Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

Sofia Simba na Sakata la Mafisadi na Wapiganaji!

CCM yafika pabaya: Waziri awalipua Malecela, Mwakyembe, Anne Kilango

Mwananchi
Na Daniel Mjema,Dodoma
11/5/2009

MALUMBANO makali yameendelea kuitikisa Kamati ya rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi baada ya makombora ya juzi kuelekezwa kwa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango na mumewe, mzee John Malecela.

Kamati hiyo imekuwa ikipokea mashambulizi makali baina ya wabunge ambao wanaonekana kuwa vinara wa vita dhidi ya ufisadi na wale ambao wanaona kuwa vita hiyo inawalenga, kiasi cha kurushiana tuhuma nzito zilizo na mwelekeo wa kuchafuana.

Baada ya kulipuana Jumanne, juzi ilikuwa zamu ya Mama Kilango na mumewe Malecela wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba alipotoa tuhuma nzito akidai kuwa wawili hao pia wamekula fedha za ufisadi.

Habari kutoka vyanzo vyetu zilieleza kuwa Simba alidiriki kudai kuwa hata harusi ya makamu huyo wa zamani wa CCM na Kilango ilifadhiliwa na mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu Patel.

Patel kwa sasa ana kesi katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kuiibia Benki Kuu (BoT) kwa kuchota takribani Sh11 bilioni kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

Akijieleza kwenye kamati hiyo, Simba alimtuhumu Malecela, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza, kuwa wakati akiwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Jeetu Patel alimpa Sh200 milioni kwa ajili ya kampeni zake.

Malecela, ambaye wakati huo alikuwa makamu mwenyekiti wa CCM, aliondolewa mapema kwenye mbio za urais, ikiwa ni mara ya pili baada ya kuenguliwa tena mapema mwaka 1995.

Waziri huyo mwenye dhamana ya utawala bora akiwa na taasisi nyeti kama Takukuru na Idara ya Usalama wa Taifa, alizidi kurusha makombora kwa wanandoa hao, akisema Mama Kilango ni mnafiki na sio msafi kiasi cha kuwanyooshea wengine vidole wakati harusi na kampeni zake za ubunge zilifadhiliwa na mtuhumiwa huyo wa ufisadi.

Habari zinasema kuwa Mama Simba alikuwa akizungumza kwa kujiamini na kwa ujasiri na kumtuhumu Mama Kilango kuwa kelele zake zote zinatokana na nongwa ya 'kuukosa U-first lady (kuwa mke wa rais).'

Alieleza kuwa kelele zote za mbunge huyo wa Same Mashariki zinatokana na chuki na uchu wa madaraka na si kweli kwamba ni mpinga ufisadi, kwa mujibu wa mtoaji habari wetu.

Lakini Patel, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo za Waziri Simba kwamba alifadhili harusi ya Malecela na kampeni zake za urais, alionekana kustuka na kusema: "Haa...we nani kakwambia... Bwana ehee, mimi sijui lolote kuhusu hayo.

"Kwa sasa mimi najiangalia mwenyewe, nina matatizo yangu mengi nahangaika nayo."

Hata alipofafanuliwa kwamba, maneno hayo yalisemwa na Waziri Simba, alijibu: "Kama wao wamesema wenyewe huko, mimi sijui."

Naye Kilango alisema alishuhudia wakati wakati makombora hayo yakirushwa na kueleza kwamba anajiandaa kujibu mapigo.

Mbunge huyo machachari alisema anajua kwamba mambo yote yaliyosemwa, yanamlenga yeye na si mumewe Malecela.

"Mimi ni mwanasiasa... andikeni yote yaliyozungumzwa bila ya kuacha baadhi na siwezi kuwashtaki," alisema Kilango.

Mzee Malecela hakutaka kuzungumzia lolote kuhusu tuhuma hizo wakati alipoulizwa juu ya uhusiano wake na Patel na kama aliwahi kupokea kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kampeni.

"Ahaa... kijana naomba uniache nipumzike," alisema Malecela.

Mbali na mzee Malecela na mkewe, Waziri Simba pia alimgeukia mwenyekiti mtendaji wa IPP, Reginald Mengi akimtuhumu kuwa anaendesha vyombo vya habari vinavyoichafua CCM na serikali yake kwa maslahi yake binafsi.

Pia alimshambulia mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe na mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, akiwatuhumu kuwa ni watu wenye njaa na kwamba, wanalipwa fedha kufanya kazi hiyo.

Waziri Simba alisema kuwa hata tuhuma dhidi ya mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, zimetokana na chuki binafsi.

Simba alisema kuwa uchunguzi wa kashfa ya rada ulishamalizika na Chenge akasafishwa na kuongeza kwamba hata uchunguzi wa Richmond umebaini kulikuwa hakuna rushwa, kwa mujibu wa mtoaji habari wetu.

Suala la Richmond liliibuka tena mbele ya kamati hiyo ya Mwinyi wakati mbunge wa Bukoba Vijijini, Nazir Karamagi alipolalamika kuwa ripoti ya kamati teule ya Bunge iliyoozwa Dk Mwakyembe haikumtendea haki.

habari hizo toka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Karamagi alisema ripoti ya Richmond ilionea baadhi ya watu na akapendekeza iundwe tume huru kupitia mchakato huo kuona kama wana makosa ili haki itendeke.

Mbunge huyo ambaye alijiuzulu uwaziri baada ya Lowassa kuachia wadhifa wake wa waziri mkuu kutokana na kashfa hiyo, alisema maamuzi yake kuhusu Richmond yalitokana na mapendekezo ya Bodi ya Tanesco.

Naye Dk Mwakyembe alijibu hoja iliyotolewa Jumanne na mbunge wa Ukonga, Dk Makongoro Mahanga aliyedai kuwa ripoti ya Richmond ni 'feki', akisema tatizo la Dk Mahanga ni uelewa mdogo.

Kuhusu hoja ya Karamagi, Dk Mwakyembe alisema malalamiko yake si sahihi kwa sababu yapo maeneo mengi ambayo Karamagi alishiriki na yako bayana hayahitaji mjadala.

Aliwatahadharisha Wabunge kuacha kudodosa sana ripoti ya Richmond kwani watazidi kumchafua Lowassa na kwamba wanaweza kufungwa kwa sababu upo ushahidi dhahiri.

Dk Mwakyembe aliwataka viongozi wa CCM wenye tuhuma kuiga mfano wa Mzee Mwinyi aliyejiuzulu baada ya mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola mkoani Shinyanga.

Akizungumza mbele ya kamati hiyo, kwa mujibu wa vyanzo vyetu, alimshambulia spika wa Bunge, Samuel Sitta akidai kuwa kama si mizengwe, suala la Richmond lingemalizwa kwa taratibu za kichama.

Habari hizo zinadai kuwa Chenge, aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali, alisema Lowassa alizungukwa na kwamba kulikuwa na njama za kummaliza ingawa hakusema njama hizo zilifanywa na nani.

Chenge aliitetea serikali ya awamu ya tatu kuhusu kuingia mikataba mibovu na kusisitiza hakukuwa na uzembe kwani mikataba yote ilipitiwa na kukubaliwa na Baraza la Mawaziri.

Hata hivyo, mbunge wa Muleba Kusini, Wilson Masilingi alisimama na kuomba kutoa taarifa na kumwomba Mzee Mwinyi na kamati yake wawabane wabunge wanaodai wanasema ukweli.

Masilingi alipinga maelezo ya Chenge kuhusu mikataba na kusisitiza kuwa maelezo yake yalijaa ushabiki na kusema Baraza la Mawaziri liliridhia mikataba kutokana na ushauri wake (Chenge).

Mbunge wa Kwela, Dk Chrisant Mzindakaya, ambaye aliwahi kupata umaarufu kwa kulipua kashfa, aliwataka wabunge wakubali matokeo kuhusu Ripoti ya Richmond ili taifa lisonge mbele badala ya malumbano yasiyokwisha.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Mzindakaya aliwataka wabunge wafahamu kuwa ripoti hiyo ilishapitishwa na Bunge na haiwezi kurejeshwa ianze tena upya.

Naye Dk Mlingwa (Shinyanga Mjini), alisema mpasuko unaoinyemelea CCM unatokana na chama hicho kuacha misingi yake ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na badala yake kinawakumbatia wafanyabiashara. Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Emanuel Nchimbi alitumia nafasi yake kuomba maridhiano ya wabunge wa CCM, kujenga moyo wa kusameheana ili chama kisonge mbele.
 
- Auntie Sophia, anajidhalilisha sana kwa sababu ni majuzi tu alisema anawaunga mkono wapiganaji sasa leo tena amegeuka anawasaidia mafisadi, na huyu ni waziri wa Usalama tena kutoka ofisi ya rais, inasikitisha sana maana kwenye haya maelezo yake amejishusha na kurudi kule kule mtaani anakotokea, alipaswa kukumbushwa kwamba hapo kwenye kikao ni mambo ya serious ishus za taifa na masilahi ya wanachi, waziri mzima wa jamhuri huwezi kwenda kwenye kwenye kamati serious kama hii na kudai maneno ya wivu na chuki ambayo huwezi yathibitisha unless unashiriki kufikiri kwenye kichwa cha unayemtuhumu.

- Halafu hii maneno ya harusi ndio uongo wake utakapoishia na kuanzia, kwa sababu yes alikuwepo na tumeshirikiana naye akiwa mbunge wa viti maalum, na pia tumeshirikiana na viongozi wengine wengi sana, na hata siku mzee analalamika kwamba hana hela za honeymoon yeye alikuwepo na viongozi wengine kama Mzee Mwinyi, Marehemu Sammy Mdee, Mama Zabeni, Mzee Msuya, Mama Nyoni, na Mama Makinda wote tulikuwa pamoja kule Area C, nyumbani kwa then Mheshimiwa Kilango alipokuwa akiishi zamani, na kila aliyekuwepo pale alipigwa na mshangao kwamba Mzee Malecela hana hela za honeymoon!, kabla sijajitokeza kubeba msalaba.

- Kwenye haya ya harusi na hela za kampeni Auntie Sophia amejishusha hadhi sana na ninajaribu sana kumuomba Mheshimiwa Kilango, asimchafue Auntie Sophia siku ya zamu yake maana itakuwa kiama hiyo siku, I mean utamuanzia wapi na kuishia wapi huyu masikini ya Mungu! kila mahali ni aibu tupu, inatia kinyaa sana!

William.
 
Mkuu DC,

Amini usiamini kny thread hii na ile ya Zitto kuna mambo mengi sana mapya nimejifunza kwa kweli!

Siasa za Tanzania ni zaidi ya tunavyozijua!

Siyo utani ndugu, yaani kuishi kwingi ni kuona mengi. Kwetu sisi tuliomwona Mwalimu JK Nyerere na mawaziri waliokuwa wanashindana kuvaa suti kama zake na kuongea kama yeye, hatuwezi kuamini kama kweli haya yanatokea TZ. Yaani tunakuwa na viongozi hadi ngazi uwaziri ambao wanafanya vioja kama vya watoto wa chekechekea na kuzua kelele kwenye vikao kama kwenye kliniki za wototo wadogo wanapopata chanjo MCH. Kaaazi kweli kweli!!
 
- Kuhusu harusi na ufadhili wake, Auntie Sophia hakusema ukweli kwa sababu harusi iliandaliwa na kamati maalum kama inavyokuwa kwenye harusi zote bongo, Mwenyekiti wa kamati alikuwa Chiligati, akishirkiana na DC wa Dodoma Mjini, ikiwa ni pamoja na wanakamati kama Kimbau na Kitwana Kondo, na kina General Gau, sasa hawa hasa Chiligati wangetakiwa kuonyesha mahesabu waliyoyatumia ili kuweka ukweli unapotakiwa, kwa sababu ninazo copies zote za matumizi ya ile harusi na pesa zilizochangwa na majina wala sio tatizo.

- Maneno ya Auntie Sophia, siyaamini hata kidogo na ni uzushi mtupu kwa sababu ni mimi ndiye niliyetoa hela zangu za mfukoni kwanza kununua suti zote mbili za bwana harusi, na pia nilitoa hela zangu za mfukoni za kulipia honeymoon yao, ama sivyo hata honeymoon isingekuwepo, na kama kawaida yangu huwa ninatunza risiti ya kila kitu ninachofanya duniani, kwa hiyo ninasema kwamba Auntie Sophia, ana kazi kubwa sana kuthibitisha madai yake akiwa waziri wa Usalama wa taifa, kwa sababu ninazo risiti nyingi sana za hela zangu nilizotumia on the harusi, sasa kama kweli harusi ilifadhiliwa na fisadi, mimi na ndugu zangu hatukuwa na sababu ya kutoa hela nyingi sana tulizotumia kwenye ile harusi.

- Ya kugombea urais, hivi Mzee si alikuwa na hela za Iran, zilizobaki toka mwaka 1995. Halafu Auntie Sophia hapa tena anakuwa sio mkweli wala anayejali sheria, kwa sababu kampeni za urais wagombea wote walipokea hela toka kwa watu na sekta mbali mbali na haikuwa uvunjaji wa sheria za jamhuri, na ukweli niujuao ni kwamba kampeni ya mzee ilifadhiliwa na Shabibu, na kampeni ilikuwa na hela ndogo sana ndio maana haikufanikiwa, unless Shabibu ni fisadi then kweli mzee alichukua hela chafu, na kama ilivyokuwa kampeni ya Rais wa sasa ambako Auntie Sophia alikuwa mshiriki sasa angelinganisha hela zilizotumiwa na kambi zote na walikozitoa hela zao ndio ingependeza, lakini si kweli kabisa kwamba Patel ndiye aliyefadhili ile kampeni, walioifadhili kampeni ni shabibu na Mstaafu wa Idara, sasa the question inapaswa kuwa alikuwa akizitoa wapi zile hela kama at the sametime alikuwa akishirikiana na kina Rsotam na Lowassa? Kwa sababu all this came to the light baada ya uchaguzi na mtoto wa mstaafu kupewa ubunge wa bure na mtandao Sophia angekuwa mkweli angeisaidia sana hii kamati na taifa kwa ujumla na hasa kutokana na nafasi yake ya uwaziri wa Usalama wa Taifa.

Pole mkuu kwa yote, mi nilidhani ni jina tu unatumia na hakuna uhusiano wowote na JS Malecela maana wengine tulimzoea sana Ipyana (RIP).
 
mhhhh...Kiongozi asante kwa taarifa hii..kwa kweli CCM imefika pabaya
 
- Auntie Sophia, anajidhalilisha sana kwa sababu ni majuzi tu alisema anawaunga mkono wapiganaji sasa leo tena amegeuka anawasaidia mafisadi, na huyu ni waziri wa Usalama tena kutoka ofisi ya rais, inasikitisha sana maana kwenye haya maelezo yake amejishusha na kurudi kule kule mtaani anakotokea, alipaswa kukumbushwa kwamba hapo kwenye kikao ni mambo ya serious ishus za taifa na masilahi ya wanachi, waziri mzima wa jamhuri huwezi kwenda kwenye kwenye kamati serious kama hii na kudai maneno ya wivu na chuki ambayo huwezi yathibitisha unless unashiriki kufikiri kwenye kichwa cha unayemtuhumu.

- Halafu hii maneno ya harusi ndio uongo wake utakapoishia na kuanzia, kwa sababu yes alikuwepo na tumeshirikiana naye akiwa mbunge wa viti maalum, na pia tumeshirikiana na viongozi wengine wengi sana, na hata siku mzee analalamika kwamba hana hela za honeymoon yeye alikuwepo na viongozi wengine kama Mzee Mwinyi, Marehemu Sammy Mdee, Mama Zabeni, Mzee Msuya, Mama Nyoni, na Mama Makinda wote tulikuwa pamoja kule Area C, nyumbani kwa then Mheshimiwa Kilango alipokuwa akiishi zamani, na kila aliyekuwepo pale alipigwa na mshangao kwamba Mzee Malecela hana hela za honeymoon!, kabla sijajitokeza kubeba msalaba.

- Kwenye haya ya harusi na hela za kampeni Auntie Sophia amejishusha hadhi sana na ninajaribu sana kumuomba Mheshimiwa Kilango, asimchafue Auntie Sophia siku ya zamu yake maana itakuwa kiama hiyo siku, I mean utamuanzia wapi na kuishia wapi huyu masikini ya Mungu! kila mahali ni aibu tupu, inatia kinyaa sana!

William.

Kwani hayo maneno ni yake binafsi au ni dossier aliyopewa aifikishe mbele ya kamati?
 
Kwani hayo maneno ni yake binafsi au ni dossier aliyopewa aifikishe mbele ya kamati?

kama maneno si yake binafsi, basi yeye ni mtu hatari sana hapaswi hata kuwa karibu na jamii, kesho anaweza pewa silaha azuru na akafanya,maana ajiongozi anaongozwa.
 
Habari kutoka vyanzo vyetu zilieleza kuwa Simba alidiriki kudai kuwa hata harusi ya makamu huyo wa zamani wa CCM na Kilango ilifadhiliwa na mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu Patel.

Akijieleza kwenye kamati hiyo, Simba alimtuhumu Malecela, ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya awamu ya kwanza, kuwa wakati akiwania kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Jeetu Patel alimpa Sh200 milioni kwa ajili ya kampeni zake.

Waziri huyo mwenye dhamana ya utawala bora ... alizidi kurusha makombora kwa wanandoa hao, akisema Mama Kilango ni mnafiki na sio msafi kiasi cha kuwanyooshea wengine vidole wakati harusi na kampeni zake za ubunge zilifadhiliwa na mtuhumiwa huyo wa ufisadi.
Patamu hapo...napenda kusoma mara mbili mbili kama posho za wabunge vile...hii ni kama Halbadiri...wanatajana sasa...watatajana...weeeee...wacha niketi na kikombe cha chai nitazame tu...

CCM ileeee inaelekea maji ya shingo...kuendea kuzama...niliwahi kusema na nasisitiza CCM haina mpiganaji wa ufisadi, makelele na makeke yote yale yalikuwa na ajenda ya matumbo yao tu na kuwazubaisha watanzania waliochoka na njaa na umasikini wa kutafutiwa,CCM yote imeoza haina dira, matumaini wala siasa ya kubadilisha hali za maisha ya wanananchi, si mnaona wanavyotajana hivyo...machafu yao hayo wanasema wenyewe kama wanavyonukuliwa na vyombo vya habari, hayajasemwa na wapinzani wakasema kuwa wanasingiziwa au na Hosea wakasema wanaonewa gere

...wenyewe na bado tunasubiri utetezi wa Yona, Mramba na Mgonja...nao wamkome nyani ...watanzania muone chama kinachotaka kukuleteeni maisha bora kilivyo na viongozi wake walivyo wanatumia migongo yenu iliyochoka kuinama kwa kufikiri na kulima kwa faida yao tu

...amkeni wajamaaa ...kusoma hamjuwi hata picha hamuoni?
 
Unajua hata kama hayo yote aliyosema Bi Simba yangekuwa kweli .... mbona bado naona hakuna hoja yoyote ya maana? Suala ni Richmond sasa mbona naleta mambo ya harusi ? Kupokea mchango hatat kama ni kweli kuna ubaya gani? Jamani hivi ni sifa zipi zinakupa uwaziri katika serikali? i thought it is a serious position ...
 
Mzee Nyerere aliwahi kusema kuwa CCM sio Baba wala Mama yake, angeweza kusepa wakati wowote-kwa nini watu wasijichomoe tu kutoka kwenye hili dubwana linaloitwa CCM?.
 
Kwani hayo maneno ni yake binafsi au ni dossier aliyopewa aifikishe mbele ya kamati?

- Ninamfahamu sana huyu waziri tena kwa karibu sana, na kwa yoyote anayemfahamu vizuri anajua kwamba haya ni maneno yake binafsi kwa sababu ndio kawaida yake kuzungumza maneno low na out of sense.

- Angekua ametumwa basi wangempa hoja nzito kidogo kuliko hizi ngonjera, ambazo hawezi kuzithibitisha. Kinachosikitisha ni kwamba huyu ni Waziri wa wizara muhimu kama aliyonayo na pia ni Mwenyekiti wa Umaoja wa Wanawake wa Tanzania,

- Sasa akija mgeni toka nje ya nchi yetu, kwanza anahitaji kuelewa kwamba huyu waziri wa ofisi ya rais je huyo rais anafanana vipi? Na hao wanawake wa Tanzania kama huyu ndiye Mwenyekiti wao wanafanaje? Na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kama tuna viongozi wa juu kama huyu na sisi tunafananaje?

- It is very sad!

William.
 
Kwani hayo maneno ni yake binafsi au ni dossier aliyopewa aifikishe mbele ya kamati?

Na Willy kama unawasilianan na mama Kilango mshauri asimjibu Bi Simba kwa Mipansho .. alenge kwenye hoja tu basi .. asiingie kwenye mtego wa kuanza kusutanan .. watu watawaweka kundi moja ... aonyeshe tofauti kwa kustick kwenye hoja tu na kuepuka character assasination... unajua pumba na mchele zinajulikana... asisutane kabisa .. awarudishe kwenye hoja basi ... Bi Simba na maneno yak kajimaliza mwenyewe ..
 
sidhani kama ntakuwa nimekosea nikisema hii nchi imepoteza muelekeo..sawa watu watamlaumu mama Sofia Simba ,but at least amebwatuka na kumbe tumejua leo kuwa Mzee malecela alichukuwa 200m kwa Jeatu Patel...hahaaa na harusi yake ilikuwa funded na Jeatu..these are very good news to me..na ule usemi wa mama Anna Kilango kuwa patachimbika bungeni ndo tunangoja pachimbike katika kujibu haya
 
- Mkuu ndio maana nimesema ninajaribu sana kumsihi Mama K, asiingie huu mtego wa kalubandika, maana wenye akili watashindwa kuwatofautisha, point yako ni nzito sana.

Ahsante.

William.
 
- Ninamfahamu sana huyu waziri tena kwa karibu sana, na kwa yoyote anayemfahamu vizuri anajua kwamba haya ni maneno yake binafsi kwa sababu ndio kawaida yake kuzungumza maneno low na out of sense.

- Angekua ametumwa basi wangempa hoja nzito kidogo kuliko hizi ngonjera, ambazo hawezi kuzithibitisha. Kinachosikitisha ni kwamba huyu ni Waziri wa wizara muhimu kama aliyonayo na pia ni Mwenyekiti wa Umaoja wa Wanawake wa Tanzania,

- Sasa akija mgeni toka nje ya nchi yetu, kwanza anahitaji kuelewa kwamba huyu waziri wa ofisi ya rais je huyo rais anafanana vipi? Na hao wanawake wa Tanzania kama huyu ndiye Mwenyekiti wao wanafanaje? Na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kama tuna viongozi wa juu kama huyu na sisi tunafananaje?

- It is very sad!

William.

Mkuu ili kuepusha kuongezeka kwa beti za hii ngonjera aliyoanzisha Auntie Sophie naomba umwambie/mshauri Mama Kilango asiendeleze haya malumbano.Ukweli utajulikana tu bila kuutetea maana kama ni mstari basi auntie ameenda kiwango cha chini mno.
 
- Kuhusu harusi na ufadhili wake, Auntie Sophia hakusema ukweli kwa sababu harusi iliandaliwa na kamati maalum kama inavyokuwa kwenye harusi zote bongo, Mwenyekiti wa kamati alikuwa Chiligati, akishirkiana na DC wa Dodoma Mjini, ikiwa ni pamoja na wanakamati kama Kimbau na Kitwana Kondo, na kina General Gau, sasa hawa hasa Chiligati wangetakiwa kuonyesha mahesabu waliyoyatumia ili kuweka ukweli unapotakiwa, kwa sababu ninazo copies zote za matumizi ya ile harusi na pesa zilizochangwa na majina wala sio tatizo.

- Maneno ya Auntie Sophia, siyaamini hata kidogo na ni uzushi mtupu kwa sababu ni mimi ndiye niliyetoa hela zangu za mfukoni kwanza kununua suti zote mbili za bwana harusi, na pia nilitoa hela zangu za mfukoni za kulipia honeymoon yao, ama sivyo hata honeymoon isingekuwepo, na kama kawaida yangu huwa ninatunza risiti ya kila kitu ninachofanya duniani, kwa hiyo ninasema kwamba Auntie Sophia, ana kazi kubwa sana kuthibitisha madai yake akiwa waziri wa Usalama wa taifa, kwa sababu ninazo risiti nyingi sana za hela zangu nilizotumia on the harusi, sasa kama kweli harusi ilifadhiliwa na fisadi, mimi na ndugu zangu hatukuwa na sababu ya kutoa hela nyingi sana tulizotumia kwenye ile harusi.

- Ya kugombea urais, hivi Mzee si alikuwa na hela za Iran, zilizobaki toka mwaka 1995. Halafu Auntie Sophia hapa tena anakuwa sio mkweli wala anayejali sheria, kwa sababu kampeni za urais wagombea wote walipokea hela toka kwa watu na sekta mbali mbali na haikuwa uvunjaji wa sheria za jamhuri, na ukweli niujuao ni kwamba kampeni ya mzee ilifadhiliwa na Shabibu, na kampeni ilikuwa na hela ndogo sana ndio maana haikufanikiwa, unless Shabibu ni fisadi then kweli mzee alichukua hela chafu, na kama ilivyokuwa kampeni ya Rais wa sasa ambako Auntie Sophia alikuwa mshiriki sasa angelinganisha hela zilizotumiwa na kambi zote na walikozitoa hela zao ndio ingependeza, lakini si kweli kabisa kwamba Patel ndiye aliyefadhili ile kampeni, walioifadhili kampeni ni shabibu na Mstaafu wa Idara, sasa the question inapaswa kuwa alikuwa akizitoa wapi zile hela kama at the sametime alikuwa akishirikiana na kina Rsotam na Lowassa? Kwa sababu all this came to the light baada ya uchaguzi na mtoto wa mstaafu kupewa ubunge wa bure na mtandao Sophia angekuwa mkweli angeisaidia sana hii kamati na taifa kwa ujumla na hasa kutokana na nafasi yake ya uwaziri wa Usalama wa Taifa.

Pole mkuu kwa yote, mi nilidhani ni jina tu unatumia na hakuna uhusiano wowote na JS Malecela maana wengine tulimzoea sana Ipyana (RIP).

aaaaagh sasa kwani kamati ndo inatoa hela..Jeatu alitoa 200m kama wachangiaji wengine.hapa ndo pakushika wanaojidai wapiganaji kumbe nao wananuka rushwa.Wizi mtupu hapaa
 
Shule ikiwa tatizo mara nyingi mtu akifungua mdomo tu unamjua. Ndiyo maana Sumaye akajiamulia hata baada ya uwaziri Mkuu aende shule, tatizo letu watu bongo wanaongoza kwanza, halafu kama wana interest ndio wanaenda shule, au wengine wananunua vyeti.

Kwa jinsi mambo yalivyoandikwa hata kama kungekuwa na issue inaonekana mtu anaropoka.
 
- Ninamfahamu sana huyu waziri tena kwa karibu sana, na kwa yoyote anayemfahamu vizuri anajua kwamba haya ni maneno yake binafsi kwa sababu ndio kawaida yake kuzungumza maneno low na out of sense.

- Angekua ametumwa basi wangempa hoja nzito kidogo kuliko hizi ngonjera, ambazo hawezi kuzithibitisha. Kinachosikitisha ni kwamba huyu ni Waziri wa wizara muhimu kama aliyonayo na pia ni Mwenyekiti wa Umaoja wa Wanawake wa Tanzania,

- Sasa akija mgeni toka nje ya nchi yetu, kwanza anahitaji kuelewa kwamba huyu waziri wa ofisi ya rais je huyo rais anafanana vipi? Na hao wanawake wa Tanzania kama huyu ndiye Mwenyekiti wao wanafanaje? Na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kama tuna viongozi wa juu kama huyu na sisi tunafananaje?

- It is very sad!

William.

Mkuu naona unalenga kwenye hoja ambayo nimeigusia sana kwenye post zangu zilizopita. Kwani kama mtu kapewa kazi na anaifanya ndivyo sivyo ila bado anapewa pongezi na bonus, nani wa kulaumiwa? Ukitengeneza program (software) bomu halafu ikashindwa kukupa ulichokitegemea utalaumu kompyuta? Ila itakuwa nafuu kama utakuwa unajua unachokitegemea. Lakini kama hujui unachotakiwa kupata kwenye hiyo software itakuwaje? Naona kinachotokea hapa Tanzania kinatia kichefu chefu na kutudhalilisha Watanzania wote kana kwamba wote tuna vichwa vya kuku! Very sad in deed😕
 
Back
Top Bottom