Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Wana JF!
Nimebahatika kuongea na moja ya mawakili wanaomtetea Lwakatare, akaniambia moja ya mashahidi wanaompango wa kuwatumia ni Mwigulu Nchemba ambapo watamtaka aelezee hiyo video yake aliyosema tar. 29/12/2012, ndiop hiyo iliyoko polisi au la! Vilevile mawasiliano yao ya karibu na Ludovick Joseph kuanzia Facebook (kumbuka hawa nimarafiki ktk FB) hadi simu walizokuwa wakipigiana vitawekwa hadharani kwa ajili ya cross qns.
Vilevile wanaangalia uwezekano wa kuomba kuundwa kwa mahakama ya Coroner kuchunguza vifo vyote na utekaji wenye utata uliotokea siku za karibuni hapa TZ .

My take!
Mwisho wa hili sakata kuna watu wanaweza umbuka kuliko ilivyokuwa imedhaniwa.



Neno la leo;

It is what we think we know already often prevents us from learning.

By Mpigania Uhuru.

It is what

ili swali naona litakuwa gumu sana kwa uyu jamaa Mwigulu wa nchemba iyo video clip ndo uliosema ndo hii? au sio nyenyewe hapo sasa ni swali mmoja lakini yanyongeza yapo kama 50 hivi.
 
Kwani chafya ni ugaidi?
Mkuu,nilikuwa ninashangaa anavyokiri kila kitu na kukataa sauti katika statement ya police.Chafya inaweza kuwa ugaidi hivi leo kama unamafua ya ndege na kwa makusudi ukaama kuyaeneza sio jinai?
 
Naililia sana hii nchi iliyokuwa imetulia sasa hivi inapelekwa wapi jamani.ninachoweza kuwaasa hawa wanaosimamia haya maovu hakika nao watalipwa hayohayo hapa duniani kama sio wao basi watoto wao.haya mambo mwenyenzi mungu anayaona yote hivyo malipo yao ni hapahapa duniani
 
Na wewe nawe ni mwanasheria toka wapi? Hebu kuwa mwangalifu na maandishi yako kwanza. In tandem na sio intandem!

Wenzio wanadeal na substantive law wewe unahangaika na procedural laws, sio kosa lako ukanjanja tutakutana AGM ya TLS tufundishane zaidi bwana mdogo
 
Daaaahngoma inogile! Kumtenganisha nchemba na hii case ni utovu wa nidhamu!
Cc Molemo
 
Last edited by a moderator:
Ninawasiwasi kama hata Mwigulu mwenyewe kama anafahamu kitu alichocheza nacho kwamba kina maafa kiasi gani kwake mwenyewe,familia yake na Taifa kwa ujumla.Labda ni ile kujiona kujua sana kila kitu mwisho wa siku unaangukukiwa na nyumba mbovu.
elimu ya Madelu na mambo anayo yafanya havifanani kabisa!
 
Nauona mtego wa ndege mjanja ila ngoja kwanza nisafishe tena kioo cha mauwani yangu ..ni sawa, ndo yeye Mugulu Mcheba!!
 
Wenzio wanadeal na substantive law wewe unahangaika na procedural laws, sio kosa lako ukanjanja tutakutana AGM ya TLS tufundishane zaidi bwana mdogo
Hio sheria unayoiongelea wengine tulihitimu zaidi ya miongo mitatu iliyopita. Tulia dogo, usilete kujua sana. Tutabanana humu humu na watoto kama nyie mnaojifanya kujua. Kudaadadeki!
 
Mkuu Mpaka Kieleweke,
Kwanza poleni kwa yote!.
Pili mnayo team nzuri sana ya wanasheria, lakini nashauri, mara moja moja, muwe mnasikiliza maoni ya ma layman kama sisi kupitia humu jf.

Nasikitika kuwaambia kitendo cha kufungua kesi kuhoji mamlaka ya DPP, its a wastage of time!. Mamlaka ya DPP haihojiwi na mamlaka yoyote hata rais wa nchi, hawezi kuyahoji, hivyo you are fighting a loosing battle!.

Ni kweli timu yenu ya sheria is a good team, nashauri please seek legal opinion ya best criminal lawyers around, kwa sababu baadhi ya wanasheria wenu ni politiciancs, wajiangalie wasije wakaipoliticise hii kesi kuonekana its a political case, bali muendelee kuipigania iwe abduction na sio terrorisim!.

Mwisho mtake msitake, lazima Chadema kama chama, kitoe statement kuwa whatever mashitaka yanayomkabili Rwakatare, ni yake mwenyewe kama Rwakatare, vingenevyo hali ikiachwa ilivyo, kuna hatari ya jamii kuaminishwa kuwa hayo yaliiyotendeka, yamendwa kwa maelekezo ya chama, hivyo kuja kuwaingiza hata wasiokuwemo!.

Huu ni ushauri wa bure tuu toka kwa layman.

Pasco.


Pasco, wewe ni layman kweli hata huna mfano: Issue nzima ni ya kisiasa na haina mashiko yoyote: kumfutia mtu mashitaka halafu ukamwachia then ukamkamata tena hapohapo ni kuwa Serikali hawajui wanalolifanya!! Sasa kati ya CDM na Serikalimkwa maana ya DPP nani hajajipanga??!! Tatizo ulayman wako ni wa makusudi!!
 
Hio sheria unayoiongelea wengine tulihitimu zaidi ya miongo mitatu iliyopita. Tulia dogo, usilete kujua sana. Tutabanana humu humu na watoto kama nyie mnaojifanya kujua. Kudaadadeki!

Haya babu kanjanja ze paralegal talk to my avatar, tuache thread ya watu
 
Mkuu we ni mshamba sana, yaani una-quote maneno mwenyewe kwamba .......''video imewekewa baadhi ya maneno''......hapo hapo unafurahi eti wamekiri wenyewe kuwa sio fake.......ivi inapobadilishwa baadhi ya maneno inabaki kuwa origino.....we wa wapi aiseee
Hakuna binadamu asiye mshamba hapa duniani kama unafahamu maana ya neno mshamba. Back to topic,

Hakuna ushamba wowote kwenye hilo bandiko langu kwa mtu atakayesoma na kuelewa nilichokiandia.

Picha na sauti ni vitu viwili tofauti, kama sound imekuwa edited, haimaanishi na picha nayo inakuwa edited and vise-versa, otherwise vyote viwili vifanyike.

Wanasheria wanadai kichokuwa edited ni sound lakini picha ni ya Lwakatare. Sasa kitu gani umeshindwa kuelewa hapo mpaka kwa mawazo na mtazamo wako nikawa mshamba.
 
Hii Movie mbona inaanza kunoga.
Jinsi nilivyokusoma inaonekana kuna mchezo mchafu kati Ludovick, Mwigulu na Dennis.

My Take: Katiba Mpya itaamke wazi, hizi Taasisi na Mihimili za Serikali kama Mahakama, TISS (Usalama wa Taifa), Polisi, Bunge vitumikie KATIBA na sio Rais na Taasisi yake. Kuna Wazalendo wengi kwenye hizi Taasisi wenye Uzalendo na Mapenzi Mema na Nchi yetu. Mungu azidi kuwapigania kuushinda Udhalimu, Udanganyifu. Tunataka HAKI sawa kwa Wote.


Hivi sasa wanasheria wa CHADEMA wanafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la Lwakatare na makosa ambayo alishitakiwa nayo.

Anaeleza kuwa kama ameshitakiwa kwa ugaidi lazima makosa hayo yawe ni ya kigaidi, ila makosa ya Kidnapping na abduction ni makosa ya kawaida ya jinai , na kama ili yawe ya kigaidi ni lazima hayo makosa yawe yamefanyika kwa malengo ya kigaidi , na hata hati ya mashitaka haina maelezo ya makosa ya ugaidi .


Nyongeza: kuhusu video amesema tayari kuna ushahidi wa kimawasiliano baina ya Mwigulu Nchemba ya tarehe 28.12.2012 wakiwasiliana na Ludovick saa 5:55 asubuhi , na Lwakatare amesema kuwa yeye alikutana na Ludovick kuanzia saa tano asubuhi tarehe 28.

Aidha , ameongeza kuwa tarehe 27.12.2012 Denis Msacky alimpigia simu Lwakatare wakati akiwa njiani kurejea akitokea Kagera , akiwa Morogoro na kumuuliza kama yupo DSM , akamjibu yuko njiani.

Tatu, tarehe 29.12.2012 Mwigulu Nchemba , akiwa na Zitto na Mtatiro Star Tv , kipindi cha tuongee asubuhi ndipo alisema kuwa ana mkanda wa viongoz i wa chadema wakipanga mauaji ......sasa haya yote yatajulikana mahakamani.

Ziada .

Maelezo aliyotoa Lwakatare polisi kuhusu maneno yaliyoko kwenye video alisema kuwa yeye anakumbuka siku ya tarehe 28, alikuwa nyumbani kwake na Ludovick ndio alienda kwake , ila picha ya video ni ya kwake , sura ni ya kwake ila baadhi ya maneno yaliyoko sio ya kwake na ameandika hivyo , kwa hiyo kuhusu ukweli wa mkanda majibu ya kina yanatakiwa kutoka polisi , Mwigulu na Denis ndio wanajua nini kipo kwenye mkanda . Hivyo picha limeanza kuonekana , na kwa taarifa zaidi ni kuwa polisi wana video yenye dakika 27.06 na maneno yanatofautiana sana na yaliyoko kwenye You tube iliyowekwa kwenye mitandao .

Sasa polisi nao waliulizwa ni kwanini hawajamkamata aliyeweka hiyo you tube kwenye mitandao walitoa majibu yao na mawakili wanaendelea na uchunguzi wao.
 
Mkuu Bams,

Sasa naanza kupata mwanga. Kuna mdau mmoja majuzi alielezea sababu kadhaa za kwa nini ile video ya youtube iwe ni 'feki'. Mojawapo ya sababu alizoeleza ni kwamba, kuna mahali inasikika watu wanakoroga chai na kijiko kinawekwa mezani. Lakini watu hao hawaonekani na WL anaonekana anaongea tuuu, pasipo kuwa interfered na tukio la chai.

Hapa napata jibu moja; Ludo alipofika kwa WL, akikaribishwa chai na akawa anarekodi mazungumzo yao kwa simu au kwa njia yeyote na baada ya hapo akatumia hayo maneno baadhi kuingiza kwenye script lakini akasahau kufuta vijiko vikikoroga chai.

Twende mahakamani, tutayajua mambo mengi!

Cc Molemo

Kuongezea tuu pia kuna mtu aliuliza mwanzo kabisa mwa video ilipowekwa jamvini kuwa alikuwa hasikii vizuri maneno yake afu mdau mmoja akamjibu kuwa asikilize kuanzia dk ya tatu 3) nadhani hapo ndipo uchakachuaji ulipofanyika.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom