Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

mara mia mungu akunyime sura akupe akili! sita mimi sijui namfananisha na nani ndani ya ccm!pamoja na kuwa ndani bado anapambana sasa nani kama yeye!haya waliohoji kuhusu nyumba, benzi na ccj yote kayasema, haya mnataka nini zaidi?na wasio wanafiki ni akina nani tuwaone au wale ambao wanachagua maswari ya kuulizwa????tumepewa akili basi tuitumie kupambanua mambo!!!!!!!!!!
 
fikira pevu ndo zinahitajika hapa jamvini! yeye kama yeye jd yake ni ipi???alichofanya nadhani alitoa mwanga kwa watendaji waendelee na process zinazotakiwa au mlitaka achukue maamuzi !
 
Sitta ni mwana siasa na yuko mbioni kugombea Urais 2015. Hana zaidi anatafuta umaarufu.
 
huyu jamaa sitta mbona simwelewi elewi!

Inavyoonekana huyu jamaa roho inataka kumtoka kwa kuukosa uspika. amesahau yeye na hao hao anao waita leo mafisadi walivyomfanyia zengwe mzee msekwa mpaka wakamwaga. Alidhani atakuwa spika mpaka kufa. Makinda naye wakimchoka watamtosa aache kulalama akumbuke kuwa 'MPANDA UPEPO UVUNA TUFANI' Muda wake ushapita akapumzike naona ni kama mtu aliyeanza kuchanganyikiwa!
 
Source: dakika 45.
Kasema mafisadi ambao wako tayari kumtoa roho ndio waliobadili utaratibu wa uchaguzi wa spika.
Anasema walishindwa kushindana naye kwenye box la kura wakaamua kuweka kigezo cha jinsia.
My take: kama JK aliridhia naye ni fisadi

Mh Sita anatoa single kila siku, si atengeneze album? aache kulilia Uspika kwa kulala bungeni..
 
Nakumbuka alitoa shutuma mbaya sana dhidi ya CDM, wiki mbili ivi kabla ya kikao cha bunge kuahirishwa.
 
kwa huo mkwara wa mansix
sijui kama utapona ban
kwa leo karibu sana mkuu
 
kila mtu karibu karibu karibu!!!!basi na mm najiunga humo humo Karibu saaana!!
 
Source: dakika 45.
Kasema mafisadi ambao wako tayari kumtoa roho ndio waliobadili utaratibu wa uchaguzi wa spika.
Anasema walishindwa kushindana naye kwenye box la kura wakaamua kuweka kigezo cha jinsia.
My take: kama JK aliridhia naye ni fisadi

Nani alikwambia sio
 
Hongera Waziri Sitta. Ulipokuwa spika ulifanya kazi iliyotukuka, na sasa unaendelea na kazi yako njema. Nakuombea ww na Magreth afya njema na maisha marefu. Ww ni shujaa wangu.

mkuu umenena,huyu mzee ni bonge la jasiri,amethubutu kuisema ccm mara kibao tu.this oldman is ma here.
 
Sitta kama binadamu wengine wote ana mapungufu yake, lakini hebu semeni ni kiongozi gani wa Tanzania ambaye amekuwa jasiri kusema ukweli kuhusu ufisadi na udhaifu wa serikali na upole usio kifani wa Mh Kikwete. Hamkumbuki ni huyu huyu Sitta, akimkaribisha Mh Kikwete kuhutubia bunge, alimuomba au alimwambia awe mkali kidogo ili wananchi warudishe imani na serikali. Ni chini ya huyu huyu Sitta, bunge au wabunge waliweza kuwa huru na kutoa siri nyingi za maovu. Na mpaka sasa anasimama kidete kutetea yaliyo ya kweli, sasa wale mnaoona Lowasa anaonewa, simameni mseme wapi anaonewa?

Ukweli ni kuwa wengi ndani ya CCM wanaogopa kuwa akishika mpini, watu kama Mkapa wankwenda mahakamani, na huyu mzee hataki kabisa kummsikia Sitta. Na CDM, nao wanajua Sitta akisimama, mpira utakuwa mgumu saana kwa kwa Dr Slaa. Huu ndo ukweli, wote wanajua CCM ikimuweka EL, basi Dr anapeta
 
Back
Top Bottom