Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Hivi sasa wanasheria wa CHADEMA wanafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la Lwakatare na makosa ambayo alishitakiwa nayo.

=========
Kiongozi wa jopo la wanasheria watano (5) wanaomtetea Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare, Wakili Tundu Lissu, akiwawakilisha wenzake, ameongea na vyombo vya Habari akiwa Makao Makuu ya CHADEMA na kuzungumzia masuala kadhaa kutokana na sakata hili.

Lengo kuu la mkutano huo na wanahabari lilikuwa ni kuutarifu umma wa Watanzania kupitia kwa wanahabari juu ya hatua ambayo mawakili hao wameamua kuchukua kwa kupeleka ombi Mahakama Kuu ya Tanzania, chini ya hati ya dharura ili Mahakama hiyo ya juu iitishe mafaili yote mawili yaliyofunguliwa kuhusu kesi ya Lwakatare, yaani faili la kesi iliyofutwa na faili lililofunguliwa baada ya kesi ya awali kufutwa, wakiiomba mahakama iangalie na kujiridhisha…


Kuhusu video
Wanahabari walitaka kujua maoni yake kuhusu video na namna kesi hiyo ilivyo, hasa kutokana na alivyoielezea 'charge' ilivyo 'defective', ambapo Wakili Lissu kwa maoni yake, alisema kuwa kuna masuala mengi yanatakiwa kuwekwa wazi kuhusu video yake, akihoji maswali kadhaa:


- Nani aliyemrekodi Lwakatare? Je, Lwakatare alijua kuwa anarekodiwa? Je, aliruhusu? Kama hakuruhusu, ilifanyika kihalali? Je, haivunji katiba ya nchi inayozungumzia privacy ya mtu? Je, baada ya kurekodiwa mkanda huo ulipelekwa wapi? Nani alikuwa nao? Je, umefanyiwa uhariri (editing) na nani? Je, aliyemrekodi alitumwa na nani?

Ushahidi mwingine
Ameongeza kuwa, video inaonekana imechukuliwa tarehe 28 Desemba, siku iliyofuata, Desemba 29, kwenye kipindi cha TV, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akaanza kusema kuwa anayo video ya viongozi wakuu wa CHADEMA wakipanga mipango ya mauaji ya dhidi ya Watanzania.


Amezungumzia mawasiliano ya mtu anayeitwa Michuzi, kuwasiliana na watumishi wenzake wa OBR, akiwapongeza na kutoa kudos kwa TISS kwa kazi nzuri, akiwataka wenzake wapige sana kelele kwani hiyo ni kete muhimu kwa CCM. Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa, hawaruhusiwi kufanya surveillance dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa CCM, kwa sababu upinzani wa kisiasa ni suala lililoruhusiwa kisheria nchi hii.

Aidha, Lissue ameongeza kusema wamepata mawasiliano ya simu yakionesha kuwa siku hiyo hiyo ambayo video imerekodiwa, majira ya saa 5.59, mtu aitwaye Ludovick alimpigia simu mtu aitwaye Mwigulu Nchemba.

Kwa mujibu wa Wakili Lissu, yamepatikana pia mawasiliano ya mtu aitwaye Dennis Msacky akimpigia simu Lwakatare, ambapo wamemuuliza Lwakatare iwapo ni kweli aliwasiliana na mtu mwenye jina hilo (ambaye kwenye charge sheet ya pili, polisi wameonesha ndiye aliyekuwa akipangiwa kutekwa/kufanyiwa vitendo vya ugaidi), naye amekubali kuwa ni kweli alimpigia simu siku moja kabla ya tukio la kurekodiwa, akimuuliza kama amerudi Dar es Salaam, naye akamwambia alikuwa njiani kutoka Bukoba.

Amemaliza kwa kusema kuwa kesi hii ni kama kesi nyingine za kupikwa, ambazo polisi wamekuwa wakifungua dhidi ya CHADEMA na viongozi wa chama hicho, kwa nia ya kuiokoa CCM, kwasababu chama hicho kimekaliwa vibaya na hakiwezi tena kufanya siasa za ushindani dhidi ya wapinzani wao wakuu, CHADEMA.


===========
Habari hii unaweza kuisoma kwa kirefu -> Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA ‘wafunguka'! | Fikra Pevu
 
Anaelezea Lissu , juu ya mwenendo wa kesi ulivyoanza mahakamani , na ili kesi ya ugaidi iweze kufunguliwa ni lazima kuwa na ridhaa ya mkurugenzi wa mashitaka nchini , na ameonyesha kipande cha karatasi husika ambacho kina saini bila nembo ya serikali wala muhuri wa moto .
 
Nia yao siyo hicho kinachoelezwa na wanasheria bali ni udhalilishaji wa makusudi. ni kama mtu akuvue nguo kwa makusudi halafu aite watu wengine akishangilia ulivyo na akicheka!! maccm noma!!
 
Baada ya mabishano ya kisheria, juzi mahakamani , hakimu alisema angetoa hukumu juu ya kama mashitaka ni sahihi kwa mujibu wa sheria ama laa, ila jana asubuhi badala ya kusubiria hukumu ya awali juu ya uhalali wa mashitaka hayo hawakusubiri hukumu badala yake walipeleka hati ya kufuta kesi na baada ya dakika tano walimkamata na kumfungulia mashitaka yale yale , ila kilichobadilika. Ni namba ya file ya kesi tuu , ila mashitaka ni yaleyeale mpaka nukta ya mashitaka.

Lengo lilikuwa ni kuizuia mahakama isitoe uamuzi ndio maana waliamua kufuta kesi na kuifungua hiyo hiyo,
 
hii serekali imekaa kijoti joti,ukiangalia na ile kesi ya Lema ya ubunge utugundua dhuluma ni nyingi sana!
 
Mamlaka ya DPP ni kufuta kesi kama kufanya hivyo kutakuwa ni kwa masilahi ya taifa au kwa nia ya kulenga kupata haki, hivyo hatua za kufuta kesi jana hazikuwa kwa masilahi ya taifa bali ilikuwa ni kuizuia mahakama kutoa haki, kilichofanyika jana ni matumizi mabaya ya mamlaka ya DPP,

HATUA TULIZOCHUKUA.
1. Leo tumefungua kesi mahakama kuu kwa hati ya dharura , kwa kuiomba mahakama iitishe mafaili yote mawili ,ili iyachunguze ione kama haki imetendeka kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.

2. Wameiomba kama itakubali ifute ile hati ya DPP ya kufuta mashitaka, na ifute amri ya mahakama ya kufuta kesi iliyofanyika jana ,

3. Ielekeze mahakama ya hakimu mkazi kisutu , iendelee na utaratibu wa kutoa hukumu kama ilivyokuwa imepangwa , na hii ni kwa masilahi yab haki ionekane inatendeka.

Kilichofanyika n a mwendesha mashitaka wa serikali ni kuingilia uhuru wa mahakama katika kutenda haki.
 
Mbona wanasheria hawasemi ile video ni fake?

Kama ule mkanda nk genuine basi huo ni ugaidi.
 
Ukweli daima utasimama mwisho wa siku, kama serikali kwa makusudi kabisa wanaamua kutumia pesa za walipa kodi masikini wa Tanzania kwa kufungua kesi za kutunga kwa malengo ya kuiondoa Chadema kwenye ramani ya kisiasa, hakika watafutika wao, maana malipo ya dhambi wanayoitenda sasa ni makubwa sana na hawatakaa waisahau milele.

Tusubiri tuone, kwanza wameonesha ambavyo wasivyo makini kupitia wanasheria wao, hivyo mwisho wa siku huku kudharisha wanakofanikisha kwa Lwakatare as individual person na Chadema kwa kiwango fulani kwao itakuwa disearter very soon, tusubiri yetu macho, acha wanasheria watifuane na tuombe mahakama isimamie haki.
 
Back
Top Bottom