Mshombsy
JF-Expert Member
- Mar 15, 2013
- 372
- 180
Definitely asingesema kinyume na hivi ndio ingekuwa habari, wanasheria wanatetea waharifu siku zote na mtu kutoka au kusota lupango pia sio kigezo cha kusema alifanya au hakufanya. Ukweli utabaki kuwa video ya kwanza mngemuacha mwenyewe alierecord ndio ajitete mbele ya watanzania. Kwa aliyosema alipaswa kukamatwa hata serikali ingekuwa chini ya Lissu and etal.
Na chama kiendelee kuwa chama na msimamo wa mawakili hawa uwe tofauti na chama chao. Je wanalipwa na chama kwa kazi hii!
Walioweka sheria hawakuwa wajinga, video sawa tunamuona Lwakatare anaongea lakini aliongea akiwa na nia gani.
1. Inawezekana alitaka kumdhuru Msacky
2. Inawezekana Ludo alimwambia Lwakatare wanachotafuta akina Mwigulu Nchemba na Msacky hivyo wakaamua kurekodi video kwa kuangalia ni sheria zipi watazitumia mahakamani incase akikamatea. Wote walitaka kucheza propaganda.
3. Kulingana na maelezo ya Lissu, inawezekana Ludovick alimuingiza jamaa mkenge ili tu apate video, sheria zitaangalia je alikuwa na hiyo nia kabla hata ya Ludo kumfata, na je Ludo ana mafunzo gani kumchezea mtu saikolojia na kumpoteza aseme unachomuelekeza ( soma jinsi polisi wanavyohoji jambazi mpaka anakiri kosa au soma yule jamaa aliyemuua rais kennedy wa marekani.)
4. Mkanda una karibu miezi miwili na nusu umerekodiwa kwanini usingetolewa mapema, je kuna uwezekano wa kuhariri video? Je kuna vitu vimeyolewa pengine mwanzo alisema ngoja tuwachezee akili hawa watu.
5. Je polisi wanazo karatasi original alizoandika lwakatare au wame pause video youtube wakaprint. Kwanini? Isije ikawa ni hao hao akina lwakatare wanacheza propaganda
6. Tuiachie mahakama iamue. Akishinda mahakamani bado mahakama ya umma kwenye masanduku ya kura