Kwanza nitoe ufafanuzi ufuatao,
Moja , kuwa Wanasheria wanahoji mamlaka ya DPP sio kweli , wao wanahoji jamo linaloitwa ..abuse of the court....hii ni kutokana na ukweli kuwa hakimu alipaswa kutoa hukumu juu ya kama kuna kesi ya kujibu ama laa, wao serikali wakaamua kufuta kesi namba 37 na kufungua nyingine ambayo kimsingi ni ileile , yaani kesi iliyofutwa ndio ilifunguliwa upya bila kuongezwa hata nukta ama neno lolote jipya , sasa hapo wanatumia hukumu iliyowahi kutolewa na Jaji Mroso wa mahakama ya Rufani kuhusu jambo hili na kuonekana kuwa kama DPP akifuta kesi bila kuzingatia maslahi ya umma ama bila kuonyesha kuwa lengo lilikuwa ni kuonyesha haki inatendeka , basi mahakama inamamlaka ya kuamua juu ya hilo.
Pili, ukisoma kifungu cha 245 (3) CPA utaona mamlaka ya mahakama kuhusu kutoa dhamana ama laa , jamo ambalo wanasheria wanaona kuwa jana kama hakimu angepata mwanya wa kutoa rulling yake basi hilo lingeweza kuamuliwa na akawa nje kwa dhamana halafu mpambano wa kesi uendelee huko mahakamani .
Naitafuta hukumu ya Jaji Mroso kuhusu Nolle , then mjadala utaenda vizuri.
Kuhusu hoja yako kuwa lazima Chadema itoe kauli kuhusiana na jambo hili na unataka iseme kuwa hayo yote ni ya Lwakatare , sio busara kwani kama chama kimewapa wanasheria wake suala hilo na wao wameshaweza kuanza kutoa ushahidi wa wazi jinsi ambavyo hii ni kesi ya kutunga na kubambikiana , sasa unawataka tena chama watoe kauli ya kukubaliana na kubambikiwa kesi kwa Lwakatare na wakina Mwigulu?
Kwa sasa wenye busara wanaweza kuelewa ni mchezo gani ulikuwa unachezwa , na hata kipindi cha star tv siku hiyo nasi,ia tayari kuna nyaraka zimenaswa za kuonyesha nani alihusika kufanya mwaliko wa kipindi na lengo lilikuwa nini , tusubiri muda ukifika itajulikana mbivu na mbichi.
Wapo wanaosema kuwa Dr.Slaa ameumbuka , hawa watakuwa ni majuha tuu , kwani alichosema yeye ni kuwa mkanda ni wa kutengeneza na walichosema leo wanasheria na alichosema Lwakatare polisi ni kuwa ni kwelii amelishwa maneno , sasa hapo kaumbuka vipi? Ni suala la kuelewa content na context tuu hapo.