Serikali: Mfumuko wa Bei za Vyakula na Vinywaji bado ni Himilivu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imetabiri kwamba mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi unatarajiwa kupungua kwa asilimia moja katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huu.

Pia imesema mfumuko wa bei kwa ujumla unahimilika kwa kuwa bado uko kwenye tarakimu moja.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk. Albina Chuwa, alisema hayo jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifungua kikao kazi cha waandishi wa habari, ofisi ya takwimu na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Alisema ofisi hiyo imefanya maoteo ya mwenendo wa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Januari hadi Machi, ili kuisaidia serikali kufanya uamuzi wa kisera wenye vigezo vya takwimu.

“Maoteo hayo yanaonyesha mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi utaendelea kupungua kutoka asilimia 9.7 Desemba, mwaka jana, hadi asilimia 8.4 Machi, 2023,” alisema.

“Tanzania itaendelea kuwa na mfumuko wa bei stahimilivu ndani ya kipindi cha robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2023. Hadi kufikia Machi, baadhi ya maeneo nchini yatakuwa yameanza mavuno ya mazao, hivyo kupunguza shinikizo la bei lililoko sokoni,” alisisitiza.

Dk. Chuwa alisema mikakati ya serikali ya kudhibiti upandaji wa nishati kama mafuta kutaendelea kupunguza gharama za uzalishaji na usafirishaji pamoja na kutoa ruzuku kwenye pembejeo za kilimo kutaongeza uzalishaji wa nafaka.

Kuhusu mfumuko wa bei wa nchi mwaka jana, Dk. Chuwa alisema hadi Desemba ulikuwa asilimia 4.8.

“Bado Tanzania inafanya vizuri kwa upande wa udhibiti wa bei za bidhaa na huduma za jamii,” alisema.

Takwimu zinaonyesha kuwa nchini Uganda, mfumuko wa bei mwaka jana ulikuwa asilimia 7.2 na Kenya asilimia 7.7 wakati nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ni kati ya asilimia tatu hadi 7.0.

Utabiri wa NBS unakuja siku moja baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru, kutaja maeneo manne yatakayoisaidia Tanzania kukabiliana na mfumuko wa bei na kuleta unafuu ili nchi isiathirike zaidi kiuchumi.

Aidha, alisema mfumuko wa bei utaendelea kushuhudiwa kwa kuwa mitambo na mafuta ni bidhaa zinazonunuliwa kwenye mataifa makubwa ambayo yameathiriwa na mfumuko wa bei.

Alisema serikali inafanya jitihada, ili kuhakikisha nchi haikumbwi na uhaba wa chakula.

NIPASHE
 
No research no right to speak...nawasubiri wapika data na watengeneza takwimu.
 
Mnatengeneza porojo ofisini mnakuja kuwasomea watu wanaoishi mitaani. Bora mngepika takwimu za pato la Taifa lakini hili la bei ya vyakula tunavyonunua wenyewe acheni uongo.
 
Huyu yuko sawa kweli

Himilivu labda kwake na wenzie huko

Ila raia/mwananchi ndiyo anapata maumivu

Ova
 
Hii inaitwa statisticious corruption unawadanganya kwa takwimu ambazo uanaamini kuwa unalindwa na sheria na huyo unayemwambia unaamini hawezi kuleta takwimu tofauti na hizo na sheria ya takwimu inambana. Lakini mtu huyoo anaishi uhalisia wa maisha na hizo takwimu anaona mauza uza tu! mfmuko wa bei unaumiza; himilivu nani anahimili sasa serikali au mlalahoi>?
 
Bahati ni kwamba itafika siku ataondoka kwenye hicho kiti aje mtaani kujionea huo uhimilivu!
 
wakati wa Samia tsh 108000 inanunua kg 10 za mchele kwa tsh35000 kg 10 za maharage kwa tsh40000 na mafuta ya alizeti Lita 5 kwa tsh33000

pesa hiyo hiyo wakati wa Magufuli kg 10 za mchele ni tsh 11000 Lita 5 za mafuta ya alizeti ni tsh 17000 maharage kg10 tsh 20000

kwa hiyo kwa Magufuli kwenye 108000 unarudishiwa tsh 60000
Magufuli alikuwa genius sa
Ngoja waje
 
wakati wa Samia tsh 108000 inanunua kg 10 za mchele kwa tsh35000 kg 10 za maharage kwa tsh40000 na mafuta ya alizeti Lita 5 kwa tsh33000

pesa hiyo hiyo wakati wa Magufuli kg 10 za mchele ni tsh 11000 Lita 5 za mafuta ya alizeti ni tsh 17000 maharage kg10 tsh 20000

kwa hiyo kwa Magufuli kwenye 108000 unarudishiwa tsh 60000
Magufuli alikuwa genius sa
Vs kwa kikwete usisahau
 
Lete ya Kikwete vs Magu Sukari
Mafuta ya kupikia, nauli za mabasi na daladala, vifaa vya stationery, n.k.
Watu wanajisahaulisha kama vile maisha yalikuwa rahisi sana kipindi cha JPM. Yaani ni kama alisolve kila kitu.
 
Back
Top Bottom