Pasco, wewe ni layman kweli hata huna mfano: Issue nzima ni ya kisiasa na haina mashiko yoyote: kumfutia mtu mashitaka halafu ukamwachia then ukamkamata tena hapohapo ni kuwa Serikali hawajui wanalolifanya!! Sasa kati ya CDM na Serikalimkwa maana ya DPP nani hajajipanga??!! Tatizo ulayman wako ni wa makusudi!!
Mkuu Chungurumbira, kama kufuatilia kesi umeanza sasa, hayo ndio utakuwa huyajui, mimi mwenzio kesi nimeanza kuzisoma nikiwa darasa la nne, ile "kesi ya Mauaji Mwanza" nilikuwa naisoma kwenye gazeti la Mzalendo kila jumapili, nikaja kuisoma kesi ya Uhaini, huko ndiko nilipoijua "Nolle" na haya ni mamlaka ya DPP ambayo hayahojiwi na mamlaka nyingine yoyote!, si mahakama tuu, hata rais hawezi!, sasa hawa wanasheria wa Chadema leo ndio wanaihoji hiyo mamlaka?!.
Serikali ilipoifungua hiyo kesi mwanzo, iliipeleka mahakama ya Kisutu ili isikilizwe, imeifuta na kuifungua upya sasa sio tena ili isikilizwe, bali imefunguliwa pale ili tuu kukamilisha matakwa ya kisheria ya kutomshikilia mtu bila kufikishwa mahakamani, hivyo hapo Kisutu inapita tuu, watuhumiwa hawatatakiwa kujibu chochote mpaka uchunguzi itakapokamilika, na kuhamishiwa mahakama kuu ambako huko ndiko kesi itasikilizwa!.
Wanachotaka kufanya hawa wanasheria wa Chadema, ni kuishinikiza serikali, kuifufua ile kesi ya mwanzo iliyoshafutwa na DPP kwa kutumia Nolle, kiukweli this is total wastage of time!, najua wengi mtanilaumu, ila kisheria Nolle ni kitu ingine kabisa!, kesi ikishapigwa nolle, inakuwa dead, huwezi kuifufua tena!.
Pasco.