Rostam aibukia kanisani!

Unajua watu sasa hivi wanapiga kampeni kupitia makanisani na misikitini maana ndiyo kuna makusanyiko makubwa ya watu! Vile vile wakiona mtu huyo anakubalika na viongozi wa dini baaasi hapo waumini wanamuona ni muadilifu moja kwa moja na kumpatia kura mwakani! ANGALIZO.... Tuwe macho na tukae chonjo na watu hawa!
 
Ni lile anaposali Spika Samwel Sitta... (KKKT Kinondoni).

Aichangia kwaya Tshs Milioni 7...

Amalizia na kuwaomba waumini kuiombea nchi kwani iko kwenye kipindi kibaya cha watu kutafutana uchawi na kuonesha hali si shwari nchini.

Zaidi tusubiri kutoka vyombo vya nyumbani kwani walikuwepo wengi. Wasipoandika tutaandika!

Watu tz hii wanafiki,Baniani awezi kuwa mbaya kiatu chake kikawa kizuri,wamepokea.Kama uzalendo wa kweli wasingepokea,na tena sio dhehebu lake
 
Huyu fisadi naona ana wasiwasi mkubwa. Kanisa linastahili kuzikataa fedha zake zilizotokana na ufisadi. Huyu jamaa kwanza ni mkristo au ndiyo mfa maji...?
We hujui utamu wa pesa. Pesa ya fisadi inapotoka, mpokeaji humwona mtoaji si fisadi na kanisa ndio kabisa?

Na kwa mafisadi kuliambua hilo ndio huzidi kupitishia mambo au mapesa yao kanisani na hata kuombewa dua.
 
kanisani nao wakapokea za ufisadi, Yesu na Maria na Yosef!
we unahisi makanisa yamewekwa ili yafanye nini kama sio kukusanya fedha pasipo kujali ya kahaba,haramia,tapeli,jambazi na pesa zote chafu na safi unazozijua,Suleiman Musindi alishasema hata achinjwe mtu na pesa ipakwe damu watu wataifuta na kuitumia!!Usiogope ndio hali halisi!!
 
Ni lile anaposali Spika Samwel Sitta... (KKKT Kinondoni).

Aichangia kwaya Tshs Milioni 7...

Amalizia na kuwaomba waumini kuiombea nchi kwani iko kwenye kipindi kibaya cha watu kutafutana uchawi na kuonesha hali si shwari nchini.

Zaidi tusubiri kutoka vyombo vya nyumbani kwani walikuwepo wengi. Wasipoandika tutaandika!
Nina hakika kabisa 100/100 sadaka zake hazikuchanganywa na za waumini wengine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom