Rostam na Manji watoe maelezo vinginevyo watiwe pingu!

WANAKIJIJI NA KISA CHA WANYAMA WALA MIFUGO.

Wananchi wa kijiji cha Mkwapuaji wamevamiwa na wanyamapori hatari. Simba na chatu wakubwa wamekivamia kijiji hicho na kuanza kuua mifugo ya wanakijiji. Wanakijiji wamekosa pa kukimbilia, kwani simba ameshafanya jaribio la kula mtu pia, bahati mtu huyo aliponea chupuchupu kwa kuokolewa na wanakijiji wenzake. Kijiji kizima kinaonekana kukosa msaada, kinatahamaki kifanye nini, makao ya wilaya wako kimya mpaka sasa. Ghafla, jamaa mmoja ambaye hakuwepo muda mrefu amewasili kijijini. Jamaa huyu amerudi na mkuki na bunduki ambazo kutokana na minong'ono ya chinichini zote zinasadikika kuwa ni mali ya wizi. Jamaa alijipatia silaha hizo katika mazingara ya kutatanisha huko wilayani. Mara barua inawasili kwa mzee wa kijiji kutoka makao makuu ya wilaya. Ya kwamba, silaha hizo mbili, na zile risasi zilizomo kwenye bunduki zishikiliwe zisitumike, maana ziko kwenye kesi huko makao makuu ya wilaya.

Wanyama wanaendea kuua mifugo ya wananchi. Na siku chache zilizopita ile bahati mbaya ikawafika wanakijiji, mmoja wao ameuawa na simba. Bunduki na risasi zilizopo zinaweza kutumika kuwaangamiza wanyama hao. JE WANAKIJIJI WATUMIE HIZO SILAHA?!

SteveD.

unaweza kutumia JINI kupepea JINI na hali ikawa shwari.......however suala linakuja pale hayo MAJINI yatakapokaa na kukubaliana kushirikiana ili kuendeleza life yao.........

dawa ni kuliondoa JINI(simba/chatu).......period.......How....Mwenyezi Mungu ametupa akili..........hata kwa kuchonga mawe simba tutamuwinda na moto wa asili tutawasha na chatu ataungua.........

BTW....yule jamaa aliyeleta silaha ni Msaniii tu...hana lolote
 
Mengi amejitahidi kuwa 'jasiri' kwa kuwataja hao anaowaita mapapa wa rushwa. Hata hivyo kuna vitu kadhaa vya kuvitazama kama angalizo kabla ya kukimbilia kummininia sifa Mengi. Mosi, hawa wote aliowataja Mengi hawawajibiki kwetu. Pili, ufisadi tunaongelea hapa ni ufisadi uliofanyika serikalini kupitia, pamoja na njia nyingine za kishetani, tenda za ujanjaujanja. Kama ni tenda ya Dowans/Richmond, Rostam hakujipa, alipewa na viongozi wetu. Kama ni ndege ya kitapeli ya Rais, ni viongozi wetu ndio waliong'ang'ania tununue hata walipoambiwa na wataalamu kwamba haifai. Hiyo IPTL ni viongozi wetu ndio walioshinikiza tuingie mkataba. Waliosaini mikataba ya kitapeli ya madini ni viongozi wetu, huku wakiwa na taarifa sahihi kabisa kwamba hiyo mikataba haina tija kwa nchi. Walichofanya hawa ambao Mengi anawaita mapapa wa ufisadi ni kutumia ulafi na ujinga wa viongozi wetu katika kujineemesha kibiashara; na kwa kweli hata wao waliwahi kusema wazi kabisa kupitia nyaraka zao (rejea waraka wa Jeetu Patel katika mitandao). Kwa maneno mengine hawa aliowataja Mengi ni mawakala tu wa ufisadi; mafisadi hasa ni hao viongozi wetu na ndio tunapaswa kuwabebea bango.

Sasa, ambacho kinanisumbua mimi ni kwa nini sisi tunafurahia sana Mengi kuwataja watu waliotumia ulafi na udhaifu wa viongozi wetu kujineemesha badala kuwataja hao viongozi wenyewe? Wajibu wetu wa msingi kama wananchi, akiwemo Mengi, ni kuwajibisha viongozi wetu, ikiwa ni pamoja na kuwaajibisha kwa kushindwa kuwaajibisha wavunjifu wa sheria kama hao aliowataja Mengi.

Kwangu mimi alichofanya Mengi ni kujaribu kututoa katika msingi wa vita hii dhidi ya ufisadi, ambayo kimsingi ni vita dhidi ya viongozi walafi na dhaifu ndani ya serikali ya CCM.

Na kwa maoni yangu, vita ya kweli dhidi ya ufisadi katika nchi yetu haijaanza. Itaanza siku tutakapofanikiwa kuoanisha uwepo wa CCM madarakani na uwepo wa huo ufisadi. Ndio kusema vita ya kweli ya ufisadi itaanza siku tutakapoanzisha vita ya kweli ya kuitoa CCM madarakani, na tukianza vita hii sidhani kama Mengi atakuwa moja wa wapiganaji!

Nakubaliana na wewe kwa saana tu.....however, ukiangalia kw aundani utagundua kuwa Mastermind wa hayo madili machafu ni hao akina Rostam et al.....unakumbuka jinsi viongozi walivyoingizwa mkenge wa Madeni na kijana Manji......yes ilitokana na ulafi wa viongozi wahusika lakini initial move ilitoka kwa Manji baada ya kuona anaweza kupata dili kupitia viongozi

Trust me viongozi wetu wengi ni vilaza.....Just put Mkulo in every aspect the dude ni Kilaza mpaka hajui anachofanya na Bosi wake PM ame-reveal hivyo........

Well, wananchi pia tuna nafasi yetu ktk huu UOVU.....sasa wanaharakati inabidi kuongeza nguvu ili kuwaamsha wananchi waone UOVU wa viongozi wao (mfano mzuri ni debate inayoendelea sasa ndani ya Bunge kuhus siri za serikali)........yaani MIBUNGE MIJINGA IPO PALE badala ya kuchukua that as an opportunity ya kukemea UOVU uliofichuliwa yenyewe inasema eti siri za serikali.....thinking siku moja nao watakuwa kwenye nafasi za kuendeleza UOVU.........

.........sasa basi MIBUNGE kama ile ndio ya kuanza nayo.......tuwaelimishe wananchi na kuishikia bango ili isirudi bungeni........
 
Trust me viongozi wetu wengi ni vilaza.....Just put Mkulo in every aspect the dude ni Kilaza mpaka hajui anachofanya na Bosi wake PM ame-reveal hivyo........

Agreed, hawa ni vilaza wa kutupwa, hawana vision ni vipofu na ''malaya'' Hawa mfisadi wanawadanya kirahisi sana kwa token rewards /commission...wao wanakubali kuliuza taifa kwa vipande viwili vya dhahabu chafu, mfisadi wanaishia kuchukua clean dhahabu maisha yao yote!

Well, wananchi pia tuna nafasi yetu ktk huu UOVU.....sasa wanaharakati inabidi kuongeza nguvu ili kuwaamsha wananchi waone UOVU wa viongozi wao (mfano mzuri ni debate inayoendelea sasa ndani ya Bunge kuhus siri za serikali)........yaani MIBUNGE MIJINGA IPO PALE badala ya kuchukua that as an opportunity ya kukemea UOVU uliofichuliwa yenyewe inasema eti siri za serikali.....thinking siku moja nao watakuwa kwenye nafasi za kuendeleza UOVU.........

.........sasa basi MIBUNGE kama ile ndio ya kuanza nayo.......tuwaelimishe wananchi na kuishikia bango ili isirudi bungeni..

Hi ndio fimbo halisi kwa hii MIBUNGE ambayo inaona kama ubunge ni urithi wao, alichukua babu yake, akachukua baba yake na sasa yeye so wanafanya kazi kwa mazoea na kushiriki katika maamuzi yanayowanufaisha wao binafsi badala ya wananchi wakati wametumwa na wananchi!

Ndugu wananchi adhabu ya wabunge hawa tunayo mikononi mwetu, ni kuhakikisha wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika maamuzi tata mwakani hawarudi mjengoni..please!
 
Ogah,

Mchawi wewe unadhani ni kuondoa CCM? Kenya waliondoa KANU, Zambia UNEP je leo hii rushwa Kenya mbona ndo imeongezeka?

Ni kweli mchawi ni CCM?
 
Kwani kuna mtu anasema kuwa awafungulie mashtaka NJE ya sheria? Hata kuamuru walio na uwezo huo wa kisheria kufanya uchunguzi na kama patakapoonekana kuna kesi ya kujibu wawafungulie mashtaka hana mamlaka?

Msimamo wako unazua swali lingine. Je mheshimiwa Rais ana mamlaka ya kuamuru mtu ASIFUNGULIWE mashtaka? Hata kama ushahidi upo, je anaweza kumzuia mfungua mashtaka wake asifuatilie kesi kwa sababu yeyote ile ( hali ya usalama wa taifa n.k.) au hata bila kutoa sababu?

Amandla.........

Hana nguvu hizo! Hili mbona wala halina utata. Nguvu pekee ambazo watu wanafikiri anazo ni katika Emergency Powers; na EP inatumika and certain conditions na siyo za kutumika kama anajisikia tu. Nje ya EP, Rais hana uwezo wowote wa kutaka mtu ashtakiwe au asishtakiwe.

Nguvu nyingine ambazo anazo ni zile za kusamehe aliyehukumiwa; nguvu hii ni absolute. Lakini hawezi kumsamehe mtu kabla hajashtakiwa na kukutwa na hatia!

Ndiyo maana Hosea na Marando wote wamekosea in fact and in law.
 
Ogah,

Mchawi wewe unadhani ni kuondoa CCM? Kenya waliondoa KANU, Zambia UNEP je leo hii rushwa Kenya mbona ndo imeongezeka?

Ni kweli mchawi ni CCM?

hivi kuna sehemu nimesema CCM kama KANU/UNEP waondoke?...au kuna sehemu nimesema CCM ndio wachawi?...........please usiniingize kwenye MIVYAMA YENU kiaina
 
mwanakiji, bak, invinsible na mtu mwingine yeyote fanyeni mambo mtuwekee hiyo press conf audio au video
 
Hii nchi ni yetu sote, Mengi na mimi hatuna tofauti when it comes to maslahi ya taifa. Alilofanya Mengi ni jambo kubwa sana na tunatakiwa wote tujitoe kila mmoja kwa namna yake kuendeleza huu mpambano. 'Inatakiwa afanye action...' kwani yeye ni nani nchi hii? Nchi sio yake peke yake? Angekuwa yeye ni rais tungejua anafanya kazi tuliyomwajiri kufanya. Kumbe la, anajitolea tu! Tusipende kukaa na kumtegemea mtu mmoja tu ajitolee kwa ajili yetu. Na sisi tutoe michango yetu!

maneno mazito sana haya, Mkuu! Inashangaza kuwa watanzania wameweza kuacha kufanya kazi siku nzima ili kuandamana kuunga mkono porojo za kutaka JK awe mgombea pekee wa chama lakini mpaka sasa hapa hakuna wazo lolote la watu kuandamana kuunga mkono maneno ya Mengi na kumtaka JK ayafanyie kazi!
 
Hapa inaonyesha chuki kubwa za watanzania juu ya mafanikio ya Rostam...kama aliiba si mpelekeni mahakamani basi makelele yanasaidia nini hapa.Mengi anaongea kama kichaa kimsingi na hana hoja zaidi ya kukashifu watu.....Namjua vema Mengi na Rostam...akili ya Mengi inaweza kuwa inaingia kwa Rostam kama mara mia mbili hivi au zaidi.
 
Hilo ni kweli Fisadimtoto,
Tunalijua wote RA alivo na akili sana hata ya kuweza kuwarubuni tulio waamini kutuongoza hadi akaweza kutuibia kiasi hiki, lakini kwa bahati yake mbaya, muda alio tupambaza umetosha, hata akumbatie mguu wa albino (afanye ushirikina) haimsaidii tena, tumeisha mstukia, tumegutuka, na wallah, this time lazima anyee debe ama akimbie nchi! hawezi tuibia halafu akaendelea kukatiza mtaani kutunyanyasia hela zetu alizo tuibia!

Hata kwa mabua ya mahindi tuta mpopoa nayo hadi kieleweke ebo! Yaani unakuja kulisifia lijizi hapa eti lina akili ndo maana lime tuibia? arobaini zake zinatimia sasa!

Kwanza kwa mlioko dodoma tafuteni atakapo paki gari yake mpulizie chata ya nguvu, BABA LA MAFISADI, HATA KWENYE NYUMBA YAKE HIVO HIVO! TUMIA ILE SPRAY ISIYO FUTIKA
 
Hana nguvu hizo! Hili mbona wala halina utata. Nguvu pekee ambazo watu wanafikiri anazo ni katika Emergency Powers; na EP inatumika and certain conditions na siyo za kutumika kama anajisikia tu. Nje ya EP, Rais hana uwezo wowote wa kutaka mtu ashtakiwe au asishtakiwe.

Nguvu nyingine ambazo anazo ni zile za kusamehe aliyehukumiwa; nguvu hii ni absolute. Lakini hawezi kumsamehe mtu kabla hajashtakiwa na kukutwa na hatia!

Ndiyo maana Hosea na Marando wote wamekosea in fact and in law.

Naona Mkuu unataka kutuchanganya. Rais inawezekana hana mamlaka hayo kisheria na kikatiba lakini nguvu anazo. Nguvu anaipata kutokana na ukweli kuwa yeye ndiye ana mamlaka ya kuwaweka au kuwatoa katika nafasi zao hao wenye mamlaka. Nguvu kutokana na mandate aliyopewa na wananchi ya kuwa kapteni wa meli yao. Kusema wakina Hosea, DPP n.k. kuwa wana nguvu kuliko Rais si sahihi. Mamlaka wanayo lakini haya mamlaka ni kutokana na kuwekwa hapo na rais. Na hicho wanajua. Si unaona wakina Gonzales walivyopindisha sheria kukidhi matakwa ya wakina George W. na Cheney. Rais akisema huyo jamaa hastahili kufunguliwa mashtaka basi hao wenye mamlaka kazi yao itakuwa ni kutafuta justification ya kitendo hicho kisheria. Ndivyo ilivyo.

Amandla.......
 
Mengi amejitahidi kuwa 'jasiri' kwa kuwataja hao anaowaita mapapa wa rushwa. Hata hivyo kuna vitu kadhaa vya kuvitazama kama angalizo kabla ya kukimbilia kummininia sifa Mengi. Mosi, hawa wote aliowataja Mengi hawawajibiki kwetu. Pili, ufisadi tunaongelea hapa ni ufisadi uliofanyika serikalini kupitia, pamoja na njia nyingine za kishetani, tenda za ujanjaujanja. Kama ni tenda ya Dowans/Richmond, Rostam hakujipa, alipewa na viongozi wetu. Kama ni ndege ya kitapeli ya Rais, ni viongozi wetu ndio waliong'ang'ania tununue hata walipoambiwa na wataalamu kwamba haifai. Hiyo IPTL ni viongozi wetu ndio walioshinikiza tuingie mkataba. Waliosaini mikataba ya kitapeli ya madini ni viongozi wetu, huku wakiwa na taarifa sahihi kabisa kwamba hiyo mikataba haina tija kwa nchi. Walichofanya hawa ambao Mengi anawaita mapapa wa ufisadi ni kutumia ulafi na ujinga wa viongozi wetu katika kujineemesha kibiashara; na kwa kweli hata wao waliwahi kusema wazi kabisa kupitia nyaraka zao (rejea waraka wa Jeetu Patel katika mitandao). Kwa maneno mengine hawa aliowataja Mengi ni mawakala tu wa ufisadi; mafisadi hasa ni hao viongozi wetu na ndio tunapaswa kuwabebea bango.

Sasa, ambacho kinanisumbua mimi ni kwa nini sisi tunafurahia sana Mengi kuwataja watu waliotumia ulafi na udhaifu wa viongozi wetu kujineemesha badala kuwataja hao viongozi wenyewe? Wajibu wetu wa msingi kama wananchi, akiwemo Mengi, ni kuwajibisha viongozi wetu, ikiwa ni pamoja na kuwaajibisha kwa kushindwa kuwaajibisha wavunjifu wa sheria kama hao aliowataja Mengi.

Kwangu mimi alichofanya Mengi ni kujaribu kututoa katika msingi wa vita hii dhidi ya ufisadi, ambayo kimsingi ni vita dhidi ya viongozi walafi na dhaifu ndani ya serikali ya CCM.

Na kwa maoni yangu, vita ya kweli dhidi ya ufisadi katika nchi yetu haijaanza. Itaanza siku tutakapofanikiwa kuoanisha uwepo wa CCM madarakani na uwepo wa huo ufisadi. Ndio kusema vita ya kweli ya ufisadi itaanza siku tutakapoanzisha vita ya kweli ya kuitoa CCM madarakani, na tukianza vita hii sidhani kama Mengi atakuwa moja wa wapiganaji!

Katika watu ninaowaheshimu ni kaka yangu Kitila. Kwa bahati mbaya hanijui, lakini tunakutana mara kwa mara alipokuwa kiongozi Mlimani na baada ya hapo. Naheshimu msimamo wake.

Naomba kuungana naye kwa sehemu kubwa ya maelezo yake, lakini naomba kuchangia kwa kutoa maelezo yafuatayo.

Kwanza kabisa, Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingi za Afrika, watu kama kina Rostam na wenzake huwa hawaguswi na wanaoguswa ni kina Mkapa, Lowassa, Karamagi, Chenge, Mkulo, Iddi SImba, Mgonja, Mramba, Yona, Ngeleja Masha etc, lakini ukweli ni kwamba kila mwaka utakuwa na kina 'Lowassa' wapya, kina Mgonja wapya kina Karamagi wapya (Ngeleja) na kadhalika, kwa sababu wanaowaweka madarakani na wanaowatumia kwa uchafu wao hawagusiki na wakiguswa mnaona matokeo yake kama mtakavyoendelea kuona yatakayomkuta Mzee Mengi na watu wake. Tukae tukijua tusipong'oa mzizi wa UFISADI (Mapapa, kama alivyowaita Mengi) hatutaweza kuumaliza ufisadi. Watatuwekea Rais, Mawaziri na hata watendaji wa vyombo nyeti. LAZIMA Ukiumwa nyoka kati, piga kichwa. MUNGU ATUEPUSHE NAO
 
Nioneshe sheria (au mtafute Marando) inayompa mamlaka Rais kuamuru mtu yeyote kwa sababu yoyote na katika mazingira yoyote ashtakiwe.

Duh! kama ndio hivyo, au kama ikiwa hivyo basi hiyo ni hatari sana maana huo ndio udikteta wenyewe. Yaani kwa mfano, raisi, kwa sababu yeyote ile asipokupenda (like) basi anaweza akatoa amri ya wewe ushitakiwe....what the hell!!!?!??

Hana nguvu hizo. Ni katika mawazo ya watu wachache kama wewe ndio mnaweza kufikiria hivyo.

Naombea asiwe na nguvu kama hizo maana akiwa nazo basi sisi tutakuwa watu wa ajabu sana kumpa mtu mmoja nguvu za kutumaliza pale ajisikiapo.
 
makubwa haya ile thread waliyonianzishia wameiondoa!
Veeeery simple,just go and find another platform where you think you will be more confortable than here.Mie/Sie wengine ni/tumeridhika na hapa.Nyani anakomwa ila sio kwa staili ya kuuliza bout 40bn kwa sentensi takribani thelathini na zaidi.Ukiambiwa substantiate ur allegations,unaleta vituko vya kuleta picha za walemavu.Halafu unadai unaonewa.My foot!!
 
Naona Mkuu unataka kutuchanganya. Rais inawezekana hana mamlaka hayo kisheria na kikatiba lakini nguvu anazo.

Sasa kama hana hayo mamlaka (nguvu) kisheria na kikatiba, hizo nguvu alizonazo anazitoa wapi? Kichwani au moyoni mwake?

Nguvu anaipata kutokana na ukweli kuwa yeye ndiye ana mamlaka ya kuwaweka au kuwatoa katika nafasi zao hao wenye mamlaka.
Hayo mamlaka yake ya kuwaweka na kuwatoa hao wenye mamlaka yako spelled out kwenye katiba na sheria za nchi na hizo ndio nguvu alizonazo

Nguvu kutokana na mandate aliyopewa na wananchi ya kuwa kapteni wa meli yao..
Kapewa mandate na wananchi ili awe chief law enforcement officer kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa wazi kwenye katiba na vitabu vingine vya sheria na si kujiamulia tu cha kufanya au kutokuzitekeleza hizo sheria alizoapa kuzitekeleza na kuzifuata.
 
Endelea kupayuka tu,ndo jinsi unavyozidi kujifunua namna ulivyo.Kweli ufisadi ni sumu mbaya!!Haya endelea maana hawachelewi kusema "wanafukuzana hao"
 
Back
Top Bottom