Rostam na Manji watoe maelezo vinginevyo watiwe pingu!

Rostam na Manji watoe maelezo vinginevyo watiwe pingu!

NN,
In a perfect word, mnayosema ni sahihi. Lakini tatizo ni kuwa mnachanganya nguvu na mamlaka. Kutokana na nafasi yake kama kiongozi mkuu wa nchi, rais ana nguvu nyingi. Hasa kwetu ambako ana mamlaka wa kuweka yeyote amtakaye bila kuhojiwa na mtu. Kwa hali hiyo kila mtendaji aliyewekwa anajua yuko pale at the whim of the president. Hii ndiyo inayompa nguvu Rais. Nakumbuka Mwalimu ambae alikuwa kama rais hana mamlaka ya kutunga sheria lakini alikuwa akiwachachamaria bunge wakikataa kumletea sheria ambayo yeye anaitaka. Kuna wakati aliwatishia kuwa wakifanya mchezo, atavunja bunge halafu waone kama watarudi. Bunge likafyata na kumtimizia anachokitaka.

Hivi tujiulize. Kama Rais hana nguvu za kuhakikisha mtu anafunguliwa mashtaka sasa kwa nini ripoti za uchunguzi wa hizi tume lukuki zinapelekwa kwake? Kwa nini basi hao wenye mamlaka wasifanye uamuzi wa kumshitaki wanaeona anastahili? Ukweli ni kuwa hawawezi kufanya hivyo bila ridhaa ya aliyewaweka. Wakifanya hivyo basi bila shaka kibarua chao kitaota nyasi! Ukweli huu ndiyo uliotufikisha mahali ambapo watendaji ( hawa ndiyo mara nyingi wenye mamlaka) hawatimizi wajibu hao bila kibali cha wanasiasa ambao wana nguvu lakini hawana mamlaka!

Amandla.......
 
watanzania wengi wamekuwa wakikwepa ukweli huu kwa makusudi kabisa, wamekuwa wakizunguka zunguka na kuogopa kusema JK ndiye muhusika na kingplayer katika haya yote.

Kunieleza kuwa RA, manji, jeetu ni mafisadi na waende jela! naona tunacheza makida makida, ni mwaka wa nne sasa , tunapenda kuzungumza , tunaogopa kusema JK wewe ndiye fisadi , si Manji, rosata wala jeetu, ni JK. kama sisi tunajua kuwa hawa jamaa ni mafisadi basi JK anajua mpaka zaidi sana kuliko sisi! yeye ana kila sababu na resources zote za kufanya mambo yatokee!

Kesho utakuta mtu anasema tena Rostam fisadi! JK mwenye mamlaka anawachora! KWA NINI TUSIELEKEZE BUNDUKI ZETU NA SHUTUMA ZETU ZOTE KWA YULE ANAYETURUDISHA NYUMA?? KUNA WATU MNATUMIWA NA JK??

KWA NINI WENGI WANAPOSEMA TUHUMA ZA UFISADI WANAMKWEPESHA JK?? WAKATI YEYE NDIYE TOP WA KUFANYA YALE TUNAYOYATAKA?? KUNA MTU ATAMLAUMU JK KWA KUWACHUKULIA HATUA MAFISADI??

Watanzania hatupendi kuambiwa ukweli, hatupendi kujua chanzo cha tatizo, tunapenda umbeya na kujitia moyo kwa vitu ambavyo havitusaidii!

Tunataka fedha zetu, tunataka waende jela, hatutaki stori zenu!
 
Mkuu Waberoya,
unayoongea ndio wote karibia wanayazungumzia au kutaka yatendeke.But,how??Hapo ndipo tunapopishana.Kwani leo h¨ªi bado tunaulizana kama tumuondolee kinga Mkapa au la!!Sasa kama hilo halina uhakika,unadhani kusema kuwa JK ni fisadi inaweza ikatusaidia(at least for now)??Tutakuwa tumeongea ukweli,ila impact ya ukweli huo inaweza isiwepo au ikawa negative.Angalia mamlaka ya rais kikatiba,composition ya wabunge(let alone ukilaza wa wengi wao),ona wananchi walivyolala usingizi mzito huku wakiwa hawazifahamu hata haki zao za msingi,tizama pia namna wanavyorubuniwa kirahisi na wale wanaotaka madaraka kwa rushwa.Baada ya hapo ndo uje tujadili kama tuendelee kupaza sauti na kutoa povu kuwa JK hivi au vile.Mi naona kwa sasa tuanze na hawa wasio na KINGA yeyote ile ya kisheria isipokuwa kama wanavyosema kuwa wanalindwa na mkulu.Hizi kelele zikizidi huyo awalindae atawaachia tu.Lets try this approach huku ikiwa ni sambamba na kuendeleza juhudi za kuwazindua wadanganyika.Taratibu tutafika,one step at a time.
 
may be! ila wako wengi, naamini wezi wako wengi sana, mbali ya hao tuwafahamu na hapa ndio tatizo, na tunakoenda kama approach yetu ni hii usishtuke kila mtu kuambiwa fisadi hata awe msafi! kama tukisema tu, na wasipopelekwa mbele ya sheria kwa amri y mkuu, basi kuna watu kibao wasafi wataambiwa wachafu! haitakuwa tofauti na mauaji ya vikongwe,vibaka, ngozi albino, wenye upara n.k!!!

nimefundishwa ukitaka kumuua nyoka piga kichwa, mbinu yako mpya sana kwangu, nadhani DPP, TAKUKURU wakiitumia hii ina weza ika-work, ila waangalie kichwa kisiwaume, kwa wale shemeji wa JK watakaokuwa pointed!
 
Waberoya,
haijalishi ni nani amekuwa pointed mkuu wangu,kama ni kweli tuhuma zinakuwa backed up na ushahidi unaokubalika kisheria then sioni kama rais anaweza akawanyamazisha wananchi wote kama watakuwa wapo makini na kinachoendelea.Naamini sauti ya Mengi imefika mbali na si bure ikasaidia katika kuwaamsha wengine.Pia naamini ushahidi wa kutosha anao,kwani kusema kama wanaona wamesingiziwa au kuchafuliwa majina pasipo sababu waende mahakamani inareflect kuwa hayo ayasemayo ana ushahidi nayo.Iwapo watanyamaza then ushahidi huo ukawekwa public,hapo ndio hao akina DPP na TAKUKURU watakapomrudia mkulu na kuuliza kuwa wawapeleke keko au la...Tuombe kuwa wananchi nao waanze kuonyesha mwamko,hapo ndipo mkulu atakapoona liwalo na liwe,wacha waende...After all THERE ARE NO PATNERS IN CRIME.
 
Naona Mkuu unataka kutuchanganya. Rais inawezekana hana mamlaka hayo kisheria na kikatiba lakini nguvu anazo.

Siyo "inawezekana hana" hana.

Nguvu anaipata kutokana na ukweli kuwa yeye ndiye ana mamlaka ya kuwaweka au kuwatoa katika nafasi zao hao wenye mamlaka. Nguvu kutokana na mandate aliyopewa na wananchi ya kuwa kapteni wa meli yao.

Nope! Hana nguvu ambayo hajapewa kisheria au kikatiba. Period. Haijalishi kama amechaguliwa kwa asilimia 100, nguvu zote alizonazo, mamlaka na uwezo wa kazi yake vyote vimefungwa na Katiba na Sheria. Nje ya hapo hana.

Kusema wakina Hosea, DPP n.k. kuwa wana nguvu kuliko Rais si sahihi.

Sijasema hivyo; wanazo nguvu walizopewa kisheria na kikatiba tu.

Mamlaka wanayo lakini haya mamlaka ni kutokana na kuwekwa hapo na rais.

Nope! mamlaka waliyonayo ni yale waliyopewa kisheria na Kikatiba na sehemu mojawapo ni kuteuliwa na Rais. Rais hawezi kumteua mtu ambaye hana mamlaka ya kumteua hata kama anampenda. Hivi hili ni gumu kulielewa?

Na hicho wanajua. Si unaona wakina Gonzales walivyopindisha sheria kukidhi matakwa ya wakina George W. na Cheney. Rais akisema huyo jamaa hastahili kufunguliwa mashtaka basi hao wenye mamlaka kazi yao itakuwa ni kutafuta justification ya kitendo hicho kisheria. Ndivyo ilivyo.

Amandla.......

Nope wakifanya hivyo kuvunja sheria hata kama aliyewaigiza ni Rais wa Mbinguni watafunguliwa mashtaka. Vinginevyo wanatakiwa kujiuzulu. Soma kesi ya Nixon.
 
Sasa kama hana hayo mamlaka (nguvu) kisheria na kikatiba, hizo nguvu alizonazo anazitoa wapi? Kichwani au moyoni mwake?

Hayo mamlaka yake ya kuwaweka na kuwatoa hao wenye mamlaka yako spelled out kwenye katiba na sheria za nchi na hizo ndio nguvu alizonazo

Kapewa mandate na wananchi ili awe chief law enforcement officer kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa wazi kwenye katiba na vitabu vingine vya sheria na si kujiamulia tu cha kufanya au kutokuzitekeleza hizo sheria alizoapa kuzitekeleza na kuzifuata.

duh.. very soon.. we can have you take the bar! I love it.
 
NN,
In a perfect word, mnayosema ni sahihi. Lakini tatizo ni kuwa mnachanganya nguvu na mamlaka. Kutokana na nafasi yake kama kiongozi mkuu wa nchi, rais ana nguvu nyingi.

Hilo halina utata; lakini siyo kwetu hata nchi nyingi duniani kiongozi mkuu wa serikali na nchi ana nguvu nyingi tu. So, this as obvious as the sun rising from the East.

Hasa kwetu ambako ana mamlaka wa kuweka yeyote amtakaye bila kuhojiwa na mtu.

Ningetumia neno moja kuelezea kauli hii lakini sitofanya hivyo; niseme kuwa dai lako hilo halina msingi katika sheria, halina msingi katika ukweli na ni zao la kufikiria kitu ambacho hakipo na kukiamini.

Kwa hali hiyo kila mtendaji aliyewekwa anajua yuko pale at the whim of the president.

Siyo "kila". Hii nayo inaitwa haste generalization. Kuna watu ambao Rais hata akitaka kuwafukuza hawezi; miongoni mwao ni majaji (ambao amewateua), DPP (ambaye amemteua) na Makamu wa Rais (ambaye ni mgombea mwenza wake). HIvyo siyo "kila mtendaji" anafanya kazi at the "whim" of the President. Ila wapo ambao wanafanya kazi kwa ridhaa ya RAis (at the pleasure of the president). Ndio maana wakati BWM alipowafukuwa wale maafisa wa Polisi akiamini ana nguvu hizo serikali ilijikuta inashtakiwa na kushindwa kesi na kutakiwa kuwalipa mamilioni ya fedha.

Hii ndiyo inayompa nguvu Rais. Nakumbuka Mwalimu ambae alikuwa kama rais hana mamlaka ya kutunga sheria lakini alikuwa akiwachachamaria bunge wakikataa kumletea sheria ambayo yeye anaitaka. Kuna wakati aliwatishia kuwa wakifanya mchezo, atavunja bunge halafu waone kama watarudi. Bunge likafyata na kumtimizia anachokitaka.

Hilo mbano si la ajabu, kwa sababu kisheria alikuwa na nguvu ya kuvunja Bunge. Hata leo hii Rais akitaka kuvunja Bunge anaweza lakini utaratibu wake ni mgumu kidogo, lakini hawezi tu kuamka na kusema "bunge vunjika" likavunjika.

Hivi tujiulize. Kama Rais hana nguvu za kuhakikisha mtu anafunguliwa mashtaka sasa kwa nini ripoti za uchunguzi wa hizi tume lukuki zinapelekwa kwake?

Wengine tulishajiuliza swali hilo na binafsi nilipinga hata yeye kuteua tume ya kina Mwanyika! So, welcome to the club. Kuna mambo yanafanyika kwa sababu watu wanaamini wewe unavyoamini pasipo msingi wowote wa kisheria. Wangeamua kuangalia sheria kuna mambo yangekuwa hayafanyiki. Tatizo jingine ni kuwa Rais mwenyewe analea mawazo ya namna hiyo.

Kwa nini basi hao wenye mamlaka wasifanye uamuzi wa kumshitaki wanaeona anastahili?

Swali jingine zuri ambalo wengine tumeshauliza huko nyuma.

Ukweli ni kuwa hawawezi kufanya hivyo bila ridhaa ya aliyewaweka.

Hili linawezekana kuwa ni kweli lakini si kwa sababu ya ridhaa bali kwa sababu ya woga.

Wakifanya hivyo basi bila shaka kibarua chao kitaota nyasi! Ukweli huu ndiyo uliotufikisha mahali ambapo watendaji ( hawa ndiyo mara nyingi wenye mamlaka) hawatimizi wajibu hao bila kibali cha wanasiasa ambao wana nguvu lakini hawana mamlaka!

Amandla.......

ndiyo woga wenyewe huo
 
Ninapotofautiana na wewe ni hapo kwenye neno "kisheria". Mimi nazungumzia nguvu za ushawishi zinazotokana na nafasi yake na si nguvu za utekelezaji kisheria. Ninachopingana na wewe ni huko kudai kuwa Rais ni helpness inapokuja kwenye suala la kumfungulia au kutomfungulia mtu mashtaka. Nguvu za kisheria, kikatiba inawezekana hana lakini nguvu za ushawishi anazo na hizi si haba kama pengine unavyotaka tuamini. Kama Rais hataki mtu fulani ashitakiwe kwa sababu yeyote ile, na akaonyesha hivyo basi ni DPP shupavu atakaefungua mashtaka dhidi ya mtu huyo. Tumesikia mara ngapi DPP amekataa kumfungulia mtu mashtaka bila kutoa maelezo! Nakumbuka kesi ya mtoto wa mzito mmoja ambae alimuua mfanyakazi wake wa shamba. Mamlaka haya anayo kisheria. Sasa kitu gani kitamzuia kufanya hivyo kwa sababu Rais wake amemwagiza?

Nope! mamlaka waliyonayo ni yale waliyopewa kisheria na Kikatiba na sehemu mojawapo ni kuteuliwa na Rais. Rais hawezi kumteua mtu ambaye hana mamlaka ya kumteua hata kama anampenda. Hivi hili ni gumu kulielewa?

Tangu lini kuteuliwa na rais kumekuwa ni mamlaka? Mamlaka yanatokana na nafasi husika ilivyoainishwa katika sheria na katiba. Mtu yeyote anaekuwa katika nafasi hiyo ndiye mwenye mamlaka hayo. Kwenye nafasi hizi tunazoziongelea, mwenye mamlaka ya kuteua mtu wa kuzishika ni Rais na si mwingine. Mamlaka hayo ya Rais ni absolute. Uteuzi huo wa Rais hauwezi kubatilishwa na mamlaka nyingine yeyote. Na hao anaowateua hawahitajiki kupitishwa na chombo kingine chechote. Kusema kuwa rais hawezi kuteua mtu ambae hana mamlaka ya kumteua ni kutufanya wengine ni wajinga. Wote tunajua kuwa mamlaka hayo ni kwenye sehemu kadhaa za uongozi na si zote. Kwenye hizo nafasi anaweza kuweka yeyote ampendae. Ndiyo maana anaweza kumtoa mtu aliye na uzoefu wa financial institutions akamkabidhi utility company. Ndiyo maana anaweza kumtoa mtu ambae ni relatively junior akampa uongozi wa wizara. Ninachokisema ni kuwa kutokana na mamlaka haya, rais ana nguvu kubwa ya ushawishi juu ya wale aliowateua. Kipi hapa kigumu kuelewa?

Amandla......
 
Siyo "kila". Hii nayo inaitwa haste generalization. Kuna watu ambao Rais hata akitaka kuwafukuza hawezi; miongoni mwao ni majaji (ambao amewateua), DPP (ambaye amemteua) na Makamu wa Rais (ambaye ni mgombea mwenza wake). HIvyo siyo "kila mtendaji" anafanya kazi at the "whim" of the President. Ila wapo ambao wanafanya kazi kwa ridhaa ya RAis (at the pleasure of the president). Ndio maana wakati BWM alipowafukuwa wale maafisa wa Polisi akiamini ana nguvu hizo serikali ilijikuta inashtakiwa na kushindwa kesi na kutakiwa kuwalipa mamilioni ya fedha.

Kwenye hili, I stand corrected.

Amandla.........
 
Ninapotofautiana na wewe ni hapo kwenye neno "kisheria". Mimi nazungumzia nguvu za ushawishi zinazotokana na nafasi yake na si nguvu za utekelezaji kisheria.

Mjadala hauko kwenye nguvu ya ushawishi au mamlaka ya kushawishi. Kama hana nguvu ya kisheria to effect what desires then he has no power au authority whatsoever. Mengine yote tunaweza kujadili kama burudani tu.

Ninachopingana na wewe ni huko kudai kuwa Rais ni helpness inapokuja kwenye suala la kumfungulia au kutomfungulia mtu mashtaka.

Neno "helpless" ni la kwako; mjadala ulikuwa kwenye uwezo na mamlka ya kisheria na msimamo wangu uko pale pale. Kama unakubaliana na mimi kuwa hana nguvu, mamlaka au madaraka ya kisheria ya kumshtaki au kutomshtaki mtu basi hakuna mjadala.

Kwamba anaweza kutoa maoni yake au kujaribu kushawishi either way hilo si geni kwani hata mimi na wewe tuna uwezo huo na tumeutumia vizuri tu.

Nguvu za kisheria, kikatiba inawezekana hana lakini nguvu za ushawishi anazo na hizi si haba kama pengine unavyotaka tuamini.

Na hapa pia tunaweza kwenda mbali, hata nguvu za kushawishi kitu nje ya sheria hana. Ushawishi wake unabakia kwake na kwa familia na ndugu zake. Akishawishi au kujaribu kushawishi kitu nje ya sheria anaweza kuwa impeached.

Kama Rais hataki mtu fulani ashitakiwe kwa sababu yeyote ile, na akaonyesha hivyo basi ni DPP shupavu atakaefungua mashtaka dhidi ya mtu huyo.

Wala haiitaji DPP shupavu, inahitaji mtu anayeangalia sheria tu. Period.

Tumesikia mara ngapi DPP amekataa kumfungulia mtu mashtaka bila kutoa maelezo!

Kwa sababu ana nguvu na mamlaka hayo kisheria. So, nothing new there. Ana uwezo wa kuingilia kati kesi yoyote, kufuta kesi yoyote na kumshtaki mtu yeyote pala anapokuwa na sababu ya kufanya hivyo. Nguvu hii haitegemei Rais.

Nakumbuka kesi ya mtoto wa mzito mmoja ambae alimuua mfanyakazi wake wa shamba. Mamlaka haya anayo kisheria. Sasa kitu gani kitamzuia kufanya hivyo kwa sababu Rais wake amemwagiza?

Hili ni swali ambalo DPP peke yake anaweza kujibu, sitojaribu.

Tangu lini kuteuliwa na rais kumekuwa ni mamlaka? Mamlaka yanatokana na nafasi husika ilivyoainishwa katika sheria na katiba.

Finally!

Mtu yeyote anaekuwa katika nafasi hiyo ndiye mwenye mamlaka hayo. Kwenye nafasi hizi tunazoziongelea, mwenye mamlaka ya kuteua mtu wa kuzishika ni Rais na si mwingine.

true

Mamlaka hayo ya Rais ni absolute.

Not true, mtu mwengine anaweza kukaimishwa baadhi ya teuzi hizo. Si lazima Rais personally azifanye.

Uteuzi huo wa Rais hauwezi kubatilishwa na mamlaka nyingine yeyote.

Unaweza kwa mujibu wa sheria.

Na hao anaowateua hawahitajiki kupitishwa na chombo kingine chechote.

No argument from me there.
Kusema kuwa rais hawezi kuteua mtu ambae hana mamlaka ya kumteua ni kutufanya wengine ni wajinga.

Ujinga ni kitu ambacho kila mmoja wetu anacho kwa kiasi fulani na katika eneo fulani. Hivyo, kuwa mjinga kwenye jambo moja haina maana si mjuzi wa mengine.

Wote tunajua kuwa mamlaka hayo ni kwenye sehemu kadhaa za uongozi na si zote.

Sijui kama ni "wote".. maana kwa jinsi inavyojadiliwa hapa nina mashaka ya "wote" wanajua.

Kwenye hizo nafasi anaweza kuweka yeyote ampendae. Ndiyo maana anaweza kumtoa mtu aliye na uzoefu wa financial institutions akamkabidhi utility company.

Nope, ni mtu ambaye anatimiza masharti ya sheria. Kwa mfano hawezi kumteua mtu yeyote kuwa Jaji! Ili mtu awe jaji kuna sifa za kisheria.

Ndiyo maana anaweza kumtoa mtu ambae ni relatively junior akampa uongozi wa wizara.

Kwa sababu sheria inasema vipi. Je anahitajika Senior? Uteuzi wake unaongozwa na sheria vile vile.

Ninachokisema ni kuwa kutokana na mamlaka haya, rais ana nguvu kubwa ya ushawishi juu ya wale aliowateua. Kipi hapa kigumu kuelewa?

Hilii neno "ushawishi" ni kujaribu kukwepa hoja zako za awali ambazo sitazirudia. Umeliingiza sasa hivi kama kuhamisha goli. Rais anazo nguzu za kushawishi kama vile mtu mwingine alivyonavyo nguvu zao. Hizo nguvu za kushawishi zinaishia hapo tu kwenye "ushawishi". Sasa sijui ni kipi hapa ambacho ni kigumu sana kuelewa.

Amandla......

Well
 
Wewe umesoma vizuri kichwa cha huu mjadala hapa au unaleta mambo yako ya ubaguzi wa rangi?

Mkuku amekugusa sana nini kakisoma kiwa cha habari lakini kajitahidi kuwaongezea wengi Mengi kataja wa chache
 
Mmoja atoe maelezo ya kuhusika kwake na wizi wa EPA na Dowans (kabla sijaamua kujitolea kumsaidia kurahisisha kutiwa pingu kwake ) na tena aeleze kwanini ya Al-Adawi walibuni hii mbinu ya kufungua kampuni ya Dowans kwenye Free Trade Zone kule Costa Rica mahali ambapo hawana ofisi wala jengo na kampuni hiyo iko mfukoni mwa mwanasheria asiyejuliikana na haionekani kwenye taasisi zinazoandikisha biashara na wale kwenye orodha ya makampuni yaliyopo kwenye hiyo trade zone! na mwingine ajitolee kutoa maelezo kwanini alisema fedha alizorudisha za Kagoda ni za baba yake marehemu wakati jina lake na jina la baba yake hayaonekani kwenye nakala za Kagoda.

Vinginevyo, time is up!

Uongo mtupu, fanya kweli kama unaweza! unangoja nini?
 
Nani awatie pingu?

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=Rw_3ml30UKI&feature=related]YouTube - Ngwair - CCM[/ame]
 
Hilii neno "ushawishi" ni kujaribu kukwepa hoja zako za awali ambazo sitazirudia. Umeliingiza sasa hivi kama kuhamisha goli. Rais anazo nguzu za kushawishi kama vile mtu mwingine alivyonavyo nguvu zao. Hizo nguvu za kushawishi zinaishia hapo tu kwenye "ushawishi". Sasa sijui ni kipi hapa ambacho ni kigumu sana kuelewa.

Neno ushawishi nimeliweka baada ya kuona wewe unakazania kuniingizia neno nguvu kwa mujibu wa sheria. Tunapotofautiana na tutakapoendelea kutofautiana ni kwenye hilo. Mimi naamini kuwa nguvu za rais ni zaidi ya zile ambazo zimeainishwa kwenye sheria na katiba. Mimi hizo nguvu za kisheria na kikatiba nimeziita mamlaka ili kutofautisha na nguvu za ushawishi. Lakini naona unajaribu kubadilisha nisemalo ili kujenga hoja yako kuwa nguvu za rais ziko kwenye sheria na kikatiba tu. Na pale ambapo mamlaka hayo wamepewa wale walio chini yake yeye basi mikono yake imefungwa! Yani kweli unataka kuniambia kuwa kwa sababu rais hana mamlaka (kisheria) ya kumfungulia mtu mashtaka basi yeye mikono yake imefungwa hata pale anapoona kuwa fulani anastahili kupelekwa au kutopelekwa mahakamani? Kama ni hivyo, basi tunamuonea rais kwa kudai awajibike kwa utendaji wa serikali yake maana mamlaka ya utekelezaji kisheria na kikatiba katika sehemu nyingi hana! Watu wa kushikwa na kulaumiwa ni makatibu wakuu na watendaji wakuu wengine maana hao ndio wenye mamlaka ya kiutendaji.

Nope, ni mtu ambaye anatimiza masharti ya sheria. Kwa mfano hawezi kumteua mtu yeyote kuwa Jaji! Ili mtu awe jaji kuna sifa za kisheria.

Ni vigezo gani vinavyombana rais katika uteuzi wake wa majaji kisheria zaidi ya pengine hicho basic kuwa awe mwanasheria? Zitaje hizo sifa badala ya kudai tu kuwa zipo kwenye sheria. Halafu tuangalie kama teuzi zake zote zimeongozwa na hizo sheria) kanuni.

Pamoja na yote haya, shukrani kwa jitihadazako za kujaribu kunifahamisha ingawa inaelekea kichwa changu bado ni kizito. Kwa bahati mbaya sidhani kama utaweza kuni-convince kwenye hili. Naishia hapa.

Amandla........
 
I beg to differ when Outlier states on the issue of racism..as quite frankly it is Mengi who has actually initiated this aspect.

Everyone has a right to state what they feel like we are doing in the forum but amazingly Mengi seemed to have skipped mentioning others like Mkapa,Mahalu and Yona (etc.etc)who too used their positions to aquire wealth and that too tax payer's monies along with natural resources of the country..so why not equally mention/blame those involved in the Govt levels too?Or is he too aquainted with them and the current ones?

Be brave and do not try to seperate the coffee from the milk!
 
Grow up man! '
The issue here is not their race the issue is, they 'FISADED' us, Didn't they?
 
Last edited:
Rwabugiri,

Common sense does not require to grow up.

The issue here is undeniably a fact as stated by Outlier. The bone of contention should be fair by showing all the Fisadi's without prejudice...otherwise it is like trying to put a cart before the horse!
 
Back
Top Bottom