Rostam aibukia kanisani!

Rostam aibukia kanisani!

Lakini RA alisema maneno "mazito" tu hapo Kanisani. Alisema Nchi inaelekea kubaya kwa sasa yakiwemo:
1.NDOA nyingi zinavunjika;
2.WATOTO wanaongezeka MITAANI;
3.CHUKI zimezidi miongoni mwa JAMII hadi kuombeana VIFO.
Pengine alisahau kusema kuwa UFISADI una MCHANGO wa AINA YAKE katika yote hayo.

Ni kweli Hayo uliyoyataja hapo juu yamesababishwa na Hao hao waliosema tuombe Mungu!
Mimi nasema waumini walitakiwa waombe Mungu kabla hawajamwalika kwani wamelichanganya kanisa na waumini wake.
Hizo chuki na uchawi na kuombeana VIFO ni SIMPLY..PROPAGANDA!
Kama NI UCHAWI BUNGENI ULIPREVAIL..Kuhusu MADAWA...AMINA CHIFUPA TUNAYAJUWA YALIYOMKUMBA NA NCHIMBI ANAFAHAMU HAYO!
Kuhusu KUOMBEANA KIFO...ASISAHAU KUWA BALLALI INASEMEKANA NI MPANGO WA MUNGU!
Sasa na huko KANISANI WANATKA WAUMINI WAAMINI KIFO/KUPOTEA KWA BALLALI NI MPANGO WA MUNGU?!
 
Gwiji kuja mbele ya Bwana sivyo hivyo yakhe!!! Sio kufanya kama unavyoenda kilabuni.... Kwenda mbele ya Bwana ni kutubu makosa na kubadilika... kitu ambacho Rozi Azizi hakukifanya!!!

Hilo la kutubu ama hakutubu mbele ya Mungu analijua Mungu wala halipaswi kujadiliwa.

Linalopaswa kujadiliwa kwa sheria zetu za kikaizar ni kua RA ni mwizi na afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Mambo ya kufuatiliana hadi kuingilia maamuzi ya Mungu hapo ndipo tunakosea .

Naamini ninyi nyote mnatoa sadaka kanisani/msikitini kwa namna moja ama nyingine Ni nani kati yenu si Mzinifu?? ninani kati yenu si mwongo ,ninani kati yenu asiyefanya dhambi???
 
Ni jambo lenye ugumu wake kusema kwamba Ndugu Rastom Aziz alikuwa na lengo la kujisafisha ndani ya Kanisa. Mimi ninapata kigugumizi. Je ni kwani hakutumia fursa kama hiyo kwanza ndani ya Msikiti na baadae ndani ya kanisa.

Ninaweza kuamini inawezekana ndani ya misikiti alinyimwa fursa hiyo. Je kikao hicho cha wakuu wa Kanisa wanakutana ili kutoa tamko gani? Kwani maji yakishamwagika hayazoleki. Wakati akitoa mada sijui niseme ni risala au mahubiri au kujisafisha, alipigiwa makofi ya kufa mtu na waumini wengi wa kanisa hilo alilokwenda kujiosha.

Makofi na nderemo na vifijo viliongezeka pale alipoahidi kuto millioni saba kama mchango kwenye kanisa hilo waumini walifurahi sana. Nina imani hata waliokuwa wanaendesha ibaada walipiga makofi. Je nini lengo la wakuu wa kanisa la KKKT kukutana? Je watalipana Perdiem?
 
Last edited:
Hilo la kutubu ama hakutubu mbele ya Mungu analijua Mungu wala halipaswi kujadiliwa.

Linalopaswa kujadiliwa kwa sheria zetu za kikaizar ni kua RA ni mwizi na afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Mambo ya kufuatiliana hadi kuingilia maamuzi ya Mungu hapo ndipo tunakosea .

Naamini ninyi nyote mnatoa sadaka kanisani/msikitini kwa namna moja ama nyingine Ni nani kati yenu si Mzinifu?? ninani kati yenu si mwongo ,ninani kati yenu asiyefanya dhambi???

KULIRUDISHA TAIFA UTUMWANI NI DHAMBI INAYOWEZA KUPELEKEA UMWAGAJI DAMU!

Na UZINZI...Ni dhambi inayowafanya hata wabunge wasahau majukumu yao!

Na uchawi..Umepelekwa mpaka BUNGENI PANAPODAIWA KUWA NI PATAKATIFU!

Na UKABILA...Unapandikizwa miongoni mwetu kwa kuwatumia wale WADINI na WAKABILA walioko ccm MTANDAO ambao wengine SI WATANZANIA..

Lakini wanaitumia HISTORIA YA TANZANIA VIBAYA...

Ili KULETA MACHAFUKO NA UMWAGAJI DAMU...

ILI..KUTIMIZA NDOTO YAO YA KUENDELEA KULINDA MIGODI NA KUUZA MADINI KWA MANUFAA YA MAFISADI...

ILI WANANCHI WAENDELEE KUFA KWA NJAA, NA MAGONJWA, MADAWA YA KULEVYA NA UKIMWI PAMOJA VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE..

ILI WAITAWALE AFRIKA YOTE NA KUWAFUTILIA MBALI BANTUS..

Hivi vita vikitokea HAO WAUMINI WATAPIGANIA UHURU AMA MAFISADI WANAOONGOZWA NA MUIRANI?

Should i go on?
 
Hilo la kutubu ama hakutubu mbele ya Mungu analijua Mungu wala halipaswi kujadiliwa.

Linalopaswa kujadiliwa kwa sheria zetu za kikaizar ni kua RA ni mwizi na afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Mambo ya kufuatiliana hadi kuingilia maamuzi ya Mungu hapo ndipo tunakosea .

Naamini ninyi nyote mnatoa sadaka kanisani/msikitini kwa namna moja ama nyingine Ni nani kati yenu si Mzinifu?? ninani kati yenu si mwongo ,ninani kati yenu asiyefanya dhambi???

Sio kila aliyepo hapa ni lazima awe muislam ama Mkristo, wengine hapa ni Traditionalist hatutoi sadaka za fedha kama unavyosema kuwa unaamini hivyo.

Kumbuka kuwa usitake kile unachofikiri na kukiamini basi kila mmoja anaweza kukuunga mkono wewe .

Dhambi hii italianguisha kanisa na huenda ikajirudia kwani itakumbukwa kuwa miongoni mwa vitu vilivyomfanya Martin Luther kujitoa kwenye kanisa Katoliki ilikuwa ni pale ambapo kanisa lilikuwa na sheria za kuwataka waumini kulipia na kuweza kuupata msamaha wa dhambi naye akalipinga hilo na hapo pamoja na sababu nyingine pakawa mwanzo wa kuibuka kwa uluteri.

Waanglikana nao waliweza kujitenga hivyo hivyo haswa pale mfalme Charles alipoamua kuachana na mkewe na huku akitaka aendelee kutambuliwa na kanisa na kanisa lilipoweka msimamo alijitenga na ukawa mwanzo wa Anglican.

Hapa napo Kanisa la Tanzania na haswa KKKT wasipoangalia litaweza kugawanyika kati ya KKKT ya kuwasafisha mafisadi na KKKT inayopinga ufisadi.
 
tunapochangia hapa tutumie vigezo vya kidunia katika kuchangia, ni kweli kuna watu wengi wanapeleka pesa chafu kanisani, lakini huyu RA ndo tuna data zake, hatuwezi kumwacha eti kwa kuwa kuna wengine wa kufikirika
 
Lakini hawa watu wa kanisa si walimwalika wenyewe au alijipeleka? Kuuma na kupuliza kutawaponza, inawabidi waamue haya mambo ya vuguvugu yatawasuta!

Wamekosa kazi za kufanya hwa watu wamualike wao then wamkalie vikao.Hizo fedha watakazo jilipa kama sitting allowance wangezipeleka DogoDogo Centre.
Rubbish.
 
[/SIZE][/COLOR]
Sio kila aliyepo hapa ni lazima awe muislam ama Mkristo, wengine hapa ni Traditionalist hatutoi sadaka za fedha kama unavyosema kuwa unaamini hivyo.

Kumbuka kuwa usitake kile unachofikiri na kukiamini basi kila mmoja anaweza kukuunga mkono wewe .

Dhambi hii italianguisha kanisa na huenda ikajirudia kwani itakumbukwa kuwa miongoni mwa vitu vilivyomfanya Martin Luther kujitoa kwenye kanisa Katoliki ilikuwa ni pale ambapo kanisa lilikuwa na sheria za kuwataka waumini kulipia na kuweza kuupata msamaha wa dhambi naye akalipinga hilo na hapo pamoja na sababu nyingine pakawa mwanzo wa kuibuka kwa uluteri.

Waanglikana nao waliweza kujitenga hivyo hivyo haswa pale mfalme Charles alipoamua kuachana na mkewe na huku akitaka aendelee kutambuliwa na kanisa na kanisa lilipoweka msimamo alijitenga na ukawa mwanzo wa Anglican.

Hapa napo Kanisa la Tanzania na haswa KKKT wasipoangalia litaweza kugawanyika kati ya KKKT ya kuwasafisha mafisadi na KKKT inayopinga ufisadi.

Watu mmekata ishu za EPA mpaka umahili huo sasa mnaanza kukata ishu za Mungu .
Hata wapagani hua wanatoa zaka mfano kuua watoto wa wakwanza ama wa mwisho wa kiume ama kumsaka albino hadi umuangamize.

Mimi nielewavyo Martin alijitenga na Kanisa katiliki kwa sababu yeye alikua Padre na alitaka kuoa mwanamke Na alipojitenga alitoka na kundi lake na mke wake alikua sister aliyeondoka naye.

Aglican kama sikosei huyu jamaa alikua mfalme aliyelifadhili kanisa katoliki huyu kama sikosei alikua mwingereza yeye kwa mapesa yake akataka kuoa mwanamke wa pili na akalazimishe afungeshwe ndoa na padree maombi yake yalivyokataliwa akaamua kuanzisha kanisa lake.

Harafu kama wewe kanisa ulifuatalo kama unaona kuzini si kosa ndivyo hivyo Ra yawezekana anaona pia kuiiba si kosa.
kumbe ili asiingilie kanisa lako na wewe usiingilie kanisa la mwingine ndiyo inabidi mfuate ile kitu ambayo ni mwamuzi kwa interest za wote yani MAHAKAMA ama sheria za kaizar
 
Jamani Jamani,
Mimi nadhani tatizo sio kutolewa kwa sadaka hiyo isipokuwa mwaliko wa Rostam ambaye anapewa hata wakati wa kuzungumza!.. Yaani sioni kabisa nafasi ya Mugabe kwenda Marekani kwa Mwaliko akapewa muda kuzungumza acha mbali kwenda Vatican kuonana na Pope...
Mimi nasema siku zote huwezi ku make a deal na devil.. hii haikubaliki kabisa ktk Biblia Koran wala misahafu mingineyo - isipokuwa tu sisi wenye njaa ndio tunatafsiri sura hizi kwa matakwa yetu. Inakubalika tu pale huyu Devil atakapo salimu amri na kurudi ktk njia iliyonyooka...
Ndio hayo ya Kikwete kwenda pendekeza serikali ya Mseto Zimbabwe ati Zimbabwe haiwezi kuongozwa na chama kimoja!.... Hii ni dalili ya kile kitakachofuatia Tanzania kama CCM watashindwa!
Inatisha sana!
 
Wamekosa kazi za kufanya hwa watu wamualike wao then wamkalie vikao.Hizo fedha watakazo jilipa kama sitting allowance wangezipeleka DogoDogo Centre.
Rubbish.

Siyo wote waliokosa la kufanya!
Waliokosa la kufanya ni waliotowa mwaliko!
Hapa ni MAISHA YA WANADAMU YAKO HATARINI!
So nawaunga MKONO WANAPOSIKILIZA VILIO VYA WANA JF NA WANANCHI WAZALENDO KWA UJUMLA!
 
Hilo la kutubu ama hakutubu mbele ya Mungu analijua Mungu wala halipaswi kujadiliwa.

Linalopaswa kujadiliwa kwa sheria zetu za kikaizar ni kua RA ni mwizi na afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Mambo ya kufuatiliana hadi kuingilia maamuzi ya Mungu hapo ndipo tunakosea .

Naamini ninyi nyote mnatoa sadaka kanisani/msikitini kwa namna moja ama nyingine Ni nani kati yenu si Mzinifu?? ninani kati yenu si mwongo ,ninani kati yenu asiyefanya dhambi???

Magwiji... Kinachogomba hapa sio ni kwanini RA ametoa "mchango" (hongo???)..... ambao wewe unauita sadaka. Ni namna alivyoamua kutoa: Je nini madhumuni yake? Kwanini atoe kwa vijembe?
 
tunapochangia hapa tutumie vigezo vya kidunia katika kuchangia, ni kweli kuna watu wengi wanapeleka pesa chafu kanisani, lakini huyu RA ndo tuna data zake, hatuwezi kumwacha eti kwa kuwa kuna wengine wa kufikirika

Katika dini tatizo ni ufisadi si mtu, mtu aliumbwa na Mungu kwa mfano wake
anatumiwa na shetani tu kueneza ufisadi wake mwishowe atakufa katika ufisadi ataenda hell kama kanisa halitafanya kazi yake, ila ufisadi hautakufa pamoja naye utaendelea kupitia mtu mwingine kwa jina lingine,
 
I love Mtikila...akiona chungwa anasema chungwa.

Huyu mtu anatufaa sana sehemu fulani fulani lakini sio Ikulu.

Nani anafaa kuwa IKULU?
Wewe si ndiye engineer wa MATAWI YA ccm HUKO UK?
Sasa kwanini ulifunguwa matawi wakati wa KASHFA na si KABLA?
Usitupangie wananchi nani anafaa kuwa RAIS!
WEWE WAPANGIE HAO WANANCHAMA WAKO WA ccm HUKO UK!
 
Magwiji... Kinachogomba hapa sio ni kwanini RA ametoa "mchango" (hongo???)..... ambao wewe unauita sadaka. Ni namna alivyoamua kutoa: Je nini madhumuni yake? Kwanini atoe kwa vijembe?

tatizo ni kwa nini walimualika wakati walijua ni mdhambi?
 
Siyo wote waliokosa la kufanya!
Waliokosa la kufanya ni waliotowa mwaliko!
Hapa ni MAISHA YA WANADAMU YAKO HATARINI!
So nawaunga MKONO WANAPOSIKILIZA VILIO VYA WANA JF NA WANANCHI WAZALENDO KWA UJUMLA!

Maisha gani yapo hatarini ebbo!jaribu kuwa realistic for a long as alichoiba he is trying to give it back to the society kuna shida gani?Hao waliopewa huo msaada wakiutumia kwA malengo husika basi siyo hao tuu watakao faidika bali watu wengi zaidi.
 
Rostam azua gumzo

na Martin Malera
Tanzania Daima~Sauti ya watu

HATUA ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM), kutinga kanisani na kutoa kauli nzito za kujisafisha kutokana na tuhuma za ufisadi zinazomwandama huku akiwasuta wabaya wake kisiasa, imezua maswali mengi kuliko majibu.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwisiga Baregu, alisema jana kuwa anamshangaa mbunge huyo kuamua kulitumia kanisa kujisafisha.

Alisema hali hiyo imelichafua kanisa hilo kubwa na lenye heshima kubwa nchini.

“Mimi namshangaa Rostam, lakini pia nalishangaa kanisa lenyewe. KKKT ni kanisa kubwa sana nchini na maaskofu wake kwa nyakati tofauti walishatoa kauli kadha wa kadha za kukemea ufisadi, lakini leo kanisa hilo hilo liko mbele kupokea fedha za ufisadi, hiyo mimi imenishangaza sana,” alisema mwanazuoni huyo ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

“Rostam anachotakiwa kufanya ni kujibu tuhuma zake ni kwa namna gani amehusika ama hakuhusika kabisa na Richmond au Dowans, lakini kwa stahili hii hawezi kujibu tuhuma, sana sana ataendelea kuibua maswali mengi yasiyo na majibu, na binafsi nashangaa sijui nani mshauri wake aliyemtuma kufanya hivyo,” alisisitiza Profesa. Baregu.

Kwa mujibu wa Baregu, Rostam anapaswa kujibu tuhuma zake ama kwa kutumia vyombo vya habari au mahala pengine popote au ndani ya Bunge, lakini si kutumia mimbari ya kanisa kujisafisha.

Kwa upande wa kanisa, Profesa. Baregu alishauri litoe taarifa ni namna gani limekubali kutumika kama kichaka cha kumsafisha Rostam ambaye kwa imani ni muumini wa dini ya Kiislamu.

Profesa Baregu aliwaasa Watanzania na vyombo vya habari kuwa makini na mbinu zinazotumiwa na watuhumiwa wa ufisadi kujisafisha, kwa madai kuwa wana mbinu nyingi mbaya na chafu kwa jamii kutokana na uwezo wao kifedha.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema alieleza kushangazwa kwake na hatua ya Rostam kutumia kanisa kujisafisha.

Alisema mbunge huyo ni mjanja kutokana na staili yake aliyotumia kujisafisha na tuhuma zinazomwandama.

Kwa upande wa kanisa, Mrema alilishangaa na kuyataka makanisa yote kuiga mfano na kauli ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyewahi kuyatahadharisha kujiepusha na fedha za mafisadi.

“Hilo kanisa limejidhalilisha, na linaweza kupoteza heshima yake lisipoangalia. Rostam na kanisa wapi na wapi? Halafu kwa nini hakuzungumzia kilichompeleka pale? Kwa nini ameruhusiwa kutumia kanisa kujisafisha?” alihoji Mrema na kuongeza kuwa Rostam ameibua maswali mengi kuliko majibu.

Mbali ya viongozi hao, baadhi ya wananchi waliopiga simu katika chumba chetu cha habari, walielezea kushangazwa kwao na hatua ya Rostam kuamua kuuwasha moto unaoonekana kufifia wa ufisadi wa Richmond.

Juzi, Rostam aliibuka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Kinondoni, Dar es Salaam, ambako alisema taifa liko kwenye wakati mgumu kisiasa na kijamii, hivyo kuwataka wananchi watumie makanisa kulirejesha katika mstari ulio sahihi.

Mbunge huyo anayeandamwa na jinamizi la ufisadi, alisema waumini wa dini hawamtuhumu mtu, hawamshutumu, hawapendi wenye wivu na wenye chuki bali wanapenda haki.

Alisema hivi sasa nchini, watu wameanzisha tabia ya kuchukiana mpaka kuzushiana uchawi na kuombeana vifo, na kusisitiza kuwa wananchi watumie makanisa kukemea vitu hivyo.

Ingawa katika kauli hiyo hakutaja mtu, lakini mbunge huyo ambaye hajawahi kupata mpinzani katika jimbo lake, alikuwa akizungumzia tukio la hivi karibuni bungeni, ambako Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge (CCM) na ofisa mmoja mwandamizi wa Bunge, walituhumiwa kuweka vitu aina fulani ya uchawi au sumu ya kisasa ndani ya Ukumbi wa Bunge.

Alisema ana watoto watatu ambao aliahidi kanisani hapo kwamba anataka awalee katika misingi ya dini ili wawe wananchi bora na waadilifu hapo baadaye.

“Nawashukuru kwa kuamua kunialika kuwa mgeni rasmi leo, hii ni ishara kwamba mmeamua kupuuza viji-maneno na upuuzi wa vijiweni. Nafurahi kuwa miongoni mwenu…hamtuhumu, hamshutumu, hampendi wenye wivu na wenye chuki, mnapenda haki. Ninao watoto watatu na nataka niwalee katika misingi hii,’’ alisema Rostam huku akishangiliwa na umati wa watu walioshiriki hafla hiyo.

Rostam alialikwa kanisani hapo katika hafla ya uzinduzi wa albamu ya kwaya ya Amkeni ya kanisa hilo, ambako alitoa mchango wa sh milioni tano kuchangia seti za vyombo vya muziki kwa kwaya hiyo pamoja na jenereta yenye thamani ya sh milioni 2.6.

Katika siku za hivi karibuni, Rostam amekuwa akiandamwa na jinamizi la ufisadi kiasi cha baadhi ya wabunge na wananchi kutaka achukuliwe hatua za kisheria.

Amekuwa akitajwa kuwa na uhusiano na Kampuni ya Dowans iliyokuwa inaendesha shughuli za Richmond kabla ya serikali hivi karibuni kuamua kuvunja mkataba wake. Hata hivyo Rostam alikanusha tuhuma hizo kupitia gazeti hili
 
tatizo ni kwa nini walimualika wakati walijua ni mdhambi?

Wadhambi hawaalikwi kanisani?Please mama tumia busara zako hata yesu alisema waacheni wenye dhambi waje kwangu na acha kumjudge ni mdhambi hiyo kazi ya Mungu mama eeeeeeeehhhhhhh!
 
Maisha gani yapo hatarini ebbo!jaribu kuwa realistic for a long as alichoiba he is trying to give it back to the society kuna shida gani?Hao waliopewa huo msaada wakiutumia kwA malengo husika basi siyo hao tuu watakao faidika bali watu wengi zaidi.

Unataka MATH?

Niambiye milioni mbili za jenereta zikilinganishwa na pesa anazolipwa na serikali kwa kushindwa kutupa umeme wa DHARURA kwa kupitia DOWANS!

Kweli unataka kulinganisha mabilioni ya dola na pesa za jenereta na pilau?

Ama PESA ZA KWAYA si ni za kuwafanya muendelee kusikiliza propaganda za kuwasafisha na ama maneno ya kuendeleza UKONDOO kwa kigezo cha KIKRISTO?

Ni wakristo gani hao wazungu waliowaletea hiyo dini ambao hawakupigania UHURU WAO?

AMA NI WANA WA ISRAEL?
WE KEVO NI NANI?

NB:Naomba pia huo UJUMBE KWENYE HIYO ALBAM YA KWAYA UANGALIWE KWANI INAWEZEKANA UNA LENGO LA KUMSAFISHA ROSTAM!

Kama kilichoimbwa kwenye kwaya hiyo ni cha Mungu..Basi ROSTAM ASINGETHUBUTU KUCHANGIA FEDHA!

Mamluki wa UFISADI WAUMNI MUWAKIMBIE!

Hata ikishindikana muwe wakatoliki ama walokole na ama KANISA LITOWE TAMKO KABLA HAO KKK HAMJASAMBARATIKA...! muachane na MAFISADI!
 
Unataka MATH?
Niambiye milioni mbili za jenereta zikilinganishwa na pesa anazolipwa na serikali kwa kushindwa kutupa umeme wa DHARURA!
Kweli unataka kulinganisha mabilioni ya dola na pesa za jenereta na pilau?
Ama PESA ZA KWAYA si ni za kuwafanya muendelee kusikiliza propaganda za kuwasafisha?
WE KEVO NI NANI?
NB:Naomba pia huo UJUMBE KWENYE HIYO ALBAM YA KWAYA UANGALIWE KWANI INAWEZEKANA UNA LENGO LA KUMSAFISHA ROSTAM!
Kama kilichoimbwa kwenye kwaya hiyo ni cha Mungu..Basi ROSTAM ASINGETHUBUTU KUCHANGIA FEDHA!
Mamluki wa UFISADI WAUMNI MUWAKIMBIE!
Hata ikishindikana muwe wakatoliki ama walokole na ama KANISA LITOWE TAMKO KABLA HAO KKK HAMJASAMBARATIKA...! muachane na MAFISADI!

Unataka kujua mimi ni nani?Ni mpinga unafiki,ufisadi,mzalendo wa kweli na kila aina ya uonevu.Mimi ndiye.Ila lets get back to the topic kuwa wakae vikao wasikae ameshaenda na kuongea ameongea.Hawana la kufanya ila wamuombee kwa Mungu amrejeshe kwenye njia ifaayo waijuayo wao.
 
Wadhambi hawaalikwi kanisani?Please mama tumia busara zako hata yesu alisema waacheni wenye dhambi waje kwangu na acha kumjudge ni mdhambi hiyo kazi ya Mungu mama eeeeeeeehhhhhhh!

Jamani mbona wengine huwa wanatengwa na kanisa, au kuna dhambi kubwa inayoruhusiwa mtu kumtenga na hata asishiriki kuliko dhambi ya ufisadi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom