Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,734
- 6,292
Kuna maneno ameyaandika "Bwana yule" siku ya leo yanafikirisha kidogo. Lakini ukiyatazama kwa undani haya maneno nadhani ndo kilichomkata nguvu Mange Kimambi kuendelea kushikamana na wanachadema katika the so called "Harakati wa kudai demokrasia Tz"
Bwana yule ameandika katika Twitter yake kama inavyosomeka hapo chini. Kiuhalisia Kigogo yupo 100% correct kuwa CHADEMA wamemkataa mwenyekiti wao haraka sana.
Baada ya tafakuri nachelea kusema yuko sawa. Freeman Mbowe ni kama amesalitiwa na wenzake katika hili. Aliacha msiba kwenda Mwanza kwa ajili ya kuwapa nguvu wenzake pamoja na wale walioshikiliwa. Na walipoachiwa alisisitiza Kongamano litafanyika Mwanza na hawataondoka mpaka lifanyike. Hivi sasa kila mtu amerudi nyumbani kwake na wamegeuka "Keyboard warriors" kama sisi tu. Amebaki Mbowe gerezani na msimamo wake wa kubaki Mwanza mpaka kongamano lifanyike, kama kukamatwa wakamatwe tu.
Mkutano wa mbowe na Press walikubaliana kuwa mwanachadema yeyote akikamtwa kwa kubumba basi hawatamuwekea dhamna, watawasusia polisi mpaka waachiliwe huru. Ila waliokamatwa pamoja na Mbowe wameshadhaminiwa na wamerejea makwa wakiwa na familia zao nao wanatweet na kusoma JF kama sisi.
Ukweli uliopo moyoni mwa wengi ambao ni washirika wa Mbowe ni kuongea sana na kupiga kelele nyingi za ukakamavu "Ili Mwenyekiti awaone na kuwafikiria au kuwakumbuka wakati fursa mbalimbali zikijitokeza kama za nafasi za ugombea, teuzi n.k". Ndo maana kuna waongeaji wengi "vishandu" ambao tuliwaamini kama ni imara na wakahama kambi kwa hoja ya kuunga mkono juhudi ama CDM kudai wamenunuliwa. Hawakanunuliwa hao bali ni Wachumia matumbo
Mbowe amekamatwa na ndiye mwenyekiti kitaifa , ile mihemko wanayomdanganya nayo imefyata. Hakuna wembe wala tutaingia barabarani kudai sijui nini. Wanachadema ni majasiri wa majibizano lakini si majasiri wa vitendo. Bawacha wamefanya igizo lao jana na limekwisha nao wapo na sisi kwenye Keyboards. Hakuna real Movement ya kuonesha kweli wameguswa na hawakubali mwenyekiti wao kufanywa hivi. CHADEMA WAMEMSALITI MWENYEKITI WAO KWEUPE.