Rostam asipotangazwa amekufa kama Balali mniue-Askofu Fundi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam asipotangazwa amekufa kama Balali mniue-Askofu Fundi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fred Katulanda, Jul 19, 2011.

 1. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Na Fundi Segeredi

  LEO nataka nieleze kichekesho cha mmoja wa watumishi wa Mungu aliyekuwa mtiifu na mwaminifu kwa Mungu kiasi cha kuweza kumlalamikia baada ya kukuta kiti cha Enzi kikiwa kimekaliwa na mmoja wa Madreva wa Daladala ambaye yeye alikuwa akimtambua kama Mvuta Bangi, Melevi na Mtu mwenye lugha chafu.

  Ilikuwa hivi; Muda mfupi kabla ya Mtumishi huyo kufariki Dunia, ajali mbaya ya gari (Daladala) ilitokea na kusababisha vifo vya watu 14. Miongoni mwao waliofariki katika ajali hiyo, alikuwemo mke na mtoto wa Mtumishi huyo wa Mungu ambaye alikuwa Mchungaji wa kanisa ambalo sijalijua. Inaarifiwa kuwa alifariki ghafla baada ya kupata taarifa za kifo cha mkewe katika jail hiyo ya Daladala.

  Baada ya kufika huko Mbinguni kwa (Kifo) mchungaji huyo alipangwa kwenda Jehanamu huku Dreva wa Daladala akipelekwa Peponi. Mchungaji hakuweza kuvumilia hali hiyo kwani alilalamika wazi mble za Mungu na kusema aliyoyajua. "Bwana wangu haiwezekani, huyu Dreva kukaa huko, tizama alikuwa akivuta bangi, alikuwa akitukana abiria na hata Lugha yake ilikuwa ni matusi kila uchao…. leo amekufa kwa ajali tena aliyoisabaisha yeye kwa ulevi wake na kukatili roho kibao za watumishi wako, unamuweka peponi?"

  Kauli hiyo ya Mchungaji ilijibiwa hivi na Mungu; "Ni kweli hayo unayoyasema Mtumishi wangu, lakini siku yake ya mwisho kabla ya kifo huyu Dreva alisaidia watu wengi sana kuniabudu kuliko wewe. Tizama wakati akikimbiza daladala lake kwa mwendo wake mkali, watu wote walinikumbuka kwa hofu ya kupata ajali na ndipo wengi walianza kusali na kuniomba toba na rehema, lakini wewe ambaye umekuwa ukihubiri kila siku kanisani watu wamekuwa wakipuuza na kusinzia na hata wanapotoka wamekuwa wakiendelea na wizi, uvutaji bangi, uzinzi na uchafu mwingine.

  Nilikupa uchungaji kusudi umsaidie naye aache kuvuta bangi, umesaidie kuheshimu roho za watu kwa kuendesha gari taratibu, lakini umekuwa ukijisaidia zaidi wewe kwa kuwahimiza waumini kutoa sadaka kubwa, hivyo anastaili hii Pepo ila wewe hustaili."

  Msemo huu unachekesha! Na hasa ukizingatia mwenye kazi ya kuokoa watu (Mchungaji) anapojikuta akizidiwa kete na mhuni wa Ubungo dreva, chizi wa Daladala tu. Zaidi ni kuwa umenikumbusha ‘Chaguo la Mungu' ambalo tuliambiwa na wachungaji haohao na kumchagua mwaka 2005 na leo tunaona kuwa imekuwa ni laana ya Mungu.

  Nimeamua kuanza na kichekesho hicho kutokana na taarifa niliyoisoma katika Gazeti moja la kila wiki (Nyakati toleo namba 554, Julai 10-16,2011) lilokuwa na habari yenye kichwa kinachosomeka hivi, ‘Lowassa asipokuwa Rais 2015 mniue-Askofu'.

  Katika habari hiyo Gazeti hilo lilimkariri Askofu wa Kanisa la Last Glory mwenye jina la Basileus Ezekielto Mabumba akidai kuwa amepokea ujumbe toka kwa Mungu unaodai kuwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa, ndiye atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ajaye baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Askofu huyo alisema kuwa iwapo jambo hilo halitatokea basi atawajibika na kwamba yuko tayari kuuawa.

  Habari hii usiipuuze, kwa vile mie nilitaka kuipuuza lakini pia nikatokewa na Mungu ambaye amenifunulia kuwaambia "Rostam asipotangazwa amekufa kama Balali Gavana wa Benk kuu-Mniue."

  Wengi mtabisha, kwa maana hamuendi kanisani, mmekalia fedha tu, na najua wachungaji wenzangu watanipinga hasa ukizingatia kuwa mie ni Askofu Mgeni wa kanisa la Magazeti. Lakini ukweli nimefunuliwa na Mungu. Mhmm! Sijui Mungu gani mtamtafuta nyie.

  Nimeamua kuwaeleza haya leo kutokana na ukweli kuwa Mungu amekuwa akifuata kila wakati na kunieleza kuwa Waumini wangu ni wataratibu, wapole, na wanaosahau haraka. Alinieleza jinsi ambayo mmesahau haraka kifo cha Daud Balali aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania. Uongo…ndiyo mmesahau!

  Kwa vile alikuwa muhimu sana kwa Taifa na hasa baada ya kuanza kwa mvutano wa kesi za EPA na mambo yenu ya ulaji na kuwajibisha, alifariki na shutuma zikaisha, hata leo wamebaki wangapi wakieleza na kupaza kelele za BALALI tena? Hakuna…unaona, mmesahau maskini!.

  Angalia katika unabii wa ndoto niliyopewa na Mungu, amenikumbusha kuwa dalili za Kufa wa Rostam zitakuwa ni hizi. Kucharuka kwa Bunge na mjadala kuwaelemea zaidi watu waliokuwa wafuasi wa Chama chake, kuamka kwa nguvu kwa mmoja wa mapacha mwenzake kuanza safari ya kugombea Urais (huyu ni mmoja kati ya Mapacha watatu, Rostam, Chenge na Lowassa), kushindikana kwa magamba mengine kuvuliwa na chama chake.

  Nimeonyeshwa kuwa Watu wengi watalia sana siku mkisikia amekufa, na hili nawaambiwa watalia zaidi ya walivyolia siku ya kujiuzulu kwake, watalia sana siku hiyo akitangaza amekufa, hii ni kwa sababu ya nguvu zake za fedha, kwani alikuwa akizitumia vyema kuajiri watu, alikuwa akizitumia vyema kuwaweka watu katika Ubunge, alikuwa akizitumia kusaidia wenye uchu na uongozi, alikuwa akizitumia loooh! Wote watalia kwa sababu ya Utukufu wake wa kusaidia binadamu.

  Mungu amenieleza kuwa kwa vile mmekwisha sahau kuwa Rostam ndiye mwenye majina mengi (Rostom Aziz, Rostam Aziz Sakarri, Rustom Aziz, Rustam Aziz Sakarri, Rustam Aziz Sakaari na Rustam Sakaari) basi mtasahau hata zile kampuni za Afritain, Kagoda na nini sijui. Hapa lazima niwaeleze ukweli, lazima msahau zaidi yote hayo kwa kuwa kifo chake ndicho mtakachokikumbuka zaidi.

  Tena ameniongezea, mtasahau kuwa ndiye aliyewahi kuwa Mkuu wa kampeni za chama, mtasahau kuwa ndiye aliyekuwa akipanga na kuendesha mipango ya kumnyang'anya aliyekuwa spika wa Bunge Sitta Samwel, mtasahau kuwa ndiye aliyewahi kuandaa njama za kumkamata mkewe kwa rushwa katika uchaguzi…..loooo mtasahau mengi kweli.

  Mtasahau tu! Ntasahau kwamba ndiye aliyeandikwa na Magazeti mengi hapa nchini na kuitwa Fisadi, tena mtasahau kuwa ndiye aliyekuwa kinara wa kuzalisha mikampuni na kuandaa randamu za ukandarasi wa kuchota fedha zenu za kodi, mtasahau na kusahau kuwa ndiye ambaye alikuwa mhasibu wa chama cha Mapinduzi (CCM) na magazeti yake yalikuwa yakiendesha kampeni za kumuandika aliyekuwa mgombea wenu kuwa amebeba mke wa Mtu.

  Mtasahau kama ndiye aliyanzisha radio na kuikabidhi ndani ya chama cha Mapinduzi, leo mnautumia kutangaziana kujivua kwake magamba. Mtasahau kuwa ndiye kati yenu aliyewaweka kazini na kuwapangia vyeo vya ukuu wa wilaya na ukuu wa mikoa.
  Zaidi amenieleza kuwa mtasahau mengi, na baada ya hayo yote mwisho mtasahau na Kifo chake, mmhm mbona ya Balaaaaaali! Mtasahau…. Kalaghabao!

  Kwa vile ndiye amekuwa akinitumikia sana Mungu kwa kutoa sadaka ya fedha kwa kiasi kikubwa kwa watumishi wangu wa siasa, basi kifo chake kitawahuzunisha zaidi ili muukumbuke wema wake.

  Lakini ili hayo yatokee kwanza nitamwandalia eneo la kuishi na kupumzika kama pepo, nayo nitaiweka jirani kabisa na nchi ile ya kwanza ya Bustani aya Adam na Hawa (Iran).

  Na haya ninayoongea wala si kichekesho, nitayaandika katika Magazeti yote kusababu ni lazima yapingane ya yale Maneno ya Askofu wa Kanisa la Last Glory mwenye jina la Basileus Ezekielto Mabumba niliyemweleza hapo juu akisema ameonyeshwa na Mungu kuwa Lowassa atakuwa rais wa 2015. Napinga kwa vile mimi ndiye ambaye Mungu amenifunulia zaidi kuliko huyo. Napinga na mimi naweka naziri kama asipotangazwa amekufa basi mchome na moto hii pumzi ninayovuta ili nife.

  Teh teh teheeee! Najua mtasahau, mtasahau hata haya ninayowaambiwa leo!
  Wakatabahu

  Ndimi Askofu (Bandia) Fundi.

  Source: Gazeti la Dira ya Mtanzania
   
 2. M

  Mbuyi Member

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 13
  Mmmmh, napenda ulivyijipanga. Hongera kwa 'unabii' wako.
   
 3. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa maelezo yako, Askofu/ Mchungaji na dereva wa daladala wote wako sehemu moja ( wanapata kibano kwa shetani ) kwasababu pepo ni mashetani, kwa Mungu hakuna pepo. Ndiyo maana Mungu aliamua kumkaushia Mchungaji kwa sababu alikuwa anaomba asichokijua.
   
 4. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #4
  Jul 19, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kweli mkuu tutasahauuuu!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...