NBS: Mfumuko wa bei umeshuka kutoka 4.9 hadi 4.8

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
TAARIFA KWENYE VYOMBO VYA HABARI FAHIRISI ZA BEI ZA TAIFA KWA MWEZI FEBRUARI, 2023

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imepewa mamlaka kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Sura 351 ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji na usambazaji wa Takwimu Rasmi nchini ikiwa ni pamoja na takwimu za Mfumuko wa Bei kwa ajili ya matumizi ya Serikali na wadau wa takwimu. Mfumuko wa Bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2023 umepungua kidogo hadi asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.9 kwa mwaka ulioishia mwezi JANUARI, 2023. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2023 imepungua kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi JANUARI, 2023. Kupungua kwa Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2023 kumechangiwa na kupungua kwa Mfumuko wa bei kwa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2023 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka ulioishia mwezi JANUARI, 2023.

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua kwa Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2023 ikilinganishwa na mwaka ulioishia mwezi JANUARI, 2023 ni pamoja na: ngano (kutoka asilimia 7.7 hadi asilimia 7.1); dagaa wakavu (kutoka asilimia 5.7 hadi asilimia 1.1) na vinywaji baridi (kutoka asilimia 14.0 hadi asilimia 12.7). Kwa upande mwingine, baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kupungua kwa Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2023 ikilinganishwa na mwaka ulioishia mwezi JANAURI, 2023 ni pamoja na: bidhaa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba (kutoka asilimia 7.9 hadi asilimia 5.0); gesi (kutoka asilimia 9.7 hadi asilimia 9.1); mafuta ya taa (kutoka asilimia 36.9 hadi asilimia 33.1); dizeli (kutoka asilimia 33.1 hadi asilimia 27.8) na bidhaa na huduma kwa ajili ya usafi binafsi (kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 3.7).

Mfumuko wa Bei wa Bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2023 umepungua hadi asilimia 9.6 kutoka asilimia 9.9 kwa mwaka ulioishia mwezi JANUARI, 2023. Mfumuko wa Bei ambao haujumuishi bidhaa za Vyakula na Vinywaji baridi kwa mwezi FEBRUARI, 2023 umepungua pia hadi asilimia 2.8 kutoka asilimia 3.0 kwa mwaka ulioishia mwezi JANUARI, 2023.

HALI YA MFUMUKO WA BEI KWA BAADHI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KWA MWAKA ULIOISHIA MWEZI FEBRUARI 2023

Nchini Uganda, Mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2023 umepungua hadi asilimia 9.2 kutoka asilimia 10.4 kwa mwaka ulioishia mwezi JANUARI, 2023. Kwa upande wa Kenya, Mfumuko wa Bei kwa mwaka ulioishia mwezi FEBRUARI, 2023 umeongezeka hadi asilimia 9.2 kutoka asilimia 9.0 kwa mwaka ulioishia mwezi JANUARI, 2023.

Imetolewa na: Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dodoma 09 Machi, 2023.
 

Attachments

  • TAARIFA YA MFUMUKO WA BEI_022023 (WAANDISHI WA HABARI).pdf
    48 KB · Views: 2
Hii kutoka nchi gani? Maana huku Mtaani bei ni zile zile, yaani hakuna ata kimoja kilichopungua
 
Mfumuko wa bei wa nchi gani huo?

Screenshot_20230213-135848.jpg
 
Hii taasisi Ina watu wasio na ufahamu.
Iweje Bei ya unga ipande kutoka 1800 January Hadi 2200 March,
Maharage 3000 Hadi 4000,
Mchele mzuri 2800 Hadi 4000
Nyama 8000 Hadi 9000
Nyanya fungu 500 Hadi 700
Yaani kila kitu kimepanda Bei halafu MTU mwenye elimu anakuambia mfumuko wa Bei umeshuka. Aidha MTU huyo anawahadaa wananchi au hakai Tanzania.
Hivi wakisema urongo wanamfurahisha Nani?
Sasa hivi ukionekana unakula maharage mfukulizo unaonewa wivu na majirani.
Wamechukua basket ya bidhaa zipi hizo zilizoshuka Bei?
Ndio maana PhD za Tanzania haziaminiki.
 
Yaan Hii nchi bhana,
Huwez amini mfumuko wa bei nchini
Unashushwa kwa kuagiza mchele nje
 
Back
Top Bottom