WANAKIJIJI NA KISA CHA WANYAMA WALA MIFUGO.
Wananchi wa kijiji cha Mkwapuaji wamevamiwa na wanyamapori hatari. Simba na chatu wakubwa wamekivamia kijiji hicho na kuanza kuua mifugo ya wanakijiji. Wanakijiji wamekosa pa kukimbilia, kwani simba ameshafanya jaribio la kula mtu pia, bahati mtu huyo aliponea chupuchupu kwa kuokolewa na wanakijiji wenzake. Kijiji kizima kinaonekana kukosa msaada, kinatahamaki kifanye nini, makao ya wilaya wako kimya mpaka sasa. Ghafla, jamaa mmoja ambaye hakuwepo muda mrefu amewasili kijijini. Jamaa huyu amerudi na mkuki na bunduki ambazo kutokana na minong'ono ya chinichini zote zinasadikika kuwa ni mali ya wizi. Jamaa alijipatia silaha hizo katika mazingara ya kutatanisha huko wilayani. Mara barua inawasili kwa mzee wa kijiji kutoka makao makuu ya wilaya. Ya kwamba, silaha hizo mbili, na zile risasi zilizomo kwenye bunduki zishikiliwe zisitumike, maana ziko kwenye kesi huko makao makuu ya wilaya.
Wanyama wanaendea kuua mifugo ya wananchi. Na siku chache zilizopita ile bahati mbaya ikawafika wanakijiji, mmoja wao ameuawa na simba. Bunduki na risasi zilizopo zinaweza kutumika kuwaangamiza wanyama hao. JE WANAKIJIJI WATUMIE HIZO SILAHA?!
SteveD.
unaweza kutumia JINI kupepea JINI na hali ikawa shwari.......however suala linakuja pale hayo MAJINI yatakapokaa na kukubaliana kushirikiana ili kuendeleza life yao.........
dawa ni kuliondoa JINI(simba/chatu).......period.......How....Mwenyezi Mungu ametupa akili..........hata kwa kuchonga mawe simba tutamuwinda na moto wa asili tutawasha na chatu ataungua.........
BTW....yule jamaa aliyeleta silaha ni Msaniii tu...hana lolote