Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Anaitwa baharia mchomoa betri wa huku jf.
Naomba nitoke kwenye huu Uzi.
Baharia wapi huyu koko tu, kwenye msafara wa mamba hata kenge utawakuta, hakuna kitu kinanikera kama mwanaume kujishaua mbele za watu hususani mbele za wanawake sijui ndiyo kujitafutia umaarafu, tena anajifanya wa matawi ya juu nyau kweli huyu, eti kujinadi mwenye vitu vizuri ni ujinga sana mbaya zaidi ana dharau za kama za mademu,
 
Wewe utabaki kuwa kielelezo bora kwa aina ya wanawake wenye akili na hekima zao.
Sitakusahau wakati flani nikiwa ninashambuliwa bila sababu na wenye akili zao...ulituliza moto kwani nilichokuwa nakiwaza kukifanya "shetani anajua" kwani najijua mwenyewe nilivyo na hasira kwa wapumbavu...ubarikiwe sana bila kumsahau kipenzi CUTE B
Mkuu ulikata tamaa mpaka ulitaka kuji murder ? Life is too precious to hold on dont kill yourself for cheap reasons
 
Ubarikiwe kwa kuuchangamsha na kuupamba uzi wetu,, nimeona mapicha picha kama yote nikajisemea ihiiiiiiiiii sipitwi,,

Una rangi nzuri, na mwili mzuri uupunguzepo, (navyojitia mama ushauri sasa), kingine itabidi tukufanyie kampeni tukupe mume hizi bata zako zinatuumiza roho ......Hahahaha karma kashaanza ikishindikana mi ntamalizia

Wapendwa leo nina kazi nzito tutaonana jioni, goodmorning

Nb; msifute picha mpaka nimegonga like
Hahahaa. Nitafutieni tu mume. Bata zangu mie sio za gharama maana nalipiwa kila kitu hata msione wivu sio hela yangu ile . Unene unapungua mwaya. Nakimbia nipungue kidogo. Sema sipendi wembamba pia
 
Mi nasifia sana jamani. Rafiki zangu washaniambiaga mi sio kipimo kizuri cha kuongelea uzuri. Wanasema mi nasifia kila mtu
Nani kasema?? Mie mwenyewe wale wale tu ndiyo maana nasema wazuri "walikuwa wanahesabika" lakini uzuri unatofautiana kati ya mtu na mtu maana mimi binafsi hadi mwanamke mwenzangu nimuone kama ni mzuri basi nimempitisha kwenye chujio hasa

Yaani sifa nilizoziweka za mimi kusema kwamba huyu mwanamke kweli ni mzuri hata mimi sina hizo sifa ndiyo maana hata mimi sijihesabii kama ni mzuri na wala hata siku moja hauwezi nikuta najisifia kuwa eti mimi ni mzuri yaani sijawahi kujikubali!!
 
Mbona unatushusha hivyo dear?
Hahah nimemjibu mwenzenu huko juu najua mnatamani kunifahamu na pia kufahamu ninapokojolea ila ndio hivyo tena haiwezi tokea...

Niwe Mkweli tu, yule sio mtu wangu ni picha nilichukua mtandaoni huko na nilipost kimakusudi nisike mtakuja na hoja gani na ninmegundua kitu kwenu, nitabaki nacho moyoni siwezi weka hapa kuleta mgongano kwenye nyuzi za watu...

Kuhusu Itel, ni mmoja wapo ya simu zangu ndogo ninazotumia kwa sababu inakaa na charge muda mrefu, na kuhusu smartphone natumia simu yenye bei tu sina haja ya ku prove hilo kwa sababu wengi wenu najua mnatumia tecno tu ndio maana picha zenu haziko clear kiasi hicho...

Na kingine, kuhusu kazi wala sina haja ya kujisifia sehemu ninazoingia hapa Nchini itachukua muda pengine koo/familia yenu kuja kuingia, na nimegundua humu wadada wengi hamna kazi zinazoeleweka ndio maana mko online 24/7 mjitahidi kufanya kazi pengine mtaepuka hii psychology ya kushinda mtandaoni masaa yote hayo...

Kuhusu mama watoto wangu sijui hata kama umemsogelea kielimu, kiuchumi, kifikra n.k... Jua tu yuko X100 ahead of you...

NB: Ukitaka picha zaidi za huyo mdada naweza kukupa jina ukaenda kumtazama huko mtandaoni..
 
Back
Top Bottom