Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,447
2,000
Chahali kama unadindisha rudi upambane hapa. Angalau CDM Mbowe yuko hapa, w ulikimbia kama Jike!
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
13,587
2,000
Mataga hamuoni hata aibu kuwa na cha kuongea kuhusu cdm Mbowe au Lissu?

Nini ambacho cdm, Mbowe au Lissu hawakukijua:


Kimya kingi? Mbona walisema kina mshindo mkuu? Wewe waona kimya?


Ninyi tulieni hapo hapo. Tuna ya muhimu zaidi kwanza.Kuna maneno ameyaandika "Bwana yule" siku ya leo yanafikirisha kidogo. Lakini ukiyatazama kwa undani haya maneno nadhani ndo kilichomkata nguvu Mange Kimambi kuendelea kushikamana na wanachadema katika the so called "Harakati wa kudai demokrasia Tz"

Bwana yule ameandika katika Twitter yake kama inavyosomeka hapo chini. Kiuhalisia Kigogo yupo 100% correct kuwa CDM wamemkataa mwenyekiti wao haraka sana.


Baada ya tafakuri nachelea kusema yuko sawa. Freeman Mbowe ni kama amesalitiwa na wenzake katika hili. Aliacha msiba kwenda Mwanza kwa ajili ya kuwapa nguvu wenzake pamoja na wale walioshikiliwa. Na walipoachiwa alisisitiza Kongamano litafanyika Mwanza na hawataondoka mpaka lifanyike. Hivi sasa kila mtu amerudi nyumbani kwake na wamegeuka "Keyboard warriors" kama sisi tu. Amebaki Mbowe gerezani na msimamo wake wa kubaki Mwanza mpaka kongamano lifanyike, kama kukamatwa wakamatwe tu.

Mkutano wa mbowe na Press walikubaliana kuwa mwanachadema yeyote akikamtwa kwa kubumba basi hawatamuwekea dhamna, watawasusia polisi mpaka waachiliwe huru. Ila waliokamatwa pamoja na Mbowe wameshadhaminiwa na wamerejea makwa wakiwa na familia zao nao wanatweet na kusoma JF kama sisi.

Ukweli uliopo moyoni mwa wengi ambao ni washirika wa Mbowe ni kuongea sana na kupiga kelele nyingi za ukakamavu "Ili Mwenyekiti awaone na kuwafikiria au kuwakumbuka wakati fursa mbalimbali zikijitokeza kama za nafasi za ugombea, teuzi n.k". Ndo maana kuna waongeaji wengi "vishandu" ambao tuliwaamini kama ni imara na wakahama kambi kwa hoja ya kuunga mkono juhudi ama CDM kudai wamenunuliwa. Hawakanunuliwa hao bali ni Wachumia matumbo

Mbowe amekamatwa na ndiye mwenyekiti kitaifa , ile mihemko wanayomdanganya nayo imefyata. Hakuna wembe wala tutaingia barabarani kudai sijui nini. Wanachadema ni majasiri wa majibizano lakini si majasiri wa vitendo. Bawacha wamefanya igizo lao jana na limekwisha nao wapo na sisi kwenye Keyboards. Hakuna real Movement ya kuonesha kweli wameguswa na hawakubali mwenyekiti wao kufanywa hivi. CHADEMA WAMEMSALITI MWENYEKITI WAO KWEUPE.
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
4,063
2,000
Mbowe alijua kuwa atakamatwa na kuunganishwa na wenzake ktk kesi ya Ugaidi case no.63/2020, kesi hii ilikuwepo na wasaidizi wa chadema ni miongoni mwa watuhumiwa wa ugaidi.

Viongozi wenzake hawakumsaliti kwa sababu wanafahamu jambo lolote likiwa mbele ya mahakama hakuna jinsi zaidi ya kupambana kisheria na sio kuendelea kuvunja sheria kama walivyo fanya Bawacha.

huwezi kushinikinza taratibu za kisheria kwa maandamano au kukaidi ktk nchi inayo fuata utawala wa sheria, Mbowe kapelekwa mahakamani na hatua zingine za kisheria zitafuatwa.

viongozi wenzanke hawajamsaliti bali wanaheshimu Utawala wa kisheria.

unataka waikemee na kuilazimisha mahakama wamtoe Mbowe?! kweli hilo limekaa sawa? hapana.
 

ProMagufuli

Senior Member
Apr 6, 2021
139
250
Kuna maneno ameyaandika "Bwana yule" siku ya leo yanafikirisha kidogo. Lakini ukiyatazama kwa undani haya maneno nadhani ndo kilichomkata nguvu Mange Kimambi kuendelea kushikamana na wanachadema katika the so called "Harakati wa kudai demokrasia Tz"....
Ukiacha hayo tu.
Kitendo cha Mwenyekiti kukamatwa halafu hakuna hata alieumizwa kilinishangaza.

Nikasema tuna safari ndefu bado.
 

Mamserenger

JF-Expert Member
Oct 14, 2019
664
1,000
Ngangari walikutana na NGUNGURI...

Ukitaka uwajue WATANZANIA waangalie kwenye yafuatayo:

1)Mathalani umaarufu wa MZEE MPILI na NGUVU YA KIUSHAWISHI ya askofu Gwajima

2)Huku mitaani bado wanabishania ile CHANJO aliyowepa Rais wetu msikivu mh.SSH...wako wanaosema amechomwa sindano ya TETANUS

3)Huku vijiwe vya kahawa wako wanaobishana kuwa leo MO DEWJI hakuweka hizo B.20

Hii inatoa taswira gani?!!!

WATANZANIA NI WATU WATULIVU WASIOPENDA SIASA ZA VURUGU NA MIVITANO ISIYO MAANA "tug of war"......

UTULIVU wao unaweza kuuita UJINGA...ila ndiyo salama yao....

Chadema hawatofanikiwa kwa SIASA ZAO ZA KUTAKA "REGIME CHANGE through endless strikes"...

Kuna MKENYA mmoja amepost humu JF akitukebehi kuwa "eti nchi yetu ina 3.3 skilled labour out of 60 million"

Amesahau kuwa NIGERIA ina unskilled labour 21.4....bado haijawasaidia kuinua UCHUMI WA WALALAHOI....bado haijawazuia MEND na BOKO HARAM kufanya yao....

Tanzania litabaki taifa la KIPEKEE...KIPEKEE KABISA....

"Ujinga tunaotaniwa nao" ndio USALAMA WETU wa kunywa kahawa kwa kujiachia huku mitaani.....


#SiempreTanzania
#SiempreCCM
#NchiKwanzaKablaYaNafsiZetu
#SerikaliMbiliMilele
Facts na ujue kucheza na Akili ya mtanzania.

Na hii kwa uchunguzi wangu umetokana kuwa Dar ndo jiji lenye Taswira ya Tanzania.
Hivyo wenyeji wa Dar ni hasa watu wa Pwani watu hawa sio wakorofi wapenda mapenzi na Ghahawa mtu kama huyu hiweziwambia andamane wala aburuzane na Police.

Asantee Tanzania asante Nchi yangu

Nakupenda Tanzania.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
9,361
2,000
Facts na ujue kucheza na Akili ya mtanzania.

Na hii kwa uchunguzi wangu umetokana kuwa Dar ndo jiji lenye Taswira ya Tanzania.
Hivyo wenyeji wa Dar ni hasa watu wa Pwani watu hawa sio wakorofi wapenda mapenzi na Ghahawa mtu kama huyu hiweziwambia andamane wala aburuzane na Police.

Asantee Tanzania asante Nchi yangu

Nakupenda Tanzania.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
🤣🤣
Mkuu wangu eee...
Komredi eee...karibu kijiweni kwangu Majohe unywe kahawa na Al Kasus mujarabu.....

Siye hatuna tabu....

Wateja wangu wanakunywa kahawa na vijana wenzangu "kubeti" katika masimu yao makubwa.....

#AmaniKwanza
#UtulivuKwanza
#HatunaNchiNyingineZaidiYaTanzania
#KaziIendelee
 

tobiasi

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
524
500
Watawala wamezidiwa nguvu za HOJA kukabiliana na Chadema.CCM haiwezi kukabiliana na Chadema kwenye uwanja wa siasa sawa.Freeman Mbowe ndiye MHIMILI wa siasa za upinzani.Ni jabali la siasa za Tanzania.Bila nguvu za dola kukabiliana na Mbowe na chama chake,CCM tungeshaisahau.

Kwa hiyo, kunahitajika umakini mkubwa katika maamuzi yao kipindi hiki ambacho mwenyekiti wao yupo gerezani.Hapa ndipo Chadema inapopaswa kuonysha kuwa Chadema ni Taasisi .Ukimya wao umekuwa mzuri mno maana umewapa nafasi ya kutafakari zaidi namna bora ya kupata ufumbuzi.Mbowe ni mtu imara na jasiri.ATAVUKA SALAMA na ataushangaza ulimwengu.
Nawapongeza Chadema kwa utulivu wao.Kesho siyo mbali.Tusubiri.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,586
2,000
Ndiyo aina ya Watanzania ambao wana ufinyu mkubwa wa kupambanua mambo. Wao kuteswa na kubambikiwa kesi FEKI Viongozi na Wanachama wa Chadema ni shangwe na furaha kubwa, ngoja wabambikiwe kesi FEKI wao.
Una usalama gani, unafiki tu!
 

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
1,522
2,000
Hajasalitiwa bali anatetea wapumbavu ambao ni watanzania

BARUA YA WAZI KWA TUNDU LISU

Na, Robert Heriel
Taikon wa Fasihi,
S.L.P 9977, JIBI,
Kutoka Nyota ya Tibeli.
30, 07. 2020.

YAH: KUKUONYA DHIDI YA KUTETEA MASIKINI NA WAPUMBAVU.

Ndugu Mhe Lisu, Kichwa cha habari hapo juu cha husika.

Ninafuraha kubwa kukuandikia barua hii ya wazi ambapo najua watu wengi wataisoma nawe itakufikia. Utanisamehe ikiwa njia hii niliyoitumia pengine isikufurahishe lakini ni katika hali ya kukupa ujumbe wenye manufaa wewe na wale wote wenye tabia kama zako, mimi nikiwa mmoja wao.

Mhe. Lisu, nimekufuatilia kwa miaka saba sasa, sisemi nakufahamu lakini angalau ninachakusema kidogo kukuhusu. Umejipambanua kama mtu apendaye haki, mtu apendaye utawala wa sheria, mtu apendaye demokrasia. Lisu umekuwa mstari wa mbele kukemea maonevu uyaonayo ndani ya nchi yako, umejigeuza kama msemaji wa wanaoonewa, kutetea wanyonge wanaonyimwa haki zao. Upo sawa, lakini umekosea jambo moja; nalo ni kushindwa kujua unatetea watu wa aina gani. Hilo ndilo kosa lako kuu.

Huwezi tetea haki za masikini ukabaki salama, huwezi tetea haki za wapumbavu ukabaki salama. Huwezi tetea watu wasiojielewa, huwezi tetea watu wasiojua unapigania nini kwao, huko ni kujitafutia matatizo makubwa ambayo hao unaowatetea hawatakusaidia kitu kwa sababu wao ni wapumbavu na masikini.

Kikawaida masikini ni watu wasiojithamini, watu wasio na shukrani, watu wasiojitambua, wengi wao ni wachawi, wanga, watu wasio na fadhila, masikini ukimsaidia huyo huyo ndio atakuja kukusema unajidai, ukimtetea masikini au mpumbavu huyo huyo ndio atakuambia unakihere here. Kamwe nakusihi acha mara moja kuhangaika na masikini.

Masikini unachoweza kuwasaidia ni kuwadhulumu hata kile kidogo walichonacho, kuwabagua, kuwatenga, kuwadharau, hicho ndicho wakipendacho masikini. Lakini ukijifanya unawapenda, unawajali nakuhakikishia unajiingiza mkenge, utaumia, utasagika na hakika utamalizika.

Nikukumbushe Ndugu Mhe. Lisu, hakuna aliyewahi kuwatetea masikini, na kuwapigania masikini akabaki salama. Wote waliojiingiza katika harakati hizo walikufa vifo vibaya, wengine walipewa adhabu kali za kuliwa na mamba, kuliwa na simba, kuchomwa moto, wakapotea na kuangamia.

Katika Dini, wapo Manabii walikuja kutetea haki za wanyonge, haki za masikini lakini wote waliuawa, tena wakazomewa na hao hao masikini. Nakupa mifano ya watu katika dini waliokuwa wanaharakati kama wewe, Musa, ndiye yule Mlawi aliyewatoa waisrael Misri, naye aliwapigania watumwa wale na kutaka kuwa uhuru wao. walichomlipa wote tunajua, walianza kulalamika kuwa bora warudishwe utumwani Misri kuliko kuwa huru Kanaani katika nchi yao. Mungu alitaka kuwaua lakini Kihere here cha Musa akawatetea, siku zilizofuata wakataka kumuua Musa wasijue huyo ndiye aliwatetea wasiuawe na Mungu. Musa alipowashtaki kwa Mungu, Mungu akamuambia, wewe si uliwatetea hao masikini, watumwa, wapumbavu wasiojielewa. Acha wakuue ili uwe na akili. Musa akabaki katumbua macho. Biblia inasema, Mungu aliwafyeka wote njiani, akambakiza Joshua na Kalebu. Huwezi kukomboa masikini, huwezi komboa watumwa, huwezi komboa wapumbavu ukabaki salama. Kuwatetea wapumbavu ni kutaka kutofika kanaani, usishangae kwa nini Musa hakufika Kanaani, aliwaendekeza wapumbavu wale.

Yesu naye walimuua, wakamsulubisha, na kumtemea mate. Na wale aliokuwa anawatetea ndio hao hao waliomtukana, walioimba asulubiwe. Huwezi Mkomboa masikini hata siku moja. Huwezi komboa mtu mpumbavu ukasalimika.

Hata kwenye maisha ya kawaida, wale unaowasaidia ndio hao hao watakaogeuka maadui zako. Hao hao ndio watakao kuteta.

Mhe Lisu, naomba nikuonye, na ikikupendeza fuata ushauri wangu. Acha kutetea haki za wapumbavu, haki za masikini, haki za wanyonge sijui upuuzi gani. Mungu mwenyewe atahangaika na watu wake. Ikiwa yeye kaacha watu waonewe wewe unakuja kuwatetea huoni unatafuta maneno.

Masikini ni kama swala au digidigi mbugani, huwezi mgeuza digidigi akawa simba alafu ukabaki salama. Ili mbuga iwe na amani ni lazima swala aliwe, kumtetea swala ni kuchafua amani ya mbugani.

Nature inataka dunia iende hivyo, wote waliojifanya kutetea tabaka la chini walipotezwa, na uhakika ni kuwa watazidi kupotezwa.

Nakushauri; tetea watu wenye akili, watu matajiri, watu wenye nguvu, hao utapata ulinzi, hao hawana unafiki, hao utapata cheo, na utaishi kwa amani.

Matajiri ukiwatetea wanajua thamani ya kile unachokifanya, hivyo nawe watakutetea siku yakikukuta yako. Lakini masikini ukiwatetea kwanza wao wenyewe hawajui thamani yao iweje wajue thamani ya kile ukifanyacho, zaidi sana watakutelekeza siku yakikupata kisha watakuambia ulikuwa unakihere here.

Watu wenye akili ukiwatetea watakulinda, kwa maana wanajali kile ukifanyacho, watakulipa hisani na fadhila. Lakini wapumbavu ukiwatetea hao hao watakuwa wakwanza kukusnitch na kukuuza kwa bei ya kutupwa, mwisho utauawa na kuangamizwa.

Wenye nguvu ukipendekeza kwao, watakulinda. Wao wanajua na kuthamini mchango wako kwao. Lakini sio kwa watu wanyonge na fukara. Wanyonge wataishia kukusengenya na kukuloga, ukiwa mbele yao wanakushangilia ukitoka wanakusema. Wataachaje kukusema ikiwa hawana kazi, kazi yao ni kusengenya watu vijiweni.

Mhe. Lisu, acha kupoteza muda wako. Hutapata zawadi popote pale iwe huku duniani au kwa yule aliyeiumba hii dunia.

Aliyeumba hii dunia ndiye anataka dunia iwe hivi ilivyo, wapumbavu wahenyeke, wenye hekima wale bata. Masikini wachapike, matajiri wale upepo mwanana.

Namna bora ya kumsaidia masikini ni kumdhulumu na kumuonea. Namna bora ya kumsaidia mpumbavu ni kumfundisha upumbavu,.

Kufikia hapa Mhe, Lisu niseme ni matumaini yangu barua hii utakuwa umeielewa. Na utaifanyia kazi.

Wako katika majukumu

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
robertheriel99@gmail.com

Nakala moja kwa

1. Tundu Anthipas Lisu
2. Wanaharakati wote
3. Wanamageuzi

Nakala nyingine nitabaki nayo.
wewe kijana ni mpumbavu,tena kijana uwe na adabu.yaani unawasaminisha watanzania wote na Yule mtuhumiwa wa ugaidi!?. enzi za nyerere ungewekwa ndani na bakora za makalio za kutosha !
 

Terrible Teen

JF-Expert Member
May 1, 2017
803
1,000
Katika nyakati za karibuni huyu Kigogo2014 alitumiwa na Chadema kama msemaji wao kwa kutukana viongozi wengine wa upinzani kama wasiofaa na kuwa chama cha upinzani kilichopo ni chadema tu.

Kigogo2014 akaonekana ndio mtu wa maana kuliko hata wanachedema wakongwe. Ila kwa tunaojua huyu bwana hana lolote la maana hasa baada ya waliokuwa wakimpa taarifa wakati wa JPM kuondolewa maeneo yao ya kazi.

Alipokosa ajenda ndio akajifanya kuipenda sana chadema ili abaki kuwa relevant kwenye mitandao. Leo baada ya Mbowe kuwekwa kizuizini anawatukana sana chadema kuwa wamekaa kimya hawafanyi lolote kuhusu mbowe. Hivi alitaka wafanyaje labda katika mazingira tulionayo.

Hili liwe funzo kwa wanasiasa kushabikia hustlers wa mitandao kama kigogo asiyekuwa na ajenda na anayetaka kuwa juu ya kichwa cha kila mtu. Amewatukana sana akina zito, lipumba na mbatia mkakaa kimya. Leo anawatukana chadema wote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom