- This is very interesting,
- Kuhusu harusi na ufadhili wake, Auntie Sophia hakusema ukweli kwa sababu harusi iliandaliwa na kamati maalum kama inavyokuwa kwenye harusi zote bongo, Mwenyekiti wa kamati alikuwa Chiligati, akishirkiana na DC wa Dodoma Mjini, ikiwa ni pamoja na wanakamati kama Kimbau na Kitwana Kondo, na kina General Gau, sasa hawa hasa Chiligati wangetakiwa kuonyesha mahesabu waliyoyatumia ili kuweka ukweli unapotakiwa, kwa sababu ninazo copies zote za matumizi ya ile harusi na pesa zilizochangwa na majina wala sio tatizo.
- Maneno ya Auntie Sophia, siyaamini hata kidogo na ni uzushi mtupu kwa sababu ni mimi ndiye niliyetoa hela zangu za mfukoni kwanza kununua suti zote mbili za bwana harusi, na pia nilitoa hela zangu za mfukoni za kulipia honeymoon yao, ama sivyo hata honeymoon isingekuwepo, na kama kawaida yangu huwa ninatunza risiti ya kila kitu ninachofanya duniani, kwa hiyo ninasema kwamba Auntie Sophia, ana kazi kubwa sana kuthibitisha madai yake akiwa waziri wa Usalama wa taifa, kwa sababu ninazo risiti nyingi sana za hela zangu nilizotumia on the harusi, sasa kama kweli harusi ilifadhiliwa na fisadi, mimi na ndugu zangu hatukuwa na sababu ya kutoa hela nyingi sana tulizotumia kwenye ile harusi.
- Ya kugombea urais, hivi Mzee si alikuwa na hela za Iran, zilizobaki toka mwaka 1995. Halafu Auntie Sophia hapa tena anakuwa sio mkweli wala anayejali sheria, kwa sababu kampeni za urais wagombea wote walipokea hela toka kwa watu na sekta mbali mbali na haikuwa uvunjaji wa sheria za jamhuri, na ukweli niujuao ni kwamba kampeni ya mzee ilifadhiliwa na Shabibu, na kampeni ilikuwa na hela ndogo sana ndio maana haikufanikiwa, unless Shabibu ni fisadi then kweli mzee alichukua hela chafu, na kama ilivyokuwa kampeni ya Rais wa sasa ambako Auntie Sophia alikuwa mshiriki sasa angelinganisha hela zilizotumiwa na kambi zote na walikozitoa hela zao ndio ingependeza, lakini si kweli kabisa kwamba Patel ndiye aliyefadhili ile kampeni,
Ahsanteni.
William.