Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA walonga

Usije shangaa hili likaipatia umaarufu Chadema. Naanza kuiona kama ni movie iliyopangwa kila upande ukitaka kumwingiza mwingine matatani. Wasipocheza vizuri CCM watajikuta wamenasa kwenye mtego wa Chadema. Nani alijua Lema angerudishiwa ubunge baada ya kuvuliwa na mahakama? Katika mazingira haya kuna uwezekano wa kila upande kuwa na 'mapandikizi' Serikali inaangushwa na wataalamu wake ambao wamelewa madaraka kiasi cha kutoonyesha umakini katika utendaji wake loophole ambayo wataalamu wa Chadema wanaweza kuitumia kukuza majina yao na kukiongezea chama umaarufu. Ni mapema kujua nani atatoka na kicheko hapa. Tuvute subira ni mchezo usiotabirika!

mkuu hii movie naifananisha na game ya barca(cdm) vs ac milan(ccm) agr 2-4
 
Wewe si ndio nimekuambia maji yako shingoni ukajifanya hujui?.
Acha kusingizia uwezo wa wanasheria wa serikali, Kutetea uwongo huwa ni ngumu hata uwe mwanasheria vipi.

Acha ifahamike tu.
Mkuu, hivi una matatizo gani. Maji yako shingoni kwa nani?.

I'm not a blind follower kama unavyojitandaza kwenye mabandiko yako. Uongo upi unaousema?.

Ninapenda open discussion na ndiyo hiyo tulikuwa tunajadili na Lukolo.

Wewe unataka kwa nguvu zote na kwa njia yoyote mawazo yako yawe ndiyo kweli daima wakati hata hufahamu matokeo ya kesi yenyewe.

Tafuta mtu mwingine mwenye mawazo kama yako ndiyo mtaelewana.

Mitanzania mingine bana. Khaa
 
Last edited by a moderator:
Mie kwa mtazamo wangu nafikiri serikali ya CCM kupeleka hii kesi mahakamani kwa kutumia cheap video watakuwa wamejichoma kijiti cha muhogo masaburini. Kwa uelewa wangu: Unapotumia digital file(s) as evidence before the court(s), hapa una- involve computer forensic.

Kwa faida ya JF mambers and non-members: Wale mliosoma Cyber-crime or Cyber-security, Once you decide to present digital evidence before the court, you are mandated by law (sijui sheria ya kwetu) to show/prove that you're disciplined in associating elements of law and computer science to gather, secure, examine, and analyze data from computer systems, networks, wireless communications, and storage devices in a way that is admissible as evidence in a court of law. Kwa serikali yetu sina hakika if that happened.

1. The Magamba's gov needs to prove that whatever they gathered during their raid(s) wasn't contaminated.

2. The Magamba's gov needs to show how they examined the data collected (Ni computer lab gani waliweza ku-examine digital file from public domain in less than 17 hrs) iwapo mpaka dakika hii wameshindwa kukamata wale wezi wa TRA waliotumia mtandao 2 yrs ago (Kitillya knows what I'm talking about).

3. The Magamba's gov needs to prove they analyzed the collected data thoroughly and none of information byte(s) omitted/added.

4. The gov also needs to prove before the court that people who collected, secured, examined, and analyzed the data from Youtube domain are ethical and the whole process wasn't interfered by external pressure.

Inasemekana hiyo video ilikuwa edited, na sehemu nyingine ikiwa imeondolewa. Kwa mtazamo wangu, Information gathered wasn't secured before presented kwa mahakama ya Umma (video haijaonyeshwa mahakamani). Serikali inatakiwa ionyeshe hatua kwa hatua jinsi walivyoweza ku-secure hiyo process nzima hadi kumpeleka Lwakatare before the court.
Waeleze kama walikuwa na hiyo video kabla haijawekwa kwenye public domain (Youtube). Kama walikuwa hawana, waeleze hiyo process ya ku-gather and analyze digital file ilivyochukuwa muda mfupi bila ya kuwa na original storage media. Na kama walikuwa na original storage device(s), kwa nini sehemu ya video imekatwa?

Huu ni mtazamo wangu tu ingawa mimi si mwanasheria lakini nina background ya Digital Forensic Investigations.

well said mkuu aliyechora huu mchezo na walioshiriki kutekeleza wanifikiri mwisho wa pua. Mwisho wa ubaya ni aibu hofu yangu mwendelezo wa kesi hii kunaweza kupelekea mwisho wa mwaka tuka export container la kucha
 
Mkuu, hivi una matatizo gani. Maji yako shingoni kwa nani?.

I'm not a blind follower kama unavyojitandaza kwenye mabandiko yako. Uongo upi unaousema?.

Ninapenda open discussion na ndiyo hiyo tulikuwa tunajadili na Lukolo.

Wewe unataka kwa nguvu zote na kwa njia yoyote mawazo yako yawe ndiyo kweli daima wakati hata hufahamu matokeo ya kesi yenyewe.

Tafuta mtu mwingine mwenye mawazo kama yako ndiyo mtaelewana.

Mitanzania mingine bana. Khaa
Mkuu, mimi nina matatizo na watu kama wewe wanaotetea maovu kwa kujifichaficha.
Maji ni ya shingo kwa watetezi wa filamu, ninaamini wewe ni mmoja wao, kitu unachojidanganya ni kudhani kuwa unaandika ki tactic sana na kwamba unaficha mrengo wako, sio kweli, unaeleweka vizuri mno wa kwetu.

Nahisi wewe ndio unaweza kuwa blind follower kwa sababu ukiunganisha matukio ni lazima uamini kuwa clip imepikwa, na ndio uongo ninaouzungumzia. soma tena post hapo juu vizuri.

OMISHA MHOLA NKOYI?
 
Mbona wanasheria hawasemi ile video ni fake?

Kama ule mkanda nk genuine basi huo ni ugaidi.

hao ni wanasheria hawawezi kuropoka kitu ata kama ni cha kweli kama hawana ushahidi wa kuithibitishia mahakama. Na kama akili yako ni nzuri utagundua hoja zao za kisheria juu ya VIDEO hiyo ni kutaka kusibitisha kuwa ni feki na kutengeneza kwa maswali yafuatayo?
Nani kairekodi ili aelezee mazingira yote ya tukio ata yasioönekana watu wote waliokuwepo na jinsi alivyoirekodi
2. Je alikuwa na kibali cha kuirekodi? Kama sivyo si halali
 
Lissu kabla hajayasema haya aliwasiliana na Katibu mkuu wake? Maana huyo babu alikwisha sema hii video ni ya kuchakachua hadharani. Kweli Lissu kesi imefikia patamu sana na kwa kazi ya kumlinda Slaa Ludo atakuwa na mengi mno ya kushare na dunia.

nduka kijana wa kichaga mwenye makuzi ya tabora vuta subira sindano imeshaingia dawa inafuata.
 
Lissu kabla hajayasema haya aliwasiliana na Katibu mkuu wake? Maana huyo babu alikwisha sema hii video ni ya kuchakachua hadharani. Kweli Lissu kesi imefikia patamu sana na kwa kazi ya kumlinda Slaa Ludo atakuwa na mengi mno ya kushare na dunia.

nduka kijana wa kichaga mwenye makuzi ya tabora vuta subira sindano imeshaingia dawa inafuata.kwani kuna mahali lissu amesema hii video ni genuine?
 
Tundu Lissu siku ile alijidhalilisha sana pale mahakamani mpaka akachekwa na umati wa watu!!!​



 
Ccm inabaka uhuru wa mihimili mingine ya dola.
Ccm utawala wako umepimwa kwenye mizani na umeonekana umepungua, siku zako zinahesabika, jiandae kuwa chama cha upinzani.
Tunataka ccm imara itakayochalenge chama tawala, ccm hii ya akina Nchemba haitoshi kuwa chama makini cha upinzani.
Tafadhali tunataka watu wanaofaa kuwa wapinzani mwaka 2015.
 
Lissu: Mwigulu na Ludovick ndio waliotengeneza video ya Lwakatare

Published on 21 Mar 2013Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu amesema video iliyowekwa mitandaoni imetengenezwa na Mwigulu akishirikiana na Joseph Ludovick. Lissu amesema endapo kesi hiyo itafika Mahakamani hawatamaliza hada masaa matatu (3) watakuwa wameshinda;


source: chadematv youtube
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, mimi nina matatizo na watu kama wewe wanaotetea maovu kwa kujifichaficha.
Maji ni ya shingo kwa watetezi wa filamu, ninaamini wewe ni mmoja wao, kitu unachojidanganya ni kudhani kuwa unaandika ki tactic sana na kwamba unaficha mrengo wako, sio kweli, unaeleweka vizuri mno wa kwetu.

Nahisi wewe ndio unaweza kuwa blind follower kwa sababu ukiunganisha matukio ni lazima uamini kuwa clip imepikwa, na ndio uongo ninaouzungumzia. soma tena post hapo juu vizuri.

OMISHA MHOLA NKOYI?

Hayo unayoniambia ni mawazo yako, kwa nini unataka nami niunge dots kama ulivyounga wewe ili nikubaliane na wewe.

Halafu umekazania maji yamenifika shingoni kwa sababu unafikiri kila mtu yuko jukwaa la siasa kwa malengo.

Swala la kuandika kwa tactics hilo la kwako kadri unavyofikiria.

Kitu cha kushangaza umeng'ang'ania video na maneno ya wanasheria wa Lwakatare. Wa kwetu ulitegemea watasema nini zaidi ya hayo.

Hatuwezi kurumbana wakati kesi iko mahakamani. Mahakama itatoa majibu.

Binadamu tuko tofauti na cha muhimu ni kukubali kutokubaliana.

NALE KULE, NAJA KULALA EHAHA, ULE NAMA MASAA 7 MBELE YANE.
 
Kuna kitu ambacho Wanasheria wa CHADEMA wanashindwa kukisema badala yake wanaweka privacy law mbele na kusema imevunjwa kwa Lwakatare kurekodiwa bila idhini yake.

Swala la mtu kurekodiwa anafanya kosa haliwezi kufunikwa na privacy law. Lwakatare amerekodiwa anatenda kosa na kosa hilo haliwezi kuwa siyo kosa kwa sababu privacy law imevunjwa.

Kitu cha muhimu kabisa katika kesi hii, ufunguo wa kesi hii uko na Ludovick kama kweli alikuwa ndiye anarekodi. Ushahidi wake ndiyo utatoa picha mbadala ya nini kilikuwa kinafanyika CHADEMA.

Tusibiri tusikie upande wa pili katika kesi hii kwa sababu kwa sasa tunafanya judgement kwa maelezo ya upande mmoja.

ingekuwa busara kama mngewashauri hao ndugu zenu kabla hawajatoa movie yao.jielekeze pia kuwashauri mawakili wa serikali coz wao ndiyo wanahitaji msaada wa waandaji wa tukio na movie
 



286_muganyizi.jpg



  • Orodha ya watuhumiwa ndefu, msako wa polisi
  • waendelea

WINGU limeendelea kutanda kuhusu mkanda wa video wenye picha ya Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Bukoba Mjini, kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Wilfred Lwakatare.

Wingu la sasa linahusisha taarifa za uhakika ambazo gazeti hili limezipata zinaendelea ya kuwa operesheni ya kusaka watuhumiwa zaidi katika sakata hilo imeshika kasi, ikiwa ni matokeo ya mahojiano yaliyoendeshwa kati ya maofisa wa polisi na Lwakatare, pamoja na mwenzake, Ludovick Rwezaura.

Swali kubwa sasa ni je, nani wengine wataingizwa katika orodha ya watuhumiwa wa vitendo dhidi ya baadhi ya watu, akiwamo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda, aliyetekwa, kupigwa na kujeruhiwa vibaya kiasi cha kupoteza jicho lake moja.

Wingu hilo linazidi kutanda katika wakati ambao Lwakatare amefikishwa mahakamani akishitakiwa kwa makosa manne, likiwamo la kula njama ya kutenda kosa la jinai la kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru Dennis Msacky, ambaye ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, njama ambazo wanadaiwa kuzipanga eneo la King'ong'o, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Shitaka jingine la pili linalomkabili Lwakatare na mwenzake, Ludovick Rwezaura ni kula njama ya kufanya kosa la jinai kinyume cha kifungu cha 24 cha Sheria dhidi ya Ugaidi. Na tatu ni kufanya mkutano wa vitendo vya kigaidi, kinyume cha kifungu cha 5 (a) cha sheria namba 21 inayopinga ugaidi, wakati shitaka la nne dhidi yao ni kudaiwa kuhamasisha vitendo vya ugaidi.

"Baada ya mahojiano na Lwakatare kuna masuala ya msingi ambayo ni kama yameelekeza polisi kuendelea na msako wa baadhi ya watuhumiwa katika matukio haya ya utekaji na utesaji. Unaweza kushangazwa na majina makubwa ya watu wengine wanaoweza kunaswa," anaeleza mmoja wa maofisa wa polisi aliyezungumza na mwandishi wetu kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, inadaiwa ya kwamba, baada ya mahojiano na Lwakatare ndipo polisi walipobaini umuhimu wa kumsaka Ludovick Rwezaura na kwamba, wapo watuhumiwa wengine watatu wanasakwa na polisi katika mazingira ya usiri mkubwa.

Hata hivyo, pamoja na kuwapo kwa taarifa hizo kutoka ndani ya Jeshi la Polisi bado haijawekwa wazi kama wengine watakaokamatwa watafunguliwa mashitaka au watatumika kama mashahidi wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo dhidi ya Lwakatare na mwenzake, Ludovick.

Taarifa zilizovuja siku moja kabla ya Lwakatare kufikishwa mahakamani zinadai ya kwamba, yapo baadhi ya mambo ambayo Lwakatare aliyakana na kutoyatambua ambayo yamejionyesha katika picha ya video iliyopachikwa kwenye mtandao wa jamii forum, wiki iliyopita lakini pia, kwa upande mwingine, inadaiwa kuna ambayo yaliyomo kwenye video

hiyo kuwa alikiri kuyatambua. Gazeti hili linashindwa kufichua yapi aliyakana Lwakatare na yapi aliyatambua kutokana na suala hilo kufikishwa mahakamani tayari.

Lwakatare alifikishwa mahakamani Jumatatu wiki hii na kunyimwa dhamana na hadi jana Jumanne tunakwenda mitamboni, bado dhamana ilikuwa haijapatikana, huku mawakili wa pande zote wakiendelea kupambana kisheria ili ama apate dhamana hiyo au anyimwe.

Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka unaongozwa na Wakili wa Serikali, Prudence Rweyongeza na upande wa utetezi unawahusisha mawakili, Peter Kibatala, Tundu Lissu, Profesa Abdalah Safari na Nyaronyo Kicheere
.
http://www.raiamwema.co.tz/lwakatare-utata










 
Kesi yenyewe kama magumashi vile,ya kuchongwa chongwa au ya kuungaunga. Hao wengine basi wakamatwe mapema.
 
Nataka Mwigulu, Membe na wengine waingizwe kwenye hili sakata. Wasipowaingiza hao na wengine, kesi hii ni upuuzi mwingine na dhulma dhidi ya upinzani.
 
Hivi sasa wanasheria wa CHADEMA wanafanya mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la Lwakatare na makosa ambayo alishitakiwa nayo.

=========
Kiongozi wa jopo la wanasheria watano (5) wanaomtetea Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare, Wakili Tundu Lissu, akiwawakilisha wenzake, ameongea na vyombo vya Habari akiwa Makao Makuu ya CHADEMA na kuzungumzia masuala kadhaa kutokana na sakata hili.

Lengo kuu la mkutano huo na wanahabari lilikuwa ni kuutarifu umma wa Watanzania kupitia kwa wanahabari juu ya hatua ambayo mawakili hao wameamua kuchukua kwa kupeleka ombi Mahakama Kuu ya Tanzania, chini ya hati ya dharura ili Mahakama hiyo ya juu iitishe mafaili yote mawili yaliyofunguliwa kuhusu kesi ya Lwakatare, yaani faili la kesi iliyofutwa na faili lililofunguliwa baada ya kesi ya awali kufutwa, wakiiomba mahakama iangalie na kujiridhisha…


Kuhusu video
Wanahabari walitaka kujua maoni yake kuhusu video na namna kesi hiyo ilivyo, hasa kutokana na alivyoielezea ‘charge’ ilivyo ‘defective’, ambapo Wakili Lissu kwa maoni yake, alisema kuwa kuna masuala mengi yanatakiwa kuwekwa wazi kuhusu video yake, akihoji maswali kadhaa:


- Nani aliyemrekodi Lwakatare? Je, Lwakatare alijua kuwa anarekodiwa? Je, aliruhusu? Kama hakuruhusu, ilifanyika kihalali? Je, haivunji katiba ya nchi inayozungumzia privacy ya mtu? Je, baada ya kurekodiwa mkanda huo ulipelekwa wapi? Nani alikuwa nao? Je, umefanyiwa uhariri (editing) na nani? Je, aliyemrekodi alitumwa na nani?

Ushahidi mwingine
Ameongeza kuwa, video inaonekana imechukuliwa tarehe 28 Desemba, siku iliyofuata, Desemba 29, kwenye kipindi cha TV, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akaanza kusema kuwa anayo video ya viongozi wakuu wa CHADEMA wakipanga mipango ya mauaji ya dhidi ya Watanzania.


Amezungumzia mawasiliano ya mtu anayeitwa Michuzi, kuwasiliana na watumishi wenzake wa OBR, akiwapongeza na kutoa kudos kwa TISS kwa kazi nzuri, akiwataka wenzake wapige sana kelele kwani hiyo ni kete muhimu kwa CCM. Amesema kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa, hawaruhusiwi kufanya surveillance dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa CCM, kwa sababu upinzani wa kisiasa ni suala lililoruhusiwa kisheria nchi hii.

Aidha, Lissue ameongeza kusema wamepata mawasiliano ya simu yakionesha kuwa siku hiyo hiyo ambayo video imerekodiwa, majira ya saa 5.59, mtu aitwaye Ludovick alimpigia simu mtu aitwaye Mwigulu Nchemba.

Kwa mujibu wa Wakili Lissu, yamepatikana pia mawasiliano ya mtu aitwaye Dennis Msacky akimpigia simu Lwakatare, ambapo wamemuuliza Lwakatare iwapo ni kweli aliwasiliana na mtu mwenye jina hilo (ambaye kwenye charge sheet ya pili, polisi wameonesha ndiye aliyekuwa akipangiwa kutekwa/kufanyiwa vitendo vya ugaidi), naye amekubali kuwa ni kweli alimpigia simu siku moja kabla ya tukio la kurekodiwa, akimuuliza kama amerudi Dar es Salaam, naye akamwambia alikuwa njiani kutoka Bukoba.

Amemaliza kwa kusema kuwa kesi hii ni kama kesi nyingine za kupikwa, ambazo polisi wamekuwa wakifungua dhidi ya CHADEMA na viongozi wa chama hicho, kwa nia ya kuiokoa CCM, kwasababu chama hicho kimekaliwa vibaya na hakiwezi tena kufanya siasa za ushindani dhidi ya wapinzani wao wakuu, CHADEMA.


===========
Habari hii unaweza kuisoma kwa kirefu -> Sakata la Lwakatare: Wanasheria CHADEMA ‘wafunguka’! | Fikra Pevu
Is the video authentic?That's a legitimate question ,the rest will flow.
 
Back
Top Bottom