Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,174
2,000
B904E014-DD3E-45FD-9DF1-E8F0D37C7298.jpeg

CDDA64F8-D20D-40FA-958F-E6E31958F1D0.jpeg

B5B719E0-9F14-4CC4-87F2-D014E57FC3DF.jpeg

Usiku majira ya saa tisa, Polisi walivamia Hoteli aliyokuwa amefikia Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na wageni wengine pamoja na wenyeji wao.

Waliochukuliwa:
1. Freeman Mbowe
2. John Pambalu
3. John Heche
4. Rose Mayemba
5. Masenya(Mwenyekiti BAVICHA Ilemela)
6. Steven Odipo
7. Dr. Rwaitama
8. Seti (Dereva kanda ya Victoria)
9. Apollo (Afisa Habari Taifa)
10. Frank Novatus (CHASO)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benja (BAVICHA Kinondoni)

Mpaka sasa haijajulikana wamechukuliwa kwa kosa gani.

=====

My Take.
Uonevu, uvunjifu wa haki za kiraia, kutoheshimu katiba ya nchi unaendelea kwa kasi katika serikali ya Samia Suluhu Hassan.
Anyway, Aluta continua, uonevu huu utaisha oneday, dawa tutaipata tu.

Nimkumbusha Samia kuwa alikuwepo mtu katika nchi hii anaitwa Magufuli, tulimuita Chuma, Jiwe—Leo yuko wapi?

====

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Taarifa Kwa UMMA

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe..Freeman Mbowe alivamiwa na Jeshi la Polisi hotelini alipokuwa ( Kingdom Hotel) majira ya saa nane na nusu usiku na kumkamata pamoja na viongozi wengine waliokuwa naye.

Viongozi wengine walipelekwa Kituo cha Kati cha Polisi Mwanza,Ila Mwenyekiti Mbowe haijulikani alipelekwa wapi na mpaka Muda huu hakuna taarifa zozote za mahali alipo.
Waliokamatwa ni wafuatao;

1. Mhe .Freeman Mbow
2. Mhe.John Pambalu
3. Mhe. John Heche
4.Mhe. Rose mayemba
5. Masenya( Mwenyekiti Bavicha ilemela)
6. Steven Odipo
7.Dr. Azavel Lwaitama
8. Seti ( Dereva Kanda ya Victoria)
9. Apolinary Appolo (Afisa habari Taifa)
10. Frank Novatus (Chaso Mwanza)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benjamin Kambarage ( M.kiti Bavicha kinondoni)

Tunalitaka Jeshi la Polisi kujitokeza na kusema alipo Mwenyekiti wa Taifa na sababu za kumkamata zilikuwa nini.

Tunalaani ukandamizaji huu wa Haki za Watanzania Kwa nguvu zote , na hizi NI dalili za wazi kuwa Udikteta uliokuwepo enzi za utawala wa Rais Magufuli bado unaendelea .

Tutatoa taarifa kadiri ya Muda na jinsi tutakavyozipokea .

====

UPDATES:

=====

Jeshi la polisi mkoani Mwanza limefunga barabara ya Bwiru maarufu kona ya Bwiru jirani na ukumbi uliopangwa kufanyia kongamano la Chadema la kudai Katiba, hakuna kinachoendelea kwa sasa polisi wametanda barabara nzima wakiwa na magari na silaha za moto
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,251
2,000
Ndicho alichokuwa anataka, huko machama hata matanga hawajaanua yeye kigulu na njia
View attachment 1861742

View attachment 1861743

My Take.
Uonevu, uvunjifu wa haki za kiraia, kutoheshimu katiba ya nchi unaendelea kwa kasi katika serikali ya Samia Suluhu Hassan.
Anyway, Aluta continua, uonevu huu utaisha oneday, dawa tutaipata tu.

Nimkumbusha Samia kuwa alikuwepo mtu katika nchi hii anaitwa Magufuli, tulimuita Chuma, Jiwe—Leo yuko wapi?
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
7,224
2,000
View attachment 1861742

View attachment 1861743

My Take.
Uonevu, uvunjifu wa haki za kiraia, kutoheshimu katiba ya nchi unaendelea kwa kasi katika serikali ya Samia Suluhu Hassan.
Anyway, Aluta continua, uonevu huu utaisha oneday, dawa tutaipata tu.

Nimkumbusha Samia kuwa alikuwepo mtu katika nchi hii anaitwa Magufuli, tulimuita Chuma, Jiwe—Leo yuko wapi?
Sio uonevu,anaupiga mwingi..hamna adabu nyie mlianza kumtisha Rais,anawapa utaratibu msubirie mnstukana ,safi Sana ngoja aupige mwingi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom