Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

[h=3]KESI YA LWAKATARE: TUNDU LISU AMLAUMU "ISSA MICHUZI" NA " MWIGULU NCHEMBA"[/h]

Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu leo amefanya mkutano wa wanahabari. Katika mkutano huo, Lissu ameongea yafuatayo:

1. Atafungua kesi Mahakama kuu kuiomba iiamuru Mahakama ya Kisutu kuendelea kusikiliza kesi ya awali iliyofutwa na DPP katika kesi inayomhusu Lwakatare kwani DPP amevuka mipaka yake inayomruhusu kufuta kesi na isitoshe kesi aliyofungua ni ile ile hivyo Mahakama iamuru shauri la awali liendelee.

2. Kuhusu video iliyoonyeshwa kwenye mitandao Lissu anasema kuna mashaka makubwa sana kuhusiana na video ile na kisheria kesi hiyo ikifika mahakamani haitachukua hata nusu saa ataibuka mshindi.

Lissu anasema
- Hakuna mtu anayepanga mauaji katika hadhara mahali ambapo watu wanapitapita kama inavyoonekana kwenye video ile.

-Lwakatare kama alirekodiwa basi lazima ielezwe je ilikuwa ni kwa hiari yake kama si hivyo ni makosa

-Issa Michuzi Mpiga picha wa Rais alikuwa akipongezana na watu wa Ikulu wenzake kuwa TISS (Usalama wa Taifa) wamefanya kazi nzuri kwa kurekodi ile video. Kisheria usalama wa taifa hawatakiwi wala hawaruhusiwi kurekodi au kuvifanyia ushushu vyama vya siasa kwa maslahi ya Chama tawala.

-Ludovick baada ya kukutana na Lwakatale tarehe 28 Desemba mwaka jana saa 5 muda mfupi baadaye yaani saa 5:59 alimpigia simuMwigulu Nchemba kwa kutumia namba ya simu ya Mwigulu ambayo ameiandikisha kwenye kumbukumbu na vitabu vya Bunge Lissu anadai wana rekodi ya mazungumzo yao.

-Siku iliyofuata tarehe 29 Desemba mwaka jana akiwa kwenye kipindi cha Tuongee asubuhi cha Star TV alidai ana mkanda wa video unaowaonyesha CHADEMA wakipanga mauaji.

-Pia amedai itabidi waambiwe video hiyo imerekodiwa studio gani, maneno gani yameondolewa na yapi yameongezwa.

Anamalizia kwa kusema walianza kwa kusema CHADEMA ni chama cha familia wakashindwa, wakasema ni chama cha wachaga wakashindwa, wakesema ni chama cha wakatoliki wakashindwa, wakasema ni chama cha wakristo wakashindwa, wakasema ni chama cha ukanda wakashindwa leo wanasema ni chama cha kigaidi WATASHINDWA.

(Picha / Habari na Kurugenzi Ya Habari Chadema)

KESI YA LWAKATARE: TUNDU LISU AMLAUMU "ISSA MICHUZI" NA " MWIGULU NCHEMBA" - MPEKUZI
 
Mnateteaje waovu? Haingiu akilini wote humu mnatetea magaidi
Machoni pa gaidi wa ukweli kamwe ataona wasiomagaidi kuwa ndio magaidi. Kama ilivyo machoni mwa mwendawazimu anavyoona wazima ndio wazimu
 
Wakuu Candid scope na Posco,

Nafuatilia kwa karibu mijadara yenu ktk uzi huu. Inaelimisha! Jambo ninaloliona kunakuaibika kwa baadhi ya taasisi hapa (mainly tiss) na ugumu wa kuachiwa kwa Rwakatale. All in all, kwa sababu cdm nao vichwa vikari wataamua kutafuta msaada wa uchunguzi wa video hii beyond expectations za magamba na matokeo yake yana athari kubwa ktk mwelekeo wa siasa za tnz ndani na nje. I am still learning hence in short of comments.
 
This is risky for CCM! Haya mambo wanayafanya na sasa inaonekana inatafuna vibaya kwao. The plan was not correctly put - kuichafua Chadema. Nadhani wamekutana na watu smart kuliko wao -- thinkers beyond scope. Swala la kumfungulia Lwakatare kesi ya ugaidi na si jinai ilikuwa pia ni strategy ya kutafuta huruma na participation ya US lengo likiwa kuiblacklist Chadema internationally. Baada ya kuona US hawana interest, wanatafuta namna ya kuondoa kesi...shame shame!!
 
dogo kila anayekupinga unadhani unamfahamu unaanza ushehe yahaya my web ukadhani ni mchange umekuwa tahira mbeba sumu wewe
Jibu swali unaficha kichwa kama mbuni kiwiliwili na masaburi nje.
 
If wishes were horses.....!

Ni nani aliyeweka youtube?

Iko wapi video ya Mwigulu Nchemba?

Ni kwa nini polisi waweke video tofauti na ile iliyopo youtube?

Inawezekana kulikuwa na two recording devices ndio maana muda ulitofautiana lakini maneno yako sawa.

Swali la msingi: Kama kuna maneno ambayo Lwakatare anayakubali katika ile clip, ni maneno gani aliyasema yeye?
 
Kiongozi wa jopo la wanasheria watano (5) wanaomtetea Lwakatare, Wakili Tundu Lissu mezungumzia mawasiliano ya mtu anayeitwa Michuzi, kuwasiliana na watumishi wenzake wa OBR, akiwapongeza na kutoa kudos kwa TISS kwa kazi nzuri, akiwataka wenzake wapige sana kelele kwani hiyo ni kete muhimu kwa CCM. Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa, hawaruhusiwi kufanya surveillance dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa CCM, kwa sababu upinzani wa kisiasa ni suala lililoruhusiwa kisheria nchi hii.

Aidha, Lissue ameongeza kusema wamepata mawasiliano ya simu yakionesha kuwa siku hiyo hiyo ambayo video imerekodiwa, majira ya saa 5.59, mtu aitwaye Ludovick alimpigia simu mtu aitwaye Mwigulu Nchemba. Kwa mujibu wa Wakili Lissu, yamepatikana pia mawasiliano ya mtu aitwaye Dennis Msacky akimpigia simu Lwakatare, ambapo wamemuuliza Lwakatare iwapo ni kweli aliwasiliana na mtu mwenye jina hilo (ambaye kwenye charge sheet ya pili, polisi wameonesha ndiye aliyekuwa akipangiwa kutekwa/kufanyiwa vitendo vya ugaidi), naye amekubali kuwa ni kweli alimpigia simu siku moja kabla ya tukio la kurekodiwa, akimuuliza kama amerudi Dar es Salaam, naye akamwambia alikuwa njiani kutoka Bukoba.

Amemaliza kwa kusema kuwa kesi hii ni kama kesi nyingine za kupikwa, ambazo polisi wamekuwa wakifungua dhidi ya CHADEMA na viongozi wa chama hicho, kwa nia ya kuiokoa CCM, kwasababu chama hicho kimekaliwa vibaya na hakiwezi tena kufanya siasa za ushindani dhidi ya wapinzani wao wakuu, CHADEMA.

"Ni mambo yale yale, walianza chama hiki cha familia ya Mtei na Mbowe, ikashindikana, chama hiki cha kikabila, cha Wachaga… ikashindikana, wakasema chama hiki cha kaskazini, imeshindikana, wamesema chama hiki cha wakatoliki, ikashindikana, wamesema chama hiki cha wakristo bado Watanzania wamekataa, iemshindikana pia… Sasa unafanyaje? Tengeneza hii kitu, sasa kiwe chama cha magaidi…ITASHINDIKANA pia," alisema Wakili Lissu.
 
Sasa hata kina tundu lisu wanauhakika kuwa lwakatare alikula njama za kufanya mateso na video ile ni halisi si feki. Wanachotaka kujengea hoja eti kama ali rikodiwa kwa hiari au lazima! Sasa watanzania wanajua na hata cdm wanakubali kupitia kina tindu lisu kuwa ni lazima mbinu nyingine itumike ya kuinusuru cdm na lwakatare mwenyewe kwa ku-complicate issue nzima kwa maswali yasio ya msingi kama yalivyoelezwa na tindu lisu. Hilo ni parapanda.
 
Kiongozi wa jopo la wanasheria watano (5) wanaomtetea Lwakatare, Wakili Tundu Lissu mezungumzia mawasiliano ya mtu anayeitwa Michuzi, kuwasiliana na watumishi wenzake wa OBR, akiwapongeza na kutoa kudos kwa TISS kwa kazi nzuri, akiwataka wenzake wapige sana kelele kwani hiyo ni kete muhimu kwa CCM. Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa, hawaruhusiwi kufanya surveillance dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa CCM, kwa sababu upinzani wa kisiasa ni suala lililoruhusiwa kisheria nchi hii.

Aidha, Lissue ameongeza kusema wamepata mawasiliano ya simu yakionesha kuwa siku hiyo hiyo ambayo video imerekodiwa, majira ya saa 5.59, mtu aitwaye Ludovick alimpigia simu mtu aitwaye Mwigulu Nchemba. Kwa mujibu wa Wakili Lissu, yamepatikana pia mawasiliano ya mtu aitwaye Dennis Msacky akimpigia simu Lwakatare, ambapo wamemuuliza Lwakatare iwapo ni kweli aliwasiliana na mtu mwenye jina hilo (ambaye kwenye charge sheet ya pili, polisi wameonesha ndiye aliyekuwa akipangiwa kutekwa/kufanyiwa vitendo vya ugaidi), naye amekubali kuwa ni kweli alimpigia simu siku moja kabla ya tukio la kurekodiwa, akimuuliza kama amerudi Dar es Salaam, naye akamwambia alikuwa njiani kutoka Bukoba.

Amemaliza kwa kusema kuwa kesi hii ni kama kesi nyingine za kupikwa, ambazo polisi wamekuwa wakifungua dhidi ya CHADEMA na viongozi wa chama hicho, kwa nia ya kuiokoa CCM, kwasababu chama hicho kimekaliwa vibaya na hakiwezi tena kufanya siasa za ushindani dhidi ya wapinzani wao wakuu, CHADEMA.

"Ni mambo yale yale, walianza chama hiki cha familia ya Mtei na Mbowe, ikashindikana, chama hiki cha kikabila, cha Wachaga… ikashindikana, wakasema chama hiki cha kaskazini, imeshindikana, wamesema chama hiki cha wakatoliki, ikashindikana, wamesema chama hiki cha wakristo bado Watanzania wamekataa, iemshindikana pia… Sasa unafanyaje? Tengeneza hii kitu, sasa kiwe chama cha magaidi…ITASHINDIKANA pia," alisema Wakili Lissu.

Duh! kama ni hivyo na Michuzi, Dennis Msacky na Mwigulu wote wakamatwe. Kumbe hawa ni magaidi hatari. Awemo na yule mtangazaji wa Clouds fm
 
Watanzania wengi bado tunaamini kuwa: chama hiki ni cha kikabila, cha Wachaga, chama hiki cha kaskazini, cha wakatoliki, , chama hiki cha wakristo. Tunakikataa sasa na tutakikataa 2015 kama kitafika huko.
 
ukweli utajulikana tu na magamba watakoma tu
 
Watanzania wengi bado tunaamini kuwa: chama hiki ni cha kikabila, cha Wachaga, chama hiki cha kaskazini, cha wakatoliki, , chama hiki cha wakristo. Tunakikataa .

nasi tunaamini kuwa CCM ni cha wachawi, mafisadi na waislam wa BAKWATA. Ndo maana marais wote 5 wa bara na visiwani ni ma alhaji. Wenye haki ya kuchinja ni waislam na mahakama ya kadhi itawekwa na hii CCM ya waislam. Mkuu wa polisi, mahakama, TISS.
 
Mkuu Mkeshaji
Ndugu yetu Pasco anataka kuwafundisha magwiji wa sheria jinsi sheria zilivyo wakati yeye ni muandishi wa habari! Yaani ni sawa na mvuvi kufungua darasa la kumfundisha samaki jinsi ya kuogelea.

Huyu naye ni mwanasheria,amesoma sheria,nakumbuka alikuwa anaishi pale block F
 
mimi ninachomshangaa lisu ni kutobainisha kama yaliyofanywa na lwakatale ni uongo au ya kweli mbona anaongea sana bila fact

Lissu anakubali kitu kimoja cha msingi: Lwakatare alishiriki kwenye lile tukio la kigaidi ila alirekodiwa bila idhini yake.

Aliyemrecord alifanya hivyo kwa maslahi ya taifa kufichua ugaidi anastahili pongezi.
 
Jamii ipi Pasco, ya Lumumba?

Mfumo wa kubambikizia kesi umeshatumika mno, na ni maajab bado wakubwa wanaugemea! Umechuja kupita maelezo.

Lakini pia utambue, ukishajijengea sifa ya kubambikizia watu kesi za uwongo, hata ikitokea ya kweli watu hawatajishughulisha kukusiliza. Na hili ndilo tatizo walilonalo watu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Imani ya wananchi ni zero!

Mkuu, wananchi wenyewe ni waathirika wa kesi za kubambika. Na huku mtaani tunaujua sana mchezo wa kubambikiana kesi katika levels zetu. Usidhani wananchi hawatajua pia kama mchezo huu unachezwa pia kwenye levels za juu kwa sababu za kisiasa au hata binafsi!
 
Back
Top Bottom