Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

Kipindi kitarushwa mda si mrefu ITV tafadhali wadau wote tufuatilie tumsikie live kuanzia saa 3.00 leo
 
mbona hakusema haya mara alipotemwa uspika?sitta acha porojo zako zinatuchosha.
 
Huyu mzee pamoja na unafiki wake, lakini hili la uspika wa makinda kuteuliwa na Rostam liko wazi kabisaa na wala halina ubishi, kwani hata Makinda mwenyewe alishakiri kwamba Rostam alimfuata akamshauri agombee uspika.
 
Jamani leo dkk 45 ITV ccm inapasuka maana s6 ana mambo si kidogo..tuwepo sote tuone
 
Sitta anasema Madaktari wa Tanzania hawakujua ni nini kinamsumbua Mwakyembe ila inawezekana ni sumu..
 
Huyu sitta mimi sina imani naye sana. Yeye kama anataka aonekane ana uchungu basi aungane na kina Slaa.

Sitta ni mnafiki nambari one, anatafuta umaarufu na huruma ya wananchi!
 
Naamini kwa hapa alipofikia siku zake ccm zinahesabika! Jamaa hawatakaa kimya tena, ila tusubiri tuone. CDM tunaanza kujiandaa na uchaguzi maana jamaa lazima wamtose.
Kikwete atajifanya kafanya maamuzi magumu.
 
nguvu ya pesa ya mafisadi inapolomoka sana na watajikuta wapo kwenye mikono ya sheria
 
Duh jamaa anasema kila k2 mafisadi vs wasio mafisadi
 
Sitta anasema kuna watu wasafi ndani ya CCM ndiyo watachukuwa nchi..

Huyo ndiyo Sitta
 
Sitta amtuhumu Kubenea kununuliwa na mafisadi.
adai ameitwa kujiunga na vyama vingi vya siasa na kukiri kuwa na mazungumzo.
asema kuna madudu ambayo mwakyembe amefanyiwa na anahisi ni sumu.
adai pia kuwa chama chake (CCM) kimemfanyia mambo mabaya hata kwa kutamkwa
adai kupigwa zengwe kwenye ugombea wa spika kwa kubadilishwa utaratibu ghafla wa kutakiwa mwanamke ndiye agombee
Adai hawezi kususa nafasi yake kwa sababu ya kuisema serikali na atendelea kuisema na itakapofikia hatua ya kuwekewa maneno mdomoni basi atafanya maamuzi mengine na kupiga magoti ili Mungu amuoneshe pa kwenda
aisifu chadema kwa jinsi kinavyojipanga kwenye uchaguzi hasa wa igunga na kuifanya ccm kuingia ICU
Adai ccm inahitajika kufanya marekebisho kabla ya kiama na kuacha uchafu uliojaa ndani yake
Ashangaa vijana kutofanya maandamano kupinga hali yeyote mbaya nchini kwa uzalendo
Aunga mkono maandamano kupinga ufisadi wa DOWANS


Source:ITV
 
Back
Top Bottom