Rostam aibukia kanisani!

Rostam aibukia kanisani!

Hawajakutana Maaskofu wowote. Wanaozungumza sasa ni Mtikila na wenzake. Mchungaji amekwepa waandishi anasema yuko LIKIZO.... inawezekana anaweza kachukuliwa hatua.

Ni kweli mchungaji yupo likizo lakini kondooo wa Bwana huendelea kuchungwa hata wachungaji wanapokuwa likizo...
 
Wanamjadili Rostam ili wamrudishie sadaka yake?

Tehe tehe tena lazima alitoa kubwa sana, ila sina uhakika kama RA anajua nini maana ya sadaka kwani bible inasema kama umekosana na mwenzako nenda kasuluhishe ugomvi kwanza ndo utoe sadaka sasa mambo ya kujisafisha... hayo.
 
Uongozi mzima wa Usharika hauwezi kukwepa hiyo kashfa. Hata kama shughuli ilikuwa ni ya Kwaya, kabla ya kufanya mwaliko lazima Baraza la Wazee wa Kanisa, Mchungaji na Uongozi wa Kwaya walishirikishwa katika maandalizi ya hiyo shughuli. Kwaya haiwezi kumwalika mtu bila baraka za Baraza la Wazee wa Kanisa pamoja na Mchungaji wa Usharika husika.

Mchungaji wa Usharika anakwepa kwamba yuko likizo lakini lengo lake ni kujiweka pembeni ya hiyo kashfa kwa kuwa yeye ndiyo mwajiriwa wa kanisa. Wazee wa Kanisa ni watu wa kujitolea waliochaguliwa na waumini. Kitakachofanyika ni kumuweka kando mchungaji ili kama uongozi wa Jimbo la Kinondoni na/au Dayosisi ya Mashariki na Pwani wataamua kufuatilia hiyo kashfa basi Mchungaji wa Usharika apone.

Ngoja tuone hili saga litaishia wapi. Lakini nina uhakika Mamvi ataingilia kati na inawezekana ni mchongo wa mamvi ili RA apate jukwaa la kujisafisha kupitia kanisa.
 
Wanamjadili Rostam ili wamrudishie sadaka yake?

Kwa kadri nijuavyo "rituals" za kanisa, sadaka huwa hairudi na kanisa wanaamini wanaweza kuzigueza hela chafu kuwa safi kwa kufanya kazi takatifu ya bwana kwi..kwi..kwi.. acha nicheke mie, dunia hii ina mambo! Heri waliojiamulia kuwa atheists!
 
Let it better remain in political point of view, because inapokuja kwa swala la dini ama kanisa it becomes very complicated, tutatakiwa tushughulike na vibanzi ndani ya macho yetu kabla ya kutizama boriti ndani ya jicho la mwingine
 
Hongera sana kwa Kanisa kumualika huyo FISADI na tumeweza kuyapata yaliyokuwa MOYONI mwake. Bila mwaliko huo tungejua yote hayo> Huyu Rostam aliongea kama vile watoto wanavyotoa siri kwa Baba mara anaporudi safari. NIMEMSHANGAA SANA LAKINI NIMEFURAHI.
 
MAFISADI ndio WACHANGIAJI wazuri hata kwenye misiba, harusi, kampeni za uchaguzi,...
 
Mtikila anasema, wamelinajisi kanisa

Lakini hebu twendeni nyuma na mbele, tusilikuze sana hili jambo. Kuna waumini kibao wanaotoa sadaka zao makanisani na misikini ambazo wamechota kutoka fungu walilolipata kwa njia ya kifasadi au nyingine. Hapa tusibadilishe mada ya ufisadi, kama Rostam ni fisadi hawezi kuwa Omega na Alfa, atakuwa sehemu ya huo mfumo wa ufisadi na zaidi ya yote atakuwa ni uzao wa huo mfumo wa ufisadi.

Watetezi wa mchungaji aliyemwalika Rostam kanisani wanaweza wakaja na hoja kama hizi:

Kanisa halipaswi kuwakataa wale wanaoamua kuingia nyumbani kwa Bwana. Kwa hiyo ukiangalia kwa jicho lingine ni kwamba kanisa lilipata nafasi nadra ya kufanikiwa kumleta mbele za bwana moja ya waliopotea. Sasa cha kujiuliza Rostam alipata nafasi ya kukiri, kutubu na kumrudia bwana? Hili ndio swali la msingi la kujadiliwa na hao maaskofu. Maaskofu wasiongozwe na siasa kwenye mjadala muhumu kama huu bali roho ya Bwana tu!

Sasa kama hao maaskofu watamsuta mchungaji au kiongozi wa kanisa aliyemwalika Rostam, watajuaje kama aliongozwa na roho ya Bwana katika kumwalika huko? Na je, wanajuaje kama Rostam aliongozwa na Bwana kusema maneno aliyoyasema na kutoa sadaka aliyotoa mbele za madhahabu ya Bwana wa Majeshi? Mtikila anaweza kutusaidi kujibu haya maswali?
 
Hongera sana kwa Kanisa kumualika huyo FISADI na tumeweza kuyapata yaliyokuwa MOYONI mwake. Bila mwaliko huo tungejua yote hayo> Huyu Rostam aliongea kama vile watoto wanavyotoa siri kwa Baba mara anaporudi safari. NIMEMSHANGAA SANA LAKINI NIMEFURAHI.

Nakuunga mono Bubu. watu kama hawa wanatakiwa kuchokonolewa hadiw ajitokeze kusema yaliyo motoni mwao. Hawa watuw a kanisa waliomwalika wamefanya vema sana kwa sababu bila wao tusingejua huyu anawaza nini. kama alkuwa ana nia ya kupima joto ya kiwe, nadhani ameshafahamu hadi sasa kuwa bado lina moto wa kutosha, halijapoa
 
hakuna mwenye ujanja wa kurudisha pesa ya Rostam.nachojua ni kuwa makanisa yanapokea mpaka pesa za mashoga duniani na kuziombea ije kuwa pesa safi kama ya rostam eti kwa kuwa ana allegation ambazo hazijathibitishwa bado.
 
Lakini hebu twendeni nyuma na mbele, tusilikuze sana hili jambo. Kuna waumini kibao wanaotoa sadaka zao makanisani na misikini ambazo wamechota kutoka fungu walilolipata kwa njia ya kifasadi au nyingine. Hapa tusibadilishe mada ya ufisadi, kama Rostam ni fisadi hawezi kuwa Omega na Alfa, atakuwa sehemu ya huo mfumo wa ufisadi na zaidi ya yote atakuwa ni uzao wa huo mfumo wa ufisadi.

Watetezi wa mchungaji aliyemwalika Rostam kanisani wanaweza wakaja na hoja kama hizi:

Kanisa halipaswi kuwakataa wale wanaoamua kuingia nyumbani kwa Bwana. Kwa hiyo ukiangalia kwa jicho lingine ni kwamba kanisa lilipata nafasi nadra ya kufanikiwa kumleta mbele za bwana moja ya waliopotea. Sasa cha kujiuliza Rostam alipata nafasi ya kukiri, kutubu na kumrudia bwana? Hili ndio swali la msingi la kujadiliwa na hao maaskofu. Maaskofu wasiongozwe na siasa kwenye mjadala muhumu kama huu bali roho ya Bwana tu!

Sasa kama hao maaskofu watamsuta mchungaji au kiongozi wa kanisa aliyemwalika Rostam, watajuaje kama aliongozwa na roho ya Bwana katika kumwalika huko? Na je, wanajuaje kama Rostam aliongozwa na Bwana kusema maneno aliyoyasema na kutoa sadaka aliyotoa mbele za madhahabu ya Bwana wa Majeshi? Mtikila anaweza kutusaidi kujibu haya maswali?

Kitila ,

You are missing a point here , Tatizo sio kumualika Rostam bali ni Rostama kutumia platform ya kanisa kwa manufaa yake binafsi ya kisiasa . Mchungaji alichotakiwa kufanya baada ya Rostam kumaliza kutoa kauli zake ni kusema kuwa hayo yalikuwa mawazo ya Rostam kama Rostam na wala siyo kanisa . Alitakiwa kusema pia kanisa alifungani na chama chochote cha siasa !
 
kuna msemo husemao "Baniani mbaya ("fisadi") kiatu chake ("pesa yake") ni dawa"! waTanzania hata tupige kelele kiasi gani, ukweli ni kwamba "mafisadi" tunawalea sisi wenyewe kutokana na njaa zenu (iwe makanisani, misikitini, mashule, maofisini, ...).

Kuna mhindi mmoja alipata kuniambia "waTanzania wana nguvu na umoja kama barafu, ukiwamwagia maji-moto (pesa) wanayeyuka na kusahau umoja wao"!
 
hakuna mwenye ujanja wa kurudisha pesa ya Rostam.nachojua ni kuwa makanisa yanapokea mpaka pesa za mashoga duniani na kuziombea ije kuwa pesa safi kama ya rostam eti kwa kuwa ana allegation ambazo hazijathibitishwa bado.

JE KKKT wao wapo pamoja na mashoga? hope si kweli! angekuwa ameenda ambapo wanakubaliana na ushoga hapo kweli!
 
Kuna tamko litatolewa kwani presha kwa mkuu wa kanisa ni kubwa sana haswa kutoka kwa waumini wake na viongozi wenzake.
 
Tamko la Mtikila ni kwa niaba ya "Kamati ya Wakiristo ya Kutetea Imani lenye kichwa kisemacho, "Kitendo cha Rostam Aziz cha kulinajisi kanisa nchini"

ikisema, "Tunaolichunga kanisa nchini tumelazimika kukutana kwa dharura, kulaani kunajisiwa kwa kanisa la nchi hii, kwa makufuru ya Jumapili tarehe 6 Julai, 2008 ya kukaribishwa mtuhumiwa mkuu wa kubuni mbinu na mikakati na utekelezaji katika uporaji wa matrilioni ya fedha katika hazina na benki kuu kama mgeni rasmi katika Kanisa la Mungu"
 
Ufisadi upo hata nadani yamakanisa kadhaa. Viongozi wa makanisa wanaweka pesa mbele, hasa kkkt, ndio maana utaona watu kama akina Mengi wanaalikwa kuwa wageni rasmi kwa shughuli za kikanisa japokuwa yeye (Mengi) ndoa yake imeshindikana. Hana imani ila ana pesa yake!

Ninakubaliana na hili kwa kiasi kikubwa. Ukijaribu kuangalia matukioa mengi tu ambayo yanahusishwa na watu wa KKKT utaona jinsi gani pesa ilivyokuwa na umuhimu kwao kuliko neno la Mungu. Pesa na madaraka ndio kilikuwa chanzo cha ugomvi kule usharika wa kaskazini (Arusha/Kilimanjaro???!), na kwa wale wanaoijua vizuri Hospitali ya rufaa ya KCMC (mjini Moshi) ambayo iko chini ya KKKT watakwambia ni uozo kiasi gani uko pale ukichangiwa na na Askofu wa Kilimanjaro ambaye ni ndugu moja na Mkurugenzi wa KCMC! Sasa hii ya RA ni hitimisho la ulafi uliokithiri ndani ya KKKT, pesa kidogo tu kapewa jukwaa/altare afanye anachotaka. Mbona hawamwalika kabla ya kashfa?! So sad. Kweli ULAFI KAIZ..!
 
sadaka ni sadaka tu cha muhimu kuiombea ili kuvunja hiyo nguvu iliyoko nyuma ya hiyo sadaka inayotolewa

Sound like one of those at KKKT Magomeni who were applauding while RA were throwing some few quids on your face! Get up and get life bro, not every penny worth it!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom