Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

Sita hatafuti umaarufu kupitia tv,Sita ni maarufu tangu zamani. Nyie mnasema Sitta anatafuta umaarufu mnatakiwa mkapimwe akili.
Kwa hiyo hata Chenge ni maarufu.Ama utamwita Rostam maarufu.Au Lowassa ni maarufu. Ama wewe umaarufu unaudefine vipi? Ama Lyatonga Mrema utamwita maarufu. Unatakiwa kutafakari kwanza hoja..
 
Mie nilishaacha longtime kusoma gazeti la Mwanahalisi, as time goes linaelekea zaidi kuliko uchunguzi...

..Tofauti yake na yale ya Shigongo ni kuwa Mwanahalisi linabase kwenye udaku wa kwenye siasa wakati Shigongo amejikita kwenye udaku wa maisha ya mitaani...
Kwa hiyo umehamia kwenye Uhuru na Mzalendo nini Mkuu??
 
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 39"]
[TR]
[TD="width: 98%, bgcolor: transparent"] Sitta:Sigombei urais uchaguzi 2015 [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"] Wednesday, 26 October 2011 07:37 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"] Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta Exuper Kachenje na Kelvin Matandiko
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema hana ndoto ya kuwania urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015.Kauli hiyo ya kwanza ya Sitta ambaye pia ni kada wa CCM, imekuja wakati ambao kuna mpasuko mkubwa ndani ya chama chake hicho ambao unahusishwa na mbio za urais wa 2015, huku yeye akitajwa kuwa mmoja wa wenye nia ya kushiriki mbio hizo.

Kauli yake imeingia katika orodha ya kauli za makada wengine kadhaa ambazo zimetikisa siasa za CCM huku nyingi zikiwa na sura ya mvutano tena zikitolea nje ya vikao rasmi vya chama hicho tawala nchini.

Hata hivyo, juzi usiku akijibu swali kama ana ndoto ya kuwania urais au la, Sitta alisema: "Hapana! Sina ndoto ya kuwania urais kwa sasa, wapo vijana watajitokeza, wapo wazuri, tutawaunga mkono tu".

Sitta alifafanua kwamba matumaini yake mwaka 2015 watakuwapo wagombea wenye uwezo wakiwemo vijana, na kuongeza, "wale wazalendo wenye maadili wataungwa mkono".

Ingawa, Sitta amesema hana ndoto ya kuwania urais kwa sasa, lakini amekuwa akitajwa kama mmoja wa watu wanaoutaka baada ya Rais Jakaya Kikwete mwaka 2015, kutokana na nguvu zake kubwa alizojijengea kwa umma.

Sitta aliweza kujipatia umaarufu mkubwa kisiasa baada ya kuongoza kwa mafanikio Bunge la Tisa ambalo alikuwa na kauli mbiu yake ya Bunge la Kasi na Viwango.

Kuhusu chuki ya watu aliowaita mafisadi, Sitta alisema watuhumiwa hao walifanya mbinu mbalimbali kuhakikisha hafanikiwa katika malengo ya kurejea kwenye uspika wa Bunge la Kumi kwani waliendesha hujumu nzito dhidi yake.

Sitta aliwatuhumu watu hao akisema: "Mafisadi hawanitaki, wananichukia wako tayari hata kuniua".

Mwelekeo wa CCM

Akizungumzia mustakabali wa chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, Sitta alisema CCM kitaweza kushinda kutokana na mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa katika vikao vijavyo vya chama hicho baadaye mwaka huu, pamoja na uchaguzi wake mkuu wa mwakani.

Sitta aliongeza:, "Uchaguzi Mkuu ndani ya CCM wa mwaka 2012, utatuonyesha sura ya chama. Nina imani watapatikana wanaofuata maadili yale aliyosimamia Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere".

Hata hivyo, Sitta alionya kwamba chama hicho kinahitaji timu ya ushindi na kwamba hakiwezi kufanya hivyo ikiwa kitaendelea kuwa na watu wanaojitajirisha kwa nafasi zao za uongozi.

"CCM inastahili kufanya mabadiliko, inahitaji timu ya ushindi ili kuweza kufanya hivyo, lakini hakiwezi kufanya hivyo kama itaendelea kuwa na watu wanaojitajirisha kupitia fursa za uongozi. 2012 CCM iwe safi zaidi, tusiache watu wanunuane," alionya Sitta.

Alisema mwaka 2012, CCM itashuhudiwa ikirejea katika mstari wake, kupitia vikao vyake na falsafa ya kujivua gamba ambayo itashuhudiwa ikiwashughulikia wanaopinga kurejesha maadili na kuzaliwa upya.

Lakini, alisema katika hilo wapo wanaopinga kurejeshwa kwa maadili hayo kwa kutumia fedha zao kununua wapambe aliowaita wenye roho za kuku ambao watakuwa wakitumika kuzuia mpango huo kwa malengo ya kisiasa.

"Katika hilo wapo wenye roho ya kuku, wakionyeshwa pesa tu, basi wanabadilika. Wanaosema hawataki dhana ya kujivua gamba hawataki CCM izaliwe upya,"alisema.

Malipo ya Dowans
Sitta alirerejea msimamo wake kuhusu malipo kwa kampuni hiyo, huku akisema kuwa anaridhishwa na hatua ya kukata rufaa na kusisitiza umuhimu wa vijana kuwa na uzalendo wa kufanya maandamano kupinga mambo yasiyo ya msingi.

"Sisi zamani tulikuwa mstari wa mbele katika maslahi ya taifa. Ila kwa sasa naona vijana wako nyuma sana hawaandamani kupinga vitendo vya kifisadi katika Serikali yao, maandamano ya kizalendo yenye kuonesha hisia zao juu kupinga ufisadi huu,’’alisema Sitta.

Alisema angefurahi siku kuona kama vijana wa CCM na wengine wenye maadili wakiandamana kwa pamoja kupinga vitendo vya kifisadi, ikiwemlo kuilipa Dowans, lakini kwa sasa akasema suala hilo linashughulikiwa kisheria.

Sitta ambaye alikuwa akizungumza katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha luninga cha ITV, alisema Sh 110 bilioni za kuilipa Dowans zina uwezo wa kujenga shule za kisasa 300 mbazo kila moja ingegarimu Sh300 milioni.

Sitta alisema huo ni ulafi na kuongeza kwamba yeye kama angekuwa na fedha nyingi au sehemu angekuwa tayari mafisadi wangemchafua.

“Mimi kama ni ngekuwa hata na tuhuma ya shilingi moja ni lazima wangeniumbua maana wananitafuta sana na kama vitisho nimevipata sana kwenye simu ndiyo maana nabadilisha sana namba ya simu,’’ alisema.

Alisema stahiki anazolipwa na Serikali kama nyumba na magari si ufahari, kwani kama ni benzi aliyokuwa akitumia kipindi akiwa mbunge si lake.
Waziri Sitta alisema gari kama hilo alinunuliwa pia Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na hata Gavana wa Benki Kuu (BoT) na kuhoji, "sasa kwanini nitajwe mimi tu?"

Kauli za makada CCM
Wiki iliyopita Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa naye alivunja ukimya kwa kuzungumzia tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake, huku akisisitiza kuwa amechoka kukashifiwa na sasa kamwe hatawavumilia wanaomzulia mambo.

Lowassa ambaye pia amekuwa akitajwa kuwa na mpango wa kuwania urais wa 2015 alisema ni jambo lisiloingia akilini kumhusisha yeye na kile kinachodaiwa mkakati wa kumhujumu Rais Kikwete au CCM, wakati yeye ni mbunge anayetokana na chama hicho.

Siku moja kabla ya Lowassa kuzungumza na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Millya aliingia katika malumbano yanayoendelea miongoni mwa makada wa chama hicho pale aliposema “watoto wa viongozi wa CCM na Serikali wamejitwika madaraka ya wazazi wao kinyume cha sheria za nchi”.
Kama ilivyokuwa kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole na Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Benno Malisa, pia Millya alimshambulia Katibu wa Itikadi na Uenenzi wa chama hicho, Nape Nnauye kwamba amekuwa akikivuruga chama. Nape anatuhumiwa na kundi mojawapo ndani ya CCM kutokana na jinsi anavyosimamia utekelezaji wa maazimio ya NEC ya CCM hasa falsafa ya kujivua gamba, na hilo limekuwa likihusishwa na mbio za urais wa 2015.

Hata hivyo, Nape aliwahi kuliambai gazeti hili kwamba anashamgazwa na wale wanaopotosha utekelezaji wa maazimio hayo ya NEC kwa kuhusisha utekelezaji wake na Uchaguzi Mkuu ujao, wakati muda wa uchaguzi wenyewe bado haujafika.

Source: Mwananchi
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Huu siyo muda wa kutafuta ujiko kwa kukemea ufisadi hadharani, tunahitaji hao mafisadi wachukuliwe hatua za kisheria. Sitta anatumiwa na Kikwete ili watu waone kuwa CCM bado kuna watu wenye uchungu. Huwezi ukawa na kadi ya CCM halafu ujifanye unachukia ufisadi, hii ni sawa na kuwa Mkristo lakini humpendi Yesu Kristo.
I can't believe my legz, aaah sorry my eyes! Wewe mwenyewe au nivae miwani?
 
Wote lao moja sema wamezidiana tu kila mmoja alikuwa na target zake.
 
SITTA ameshasoma upepo kagundua kuwa tumeshamshtukia kuwa yeye na EL ni mafisadi hawachekani.
SITTA hakubaliki kwa sasa kwa sababu ya unafiki wake na hauziki kwa namna yeyote ile.
 
sitta ameshasoma upepo kagundua kuwa tumeshamshtukia kuwa yeye na el ni mafisadi hawachekani.
Sitta hakubaliki kwa sasa kwa sababu ya unafiki wake na hauziki kwa namna yeyote ile.

mbona wamshambulia mtu kwa maneno makavu yasio na hoja ndani yake? Tuambie 'hakubaliki kwa ufisadi moja, mbili, tatu! Kwa vielelezo moja, mbili taTu!' nadhani ukifanya hivyo watu waTAkuelewa!
 
Aliwekwa ili kumkomoa Sita, sasa nae sita anasema kukomolewa basi imetosha? Ngoja tuone mwisho wake.
 
SITTA ameshasoma upepo kagundua kuwa tumeshamshtukia kuwa yeye na EL ni mafisadi hawachekani.
SITTA hakubaliki kwa sasa kwa sababu ya unafiki wake na hauziki kwa namna yeyote ile.

Yani wewe unamfanaisha Sita na EL???
Mbona sisi watanganyika hatupendi kutenda haki?? yani tunafanyiana dhulma kwa kila kitu???
Inavyoonesha Mungu ataendelea kutuadhibu kwa kutupa viongozi wabaya ili waendelee kututesa kwa sababu sisi wenyewe tumejaa ushenzi tu!
 
kikwete fanya maamuzi magumu fukuza sitaaaaaaaaaa you lose nothing anakibomoa chama huku hataki kutoka? mtoe nje akaanzishe CCJ part 2

Wewe kumbuka Julias Kambarage Nyerere alitabiri kuwa Upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm......sasa huu ndio mwanzo.....CDM wanamsubiri huyu wakifanya makosa tuu ya kumfukuza.....Bila shaka bila kupingwa CCM ziiii.....na kwa taarifa yako CCM hawana ubavu wa kumfukuza 6......wakimfukuza CCM itamegeka haijawahi kutokea na ndiyo kifo cha gafla!!!!!!.......Mimi naamini 6 ameshafanya mahesabu ya ukweli..na haya anayoyafanya anayafanya kwa makusudi na huu ndio wakati sahihi kabisa kwa haya 6 anayoyafanya...Kazi wanayo CCM....hata kama ni mnafiki six sio wa kumdharau they suppose to handle him with care!!!!!
 
Pamoja na kuwa utaratibu wa kumpata spika uliingiliwa na mafisadi, lakini mzee sita kuukosa uspika ameumia sana. Mi nilidhani ameshasahau kumbe bado tu hajasahau!!!!!
 
Hapa ngoma nzito sana maana haieleweki kabisa nana ndege nani popo.
 
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, amesema nguvu ya Chama cha Demokrasia (CHADEMA) inatishia uhai na utawala wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, waziri huyo ambaye pia aliwahi kuwa Spika alisema: “Mambo kama haya nasema hata kule Igunga CHADEMA walituhangaisha na kujipatia umaarufu wa kukubalika kwa wananchi kutokana na udhaifu wetu na hasa tabia hii ya kuendelea kuwabeba watu wasio waadilifu wenye tuhuma za ufisadi.
“…CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana hawakuwa na mgombea lakini kwenye uchaguzi mdogo wameibuka na kura zaidi ya asilimia 43, wanatumia udhaifu wetu wa tuhuma za ufisadi na ugumu wa maisha halafu wanazijengea hoja wananchi wanawakubali wao. Hapa lazima tujibadilishe na kujipanga upya.”
Alisema nguvu iliyoonyeshwa na CHADEMA katika uchaguzi huo, ilitokana na udhaifu wa CCM ambayo inaendelea kuwakumbatia mafisadi.
Alisema CHADEMA wameweza kutumia udhaifu huo na ugumu wa maisha wa wananchi kuushawishi umma.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kujaza nafasi ya Rostam Aziz aliyejiuzulu kwa madai kwamba amechoshwa na siasa uchwara ndani ya CCM, mgombea wa chama hicho, Dk. Peter Kafumu, alishinda kwa kura 26,484 akifuatiwa na wa CHADEMA, Joseph Kashindye, aliyepata kura 23,260 na Leopold Mahona, wa CUF, kura 2,104.
Sitta alisema katika uchaguzi ujao ndani ya CCM, chama chake kinapaswa kujipanga na kupata safu mpya ya uongozi wenye maadili ili watue mzigo wa mafisadi ambao wanafanya vitendo hata vya kulitia hasara taifa bila kujali, kwani lengo lao ni utajiri.
Alisema mambo si shwari ndani ya CCM, akaonya kwamba endapo chama hicho hakitabadili mfumo na utendaji wake, kitakumbwa na ushindani mkubwa wa kisiasa huko mbele.
“Nadhani unaona hali ya kisiasa inavyozidi kuwa ngumu, wenzetu wa CHADEMA wanatumia mbinu ya umaskini walionao wananchi na hoja ya mafisadi ambayo inazidi kuwajengea umaarufu. Kielelezo tosha ni matokeo ya uchaguzi Igunga ambao CHADEMA walipata aslimia 43. Kumbuka ni mwaka jana tu tumefanya uchaguzi mkuu lakini wananchi wamegeuka,” alisema Sitta.
Waziri Sitta alitumia kipindi hicho kusisitiza kauli yake ya mara kwa mara kwamba hahusiki na uanzishwaji wa chama cha siasa cha CCJ na kudai kuwa yeye ni mwanasiasa na amekuwa akikutana na wanasiasa wenzake wakiwemo wale wa kambi ya upinzani na kujadili mambo mengi, hivyo haoni kuwa huo ni usaliti.
“Unajua ukishakuwa mwanasiasa utakutana na wenzako, wapo wanaokuja tunazungumza na wananiambia huko uliko hakufai njoo upande huu, naomba kukujulisha au kuujulisha umma kuwa mimi ni mwana CCM na nitabaki CCM, lakini ujue kuwa CCM si baba yangu au mama yangu nikiona yamenishinda nitajua cha kufanya,” alisema Sitta.
Hata hivyo, zipo kumbukumbu nyingi zinazoonyesha kuwa Sitta alikuwa miongoni mwa wanasiasa waandamizi ndani ya CCM walioasisi CCJ kwa malengo ya kushindana na CCM na CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa 2010.
Mbali na Sitta, makada wengine wa CCM walioasisi CCJ kwa madai kwamba wanakerwa na mwenendo wa CCM, ni Nape Nnauye, Dk. Harrison Mwakyembe na Fred Mpendazoe.
Miongoni mwao, Mpendazoe ndiye alijitoa mhanga kwa kuondoka CCM na kupoteza ubunge wa Jimbo la Kishapu; lakini CCJ kilipokosa usajili wa kudumu akajiunga na CHADEMA. Baadaye aliandika kitabu na kuwataja aliokuwa nao, ingawa wamekuwa wanakanusha kuhusika na harakati hizo.
Sitta ndiye amekuwa kinara wa kundi lililojipachika jina la “wapambanaji wa ufisadi” ambalo wachambuzi wa siasa wanasema lilijitokeza ili kuuza nguvu ya CHADEMA katika mapambano ya ufisadi.
CHADEMA ndiyo iliyosisi hoja na mapambano ya ufisadi na kwa mara ya kwanza ilianika hadharani orodha ya watuhumiwa ufisadi 11, Septemba 2007, Mwembeyanga, Dar es Salaam.
Orodha hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, baada ya Sitta, akiwa Spika wa Bunge, kukataa hoja ya Dk. Slaa kuhusu ufisadi na kutishia kumshtaki kwa maelezo kuwa alikuwa ameghushi vielelezo alivyokuwa navyo.
Hata hivyo, baada ya kuona kasi ya vita ya ufisadi imeshika moto, Sitta na kundi lake, wakiwamo pia Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, na Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka, waliibuka na kuanza kushambuliana na makundi mengine ndani ya CCM waliotajwa na Dk. Slaa.
Hata hivyo, wachambuzi wanasema kwamba nia ya kina Sitta haikuwa kupigana na ufisadi, bali kuendeleza vita ya makundi ndani ya chama chao, na kuipiku CHADEMA katika vita ya ufisadi, ili wananchi waone kwamba hata ndani ya CCM kuna wanaochukia ufisadi.
Baadaye, Rais Jakaya Kikwete amekuja kuitumia hoja ya ufisadi kuwachukulia hatua za kisiasa na kisheria baadhi ya waliotajwa katika orodha hiyo, ingawa naye ni miongoni mwa waliotajwa.
Wachambuzi wa kisiasa wanasema hatua hiyo ya Rais Kikwete ni propaganda za kisiasa za kutaka kujikosha mbele ya Watanzania, kwani sehemu ya ufisadi unaowahusu hao wanaotuhumiwa ilimhusisha au kumhusu pia yeye, kwani baadhi ya pesa zilizotumika kumwingiza madarakani zilitokana na ufisadi.
Baadhi ya makada ndani ya CCM wamekuwa wanahusisha kauli za Sitta na uchaguzi mkuu ujao, ingawa yeye amesema juzi kwamba hana nia ya urais.
Hata hivyo, inajulikana kwamba Sitta ana kundi lake, na kauli zake zinalenga kuwadhoofisha baadhi ya wanaofikiriwa kuusaka urais ndani ya chama chake, ambao wanadhaniwa kuwa washindani wake au wa kundi lake.
 
anasema kuna vijana watagombea uraisi. jamani J.makamba nini?? dah magamba hakuna dira wanatapatapa
 
mbona wamshambulia mtu kwa maneno makavu yasio na hoja ndani yake? Tuambie 'hakubaliki kwa ufisadi moja, mbili, tatu! Kwa vielelezo moja, mbili taTu!' nadhani ukifanya hivyo watu waTAkuelewa!

huelewi nini sasa..sitta ni mnafiki hana lolote ..akae chini aleee wajukuu
 
Hivi huyu babu bado akili zake zinamtuma kwamba atafulu huu mtihani aliojipa.
Sawa yetu macho

6 + POROJO= UNAFIKI
 
Back
Top Bottom