Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 58,447
- 131,262
Wanabodi,
Hii ni Makala yangu kwenye gazeti la Nipashe, Jumapili ya leo.
Leo, nimeizungumzia Ripoti ya Jaji Chande kwa kuwa mtu wa shukrani, kushukuru kwa hiki kidogo ili tupatiwe kikubwa!.
Alihamisi ya Wiki, Ripoti ya Uchunguzi wa Matukio ya October 29, mwaka 2025, maarufu kama Ripoti ya Jaji Chande, imetoka, ingawa ripoti hiyo imepooza kiu ya Watanzania, kwa kutaja idadi ya vifo, lakini ripoti hiyo, haijakata kabisa kiu ya Watanzania ya kumjua ni nani haswa alitoa amri ile ya kuua watu kwa kutumia risasi za moto?!. Ingekuwa wote waliouwawa, ni wale wahuni waandamanaji ambao wengi wao walifuata tuu mkumbo bila kujua watendalo, wala nisingeuliza hili swali kwasababu nafahamu fika jeshi letu la polisi, lina mamlaka ya kutumia nguvu kuthibiti ghasia, ila kuna ushahidi macho, mashuhuda, picha mnato na picha jongefu, kuna mamia ya watu waliuliwa sehemu nyingine tuu wala sio waandamanaji, wakiwemo wale watoto wadogo malaika wa Mungu!.
Moja ya jambo kubwa lililokuwa linasubiriwa sana na kwa hamu kubwa na watu wengi kwenye Ripoti ya Uchunguzi ya Jaji Chande, kubwa la kwanza ni kujua idadi ya watu waliokufa kwenye vurugu zile za October 29, 2025 na la pili kubwa ni nani aliyetoa amri ya polisi kutumia risasi za moto kwa kupita mitaani na kuua watu hovyo, na mpaka sasa, hakuna taarifa yoyote ya polisi yoyote kuwajibika?.
Ripoti imetoa tuu idadi ya vifo ila imeepuka kumtaja aliyetoa the order to shoot and kill. (piga risasi ua). Huko nyuma niliwahi kuandika na kusema, tusiwalaumu bure polisi wetu, usikute polisi wetu walikuwa wanatimiza wajibu wao na majukumu yao kikamilifu kwa kupokea amri halali, ya mabosi wao, ndio maana hatujasikia polisi yeyote akiulizwa chochote!.
Ripoti imetaja Idadi ya jumla ya vifo vyote officially recorded ni watu 518, kwa kitendo tuu cha kutangaza idadi ya vifo, tukubali tukatae Tume imekuwa very bold!, hii maana yake vifo hivyo viko well recorded and well documented, hadi taarifa za majina zipo na walizikwa wapi. Hivyo tunaomba familia za wahanga zipewe majina na zielezwe tuu hao watu 518, walizikwa wapi, kwa kuonyeshwa makuburi 518 yaliwazika hao watu 518 ili wafanye tuu hitma, maulid na kuwaombea misa, hii itaifuta ule uongo wa makaburi ya halaiki.
Baada ya kutangazwa idadi ya kweli ya vifo hivyo wa watu 518 vya October 29, sasa nashauri serikali yetu ifanye mambo makubwa matano
1. Ituambie aliyetoa amri au order ya kutumia risasi za moto ni nani?. Kitendo cha mpaka ripoti inatoka, CDF, IGP, na DGIS bado wako ofisini, kwa sisi tuliopitia jeshini na kufahamu kitu kinachoitwa chain of command, ni kama tunaelewa elewa hivi, ila ni kweli hadi kuuwa wale watoto malaika wa Mungu, ni maelekezo?, waliofanya vile wamefanywa nini?, na baada ya kutoka hii ripiti, hao wakubwa watu hapo juu wanasubiri nini kuwajibika?.!
2. Kama ile 1976, mikoa ya Mwanza na Shinyanga, walikufa watu 4 tuu mikononi mwa polisi, Mwali Nyerere alikasirika sana, jeshi la polisi na Idara ya Usalama wa taifa ilisafishwa kutoka juu mpaka chini, kwa hii Tanzania ya leo, tunapokea taarifa ya vifo 518, miongoni mwa vifo hivyo ni watoto 4 wa umri wa chini ya miaka 7 na watoto wawili wa umri wa chini ya miaka 5!, polisi hawa waliowaua malaika hawa kwa risasi, wamefanywa nini?!, kwenye serikali hii ya Samia, inabidi wafe watu wangapi ndipo tuanze kuwajibishana?!.
3. Kupitia balozi zetu zilizoko nchi mbalimbali duniani ambazo media zake zilitusingizia uongo, kuhusu idadi ya vifo, kwa kutangaza wamekufa maelfu, mabalozi wetu walioko huko, wakanushe uongo wa media zao ukiwemo uongo wa CNN, BBC na Aljazeera
4. Kupitia makampuni ya uwakili ya kizalendo, ikiwemo kampuni ya PPR Legal Chamber, tuwafungulie kesi za madai kuwadai fidia kutusingizia habari za uongo na kumtukana rais wetu.
5. Serikali yetu ikanushe rasmi ile idadi ya uongo na uzushi, ikiendelea kunyamaza bila kuukanusha huu uongo wa idadi ya vifo, maana yake itakuwa hii idadi ya vifo iliotangazwa leo na Tume, itakuwa ni idadi ya utekelezaji tuu wa ule ushauri wangu nilioutoa katika bandiko hili. Ushauri: Tangazeni idadi ya Vifo, na Ikibidi Hata Idadi ya Uongo tuu ili Wanyamaze!. Gazeti la “The Sun” limeiita Tanzania HOUSE OF BLOOD
Kwa vile sio mabalozi wetu wote wako competent na conversant na media, wale mabalozi competent na conversant kama Balozi Mobhare Matinyi, wasaidie kwenye hili, kufuatia kazi nzuri aliyoifanya akiwa Balozi wetu Sweden. Pongezi Balozi Wetu Sweden, Mobhare Matinyi. Alichofanya Kiigwe na Kifanywe na Balozi Zetu Zote
Huku TLS ikituma jopo la wanasheria wa International Law kuitetea nchi yetu kimataifa kwa kuwafungulia mashitaka wale wote wanaoichafua nchi yetu kwa kuizushia uongo, na kuwasema vibaya viongozi wetu, tusiwanyamazie!.
Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa, baada ya ukweli kupatikana, tusipoutumia ukweli huu kuukanusha uongo wao, then uongo wao utaonekana ni ukweli na sasa hivi tusije kushangaa ICC wakitubishia hodi kutaka kuuthibitishia ule uongo wa CNN, BBC na Al Jazeera, wakati ukweli halisi ni idadi ya ukweli ya Tume ya Uchunguzi ya Jaji Chande.
What are we doing about this?.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Update: 1
Naomba kuweka mchango wa mchangiaji mmoja very objective
Kitu cha pili ninachokupendea, wewe ni mmoja wa wanachama wenye good IQ, japo kuna hoja nyingi tunatofautiana, ili tofauti zetu ni logical, na very objective, tofauti yetu kubwa kati ya mimi na wewe ni kwenye impartiality, wewe mwenzangu umeegemea upande fulani, hati inatokea majito majinga, yanamdanganya Mfalme
kuwa yamemshonea joho la transparent, wasio na dhambi hawataliona, kisha matapeli hao wanaleta hilo joho hewa na kumvisha mflme mpaka nguo za ndani, kisha wanamwambia ajitazame kwenye kioo, jinsi alivyo pendeza, Mfalme anajiangalia kwenye kioo, anajiona kama alivyozaliwa!, ila kijiaminisha kuwa hana dhambi, anasema nimejiona nilivyo pendeza!.
Mfalme anaitisha mkutano wa hadhara na kuwaita wakuu wote na wananchi wote kujitokeza ukumbizi kwenye uzinduzi wa joho jipya la kisasa la mflme, ambalo wenye dhambi hawataliona. Wasaidizi wake wote wanajitokeza, kisha MC anatangaza here comes the King, kiukweli amependeza sana, Mfalme anaingia ukumbini kwenye kadamnasi ya watu, akiwa kama alivyo zaliwa, huku akitembea taratibu kwa madaha na joho jipya!.
Ukumbi wote, ukalipuka kwa makofi ya shangwe, hoi hoi na vigelegele kushangilia joho jipya la Mfalme, ila kuna mtoto mmoja mdogo, akamuuliza baba yake, mbona Mfalme yuko uchi?, Baba akamwambia mtoto nyamaza!. Miongoni mwa hao wapiga makofi na washangiliaji ni wewe mwenzangu!, mimi nilipokuja nikatama kumwambia Mfalme uko uchi, ila kwa vile niko nyuma, sauti zetu tujajitahidi kuzipaza, hazimfikii, kwasababu makofi na vigelegele vya washangiliaji, vimefunika sauti zetu!, kati ya mimi na wewe, nani anamsaidia kiukweli huyu Mfalume wetu?.
Wewe kwa IQ yako, kuna vitu ukweli unaujua!, usishangilie!, akiaibika Mfalme wetu ni sote tunaaibika!. Kati ya Walimzunguka Mfalme na Kumsifu Alivyopendeza na ile Invisible Robe, na yule mtoto aliyemweleza ukweli, kuwa yuko, nani anamsaidia kweli? masikini hatukumzingatia, tungemzingatia, hawa wasema ukweli, tusingefika hapa tulipofika!,
Kwa mijibu wa PGO, baada ya kukamilisha kazi, kila asikari anaporudisha ile silaha amarah ana fanya retirement ya idadi ya risasi zote alizosaini wakati anachukua silaha, na ku account kwa maandishi, kila risasi aliyofyatua, alifyatua kulenga nini, hivyo data za wauaji wa wale malaika wa Mungu, zipo!, wamefanywa nini?. Data za wauaji wale watazamaji wa TV kwenye kibanda umiza, zipo, wamewatoa nje, wakawaambia walele chini kifudi fudi na kuwamiminia!, wamefanywa nini?. Wale waliowaua wale majirani wa Sitaki Shari, data zipo, wamefanywa nini?!.
Naungana na wewe, tuisubiri hiyo Tume ya Jinai, kisha tuwapeleke kwenye tume ya ukweli, upatanisho na maridhiano, tusameheane, tusonge mbele kuelekea kwenye katiba mpya, kama nilivyo sikia kwenye sauti hii
P.

Asante Jaji Chande Kwa Ripoti Yako, Japo Ripoti Imekidhi Haja, ila Haijamaliza Kiu!. Asante kwa Kutoa Idadi ya Vifo, ila Bila ya Kumtaja, Aliyetoa Amri ya Kutumia Risasi za Moto Kuua hao Watu 518 ni Nani?, na kwa Vile, Hakuna Taarifa Yoyote ya Uwajibikaji Wowote wa Hivyo Vifo 518, Mwanza na Shinyanga ile Mwaka 1976, Walikufa Watu 4 tuu, Wizara, IGP, DIGIS, RPCs, RSOs, OCDs na DSOs Waliwajibika!, Hivi Wanatakiwa Kufa Watu Wangapi Sasa Ndipo Tuanze Kuwajibishana?!, CDF, IGP na DGIS Wanasubiri Hiyo Tume ya Pili ya Jinai?!.
Alihamisi ya Wiki, Ripoti ya Uchunguzi wa Matukio ya October 29, mwaka 2025, maarufu kama Ripoti ya Jaji Chande, imetoka, ingawa ripoti hiyo imepooza kiu ya Watanzania, kwa kutaja idadi ya vifo, lakini ripoti hiyo, haijakata kabisa kiu ya Watanzania ya kumjua ni nani haswa alitoa amri ile ya kuua watu kwa kutumia risasi za moto?!. Ingekuwa wote waliouwawa, ni wale wahuni waandamanaji ambao wengi wao walifuata tuu mkumbo bila kujua watendalo, wala nisingeuliza hili swali kwasababu nafahamu fika jeshi letu la polisi, lina mamlaka ya kutumia nguvu kuthibiti ghasia, ila kuna ushahidi macho, mashuhuda, picha mnato na picha jongefu, kuna mamia ya watu waliuliwa sehemu nyingine tuu wala sio waandamanaji, wakiwemo wale watoto wadogo malaika wa Mungu!.
Moja ya jambo kubwa lililokuwa linasubiriwa sana na kwa hamu kubwa na watu wengi kwenye Ripoti ya Uchunguzi ya Jaji Chande, kubwa la kwanza ni kujua idadi ya watu waliokufa kwenye vurugu zile za October 29, 2025 na la pili kubwa ni nani aliyetoa amri ya polisi kutumia risasi za moto kwa kupita mitaani na kuua watu hovyo, na mpaka sasa, hakuna taarifa yoyote ya polisi yoyote kuwajibika?.
Ripoti imetoa tuu idadi ya vifo ila imeepuka kumtaja aliyetoa the order to shoot and kill. (piga risasi ua). Huko nyuma niliwahi kuandika na kusema, tusiwalaumu bure polisi wetu, usikute polisi wetu walikuwa wanatimiza wajibu wao na majukumu yao kikamilifu kwa kupokea amri halali, ya mabosi wao, ndio maana hatujasikia polisi yeyote akiulizwa chochote!.
Ripoti imetaja Idadi ya jumla ya vifo vyote officially recorded ni watu 518, kwa kitendo tuu cha kutangaza idadi ya vifo, tukubali tukatae Tume imekuwa very bold!, hii maana yake vifo hivyo viko well recorded and well documented, hadi taarifa za majina zipo na walizikwa wapi. Hivyo tunaomba familia za wahanga zipewe majina na zielezwe tuu hao watu 518, walizikwa wapi, kwa kuonyeshwa makuburi 518 yaliwazika hao watu 518 ili wafanye tuu hitma, maulid na kuwaombea misa, hii itaifuta ule uongo wa makaburi ya halaiki.
Baada ya kutangazwa idadi ya kweli ya vifo hivyo wa watu 518 vya October 29, sasa nashauri serikali yetu ifanye mambo makubwa matano
1. Ituambie aliyetoa amri au order ya kutumia risasi za moto ni nani?. Kitendo cha mpaka ripoti inatoka, CDF, IGP, na DGIS bado wako ofisini, kwa sisi tuliopitia jeshini na kufahamu kitu kinachoitwa chain of command, ni kama tunaelewa elewa hivi, ila ni kweli hadi kuuwa wale watoto malaika wa Mungu, ni maelekezo?, waliofanya vile wamefanywa nini?, na baada ya kutoka hii ripiti, hao wakubwa watu hapo juu wanasubiri nini kuwajibika?.!
2. Kama ile 1976, mikoa ya Mwanza na Shinyanga, walikufa watu 4 tuu mikononi mwa polisi, Mwali Nyerere alikasirika sana, jeshi la polisi na Idara ya Usalama wa taifa ilisafishwa kutoka juu mpaka chini, kwa hii Tanzania ya leo, tunapokea taarifa ya vifo 518, miongoni mwa vifo hivyo ni watoto 4 wa umri wa chini ya miaka 7 na watoto wawili wa umri wa chini ya miaka 5!, polisi hawa waliowaua malaika hawa kwa risasi, wamefanywa nini?!, kwenye serikali hii ya Samia, inabidi wafe watu wangapi ndipo tuanze kuwajibishana?!.
3. Kupitia balozi zetu zilizoko nchi mbalimbali duniani ambazo media zake zilitusingizia uongo, kuhusu idadi ya vifo, kwa kutangaza wamekufa maelfu, mabalozi wetu walioko huko, wakanushe uongo wa media zao ukiwemo uongo wa CNN, BBC na Aljazeera
4. Kupitia makampuni ya uwakili ya kizalendo, ikiwemo kampuni ya PPR Legal Chamber, tuwafungulie kesi za madai kuwadai fidia kutusingizia habari za uongo na kumtukana rais wetu.
5. Serikali yetu ikanushe rasmi ile idadi ya uongo na uzushi, ikiendelea kunyamaza bila kuukanusha huu uongo wa idadi ya vifo, maana yake itakuwa hii idadi ya vifo iliotangazwa leo na Tume, itakuwa ni idadi ya utekelezaji tuu wa ule ushauri wangu nilioutoa katika bandiko hili. Ushauri: Tangazeni idadi ya Vifo, na Ikibidi Hata Idadi ya Uongo tuu ili Wanyamaze!. Gazeti la “The Sun” limeiita Tanzania HOUSE OF BLOOD
Kwa vile sio mabalozi wetu wote wako competent na conversant na media, wale mabalozi competent na conversant kama Balozi Mobhare Matinyi, wasaidie kwenye hili, kufuatia kazi nzuri aliyoifanya akiwa Balozi wetu Sweden. Pongezi Balozi Wetu Sweden, Mobhare Matinyi. Alichofanya Kiigwe na Kifanywe na Balozi Zetu Zote
Huku TLS ikituma jopo la wanasheria wa International Law kuitetea nchi yetu kimataifa kwa kuwafungulia mashitaka wale wote wanaoichafua nchi yetu kwa kuizushia uongo, na kuwasema vibaya viongozi wetu, tusiwanyamazie!.
Uongo ukisemwa sana bila kukanushwa, baada ya ukweli kupatikana, tusipoutumia ukweli huu kuukanusha uongo wao, then uongo wao utaonekana ni ukweli na sasa hivi tusije kushangaa ICC wakitubishia hodi kutaka kuuthibitishia ule uongo wa CNN, BBC na Al Jazeera, wakati ukweli halisi ni idadi ya ukweli ya Tume ya Uchunguzi ya Jaji Chande.
What are we doing about this?.
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Update: 1
Naomba kuweka mchango wa mchangiaji mmoja very objective
Mkuu Tilatila, Tlaatlaah, kiukweli kabisa, nimetokea kukupenda sana, kwa jinsi ulivyo na heshima kwangu, huku kuniita Mwalimu, jina hili linanipa raha sana na kuniheshimisha, mimi ni miongoni mwa wanachama wa jamii forums toka ikiwa Jambo forums, hivyo huu ni mwaka wangu wa 20 humu jukwaani, na kiumri ni babu, hivyo kuna mabandiko yangu mengi, nayapandisha ili kufundisha, hivyo kiukweli mimi ni mwalimu, asante kwa hili.Mwalimu Pascal Mayalla,
Kitu cha pili ninachokupendea, wewe ni mmoja wa wanachama wenye good IQ, japo kuna hoja nyingi tunatofautiana, ili tofauti zetu ni logical, na very objective, tofauti yetu kubwa kati ya mimi na wewe ni kwenye impartiality, wewe mwenzangu umeegemea upande fulani, hati inatokea majito majinga, yanamdanganya Mfalme
kuwa yamemshonea joho la transparent, wasio na dhambi hawataliona, kisha matapeli hao wanaleta hilo joho hewa na kumvisha mflme mpaka nguo za ndani, kisha wanamwambia ajitazame kwenye kioo, jinsi alivyo pendeza, Mfalme anajiangalia kwenye kioo, anajiona kama alivyozaliwa!, ila kijiaminisha kuwa hana dhambi, anasema nimejiona nilivyo pendeza!.
Mfalme anaitisha mkutano wa hadhara na kuwaita wakuu wote na wananchi wote kujitokeza ukumbizi kwenye uzinduzi wa joho jipya la kisasa la mflme, ambalo wenye dhambi hawataliona. Wasaidizi wake wote wanajitokeza, kisha MC anatangaza here comes the King, kiukweli amependeza sana, Mfalme anaingia ukumbini kwenye kadamnasi ya watu, akiwa kama alivyo zaliwa, huku akitembea taratibu kwa madaha na joho jipya!.
Ukumbi wote, ukalipuka kwa makofi ya shangwe, hoi hoi na vigelegele kushangilia joho jipya la Mfalme, ila kuna mtoto mmoja mdogo, akamuuliza baba yake, mbona Mfalme yuko uchi?, Baba akamwambia mtoto nyamaza!. Miongoni mwa hao wapiga makofi na washangiliaji ni wewe mwenzangu!, mimi nilipokuja nikatama kumwambia Mfalme uko uchi, ila kwa vile niko nyuma, sauti zetu tujajitahidi kuzipaza, hazimfikii, kwasababu makofi na vigelegele vya washangiliaji, vimefunika sauti zetu!, kati ya mimi na wewe, nani anamsaidia kiukweli huyu Mfalume wetu?.
Wewe kwa IQ yako, kuna vitu ukweli unaujua!, usishangilie!, akiaibika Mfalme wetu ni sote tunaaibika!. Kati ya Walimzunguka Mfalme na Kumsifu Alivyopendeza na ile Invisible Robe, na yule mtoto aliyemweleza ukweli, kuwa yuko, nani anamsaidia kweli? masikini hatukumzingatia, tungemzingatia, hawa wasema ukweli, tusingefika hapa tulipofika!,
Nimemsikiliza kwa utuo Jaji Chande, kwa bahati nzuri, naomba nisiifanyie PMNA ile presentation ya Jaji Chande, nikakuambia kuna vitu amevisoma kwa stammering sana, kwasababu, viko kinyume cha dhamira yake!. Mtu wa kwanza kuhojiwa na tume, alipaswa kuwa ni yule aliyetoa ile amri ya kuzitumia za moto!, kwanini hakuhojiwa?.huenda hukumsikiliza Jaji Chande kwa umakini kuhusu hayo mambo ya kutumia silaha za moto, tena amelisema hili vizuri sana kisheria kabisa kitaifa, kikanda na kimataifa.
Bahati nzuri, mimi licha ya kuwa ni mtoto wa askari kwa wazazi wangu wote wawili, yaani Baba na Mama, mimi pia ni askari wa JKT kwa mujibu wa sheria, na baada ya JKT, nilijiunga moja kwa moja na JWTZ, hivyo mimi ni MT (Mlinzi wa Taifa) na nina MT number!, ikiibuka vita, mimi front faster!. Miongoni wa mafunzo ya kijeshi, kuna somo linaitwa MM (Mbinu za Medani), ambapo japo askari hata akiwa vitani, hawezi kufyatua risasi bila kupokea amri ya mkuu wake, ila kupitia somo la MM, mkiwa vitani, mkapigwa ambush, hapo sasa, hakuna kusubiri amri yoyote!, ni kila askari anaruhusiwa kutumia personal initiative yake kujiokoa!. Hii inamaana kilichotokea October 29, ni nchi ilipigwa ambush, hivyo askari wakatumia personal initiatives zao, kufanya sporadic shooting?.yaani askari kapewa silaha ya kwenda kulinda mathalani benki,
halafu kukurukakara ghafla wametokea majambazi au magaidi kama wale wa oct.29 wenye silaha za aina mbalimbali, wanavunja benki na kupora pesa kwenye ATMs na kumshambulia huyo mlinzi.
hivi kweli ili kutumia silaha ya moto aliyopewa, unapaswa kwenda kituoni kwake tena kuomba amri ya kutumia silaha aliyonayo?
Kwa mijibu wa PGO, baada ya kukamilisha kazi, kila asikari anaporudisha ile silaha amarah ana fanya retirement ya idadi ya risasi zote alizosaini wakati anachukua silaha, na ku account kwa maandishi, kila risasi aliyofyatua, alifyatua kulenga nini, hivyo data za wauaji wa wale malaika wa Mungu, zipo!, wamefanywa nini?. Data za wauaji wale watazamaji wa TV kwenye kibanda umiza, zipo, wamewatoa nje, wakawaambia walele chini kifudi fudi na kuwamiminia!, wamefanywa nini?. Wale waliowaua wale majirani wa Sitaki Shari, data zipo, wamefanywa nini?!.
Huu ndio uthibitisho wa high IQ yako, una uwezo to read in between the lines, umesoma tuu andiko langu hili, tayari, ukanibaini ni nani mimi ninamdhania ndie aliyetoa ile amri?!. Wewe sii mchezo!mbona ni rahisi sana kuhusu hilo mwalimu, ingawa dhamira yako i-wazi kwenye sana yakwamba umdhanie anaweza kutoa amri hiyo hakuepo hata huko yalipotokea hayo yaliyowakuta walionzisha vurugu na ghasia za october zilizopangwa na wanaharakati pomoja na wanasiasa waliokataliwa na wananchi.
Hapa nikupe kongole!, kwa mujibu wa katiba yetu, amri hiyo inaweza kutolewa na mtu mmoja tuu!, the one and only!. Mimi ni mkazi wa Dar, kwa vile amri ile kwa Dar ilitolewa na RPC wetu wa Kanda Maalum ambaye yuko chini ya RC DSM, mimi nilidhani vurugu ni Dar tuu, na nikadhani amri ile aliitoa muuaji fulani, hivyo nikawatetea polisi wetu PostGE2025 - Voices from Within: Mauaji ya wananchi Dar, tusiwalaumu Polisi. Je Amri ya kuua Ilitoka kwa muuaji huyu?Unaemdhamiria kwamba katoa amri,
anaweza kufanya hivyo kwenye hali ya vita tu kwa mujibu wa sheria.
Hapo nimemsingizia mtu yoyote?!.Lakini sio majambazi ya kisiasa yamejificha mahali, yanapanga vurugu na uhalifu halafu, kisha yanakutana na vyombo vya ulinzi na usalama na kudhibitiwa kisha unamsingizia ambae hahusiki kutoa amri ya kudhibiti ujambazi huo.
Kwa hapa, nakubaliana na wewe, na kuikubali busara yako, tena naomba nikuongezee kitu, Mhusika mkuu kwenye kadhia ile ya Mwanza ya mwaka 1976, kulikopelekea Kesi ya Mauaji Mwanza, iliyounguruma mwaka 1979, mimi nikiwa na umri wa miaka 10, niko darasa la 5, tunasoma shule moja na watoto wa wahusika wakuu wote!, kuanzia watoto wa Kawawa, Mwinyi, Siyovelwa, IGP Pundugu, DGIS Mzena, RPC Mkwawa, CJ. Nyalali, Commisioner wa Magereza Mwanguku, Mwanasheria Mkuu, Warioba, na wote hawa walisafishwa kwa kustaafishwa kwa manufaa ya umma, wengine wakalazimishwa kuandika barua kujiuzulu, kama Mwinyi na Siovelwa, weingine wengine sio tuu wakapigwa chini jumla, bali breki ya pili ni kwa pilato!, leo ripoti inatoka, wameuwawa watu 518 wakiwemo wale malaika wa Mungu, na hakuna askari yeyote aliyewajibishwa!, as if nothing happened!.kuwajibika na kuwajibishana katika suala muhimu na zito kama hili hakuhitaji kukurupuka, kunahitaji umakini mkubwa sana kwasababu kuna baadhi wanafaa kuishia jela ama vinginevyo.
ni muhimu sana kua wastahimilivu na wenye subra ili hatimae tusije kuumizana zaidi kwenye kuwajibishana.
Naungana na wewe, tuisubiri hiyo Tume ya Jinai, kisha tuwapeleke kwenye tume ya ukweli, upatanisho na maridhiano, tusameheane, tusonge mbele kuelekea kwenye katiba mpya, kama nilivyo sikia kwenye sauti hii
Wanabodi
Mimi mwenzenu mzee wa masauti wakati Watanzania na dunia tukiisubiri kwa shauku na hamu kubwa Ripoti ya Uchunguzi ya Jaji Chande, ambayo itaamua mustakabali mpya wa taifa letu la Tanzania.
Asubuhi hii, nimeisikia tena ile sauti ya "The Voices From Within", kwenye sauti hiyo nimemsikia mtu akisema
" Ndugu zangu Watanzania wenzangu wote, kwanza tupeane tena na tena, pole sisi sote katika umoja wetu, kwa kilichotokea ile October 29, poleni sana Watanzania wote na kwa dhati ya moyo wangu, nafsi yangu na kwa niaba ya serikali yangu, nawaomba sana radhi Watanzania wenzangu wote kwa...

- Pascal Mayalla
- katiba mpya ripoti ya jaji chande
- Replies: 33
- Forum: Jukwaa la Siasa
P.