Mafisadi nchini wanaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu:-
1. Mafisadi papa
2. Mafisadi sangara
3. Mafisadi dagaa
Mafisadi papa
Hawa ndio wale unaoweza kusema kwa hakika wameiweka dola mfukoni - siyo Pinda, Mwema, Manumba wala Hosea mwenye ubavu wa kuwanyoooshea kidole hawa. Ni hawa serikali imewahi kudai wanaweza kuiyumbisha nchi wakichukuliwa hatua kwa sababu wana uwezo mkubwa kifedha karibu sawa na serikali. Wao ndio huifadhili hata chama kinachounda serikali na wana influence kubwa hata katika uteuzi mbali mbali - hii inatokana na wao kuwasaidia viongozi mbali mbali kungia madarakani. Ni hawa majina yao yananong'onwa migahawani na kwa vificho kwa hofu ya kushambuliwa na hata kutishiwa kuuwawa ikibidi. Reginald Mengi hataki tena kunong'ona na sasa kathubutu kuwataja hadharani !!
Mafisadi sangara
Hawa wanaongozwa na mwenzetu ambaye sisi wenyewe tumempa dhamana ya kutuongoza bila kufahamu vizuri alivyofadhiliwa na mafisadi papa. Chini yake kuna wafuasi ambao wamepewa nyadhifa nzito katika jamii na chama tawala. Katika hali ya kujikaanga wenyewe kwa mafuta yao wenyewe hivi sasa wamegawanyika katika makundi makundi mawili yanayopingana - kundi linalojuta kwa kushikiwa bango na wananchi na kundi linalojaribu kujisafisha kwa kutumia maji taka. Lakini kwa kuwa wote wana mshikamano ndani ya chama tawala hakuna wa kuwanyooshea kidole. Wanazo nguvu za dola lakini nguvu yao ya pesa lakini benki zao wanakochota zimeshkiliwa na mafisadi papa. Dr. Slaa aliwahi kuthubutu kuwataja wengine hadharani !!
Mafisadi dagaa
Hawa nao ni wa kuogopwa kama ukoma kwa sababu ya kujali maslahi binafsi na wako tayari kuwatetea mafisadi na hivyo kudhoofisha vita yetu dhidi ya ufisadi. Humu wamo watu wa kawaida walio msitari wa mbele katika kuwadhihaki watu wanaoonekana pia kuwa msitari wa mbele kulaani ufisadi. Bahati mbaya miongoni mwao wapo waandishi wa habari ambao wako tayari kutumia taaluma yao kupotosha ukweli na kuuita uwongo. Sasa hivi tunashuhudia harakati za kujaza kipenzi chetu JF kwa michango isiyo na kichwa ama miguu wakati wowote mafisadi wanaposhambuliwa. Tulishuhudia shujaa Dr. Slaa alivyoshambuliwa wakati akitoa list of shame na hivi sasa tunashuhudia Mengi kwa kuanika list ya mafisadi papa !!
Wana JF wenzangu you cant eat youe cake and have it - ama uko kwa mafisadi au uko mbali nao, period. Pesa walizonazo mafisadi ni zetu na zimetokana na wizi wa mali zetu na investment yao kubwa ni kwenye mtandao wa ufisadi na hivi sasa wanavuna. Misaada waliyoipa chama tawala sasa wanairudisha na kwa faida kubwa kuliko hata mavuno makubwa ya mbegu za DECI !! Tungemwuunga mkono Dr. Slaa miaka miwili iliyopita labda tungekuwa tumeshakata mzizi wa fitina. Kwa bahati Mengi ameamua kum'grab the bull by its horns' - tumpe support safari hii. Mtu binafsi hawezi kupambana na Raisi tuliyemchagua kwa kura zetu lakini anao uwezo kabisa wa kukatakata mizizi inayompa uhai. Mengi kaonyesha njia - tumpe support !!

Kwani bila mizizi, mbuyu utawezaje kusimama?