Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

Sitta alonga katika 'Dakika 45' ya ITV

Tukipata "wanafiki" 20 kama Sitta bila shaka ufisadi utapungua kwa asilimia kubwa
 
six ni mnafiki mpaka basi,niliwahi kuuliza mjadala wa richmond aliuufungaje mwaka jana kama na yeye si fisadi?huyo atawasumbua wengine lakini hapo hakuna kitu.sioni tofauti na Nape
 
Huyu mzee pamoja na unafiki wake, lakini hili la uspika wa makinda kuteuliwa na Rostam liko wazi kabisaa na wala halina ubishi, kwani hata Makinda mwenyewe alishakiri kwamba Rostam alimfuata akamshauri agombee uspika.

ni kweli mkuu, makinda alibanwa kwa maswali na akasema kuwa rostam alimfata na kumtaka agombee na ukiunganisha dots na alivosema sitta unapata jibu kamili tena lililopigiwa mistari miwili chini!
 
Sita hatafuti umaarufu kupitia tv,Sita ni maarufu tangu zamani. Nyie mnasema Sitta anatafuta umaarufu mnatakiwa mkapimwe akili.
 
[Bado mnamuongelea Sitta ? Jamani ni kweli tumeishiwa kweli mada hapa JF hadi Sitta aje in betwee ]

Lunyungu ulitaka tumuongelee Lowassa ndio roho yako itulie acheni unafiki
 
Tangu lini 6 akawa na credibility ya kuwasema wenzie?

Mkuu,unajua kwa maana pana ya maneno ya Sita anatuhumu vikao vya CC na NEC ya CCM vilivyopitisha jina la mgombea wa Uspika kwamba vilisalimu amri kwa mafisadi. Na wabunge waliomchagua spika nao walihongwa. Hizi ni tuhuma nzito sana. Mimi nilikua nadhani Shibuda ni tatizo kubwa CDM,kumbe Sita ndiye kiboko zaidi. Huyu ni tatizo kwa chama chake na serikali. Nadhani anatafuta kufukuzwa,sijui ataelekea kwa ndugu yake Lipumba ama kwa wazee wenzie Cheyo na Mrema?!
 
Mmmmmmmh!

Ushauri mzuri kwa bwana 6 ni kustaafu siasa. Katika kutaka kuongea anatoa kauli nyingi zenye utata kama alivyoongelea afya ya Mwakwembe adharani. Sina hakika kama familia yake imejisikia vyema kwa maelezo aliyoyatoa 6!

Mwisho wa yote bado uzalendo wake tutautilia shaka kwa sababu ya kuona ufisadi wa mapacha watatu tu! Naendelea kuuliza; haijui MEREMETA, TANGOLD n.k mbona hao hawasemi??????????

Kama nisemavyo siku zote: " Ukiona mwanaccm anapinga ufisadi fulani basi ujue kakosa mgao au anagombea madaraka na huyo aliyefanya ufisadi"!

Chunguza njomba na utabaini!
 
kwani sitta ana kashfa zipi ukilinganisha na wengine? wote mnaomkosoa hamna sababu za msingi za ukosoaji wenu mnabaki kusema ni mnafiki mnafiki mnafiki! hamna hoja bali ni kuropoka tu.
Huyu sitta ndo alifanya watu walione bunge kuwa tamu, kwa kiasi kikubwa alijaribu sana kuwa unbiased,ishu nyingi za ufisadi zimeibukia bungeni alipokuwa spika,alijaribu sana kuweka wazi mijadala na wabunge wengi wakajenga confidence ya kusema bungeni maovu ya watendaji wa serikalini , unafikiri angekuwa msekwa ishu za richmond/dowans etc zingepata nafasi ya kujadiliwa bungeni? hata huyu mama wa sasa anapretend kuvaa viatu vya sitta lakini kuna ishu kadhaa kazificha kwenye 'underwear'! wabunge wangapi wametoa hoja zao na spika akawataka wathibitishe kwa maandishi na pindi walipoleta uthibitisho yule mama anaficha kwenye 'underwear' anapotezea moja kwa moja mpaka inasahaulika! mbunge Godbless Lema wa Arusha mjini alipotaka waziri mkuu awajibike kwa kusema uongo bungeni, mlisikia majibu ya mama na akamtaka alete maelezo na alipoleta akaficha kulekule 'kunako' na ndugu Lema alipohoji kwa mara nyingine alipotezewa, angekuwa sitta angeacha pinda ayakoge maji!
 
Huyu babu hana lolote ana subiri mgao wake siku malipo ya intrest ya Dowahns yakifika 1 trillion!
 
Sitta nilimkubali siku Jakaya Kikwete alipohutubia Bunge la Jamhuri halafu alipomaliza kabla hajakaa chini spika Sitta akachukua jukwaa akaanza kummaliza Kikwete live kwamba serikali ya Kikwete na hotuba yake huenda ikawa ni maneno matupu.
 
Source: dakika 45.
Kasema mafisadi ambao wako tayari kumtoa roho ndio waliobadili utaratibu wa uchaguzi wa spika.
Anasema walishindwa kushindana naye kwenye box la kura wakaamua kuweka kigezo cha jinsia.
My take: kama JK aliridhia naye ni fisadi
ndo unafahamu leo kuwa jk ni fisadi mwandamizi?
 
afu huyu mzee hasomeki kabisa
Huyu mzee anasomeka ,ila ukiangalia ameshavuka Life Expectancy ya mtanzania, ana miaka michache tu hai uhai sidhani kama yuko radhi kutoka jikoni ambako angalau atamalizia siku zake vyema..japo roho inamuuna,hana jinsi!
 
Mmmmmmmh!

Ushauri mzuri kwa bwana 6 ni kustaafu siasa. Katika kutaka kuongea anatoa kauli nyingi zenye utata kama alivyoongelea afya ya Mwakwembe adharani. Sina hakika kama familia yake imejisikia vyema kwa maelezo aliyoyatoa 6!

Mwisho wa yote bado uzalendo wake tutautilia shaka kwa sababu ya kuona ufisadi wa mapacha watatu tu! Naendelea kuuliza; haijui MEREMETA, TANGOLD n.k mbona hao hawasemi??????????

Kama nisemavyo siku zote: " Ukiona mwanaccm anapinga ufisadi fulani basi ujue kakosa mgao au anagombea madaraka na huyo aliyefanya ufisadi"!

Chunguza njomba na utabaini!

Mimi namheshimu sana huyu mzee wangu ila kwa leo naomba nitumie msemo huu 'Mbuzi aliyefungwa kamba huishia kulia mee'!
 
Kama unasema anachofanya Sitta ni kutoka Kikwette iweje tena ajiandae kufukuzwa uwaziri??

Hayo mawazo nimeyatoa nyakati tofauti. Maoni yanaweza kubadilika kulingana na upepo wa mjadala.
 
thumbnail.aspx

Walimu wa watoto hawa ndiyo wenye uchungu na nchi yangu..... they are my heroes!!, the rest need to shut up!!!! and get to work!!
ungeanza wewe
 
Back
Top Bottom