Rostam aibukia kanisani!

Rostam aibukia kanisani!

hata kalmeshi patni wa grand regency ya kenya aliishia kuokoka, sasa sijui na huyu wa kwetu ni hivyo hivyo?
 
Tuondoe u holier than thou for a minute, hivi toka lini kanisa likawakataa wenye dhambi na pesa zao?

Yesu si alisema asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe? Hivi watu wote wanaotoa sadaka kanisani hela zao zinachunguzwa?

Kama mnataka kumbana Rostam mtafuteni pengine, tunajua anaweza kuwa anataka kulinunua kanisa na zaidi kumnunua Spika kwa influence peddling lakini hatuwezi ku prove hilo.

Mtafuteni mnakoweza kumkamata, sio kwenye hili. After all wenzetu siku hizi ikigundulika umepewa hela chafu ndiyo kwanza wanazitoa kwa charities na vitu kama makanisa, mbona hilo halionekani kama issue? Hii uppity minded holier than thou attitude haitufai.
 
Jamani Hizo Pesa Ni Za Watakatifu Watanzania Sasa `````tusihukumu Kwanza Mungu Ana Njia Nyingi Za Kuzirudisha Na Kama Jakaya Alivyoowambiaaaaaaaaa
Tunataka Pesa Kwanza......hivyo Jamani Makanisa Msiiwaache
Wanakwaya

Nexty Mkaribisheni @#@lowassa

Karamagi

Mwanyika


Msabaha


Hosea


Huu Ndio Wakati Wa Kuzindua Kwaya Jamani Kumtukuza Mungu Kwa Nguvu Zote

Biblia Inasema Pesa Na Mali Vyote Ni Mali Ya Bwana!!!!!!!!!!!!

Mungu Anazidi Kujiidhihirisha Jamani!!!!!!!!
 
Kuna habari kwamba, baadhi ya Maaskofu wanakutana Dar es Salaam katika ukumbi wa Travatine Hotel Magomeni, kujadili na kutoa tamko kuhusu Rostam kwenda kujisafisha katika Kanisa la KKKT, Kinondoni. Kwa mwenye taarifa kamili atupatie tafadhali. Nimetumiwa sms na mtu mmoja aliyeko Dar, walioko Dar tujulisheni
 
KKKT IMEWAUMBUA WAKRISTO KWA KUMWALIKA FISADI
Sijui Wakristo wafanyeje kujisafisha na kashfa hii ya kupokea fedha ya wizi, rushwa na ufisadi wa aina mbalimbali kutoka kwa kiongozi wa mafisadi nchini, Rostam. Kwanza wamfukuze uchungaji Fisadi Mchungaji Joseph Masage halafu tuendelee na hatua nyingine. lazaros
 
Kuna habari kwamba, baadhi ya Maaskofu wanakutana Dar es Salaam katika ukumbi wa Travatine Hotel Magomeni, kujadili na kutoa tamko kuhusu Rostam kwenda kujisafisha katika Kanisa la KKKT, Kinondoni. Kwa mwenye taarifa kamili atupatie tafadhali. Nimetumiwa sms na mtu mmoja aliyeko Dar, walioko Dar jujulisheni

Nimejulishwa kwamba wanakutana pale pale Kanisani KKKT Kinondoni, inawezekana pia wakakutana katika ukumbi mwingine wowote, lakini la msingi ni kwamba wanasema ni kweli kuna kitu kama hicho
 
Nimejulishwa kwamba wanakutana pale pale Kanisani KKKT Kinondoni, inawezekana pia wakakutana katika ukumbi mwingine wowote, lakini la msingi ni kwamba wanasema ni kweli kuna kitu kama hicho

Lakini hawa watu wa kanisa si walimwalika wenyewe au alijipeleka? Kuuma na kupuliza kutawaponza, inawabidi waamue haya mambo ya vuguvugu yatawasuta!
 
Lakini hawa watu wa kanisa si walimwalika wenyewe au alijipeleka? Kuuma na kupuliza kutawaponza, inawabidi waamue haya mambo ya vuguvugu yatawasuta!

Inategemea ni nani hasa aliyemwalika. Kama mtu mmoja aliwaambia wenzake, "suala la mgeni rasmi niachieni mimi" then wakaja katika shughuli na kumkuta Rostam, huwezi kusema 'kanisa' ndio limealika. Yes ni kanisa kwa maana aliyealika alifanya hivyo kwa niaba ya kanisa. hii ni sawa na Waziri kufanya maamuzi kwa niaba ya serikali, akitumia dhamana aliyopewa, lakini kama maamuzi yake yataonekana yanakwenda kinyume na msimamo ama maslahi ya waliompa kazi (serikali/kanisa), hatua zinapaswa kuchukuliwa. Hakuna ubaya kwa hilo. Lakini watu wa aina hiyo kuwa ama wanajiandaa kujibu mapigo au wanajiandaa hata kupokea adhabu yoyote na kuacha kazi ama kujitetea
 
Wakimgeuka tuu ameumia....

Labda watumia busara za.....

Tanzanianjema
 
Mimi nadhani kanisa (uongozi mkuu) kama nao ulikuwa surprised na mtumishi wake (mch wa Kinondoni) kwa mwaliko wa Rostam ni vema sana waliweke hili jambo wazi. Huyo mchg apumzishwe kazi. Kusiwe hata na kigugumizi. In fact mimi nadhani kama leo kanisa wataji distance na mwaliko wa Rostam the whole event ya jumapili itakuwa na posive effect kwenye vita hii. Pia itakuwa hatua muhimu sana kwa kanisa lililolokuwa limekaa kimya kutoka hadharani na kusema wazi wako wapi katika hili la ufisadi. Hawahitaji kabisa kuwa vuguvugu! Mbona Askofu Mokiwa yuko wazi. Askofu Malasusa naye awe wazi - yuko upande wa mafisadi au upande wa mungu, au hayupo kote! Hata kama akina Lowasa ndio watoa sadaka, mungu haihitaji sadaka zao.
 
Ni dhahiri Rostam kuhusishwa na kashfa ya Richmond ambayo imekuwa gumzo la kila siku nchini ndicho chanzo na sababu ya yeye kualikwa kanisani hapo. Miaka yote Rostam yupo nchini humu kwa nini asialikwe anaalikwa sasa? Ni dhahiri miongoni mwa waumini hao kuna mtu ambaye anafahamiana na Rostam na kwa pamoja wakala njama kuhakikisha anaalikwa kanisani hapo ili aweze kwenda kutoa vijisenti vyake na kupata ukumbi wa kuzungumza na kuwapiga wananchi wanaohoji juu ya ufisadi. Kitendo cha Rostam kwenda kanisani na kutoa kauli alizotoa ni kulidhalilisha Kanisa lililomualika na KKKT kwa ujumla. Kwa wale waliangalia televisheni na kumuona Rostam akizungumza watakubaliana kwamba uso wake ulionyesha kutahayari wakati akitamka maneno ya kuwapiga vijembe wanaoshutumu ufisadi na kuzusha mambo ya uchawi! Cha kusikitisha sana ni kwamba baadhi ya waumini walimshangilia kwa makofi na vigelegele! Ama kweli umaskini na hali ngumu za maisha vinatupeleka pabaya. Hivi wananchi wangelikuwa na maisha bora na makanisa hayo kuweza kusimama imara kwa kujitegemea kwa kila jambo kutokana na sadaka za waumini wao, Rostam angelipata wapi ukumbi wa kwenda kulikejeli kanisa?
 
Basi angealikwa akafanya mambo yake kimya kimya bila kujisafisha na kutetea kina Chenge, angalao ingekua afadhali, lakini anatumia jukwaa la KANISA kujisafisha!!!!??? Kanisa linalazimika kujisafisha sasa. Watajiweka pabaya kwa waumini wao na wadau wengine
 
kkkt Ni Wanafiki Hawana Jeuri Ya Kumgeuka Rostam, Wakutane Wawezavyo Lakini Hakuna Lolote La Maana Kwa Watanzania Litakalotokea.

"ikiwa" Watatoa Tamko La Kumkana Rostam Na Kumrudishia Hela Zake Basi Kweli Nitakubali "ukombozi Umefika Nchini Kwetu."
 
Wanamjadili Rostam ili wamrudishie sadaka yake?
 
Kuna mahali KKKT imeamua kujichanganya...unafiki fulani unaendelea na viongozi wanafikiri waumini wao hawaoni.
 
ni Dhahiri Rostam Kuhusishwa Na Kashfa Ya Richmond Ambayo Imekuwa Gumzo La Kila Siku Nchini Ndicho Chanzo Na Sababu Ya Yeye Kualikwa Kanisani Hapo. Miaka Yote Rostam Yupo Nchini Humu Kwa Nini Asialikwe Anaalikwa Sasa? Ni Dhahiri Miongoni Mwa Waumini Hao Kuna Mtu Ambaye Anafahamiana Na Rostam Na Kwa Pamoja Wakala Njama Kuhakikisha Anaalikwa Kanisani Hapo Ili Aweze Kwenda Kutoa Vijisenti Vyake Na Kupata Ukumbi Wa Kuzungumza Na Kuwapiga Wananchi Wanaohoji Juu Ya Ufisadi. kitendo Cha Rostam Kwenda Kanisani Na Kutoa Kauli Alizotoa Ni Kulidhalilisha Kanisa Lililomualika Na Kkkt Kwa Ujumla.

Kwa Wale Waliangalia Televisheni Na Kumuona Rostam Akizungumza Watakubaliana Kwamba Uso Wake Ulionyesha Kutahayari Wakati Akitamka Maneno Ya Kuwapiga Vijembe Wanaoshutumu Ufisadi Na Kuzusha Mambo Ya Uchawi! Cha Kusikitisha Sana Ni Kwamba Baadhi Ya Waumini Walimshangilia Kwa Makofi Na Vigelegele! Ama Kweli Umaskini Na Hali Ngumu Za Maisha Vinatupeleka Pabaya.
hivi Wananchi Wangelikuwa Na Maisha Bora Na Makanisa Hayo Kuweza Kusimama Imara Kwa Kujitegemea Kwa Kila Jambo Kutokana Na Sadaka Za Waumini Wao, Rostam Angelipata Wapi Ukumbi Wa Kwenda Kulikejeli Kanisa?


Ati Alisema Nini Huyu Fisadi..?

Halafu Waumini Wakashangilia.!! Duh, Tanzania Tuna Safari Ndefu..kkkt Kama Wangekuwa Na "guts" Wangetoa Tamko Haraka Iwezekanavyo Kumkana Yeye Na Maneno Yake.

Yaani Kweli Rostam Amekwenda Kwenye Nyumba Ibada; Mahali Patakatibu Na Kupiga Wanasiasa Wenzake Vijembe??!!

Nyerere Alisema Ikulu Ni Mahali Patakatifu...lakini Kanisani Ni Patakatifu Zaidi..sasa Huyu Rostam Haheshimu Ikulu Yetu..hata Kanisa Nalo Anaona Ni Jukwaa Lake La Kutoa Kashfa.!!

Tanzania Nakulilia Tanzania.
 
Hawajakutana Maaskofu wowote. Wanaozungumza sasa ni Mtikila na wenzake. Mchungaji amekwepa waandishi anasema yuko LIKIZO.... inawezekana anaweza kachukuliwa hatua.
 
Wanamjadili Rostam ili wamrudishie sadaka yake?

Mama napendekeza ile pesa ya RA tuiite hongo au rushwa maana haikuambatana na maneno matakatifu bali maneno ya kidunia au ya mtu wa mataifa.
Kwa kuwa alizunguka mbuyu basi zile pesa ni najisi kwa hiyo hazifai hata kazi ya ufalme wa Mungu,wamrudishie zote
 
Ufisadi upo hata nadani yamakanisa kadhaa. Viongozi wa makanisa wanaweka pesa mbele, hasa kkkt, ndio maana utaona watu kama akina Mengi wanaalikwa kuwa wageni rasmi kwa shughuli za kikanisa japokuwa yeye (Mengi) ndoa yake imeshindikana. Hana imani ila ana pesa yake!
 
Mama napendekeza ile pesa ya RA tuiite hongo au rushwa maana haikuambatana na maneno matakatifu bali maneno ya kidunia au ya mtu wa mataifa.
Kwa kuwa alizunguka mbuyu basi zile pesa ni najisi kwa hiyo hazifai hata kazi ya ufalme wa Mungu,wamrudishie zote

kazoea kutoa sadaka za aina hiyo, na ndicho kilichompatia ubunge. Ningekuwa na uwezo ningewachapa viboko wananchi wote wanaolaghaiwa kihivi ili kuwapigia kura watu hawa. Hiyo pesa si ingetosha kuchimba kisima kirefu kule jimbo kwake kikawasaidia hao wapinga kura wake, au angenunua dawa akapeleka kwenye zahanati moja katika vijiji huko Ingunga. Yaani hapa kabugi step, Mungu ameamua kumwanika mwaka huu. Ataikimbia nchi mbona!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom