BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Kufuatia kuwepo kwa taarifa za kubuniwa kifaa maalum cha kupima vipaji vya watoto shuleni na moja ya shule jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda ametangaza kusitishwa kwa matumizi ya kifaa hicho kwa muda hadi hapo serikali itakapojiridhisha juu ya ubora na usalama wa kifaa hicho kwa wanafunzi.

Waziri Prof Mkenda amesema hayo jijini Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ugunduzi wa kifaa hicho, na kusema wamekuwa na maswali ambayo hayajapatiwa majibu yanayoridhisha juu ya kifaa hicho, ikiwemo ubora, usalama na ulinzi wa taarifa za watoto ambazo nyingine zinaweza kuwa ni za faragha.

Ameagiza timu ya wataalam kufanya ukaguzi wa ubora na usalama wa kifaa hicho na ikiwa watajiridisha kuwa ni salama, michakato mingine ya kukiridhia itafuata.

Chanzo: Azam TV

----

Serikali imewaagiza Wakaguzi wa Shule kuchunguza taarifa za baadhi ya Shule Binafsi kutumia Mashine za Anthropo-Biometric zenye uwezo wa kubaini Uwezo wa Akili au Vipaji vya Wanafunzi

Waziri wa Elimu na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, amewambia wakaguzi hao; "Lazima ujue jinsi kifaa hicho kinadaiwa kuwa na uwezo wa kuchanganua wanafunzi na kubaini vipaji vyao katika utendaji wa ubongo," alisema.

Machi 4, 2023, Shule ya Sekondari Alfa iliyopo Jijini Dar es Salaam ilitangaza kuzindua Mfumo wa Kupima Vipaji vya Watoto kwa kutumia kifaa kinachoitwa Anthropo-Biometric Body Machines, ambacho kwa mujibu wa Mwalimu wa Taaluma wa Shule hiyo, Fulgence Kabiligi alisema kifaa hicho kinachukua Vinasaba vya Kibaolojia Mwanafunzi na kuvituma Geneva ambako vinakwenda kuchakatwa.

Serikali imewaagiza Wakaguzi wa Shule kuchunguza taarifa za baadhi ya Shule Binafsi kutumia Mashine za Anthropo-Biometric zenye uwezo wa kubaini Uwezo wa Akili au Vipaji vya Wanafunzi.

Waziri wa Elimu na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, amewambia wakaguzi hao; "Lazima ujue jinsi kifaa hicho kinadaiwa kuwa na uwezo wa kuchanganua wanafunzi na kubaini vipaji vyao katika utendaji wa ubongo. Ninaelewa kuwa walidai pia kufanya kazi na Hospitali ya Taifa Muhimbili, lakini hili nalo linahitaji kuchunguzwa," alisema Prof Mkenda.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya Mashine hizo, Justine Daniel, amesema Anthropo-Biometriska kawaida ni mfumo wa upimaji wa njia ya 3D ambao una uwezo wa kutoa nakala ya dijiti ya jiometri ya uso wa mwili wa mwanadamu.

“Mashine haiendi zaidi ya ramani ya kimwili ya mwili; mashine zenye sura tatu za Anthropo-Biometric Body hunasa tu uso wa nje wa mwili wa binadamu kwa kutumia mbinu za macho, pamoja na vifaa vinavyoweza kuhisi mwanga, bila kugusa mwili,” amesema Daniel.

Machi 4, 2023, Shule ya Sekondari Alfa iliyopo Jijini Dar es Salaam ilitangaza kuzindua Mfumo wa Kupima Vipaji vya Watoto kwa kutumia kifaa kinachoitwa Anthropo-Biometric Body Machines, ambacho kwa mujibu wa Mwlaimu wa Taaluma wa Shule hiyo, Fulgence Kabiligi alisema kifaa hicho kinachukua Vinasaba vya Mwanafunzi na kuvituma Geneva ambako vinakwenda kuchakatwa.
 
Machi 4, 2023, Shule ya Sekondari Alfa iliyopo Jijini Dar es Salaam ilitangaza kuzindua Mfumo wa Kupima Vipaji vya Watoto kwa kutumia kifaa kinachoitwa Anthropo-Biometric Body Machines, ambacho kwa mujibu wa Mwlaimu wa Taaluma wa Shule hiyo, Fulgence Kabiligi alisema kifaa hicho kinachukua Vinasaba vya Kibaolojia Mwanafunzi na kuvituma Geneva ambako vinakwenda kuchakatwa

Serikali imewaagiza Wakaguzi wa Shule kuchunguza taarifa za baadhi ya Shule Binafsi kutumia Mashine za Anthropo-Biometric zenye uwezo wa kubaini Uwezo wa Akili au Vipaji vya Wanafunzi

Waziri wa Elimu na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, amewambia wakaguzi hao; "Lazima ujue jinsi kifaa hicho kinadaiwa kuwa na uwezo wa kuchanganua wanafunzi na kubaini vipaji vyao katika utendaji wa ubongo. Ninaelewa kuwa walidai pia kufanya kazi na Hospitali ya Taifa Muhimbili, lakini hili nalo linahitaji kuchunguzwa," alisema Prof Mkenda

Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya Mashine hizo, Justine Daniel, amesema Anthropo-Biometriska kawaida ni mfumo wa upimaji wa njia ya 3D ambao una uwezo wa kutoa nakala ya dijiti ya jiometri ya uso wa mwili wa mwanadamu.

“Mashine haiendi zaidi ya ramani ya kimwili ya mwili; mashine zenye sura tatu za Anthropo-Biometric Body hunasa tu uso wa nje wa mwili wa binadamu kwa kutumia mbinu za macho, pamoja na vifaa vinavyoweza kuhisi mwanga, bila kugusa mwili,” amesema Daniel

Machi 4, 2023, Shule ya Sekondari Alfa iliyopo Jijini Dar es Salaam ilitangaza kuzindua Mfumo wa Kupima Vipaji vya Watoto kwa kutumia kifaa kinachoitwa Anthropo-Biometric Body Machines, ambacho kwa mujibu wa Mwlaimu wa Taaluma wa Shule hiyo, Fulgence Kabiligi alisema kifaa hicho kinachukua Vinasaba vya Mwanafunzi na kuvituma Geneva ambako vinakwenda kuchakatwa
Mhh mambo ya kupeleka geneva tena ?? Usalama wa mwanangu utakuaje baada ya majibu?
 
Kufuatia kuwepo kwa taarifa za kubuniwa kifaa maalum cha kupima vipaji vya watoto shuleni na moja ya shule jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda ametangaza kusitishwa kwa matumizi ya kifaa hicho kwa muda hadi hapo serikali itakapojiridhisha juu ya ubora na usalama wa kifaa hicho kwa wanafunzi.

Waziri Prof Mkenda amesema hayo jijini Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ugunduzi wa kifaa hicho, na kusema wamekuwa na maswali ambayo hayajapatiwa majibu yanayoridhisha juu ya kifaa hicho, ikiwemo ubora, usalama na ulinzi wa taarifa za watoto ambazo nyingine zinaweza kuwa ni za faragha.

Ameagiza timu ya wataalam kufanya ukaguzi wa ubora na usalama wa kifaa hicho na ikiwa watajiridisha kuwa ni salama, michakato mingine ya kukiridhia itafuata.

Chanzo: Azam TV

===============

TAARIFA YENYEWE ILIVYOKUWA AWALI MACHI 25, 2023

Mfumo kupima vipaji vya watoto wazinduliwa

Kwa mara ya kwanza nchini mfumo wa kupima vipaji kwa watoto umezinduliwa rasmi katika Shule ya Sekondari ya Alpha iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mfumo huo utahusika kupima vipaji vya watoto kidijitali, ili kuweza kusaidia watoto kuelekezwa katika vipaji vyao na kuvitumikia ipasavyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo mjumbe wa vipaji barani Afrika maarufu kutoka Kenya, Patrice Lumumba amesema watasambaza ujumbe huo mzuri kuwa shule za Alpha ndio zimechaguliwa kuwa kitovu anzilishi kuwa na mfumo huo mpya, ambao utakuwa na manufaa kwa vijana wa kitanzania wa kike na kiume na Afrika pia.

Prof Lumumba ameeleza kuwa kupitia mfumo huo vijana watakaotambulika vipaji vyao watawezeshwa ili mafanikio yao yasikwazwe bali yapewa rutuba.

“Kupitia mfumo huo mtoto atapimwa kipaji chake na kusaidiwa kutumia vizuri kwani kila mtu ana kipaji ila wengine hawajui hivyo hawataweza kutumia ipasavyo kwa kuwa teknolojia sasa ndio kitu muhimu Duniani,”amesisitiza Prof Lumumba.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Alpha Sekondari, James Kabirigi amesema shule hiyo imejikita kugundua vipaji mapema kabla ya mashine hiyo kwa kuanzisha klabu 21 na kufundisha jinsi ya kuwa wajasiriamali.

“Hii mashine ni Watanzania wote kwa hiyo tupo wa aina nyingi wenye uwezo mkubwa,mdogo na amboa hawana watatafutiwa utaratibu,” amesema.
Mfumo-newe7b4c45c80fb-1024x768.jpg

Amesema manufaa yake inamsaidia kupima kipaji na kukijua na kuendelezwa katika shule ya kipaji husika na kusoma kwa haraka na muda mfupi, ili kuweza kutumia kipaji chake.

“Mtoto anapimwa kwa mwanasaikolojia kuchukua historia yake , asili na anapendelea nini baadae anaingia kwenye mashine inachukua vinasaba na wanatoa michoro ambayo inatumwa mtandaoni Geneva wao wanasoma na kurudisha majibu ndani ya dakika chache,”ameeleza Kabarigi.
mfumo-new-vipajie74c86cff1ce-1024x768.jpg

Amefafanua kuwa watakuwa na kliniki zitakazoendeleza vipaji na pia vyuo na watashirikiana na shirikisho la vipaji duniani na katika kupima wakigundua duniani vipaji hivyo ni vichache atachukuliwa kwenda nje kuendelezwa.
 
wamejua watoto wakimaskini ndo wenye vipaji kuliko watoto wao saa wameona watazalisha wakina daimond na harmonize wengi nchini
 
Hii kali kuna kifaa chenye uwezo wa kupima intelligence ya wanafunzi.

Only in Tanzania
 
Taifa lililofeli, mpaka kupima intelligence ya wanafunzi tunahitaji kifaa cha mchina!.

Ndio maana kila kitu kinatushinda, bandari, bunge bovu, serikali mbovu, mahakama mbovu, hatuwezi kuendesha chochote.
 
Serikali imewaagiza Wakaguzi wa Shule kuchunguza taarifa za baadhi ya Shule Binafsi kutumia Mashine za Anthropo-Biometric zenye uwezo wa kubaini Uwezo wa Akili au Vipaji vya Wanafunzi

Waziri wa Elimu na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, amewambia wakaguzi hao; "Lazima ujue jinsi kifaa hicho kinadaiwa kuwa na uwezo wa kuchanganua wanafunzi na kubaini vipaji vyao katika utendaji wa ubongo," alisema.

Machi 4, 2023, Shule ya Sekondari Alfa iliyopo Jijini Dar es Salaam ilitangaza kuzindua Mfumo wa Kupima Vipaji vya Watoto kwa kutumia kifaa kinachoitwa Anthropo-Biometric Body Machines, ambacho kwa mujibu wa Mwalimu wa Taaluma wa Shule hiyo, Fulgence Kabiligi alisema kifaa hicho kinachukua Vinasaba vya Kibaolojia Mwanafunzi na kuvituma Geneva ambako vinakwenda kuchakatwa.

Serikali imewaagiza Wakaguzi wa Shule kuchunguza taarifa za baadhi ya Shule Binafsi kutumia Mashine za Anthropo-Biometric zenye uwezo wa kubaini Uwezo wa Akili au Vipaji vya Wanafunzi.

Waziri wa Elimu na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, amewambia wakaguzi hao; "Lazima ujue jinsi kifaa hicho kinadaiwa kuwa na uwezo wa kuchanganua wanafunzi na kubaini vipaji vyao katika utendaji wa ubongo. Ninaelewa kuwa walidai pia kufanya kazi na Hospitali ya Taifa Muhimbili, lakini hili nalo linahitaji kuchunguzwa," alisema Prof Mkenda.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya Mashine hizo, Justine Daniel, amesema Anthropo-Biometriska kawaida ni mfumo wa upimaji wa njia ya 3D ambao una uwezo wa kutoa nakala ya dijiti ya jiometri ya uso wa mwili wa mwanadamu.

“Mashine haiendi zaidi ya ramani ya kimwili ya mwili; mashine zenye sura tatu za Anthropo-Biometric Body hunasa tu uso wa nje wa mwili wa binadamu kwa kutumia mbinu za macho, pamoja na vifaa vinavyoweza kuhisi mwanga, bila kugusa mwili,” amesema Daniel.

Machi 4, 2023, Shule ya Sekondari Alfa iliyopo Jijini Dar es Salaam ilitangaza kuzindua Mfumo wa Kupima Vipaji vya Watoto kwa kutumia kifaa kinachoitwa Anthropo-Biometric Body Machines, ambacho kwa mujibu wa Mwlaimu wa Taaluma wa Shule hiyo, Fulgence Kabiligi alisema kifaa hicho kinachukua Vinasaba vya Mwanafunzi na kuvituma Geneva ambako vinakwenda kuchakatwa.
Wakina Michael Jackson wakina Whitney Huston walipimwa na hizo mashine? Vipi wakina Thomas Edson, na vipi Mark Zuckerberg? Vipi Elon Musk alipimwa na hizo mashine?
 
Back
Top Bottom