Mfumuko wa bei

Wakukaya2

Member
Apr 26, 2023
75
87
Habarini wana jamii wenzangu,

Tangu muda mrefu kumekuwapo na mjadala mrefu juu ya mfumuko wa bei, hasa kwa bidhaa za chakula. Wachambuzi wengi wamekuwa wakilaani jambo hili, hasa ndugu zetu waishio maeneo ya mjini.

Sasa mimi naomba kuelimishwa, kwani kila mfumuko wa bei ni hatari katika uchumi? Mbona Mimi naona kama huu mfumuko wa bei, hasa kwenye hizi bidhaa za chakula huku kijijini kwetu kama zinasisimua zaidi watu kulima. Maana baada ya kupanda bei ya vyakula mwaka huu mashamba ya mahindi yamekuwa mengi, kila shamba la mikorosho watu wamepiga matuta na kupanda mahindi.

Na kama factor nyingine hazitatokea, mbona naona kwa Kasi hii wafanya biashara wa mahindi watamtafuta wakumuuzia, maana asilimia kubwa ya watu watakuwa wamezalisha zaidi ya nusu ya mahitaji Yao. Sasa naomba munipe darasa, kwani kila mfumuko wa bei ni hatari kwenye uchumi, au Kuna namna fulani mfumuko wa bei una stimulate production?
 
Swali zuri.

Mfumuko wa bei (inflation), ni mfumuko wa level ya bei za bidhaa na huduma kiujumla, si kitu kibaya, ukiwa kwa kiwango kinachotakiwa unachangamsha uchumi kwa kuwapa motisha wazalishaji kama ulivyosema katika swali.

Ukweli ni kwamba kukiwa hakuna ongezeko la bei kabisa, au level ya bei kuwa zinashuka kutokana na nguvu za urari wa soko, demand and supply, (deflation, not to be confused with disinflation), jambo hilo hufanya watu wakose motisha ya kuzalisha. Kitu hiki kilitokea Japan muda fulani, mpaka kukawa na negative interest rates, yani benki kuu ya Japan il8kuwa inalipa benki za ndani riba benki zikichukua mkopo, badala ya benki za ndani Japan kuilipa benki kuu riba, benki kuu ililipa benki zingine riba (-0.1% by January 2016), hizi zilikuwa jitihada za kuongeza hela katika uchumi na kuchochea ongezeko la bei ili kuongeza motisha ya kuzalisha.

Hivyo, kiujumla ongezeko la bei si kitu kibaya.

Tatizo linakuja unapokuwa na mfumuko wa bei unaopanda kwa kasi, kiingereza wanaita galloping inflation, ambayo inakuwa 10% au zaidi, hapo sasa hata ile faida ya kuwapa watu motisha ya kuzalisha inamezwa na ukweli kwamba, hata hao watakaozalisha watakabikiwa na mfumuko wa bei. Kwa mfano, unaweza kusema mfumuko wa bei utakuwa unaleta motisha kwa wakulima kulima mazao ya vyakula, wapate faida kubwa kutokana na ongezeko la bei za vyakula, lakini unaweza kujuta faida watakayopata inaenda kufidia ongezeko la bei za mbolea, pembejeo, madawa, uhifadhi na usafirishaji, kufanya mkulima akose faida, au hata kuingia hasara kabisa.

Kwa hiyo, kifupi, mfumuko wa bei ukiwa katika kiwango sawia unatakuwa na unatoa motisha kwa wazalishaji kuendelea kuzalisha, kwa sababu wazalishaji wakijua bei zinashuka wataacha kuzalisha, lakini mfumuko huo ukiwa mkubwa sana, hususan zaidi ya 10%, unafanya bei za bidhaa na huduma nyingi zipande, kiasi za gharama za uzalishaji kupanda na kumfanya mzalishaji arudishe gharama za uzalishaji bila faida (break even), au hata kuingia hasara.
 
Mfumuko wa bei kwa muda mfupi unaweza kuwa na faida kwa wauzaji ila kwa muda mrefu ni maumivu kwa wanunuzi na wachuuzi kwasababu kila ongezeko la bei linapunguza akiba au niseme kwa case ya Tanzania ambapo watu hawaishi kwa akiba zao kwa idadi kubwa tunasema inawaumiza kwa kuongeza gharama za matumizi kuwa juu.

Nitakupa mfano hai. Chukulia familia ya idadi ya watu watano ambao wanaishi Dar ambao asubuhi huwa wanakula maandazi ya 25 ambayo bei yake ni 200 kwa kila andazi so ni 5,000. Mchana wanakula Ugali ambao hupikwa na kilo 2 za unga wa mahindi, na usiku wanakula wali wa kilo 3.

Sasa bei za bidhaa zinazotumika kuandaa hivi vyakula zinapopanda sokoni, siku za mwanzoni mkulima atafaidika sababu bei imepanda sasa kwa kiasi fulani cha mazao anapata pesa zaidi.

Ila muda unavyozidi kwenda huyu mteja wa mjini ambaye kipato chake ni kile kile cha siku zote atalazimika kununua bidhaa kwa kiwango kile kile ila kwa bei ya juu au mara mbili zaidi.

Mfano maandazi yakizwa mia tano kwa moja sasa atatoa zaidi ya 10,000 ili kulisha familia asubuhi. Kama unga alikuwa ananunua kwa 1000 sasa atalizimika kulipia zaidi ya 2000 kuweza kulisha familia. Na mchele hivyo hivyo.

Hii itaharibu budget za raia, na wengi watalazimika kupunguza mahitaji aidha kwa kula mlo m'moja kwa siku. Wengine watapunguza matumizi kwa kupunguza kiwango cha bidhaa wananunua. Mfano badala ya kununua maandazi 25 watanunua maandazi 15 au 10. Badala ya kupika kilo 2 za unga watapika kilo moja, na mchele badala ya kilo 3 watapika 1.

Sasa madhara yatakurudia tena wewe mkulima kwasababu wachuuzi watapunguza kiasi cha mzigo wanachonunua kwako sababu uhitaji mjini utashuka. Na hatari zaidi ni pale akatokea waagizaji wa bidhaa wakaleta mazao yanayoweza kutumika mbadala wa yako mkulima then matokeo ni bidhaa zakp kukosa soko kabisa na kukudodea.

So mfumuko wa bei sio kitu kizuri kabisa kwenye uchumi sababu kinapelekea kushuka kwa uzalishaji, kuharibu tija, kuzorotesha mapato ya raia m'moja m'moja, kushusha thamani ya pesa sababu pesa nyingi inatumika kununua kiwango kidogo cha bidhaa, inasababisha uwiano usio sawa wa kiuchumi pesa nyingi itakwenda kwa watu wasiofanya kazi na wanaofanya kazi watanyonywa jambo ambalo ni hatari.
 
Habarini wana jamii wenzangu,

Tangu muda mrefu kumekuwapo na mjadala mrefu juu ya mfumuko wa bei, hasa kwa bidhaa za chakula. Wachambuzi wengi wamekuwa wakilaani jambo hili, hasa ndugu zetu waishio maeneo ya mjini.

Sasa mimi naomba kuelimishwa, kwani kila mfumuko wa bei ni hatari katika uchumi? Mbona Mimi naona kama huu mfumuko wa bei, hasa kwenye hizi bidhaa za chakula huku kijijini kwetu kama zinasisimua zaidi watu kulima. Maana baada ya kupanda bei ya vyakula mwaka huu mashamba ya mahindi yamekuwa mengi, kila shamba la mikorosho watu wamepiga matuta na kupanda mahindi.

Na kama factor nyingine hazitatokea, mbona naona kwa Kasi hii wafanya biashara wa mahindi watamtafuta wakumuuzia, maana asilimia kubwa ya watu watakuwa wamezalisha zaidi ya nusu ya mahitaji Yao. Sasa naomba munipe darasa, kwani kila mfumuko wa bei ni hatari kwenye uchumi, au Kuna namna fulani mfumuko wa bei una stimulate production?
Tatizo ukame mvua zikinyeshe za tija nchi hii huwezi sikia mchele ikiuzwa 2000 wilayani na unga 1500 hata kenya rwanda wanunue nafaka asubuhi mchana na jioni
 
Back
Top Bottom