Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Mzee Mwanakijiji, Sofia Simba ni mchafu, hilo unalijua, Mama Kahama alimwaga chozi kwa ajili ya matusi yake, ni wewe uliyembeba kwenye podcast yako, leo ndio umelijua hili?.
On the other side, amini nawaambieni, Lowassa is not that bad na wapiganaji are not that clean, nao wanaufisadi wao na agenda zao.

Mwanakijiji hana anticedent basis katika uchambuzi wake, hukurupuka, na hujagundua kuwa kakurupua after all odds. Naye ni mchemshaji, usiamini kila analosisema.

Ni hayo, nitakachosema, nimesema.
 
kweli huyu mama ni muimba mipasho,lakini tusubiri mpiganaji Killango atakavyokuja nadhani patakuwa apatoshi.
 
Leo Mzee Mengi kakutana na waandishi wa habari (dakika chache zilizopita) na hiki ndicho alichoongea:

TAARIFA YA MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LTD. BW. REGINALD A. MENGI KWA VYOMBO VYA HABARI
6 NOVEMBA, 2009


_____________________________________________


Ndugu Waandishi wa habari,

Nimewaita hapa leo kuzungumza nanyi kwa lengo la kuweka rekodi sawa.

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikituhumiwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba mimi si Mwanachama wa Chama hicho na kwamba sitoi misaada ya hali na mali kwa Chama Cha Mapinduzi.

Ndugu Wanahabari,

Kwa msemo wa kiingereza “Don’t argue with a fool because people may not know the difference between you and the fool”, wenye maana kwamba usibishane na mjinga kwa sababu watu wanaweza kushindwa kufahamu tofauti yako na huyo mjinga!

Hata hivyo wakati mwingine inakulazimu kujibu hoja unapomwona mtu anapotosha mambo kwa makusudi.

Kwanza, kuhusu kuropoka kwamba sitoi misaada kwa CCM, hilo ni jambo linalozushwa na watu binafsi na kwa malengo binafsi. Viongozi wakuu wa CCM ambao ni waadilifu na wanaosimamia ukweli wanajua undani wa jambo hili.

Pili, kuhusu uwanachama wangu wa CCM:

Napenda kuwaambia kwamba mimi ni Mwanachama wa CCM tangu tarehe 18 Aprili,1977 na kadi yangu ni Na. B124595, iliyotolewa na Tawi la Kisutu, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.

Hivyo basi madai yote kwamba mimi si mwanachama au nilijiunga na chama hivi majuzi kama inavyoelezwa na Mheshimiwa Waziri wa Utawala Bora Sophia Simba, Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Shaaban Kilumbe Ng’enda na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa DSM John Guninita ni uongo, uzushi na umbea wenye lengo la kudhoofisha juhudi za viongozi wa juu wa CCM na baadhi ya wanachama za kupiga ufisadi vita.

Mimi na wenzangu wengine tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba chama chetu kinaongozwa katika misingi yake ya asili ya kupiga vita rushwa na maovu mengine.

Ndugu Wanahabari,

Hawa wanaodai kuwa ndani ya CCM hakuna kiongozi msafi ni wazi kwamba wamedandia chama hiki hivi majuzi. Ningetoa ushauri kuwa waondoke na watuachie chama chetu kwa kuwa hawafahamu msingi imara wa CCM.

Mwisho napenda kumshauri Waziri Sophia Simba kwamba katika vita dhidi ya ufisadi ni vyema akanyamaza. Kwa sababu yeye si mwadilifu na hivyo hawezi kusimama kupinga vita ya ufisadi.

Aidha, ningemshauri kabla hajazungumza aombe ushauri kutoka taasisi za serikali kama vile usalama wa taifa badala ya kuropoka na kupotosha ukweli wa mambo.

Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.


Reginald A. Mengi

MWENYEKITI MTENDAJI, IPP LTD.

 
Hii ndiyo press conference nzuri kulizo zote nilizowahikuzisoma za Reginald Mengi. Short & Clear.
 
Aidha, ningemshauri kabla hajazungumza aombe ushauri kutoka taasisi za serikali kama vile usalama wa taifa badala ya kuropoka na kupotosha ukweli wa mambo.

Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.


Reginald A. Mengi

MWENYEKITI MTENDAJI, IPP LTD.

Hahaha haya maneno kwa Sophia Simba ni msumari!
 
Leo Mzee Mengi kakutana na waandishi wa habari (dakika chache zilizopita) na hiki ndicho alichoongea:

TAARIFA YA MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LTD. BW. REGINALD A. MENGI KWA VYOMBO VYA HABARI
6 NOVEMBA, 2009

_____________________________________________​



Ndugu Waandishi wa habari,

Nimewaita hapa leo kuzungumza nanyi kwa lengo la kuweka rekodi sawa.

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikituhumiwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba mimi si Mwanachama wa Chama hicho na kwamba sitoi misaada ya hali na mali kwa Chama Cha Mapinduzi.

Ndugu Wanahabari,

Kwa msemo wa kiingereza “Don’t argue with a fool because people may not know the difference between you and the fool”, wenye maana kwamba usibishane na mjinga kwa sababu watu wanaweza kushindwa kufahamu tofauti yako na huyo mjinga!

Hata hivyo wakati mwingine inakulazimu kujibu hoja unapomwona mtu anapotosha mambo kwa makusudi.

Kwanza, kuhusu kuropoka kwamba sitoi misaada kwa CCM, hilo ni jambo linalozushwa na watu binafsi na kwa malengo binafsi. Viongozi wakuu wa CCM ambao ni waadilifu na wanaosimamia ukweli wanajua undani wa jambo hili.

Pili, kuhusu uwanachama wangu wa CCM:

Napenda kuwaambia kwamba mimi ni Mwanachama wa CCM tangu tarehe 18 Aprili,1977 na kadi yangu ni Na. B124595, iliyotolewa na Tawi la Kisutu, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.

Hivyo basi madai yote kwamba mimi si mwanachama au nilijiunga na chama hivi majuzi kama inavyoelezwa na Mheshimiwa Waziri wa Utawala Bora Sophia Simba, Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Shaaban Kilumbe Ng’enda na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa DSM John Guninita ni uongo, uzushi na umbea wenye lengo la kudhoofisha juhudi za viongozi wa juu wa CCM na baadhi ya wanachama za kupiga ufisadi vita.

Mimi na wenzangu wengine tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba chama chetu kinaongozwa katika misingi yake ya asili ya kupiga vita rushwa na maovu mengine.

Ndugu Wanahabari,

Hawa wanaodai kuwa ndani ya CCM hakuna kiongozi msafi ni wazi kwamba wamedandia chama hiki hivi majuzi. Ningetoa ushauri kuwa waondoke na watuachie chama chetu kwa kuwa hawafahamu msingi imara wa CCM.

Mwisho napenda kumshauri Waziri Sophia Simba kwamba katika vita dhidi ya ufisadi ni vyema akanyamaza. Kwa sababu yeye si mwadilifu na hivyo hawezi kusimama kupinga vita ya ufisadi.

Aidha, ningemshauri kabla hajazungumza aombe ushauri kutoka taasisi za serikali kama vile usalama wa taifa badala ya kuropoka na kupotosha ukweli wa mambo.

Nawashukuru sana kwa kunisikiliza.


Reginald A. Mengi

MWENYEKITI MTENDAJI, IPP LTD.

HUYU JAMAA anatatanisha!HAKIKA NI MTATA!;
ANGALIA HAPA:

.Pia nimegundua kumbe muuwaji wa Chadema Busanda ni Mzee Mengi, baada ya taarifa za CCM kugaragazwa vibaya Busanda, ni Mzee Mengi aliyeokoa jahazi kwa kutoa Milioni 1OO, zilizotumika kusambaza kilo mbili mbili za sukari kila kaya on election eve, kesho yake Chadema Chali!
 
HUYU JAMAA anatatanisha!HAKIKA NI MTATA!;
ANGALIA HAPA:
Geoff,

Jaribu kutofautisha maoni ya mtu mmoja ndani ya JF au kwenye gazeti na taarifa rasmi. Hayo yalikuwa ni maoni ya Pasco kama member, kama angeambatanisha na ushahidi wa hizo 100mil basi ingekuwa ni ukweli usiopingika!
 
Mimi nilifikiri anatoa jibu kuhusu uhusika wake na kuwaingiza wananchi mjini kupitia NICOL. Kumbe anakitetea Chama Cha Mafisadi. Mnatuzingua tu nyie wote ni wale wale
 
Sina hakika sana na haiba ya Sofia Simba, lakini nashawishika kuamini kuwa, si mwenye maadili mema amekaa kiswahili mnoooo. Hata sijui wamemtoa wapi huyu hata akawemo kwenye mtandao ???
 
Geoff,

Jaribu kutofautisha maoni ya mtu mmoja ndani ya JF au kwenye gazeti na taarifa rasmi. Hayo yalikuwa ni maoni ya Pasco kama member, kama angeambatanisha na ushahidi wa hizo 100mil basi ingekuwa ni ukweli usiopingika!

understood!
 
Ninaamini yale tunayoyafanya huwa yanaonyesha sisi ni kina nani.Huyu mama sidhani kama ni kiongozi.Anaaibisha waliompa huo wadhifa maana ni mropokaji, mgomvi, mtukanaji etc. Kitu kibaya anabehave as if she is Invisible kama alivyo Robot wa JF!!!

Hii wizara anayoiongoza ni wizara nyeti mno na tupende tusipende inabeba mzigo mzito wa direction ya Taifa letu.Sasa kama amekaa mtu ambaye anafikiria kutafuta umbeya tu tutarajie nini?

Hatuko hapa tulipo kwa bahati mbaya.Tumejifikisha na kwa bahati mbaya badala ya kutumia nguvu zetu kusonga mbele tunapigana vikumbo wenyewe kwa wenyewe!Tunayo nafasi ya kujirekebisha na kusonga mbele kwa kuachana na watu wasio na sifa za kuwa viongozi!!
 
Ndugu Mengi angetusaidia sana kama angekuja na majibu ya maswali aliyoyatoa bwana Mayega badala na yeye kuendeleza mipasho


Maji ya mkondo hayachagui njia

Na: Paschally Mayega

RAIS wangu, Waswahili husema maji hufuata mkondo. Wazamivu katika sheria wanasema sheria pia hufuata mkondo. Waswahili na wanasheria katika hili wanakubaliana kuwa katika kufuata mkondo, sheria na maji havina utashi wa kuchagua vielekee wapi bali kule mkondo ulikoelekezwa.

Rais wangu, kama itakupendeza naomba kabla ya kuendelea na mada ya leo, kwanza nitoe fundo lililopo kifuani mwangu. Inawezekana ukawa ni ukweli kuwa mfinyanzi analia vigaeni. Unamkuta mtu kutwa anahangaika, akitangatanga huku na huko akiwalilia wenzake.

Anajinyima na kujidhiki kwa ajili ya wengine. Mara nyingine watu hawa hujikuta wamejikita katika shida za wenzao na wakasahau kuwa wao nao wana dhiki zaidi. Na hawa, huwa hawana wakuwalilia. Nani atawalilia na wao ndio wanaowalilia wengine?

Rais wangu, habari za Kampuni ya NICOL kutetereka zimenigusa kwa namna ya pekee. Wanasema mbuzi wa maskini hazai. Ikitokea akazaa, huzaa mwaka wa njaa, mtoto lazima aliwe. Nimeusikia msemo huu tangu ningali mdogo, lakini leo nausikia kwa uchungu mwingi zaidi. Nausikia kwa sononeko.

Ndugu Rais, baada ya kuhitimu masomo yangu ya falsafa, mwaka 1975 nilijiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika katika Shirika la Posta na Simu. Niliitumikia nchi yangu kwa muda wa miaka 20 hadi 1994 nilipoomba kustaafu kwa hiari.

Zaidi ya miaka 15 sasa niko mtaani naishi maisha ya kubangaiza. Mhangaikaji. Jua langu, mvua yangu. Sina mchana sina usiku mimi. Nachakurachakura kama kuku jalalani ili mimi na familia yangu tupate kitu cha kuingiza tumboni.

Kama serikali yetu ingetulipa malipo kama yalivyokuwa yameainishwa katika barua ya kustaafu kwa hiari ya mwaka 1994, leo hii dhiki yangu isingekuwapo. Kesi yetu mpaka leo iko mahakamani. Pamoja na ukwasi mkubwa wa baadhi ya viongozi wetu, serikali yetu inathubutu kutulipa pensheni ya sh 20,250 kwa mwezi.

Matumizi ya sh 675 kwa siku ni unyanyasaji. Mcha Mungu anaweza akasema mimi ni mwongo. Tunapokutana na hawa jamaa katika nyumba za ibada tunawaangalia hatuwamalizi. Mungu hadanganyiki! Viongozi wetu hawaelewi kuwa dunia njia wote tunapita tu. Tanueni na teseni kwa jasho tulilolivuja sisi, lakini mkumbuke kila mtu ana siku yake.

Waziri, baba mtu mzima analidanganya Bunge kuwa anatulipa sh 37,000 na sasa atatulipa sh 50,000. Anadanganya ili iweje? Mpaka leo tunapokea sh 20,250. Kila tulipoenda kuulizia nyongeza ya pensheni ya wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki tuliambiwa kwanza hata hizo sh 20,000 haijulikani tunalipwa na nani! Tumemwachia Mungu!

Kiongozi anashika uongozi mara tu anaanza kuotesha majumba kila mahali. Anapasua mashamba makubwa na mifugo mingi ya kisasa bila hata kuwalipa majirani fidia. Wanaendeshwa katika magari ya anasa na wakielea angani dege lao la anasa linakula sh milioni sita kwa kila saa.

Bila aibu mtu anaenda nalo hata kwa safari za kipuuzi kushabikia uchafu nchi za mbali. Katika hali kama hii ni chizi peke yake anaweza kuwaambia watu kuwa serikali haina fedha ya kuwalipa wastaafu inavyostahili au kuwasomesha watoto wetu vyuo vikuu. Naye ataitikiwa na machizi wenzake.

Nimesema mbuzi wa maskini hazai, lakini ikitokea akazaa huzaa mwaka wa njaa, mtoto lazima aliwe. Hapo katikati serikali iliamua kutupoza kidogo, ikatulipa kiduchu katika kile kingi tunachoidai. Wakatokea watu wazima na heshima zao wakatutangazia kampuni iitwayo NICOL.

Wakasema ukiwekeza utaondokana na umaskini. Nani anautaka umaskini bwana! Mimi si nikapanda mbegu zangu pale! Nikawekeza hisa 3,000. Ninapoambiwa NICOL ni DECI nyingine, nguvu zote zinaniisha mwilini. Kama ni kweli, hawa ni binadamu gani wenye roho za kinyama namna hii? Kudhulumu mpaka yatima na maskini?

Majina yao mazito. Wengine mwanzoni sikuwasikia, ningewasikia nisingepanda mbegu zangu pale kwa kuwa wamezoea kujiuzulu. Lakini tumeambiwa kuwa mwana mwema Reginald Mengi, ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya NICOL akiwa na waziri wa zamani aliyejiuzulu, Iddi Mohammed Simba.

Ningependa kujua je, ni kweli ndugu Mengi alihusika katika kuiingiza NICOL kichwa kichwa kwa ununuzi wa Pharmacetical and Beverage Limited (IPBL) iliyokuwa inafilisika kwa kutumia fedha zetu kiasi cha sh bilioni nne?

Sijui kiwanda hiki ni cha nani na sijui kuna uhusiano gani, lakini ni matumaini yetu kuwa bwana Reginald Mengi atatokeza hadharani kutufafanulia jambo hili ili kulinda hadhi yake katika nchi hii. Fundo lililojaa katika mioyo ya wanahisa juu yao kwa ufisadi huu ni hatari kwao kuliko sumu ya nyoka.

Kweli nyongo hukaa na ini. Sasa tunaanza kuwaza mambo mengi. Yawezekana wanaosimama majukwaani kila siku na kuonekana katika vyombo vya habari wakigawa fedha kama msaada wakawa wanagawa fedha hizi hizi zetu? Lazima kieleweke.

Haiwezekani tuwe wajinga ndio waliwao! Kumdhulumu mnyonge zaidi na kumpa mwenye nafuu ili wewe uonekane mwema unatoa misaada mingi ni nini kama si ufisadi uliopitiliza ufisadi papa? Unaweza kweli ukatumia jina la rais wetu au hata jina la Mwenyezi Mungu katika uovu huu?

Tunaomba serikali iwachukulie hatua za kisheria watu hawa hata kama ni kuwafilisi ili kunusuru mbegu zetu. Hapa padogo tunafisadi, tukifanikiwa kupata uongozi wa nchi kipi kitasalimika?

Ndugu Rais, na mimi ni binadamu kama wengine. Nina nyongo na moyo wangu ni wa nyama. Ninaililia nafsi yangu na wana NICOL wenzangu. Baba yetu Reginald Mengi sikuhukumu. Nayaelekeza haya yote kwako kwa sababu kati yao wewe waonekana u mwema.

Tuambie, ni nini hiki mlichotufanyia maskini wenu weusi? Wewe na sisi ni ndugu, mama yetu mmoja, Tanzania. Ukitueleza kwa ufasaha tutakuelewa. Ndugu Rais, ngoja sasa nirudi kwenye mada yangu ya leo.

Rais wangu, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umepita. Mapungufu makubwa yaliyojitokeza kama yatafanyiwa kazi ni Mungu peke yake anajua. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ameteuliwa kushika wadhifa huo na mwenyekiti wa taifa wa chama chezaji.

Ndiye aliyempa kula. Huyu ndiye refarii. Kwa maneno mepesi ni kwamba anayempa kula au ushindi mchezaji wa kinyang’anyiro cha urais, ndiye baadaye naye humpa kula yule aliyempa kula. Hii peke yake inaondoa uwezekano wa kuiona haki ikitendeka hata kama haki hiyo itatendeka.

Mwenye akili timamu anayecheza mchezo ambao mwamuzi wake ameteuliwa na mpinzani wake, hachezi kwa faida ya mchezo huo. Anacheza kutimiza lengo lake tofauti na lengo la mchezo huo.

Wagombea wetu wa urais kutoka upinzani hali hii wanaiona, lakini wanashiriki katika mchezo huo kwa sababu nia yao kubwa si urais, nia yao iko katika mioyo yao. Chama chenye wanachama wengi kwa maelfu, watakuwaje na mgombea mmoja tu anayeshindwa katika kila uchaguzi?

Kila msimu mgombea ni yuleyule na sera zake ni zilezile. Huyu hana jipya. Ikijakutokea, kama itakujakutokea, wakaupata urais utashangaa kuwaona na wao wenyewe wakishangaa kuupata urais. Haiwezekani kwa mgombea wa upinzani kuupata urais kwa mkondo huu tulionao sasa, na wao wenyewe wanalijua hili.

Mgombea urais wa upinzani atagombea urais mara ya kwanza, anashindwa. Akishindwa na mara ya pili atataka na mara ya tatu na ya nne. Huyu bila kuzuiwa atataka awe mgombea shindwa wa maisha. Tumejipangia kuwa rais hata akipendwa vipi vipindi vyake ni viwili, wewe mgombea shindwa unapendwa vipi uwe mgombea wa maisha?

Hali ya uchaguzi katika nchi yetu ni sawasawa na mfereji uliokwishachimbwa. Ukimwaga maji (uchaguzi) ndani yake maji hayachagui yaende wapi. Yatafuata kule mfereji ulikoelekezwa. Kushindwa katika chaguzi kwa vyama vya upinzani mara nyingi, ni matokeo ya ubinafsi. Hali hii itaendelea kuwepo kwa sababu viongozi wabinafsi katika upinzani wanaendelea kupewa nafasi.

Wananchi lazima waelewe kuwa, lengo, nia na madhumuni pekee ya chama chochote cha siasa ni kutaka kutawala. Kwenda Ikulu. Viongozi wa vyama hivyo ndio wanataka kutawala badala ya hawa waliopo. Si vyama vya ukombozi hivi. Wananchi lazima watofautishe kati ya chama cha siasa na chama cha ukombozi.

Wanachowaambia wapinzani ni maovu yanayotendwa na viongozi wa sasa. Lakini hiyo haionyeshi usafi wao. Wengine wanaweza kuwa wabaya hata zaidi ya hawa tulionao. Ukitaka kuona uchu wa madaraka walionao viongozi wetu wa upinzani, wengi wao wako tayari hata leo hii kwa serikali ya mseto, wao wanaita serikali ya umoja wa kitaifa.

Nia waambulie hata u-DC tu. Jaribu kutafuta mawaziri bora 20 tu kutoka katika vyama vyetu vya upinzani maarufu kama NCCR-Mageuzi, TLP, CUF na CHADEMA. Wanaoleta fujo kwenye vyama vyao hivi sasa nao watataka wawe bora mawaziri kama baadhi ya bora mawaziri tulionao hivi sasa.

Kazi njema inayofanywa na upinzani naitambua na kuiheshimu sana na hasa kufichua maovu yanayotendwa na viongozi wetu wa sasa. Lakini hii peke yake haitoshi kuonyesha kuwa wewe utakuwa mtawala bora!

Ndugu Rais, bado nakubaliana na mawazo ya Mwalimu Nyerere kuwa, rais bora lazima atoke CCM. Uongozi wa CCM sasa hivi umejawa na uozo mwingi. Wema wengi wamefunikwa na waovu wakubwa wachache.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, Bunge la Jamhuri ya Muungano limekubali kuwa Katibu Mkuu wa chama tawala – CCM, Yusuf Makamba kafanya ufisadi, yaani ni fisadi na mtu huyu bado ni Katibu Mkuu, tena wa chama kinachotawala. Chama kitakuwaje kisafi? Unatenganishaje chama na viongozi wake, na hasa wa juu?

Wale wana CCM walio wema wanapaswa kumkana mtu huyu si kunyamaza. Ikishindikana matakwa ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere yatimie kwa CCM hii kupasuka katika vipande viwili. Na hapo ndipo utakapozaliwa upinzani wenye maana katika nchi hii.

Wapo wanaosema uongozi wa juu wa CCM na serikali ni dhaifu. Wengine wanasema uvumilivu na upole vimezidi. Lakini mtu mpole kupindukia na ***** wanatofautiana vipi? Wote hukaa kimya, hata pale wanapotakiwa kutoa maamuzi muhimu.

Idadi ya watu wanaojiandikisha na kujitokeza kupiga kura inazidi kupungua siku hadi siku. Hawaoni faida yake tena. Walitaka wakipiga kura mabadiliko wanayoyatarajia yatokee, lakini hiyo haiwi. Wamechoshwa na namna wanavyotawaliwa. Kupiga kura wanaona ni sawa na kumwaga maji katika mfereji.

Kadiri watu wengi zaidi wanavyozidi kususa kupiga kura, ndivyo tunavyokaribia maangamizi makubwa. Matakwa yao ya mabadiliko yanazidi kukua na kupanuka na kwakuwa wameishaona kuwa sanduku la kura halisaidii kuleta mabadiliko wayatakayo, watayatafuta kwa njia nyingine maana kiu ya mabadiliko haiachi kusumbua.

Ole wao wote walioufupisha upeo wao wa kuona kwa sababu ya ulafi tu. Rais wa nchi atachaguliwaje kwa asilimia chini ya hamsini kama si kutaka kuleta maasi katika nchi? Kwa mkondo huu, CCM 2010 hata wakimsimamisha mbuzi agombee urais, itashinda. Baada ya ushindi huo, hakuna kingine kitakachofuata bali machafuko na maangamizi.

Maafa makubwa yatakayoichafua historia nzuri ya taifa letu. Nani atakubali kutawaliwa na mbuzi? Mwenyezi Mungu atusaidie waja wake kwa kutuondolea kwa njia yoyote ile wote anaowajua yeye kuwa ni viongozi batili. Tunahitaji amani. Amani yetu inachafuliwa na wachache.

Rais wangu Kikwete, watu wako tutakwenda mbele tutarudi nyuma, lakini hakuna tutakachokipata bali kukurudia wewe. Tuondolee hizi baruti kabla hazijatulipukia. Tutengenezee mazingira ya kupata tume huru ya uchaguzi. Mgombea ashinde kwa asilimia inayoonyesha kukubalika na wengi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya aliye chini ya mamlaka yako kusimamia uchaguzi ambao na wewe ni mgombea ni ubatili mtupu. Watu wametawaliwa na tamaa zote, madaraka na mali, wao wenyewe, watoto wao mpaka wake zao.

Maskini na watoto wao wanabaki wakiwa, hata elimu tu nayo wananyimwa, fedha za madini na rasilimali nyingine za taifa lao pamoja na kodi zao vinalambwa na baadhi ya watawala wachoyo, manyang’au.

Ni kujidanganya kusema hali hii itaendelea milele. Iko siku inakuja na wala siku hiyo haiko mbali sana. Mwenyezi Mungu anijalie nisiione siku hiyo! Siku ya kihoro!
Chanzo: Tanzania Daima
 
Hili pia linaonyesha kuwa JK anataka kufanya alichoshindwa JKNyerere.
Je ataweza?????
 
naomba nimpe saluti mzee Mengi kwa kuzungumza mambo machache lakini ya msingi.Sijui Auntie Sophie atasemaje akija kujua kuwa Mzee tangia 77 ana kadi mkononi! Kweli usilolijua ni kama usiku wa giza
 
HUYU JAMAA anatatanisha!HAKIKA NI MTATA!;
ANGALIA HAPA:

kwa wasio mjua Mengi, watashangaa, ila UUGWANA NA UADILIFU WAKE DAIMA UMEMFIKISHA HAPO ALIPO, KWANI MZEE JK NYERERE alipo mpigia debe Paul Ndombo wa NCCR mageuzi mwaka 1995 alikua amejivua uanachama wa CCM , Mengi ana marafiki wengi CHADEMA, NA SI AJABU KUKUTA ANAWASAIDIA KIFEDHA kama watamwomba, hivyo hoja ya kuwa alitumika kuiua CHADEMA Busanda au alitoa Pesa, huo ni utashi wake.

Hongera Mengi kwa kuweka haya mambo sawa.

Sofia Simba amemtusi hadi Rais kua ni fisadi maana amedai ndani ya CCM Hakuna asie fisadi.

Nitashangaa kufikia J3 kama Kikwete JK/ Rais. atakua hajamfukuza kazi
 
Aisiii!! Hongera Mzee R. Mengi kwa Umakini wa Maelezo yako. Mimi nasema huyu Mh. Simba bado tu anaendela na uwaziri? aone anavyoliaibisha Taifa jamani kama kubebana sio huku du!!!!!!!!!!!!
 
Invisible

Naomba uweke humu JF maneno aliyosema Sophia Simba Bungeni kwani wengine hatukupata bahati ya kuyasikia
 
Back
Top Bottom