Tamko la Mtikila ni kwa niaba ya "Kamati ya Wakiristo ya Kutetea Imani lenye kichwa kisemacho, "Kitendo cha Rostam Aziz cha kulinajisi kanisa nchini"
ikisema, "Tunaolichunga kanisa nchini tumelazimika kukutana kwa dharura, kulaani kunajisiwa kwa kanisa la nchi hii, kwa makufuru ya Jumapili tarehe 6 Julai, 2008 ya kukaribishwa mtuhumiwa mkuu wa kubuni mbinu na mikakati na utekelezaji katika uporaji wa matrilioni ya fedha katika hazina na benki kuu kama mgeni rasmi katika Kanisa la Mungu"
connecting to the dot....Kwani Askofu Laizer ni wa Kanisa gani??Huyu si ndiye aliongoza mapokezi ya Lowassa?
Kwani Mtikila hajawahi kula noti ya Rostam?!?
Uongozi mzima wa Usharika hauwezi kukwepa hiyo kashfa. Hata kama shughuli ilikuwa ni ya Kwaya, kabla ya kufanya mwaliko lazima Baraza la Wazee wa Kanisa, Mchungaji na Uongozi wa Kwaya walishirikishwa katika maandalizi ya hiyo shughuli. Kwaya haiwezi kumwalika mtu bila baraka za Baraza la Wazee wa Kanisa pamoja na Mchungaji wa Usharika husika.
Mchungaji wa Usharika anakwepa kwamba yuko likizo lakini lengo lake ni kujiweka pembeni ya hiyo kashfa kwa kuwa yeye ndiyo mwajiriwa wa kanisa. Wazee wa Kanisa ni watu wa kujitolea waliochaguliwa na waumini. Kitakachofanyika ni kumuweka kando mchungaji ili kama uongozi wa Jimbo la Kinondoni na/au Dayosisi ya Mashariki na Pwani wataamua kufuatilia hiyo kashfa basi Mchungaji wa Usharika apone.
Ngoja tuone hili saga litaishia wapi. Lakini nina uhakika Mamvi ataingilia kati na inawezekana ni mchongo wa mamvi ili RA apate jukwaa la kujisafisha kupitia kanisa.
Niongezee hapo,Mchungaji ndio mwenyekiti wa baraza la wazee ktk usharika.
Lakini sioni sababu ya kulihukumu kanisa kwa jambo hili,viongozi wote walituhumiwa na ufisadi wamekuwa wakizungumza na kujisafisha kila sehemu kwa kusaidiwa na serikali.
Je sisi kama wanajamii tumejitahidi kwa kiasi gani kupigavita huu ufisadi,kama sio kujahapa na kulalamika kisha tunazima kompyuta zetu na kwenda kulala.
Kama kweli tunataka kuupigavita ufisadi kwa vitendo basi tuwapeleke hawa watuhumiwa mahakamani ili sheria ikachukue mkondo wake.
Kwa mimi ninavyojua kuhusu hivi vikundi vya makanisa wao watamwalika mtu ili wao wapate kile wanachokitaka na sio maneno matamu kama asali.
kwaya ilihitaji pesa kwa ajili ya kujiendesha ktk kumtumikia mungu,hivyo wamepata wao na azizi mkataba wao uliishia hapo.
Mtikila anasema, wamelinajisi kanisa
I love Mtikila...akiona chungwa anasema chungwa.
Huyu mtu anatufaa sana sehemu fulani fulani lakini sio Ikulu.
Kitila ,
You are missing a point here , Tatizo sio kumualika Rostam bali ni Rostama kutumia platform ya kanisa kwa manufaa yake binafsi ya kisiasa . Mchungaji alichotakiwa kufanya baada ya Rostam kumaliza kutoa kauli zake ni kusema kuwa hayo yalikuwa mawazo ya Rostam kama Rostam na wala siyo kanisa . Alitakiwa kusema pia kanisa alifungani na chama chochote cha siasa !
''mamvi'' i like that.Huyo jamaa naye nuksi.kwenye hilo anahusika.Uongozi mzima wa Usharika hauwezi kukwepa hiyo kashfa. Hata kama shughuli ilikuwa ni ya Kwaya, kabla ya kufanya mwaliko lazima Baraza la Wazee wa Kanisa, Mchungaji na Uongozi wa Kwaya walishirikishwa katika maandalizi ya hiyo shughuli. Kwaya haiwezi kumwalika mtu bila baraka za Baraza la Wazee wa Kanisa pamoja na Mchungaji wa Usharika husika.
Mchungaji wa Usharika anakwepa kwamba yuko likizo lakini lengo lake ni kujiweka pembeni ya hiyo kashfa kwa kuwa yeye ndiyo mwajiriwa wa kanisa. Wazee wa Kanisa ni watu wa kujitolea waliochaguliwa na waumini. Kitakachofanyika ni kumuweka kando mchungaji ili kama uongozi wa Jimbo la Kinondoni na/au Dayosisi ya Mashariki na Pwani wataamua kufuatilia hiyo kashfa basi Mchungaji wa Usharika apone.
Ngoja tuone hili saga litaishia wapi. Lakini nina uhakika Mamvi ataingilia kati na inawezekana ni mchongo wa mamvi ili RA apate jukwaa la kujisafisha kupitia kanisa.
Mwanakijiji iko wapi ule walaka wako kwa viongozi wa dini?Tuliposema wamelala kitanda kimoja na wezi na kujifunika blanketi na mafisadi, si Kanisa walidhani tunawalaumu bure? Sasa leo wamekutana wakifanya unajisi wao hadharani, wataweza kujiweka tena wakfu?
Kwa taarifa yenu kati ya washirika prominent wa kkkt Kinondoni ni wazee wa kanisa Spika Samweli Sitta na mh.Mwambalaswa(MB),tafakari!
Ninachojua ni kuwa ni lazima kanisa litasema na kuweka mambo sawa laa sivyo linaweza kukumbwa na msukosuko wa kuanza kupambana na waumini wao ambao wanaupinga ufisadi ambao ndio wengi zaidi ya hao wenye vijisenti.
Wasiposimama wajue kuwa huu unaweza ukawa ndio mwanzo wa KKKT kupasuka na kuanzishwa kwa KKKT mbili .
Ukiangalia kwa makini lengo la RA halikuwa tu kutoa huo mchango wa pesa aliona ni mahali sahihi kwake kucheza ule Mchezo wa Karata uitwao "MAPIKU"
"Nadhani nianze kwa kuwapongeza pamoja na maneno mengi ya hivi karibuni ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi
yangu hamkuyajali na kwa maana nyingine mmeyaona kuwa ya kizushi, kijiweni na yenye wivu," alisema Bw. Aziz.
Aliwashukuru waumini hao na kusema wao si wazushi na hawana wivu dhidi ya mtu yeyote bali ni watu wanaopenda haki kama Mwenyezi Mungu anavyotaka.
Naye Mchungaji wa kanisa hilo, Bw. Joseph Masage alimtaka, Bw. Aziz kutokata tamaa na mambo mbalimbali yanayomwandama kwani alisema Mungu ndiye anayejua huduma anayoifanya hapa duniani.
"Kweli yanaweza kuwepo maneno mengi lakini yote hayo ni mapito endelea kufanya huduma ambazo unaona ni nzuri
katika jamii na Mungu atazidi kukubariki," alisema Mchungaji Masage.(majira)
Lakini hebu twendeni nyuma na mbele, tusilikuze sana hili jambo. Kuna waumini kibao wanaotoa sadaka zao makanisani na misikini ambazo wamechota kutoka fungu walilolipata kwa njia ya kifasadi au nyingine. Hapa tusibadilishe mada ya ufisadi, kama Rostam ni fisadi hawezi kuwa Omega na Alfa, atakuwa sehemu ya huo mfumo wa ufisadi na zaidi ya yote atakuwa ni uzao wa huo mfumo wa ufisadi.
Watetezi wa mchungaji aliyemwalika Rostam kanisani wanaweza wakaja na hoja kama hizi:
Kanisa halipaswi kuwakataa wale wanaoamua kuingia nyumbani kwa Bwana. Kwa hiyo ukiangalia kwa jicho lingine ni kwamba kanisa lilipata nafasi nadra ya kufanikiwa kumleta mbele za bwana moja ya waliopotea. Sasa cha kujiuliza Rostam alipata nafasi ya kukiri, kutubu na kumrudia bwana? Hili ndio swali la msingi la kujadiliwa na hao maaskofu. Maaskofu wasiongozwe na siasa kwenye mjadala muhumu kama huu bali roho ya Bwana tu!
Sasa kama hao maaskofu watamsuta mchungaji au kiongozi wa kanisa aliyemwalika Rostam, watajuaje kama aliongozwa na roho ya Bwana katika kumwalika huko? Na je, wanajuaje kama Rostam aliongozwa na Bwana kusema maneno aliyoyasema na kutoa sadaka aliyotoa mbele za madhahabu ya Bwana wa Majeshi? Mtikila anaweza kutusaidi kujibu haya maswali?