nadhani vidole kwenye keyboard vimegema kidogo. Huyo ni mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa CCM. Sidhani kama wanawake makini wa Tanzania wanaweza kuongozwa na huyo.

By the way, usishangae sana haya yanayoendelea sasa. Ni matokeo ya ccm kutotaka kujenga mfumo huru na was usawa kwa Tanzania, ili waendelee kutawala daima. Wakati Mzee Malecela akisema kuwa katiba ni nzuri na serikali ya chama chao haioni sababu ya kuifanyia marekebisho ili itoe nafasi sawa kwa wote, alisahau kuwa akiwa pembeni anaweza kutumika tu kitendea kazi (tingatinga) kwa faida ya wale wanaotawala. Hii la Simba ni fedheha kubwa sana kwa Mzee Malecela. Ama kweli, wamemgeuza Mzee malecela MUWA; sasa juice kwishney!

Hili linatufundisha kitu kimoja kikubwa tu, kujenga mazingira ambayo yatawafaa mliopo sasa na vizazi vyenu vijavyo!
 
Mama Simba anaelekea kutumia vibaya taarifa anazozipata kutoka vyombo vya DOLA vilivyo chini ya wizara yake. Watampotosha jamaa wa UwT na TAKUKURU. Yeye ni outsider kama sisi wengine. Watamwangusha tu. Anasema NDOA takatifu ya JSM na Mama Kilango ilifadhiliwa na JEETU PATEL?!

its really un - unethical to use reports he have in pocession in her political debates....au conflicts....maana kwa mtu anayejuwa ethics huwezi kumpa idara nyeti mtu mpayukaji....pale wakekaa mawaziri kwa uchache kama mheshimiwa ..bhoke munanka,peter syovelwa,kawawa,hassy kitine,masilingi...etc..Sijapata kuona waziri asiyekuwa na maadili kama SOPHIA kukaa pale wizara ya ikulu...sisemi kuwa sophia hafai kuwa waziri lah...ILA HAFAI KUWA WAZIRI WA USALAMA[UTAWALA BORA]...kwani INTERGRITY yake is QUESTIONABLE....sasa atasimamiaje intergrity za wengine....

USALAMA WA TAIFA HAWAJAWAHI KUONEKANA MBWA KOKO KAMA KIPINDI HIKI...kwanza walitumika kufanya kampeni za UWT...CCM,PCB .walisimamia ugawaji wa rushwa huku wakizuia mshindani asitoe..na mengine mengi machafu.....MWISHO WA YOTE KIKWETE AKAMTETEA KUWA MSOMI HUYU ANAFAA KUWA KINARA WA WANAWAKE......yaani kwa maana nyingine ukimuangalia sophia unapata picha ya wanawake waliowengi.....
 
Uliyoyasema kwenye kamati ya mzee Mwinyi ni ya aibu kwa aliyekuteua na wale uliojaribu kuwatetea. Sitaki niyarudie lakini kwa heshima yote uliyobakia nayo your time is up ma'am. Thank you for your unforgetable diservice to our country. Tukiamka tusikie umejiuzulu na kuwa mfano wa utawala bora. Usisubiri uundiwe kamati.

bora waendele na mpambano wao ili tuzidi kuwajua manake wenyewe wanajuana kwa kuwa wako nyumba moja hivyo kuvuja kwa mapakacha kutatuwezesha kufaidi uhondo
 
its really un - unethical to use reports he have in pocession in her political debates....au conflicts....maana kwa mtu anayejuwa ethics huwezi kumpa idara nyeti mtu mpayukaji....pale wakekaa mawaziri kwa uchache kama mheshimiwa ..bhoke munanka,peter syovelwa,kawawa,hassy kitine,masilingi...etc..Sijapata kuona waziri asiyekuwa na maadili kama SOPHIA kukaa pale wizara ya ikulu...sisemi kuwa sophia hafai kuwa waziri lah...ILA HAFAI KUWA WAZIRI WA USALAMA[UTAWALA BORA]...kwani INTERGRITY yake is QUESTIONABLE....sasa atasimamiaje intergrity za wengine....

USALAMA WA TAIFA HAWAJAWAHI KUONEKANA MBWA KOKO KAMA KIPINDI HIKI...kwanza walitumika kufanya kampeni za UWT...CCM,PCB .walisimamia ugawaji wa rushwa huku wakizuia mshindani asitoe..na mengine mengi machafu.....MWISHO WA YOTE KIKWETE AKAMTETEA KUWA MSOMI HUYU ANAFAA KUWA KINARA WA WANAWAKE......yaani kwa maana nyingine ukimuangalia sophia unapata picha ya wanawake waliowengi.....
Maneno mazito kaka, yani mpaka nasikitika, naogopa,natetemeka...sina lakusema.
 
Ukitumegea kidogo itakuwa vizuri mkuu,nina hamu kupata walau kdogo cha hayo aliyotapika.

KUCHARURANA kwa wabunge wa CCM katika kikao kati yao na Kamati ya Mzee Ali Hassan kumezidi kutoa sura mpya zaidi baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Bi. Sophia Simba kuweka wazi msimamo wake wa kumtetea mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa kuwa 'ni mwanaume shupavu'.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kwamba si tu kwamba Bi. Simba alimtetea Bw. Lowassa pekee bali hata wabunge wengine ambao wamekuwa wakirushiwa tuhuma mbalimbali za ufisadi ndani na nje ya bunge.

“Mhe. Lowassa ni mwanaume shupavu, ni mtendaji mzuri sana, kivuli chake kinatishia watu, hana hatia yoyote, alionewa tu kisiasa. Makamba ni mchapa kazi na ameisaidia sana CCM, acheni mzee achape kazi. Pia akamtupia lawama Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kwa kuruhusu mjadala wa Richmond, EPA na mijadala kuhusu ufisadi kwamba kwa kufanya hivyo, haitakii mema serikali ya CCM kwa kuwa angeweza kuzuia.

“Ndio maana wajumbe wa NEC walitaka kuchukua kadi yake, ni busara tu za mwenyekiti zilimwokoa, chanzo chetu kilimkariri waziri huyo.

Waziri huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT), aliwananga pia Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi kuwa ni mwanachana wa CHADEMA, akiwataka wabunge wa CCM wanaonufaika na misaada yake chini ya VICOBA wamfuate CHADEMA.

Habari zaidi zilieleza kwamba, kama vile Bi. Simba alikuwa anatoa taarifa za serikali, alieleza kamati hiyo kuwa Mbunge wa Bariadi Magharibi, Bw. Andrew Chenge kuwa ni mtu safi kwa kuwa amesafishwa na Kikosi Maalumu cha Kuchunguzi Ubadhirifu cha Uingereza (SFO)na pia kwamba Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Dkt. Edward Hoseah hana hatia yoyote katika sakata la Richmond.

Kamati ya Mwinyi iliundwa na Halmashauri Kuu ya CCM kuchunguza chanzo cha mpasuko miongoni mwa wabunge na kimekuwapo mjini Dodoma tangu mwanzoni mwa wiki kwa ajili ya kazi hiyo. Wajumbe wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) na Kada wa CCM Abdulrahaman Kinana.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa walihoji kama kauli za Waziri Simba ni msimamo wa ikulu au ni mawazo yake binafsi, kwa kuwa inaaminika asingeweza kusema maneno hayo kwa uzito ule bila uhakika wa ikulu.

Habari kutoka katika kundi la wabunge vinara wa vita vya ufisadi zilieleza kwamba wameamua kukaa kimya kwanza kusubiri kundi linalodaiwa kuunga mkono ufisadi kumaliza, kisha wataoa majibu kwa njia rahisi ili kuepusha mpasuko zaidi.

“Kwa sasa hatutaki kuzungumza kitu chochote, jana tulishambuliwa sana. Tulitukanwa sana tena matusi ya nguoni, wametuunganisha hata na watu ambao si wabunge, lakini sisi kwanza tunashangaa, ila kwa sasa tusubiri kwanza sisi tunajua wananchi wataoa jibu ambao ndio waathirika zaidi na ufisadi,”alisema mmoja wa wabunge hao.

Kikao hicho leo kinaendelea kwa siku ya tatu na bado haijulikani kama kitamalizika au kitaendelea pia kesho, huku ila upande ukishikilia msimamo wake.

"komaa nayo hayo hapo aliyosema mama"wengine inabidi wapimwe akili zao"
 
Back
Top Bottom