www.alhidaaya.com



34-Du’aa Unaporudi Safarini: Laa Ilaaha Illa Allaahu Wahdahu …. Aaibuwna, Taaibuwna, ‘Aabiduwna, Saajiduwna Li-Rabbinaa Haamiduwna…







عنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رضى الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا قَفَلَ مِنْ غَزْوٍ أَوْ حَجٍّ أَوْ عُمْرَةٍ يُكَبِّرُ عَلَى كُلِّ شَرَفٍ مِنَ الأَرْضِ ثَلاَثَ تَكْبِيرَاتٍ، ثُمَّ يَقُولُ: ((لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ، وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ، آيِبُونَ تَائِبُونَ عَابِدُونَ سَاجِدُونَ لِرَبِّنَا حَامِدُونَ، صَدَقَ اللَّهُ وَعْدَهُ وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ)) البخاري





Imepokelewa kutoka kwa Ibn ’Umar (رضي الله عنهما) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alikuwa pindi anaporudi vitani au kutoka Hajj au ’Umrah alikuwa katika kila akipanda mlima akileta Takbiyrah (Allaahu Akbar) mara tatu kisha akisema:



Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamd, wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Aaibuwna taaibuwna, ’aabiduwna, saajiduwna, li-Rabbinaa haamiduwna. Swadaqa-Allaahu Wa’dahu, wa Naswara ’Abdahu, wa Hazamal-ahzaaba Wahdahu




Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala hana mshirika. Ufalme ni Wake, na Himdi ni Zake, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. Tunanarudi hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, tunasujudu, tunamhimidi Rabb wetu. Amesadikisha Allaah ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi peke Yake [Al-Bukhaariy katika Kitaab Al-Hajj, Kitaab Al-’Umrah, Kitaab Al-Maghaazi, Kitaab Al-Jihaad Was-Sayr (7/163) [1797], Muslim Kitaab Al-Hajj (2/980) [1344].
 
www.alhidaaya.com



35-Maneno Manne Ayapendayo Allaah: Subhaana Allaah,

Wal-HamduliLLaah Wa Laa Ilaaha Ilaa-Allaah…..





عَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدَبٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((أَحًبُّ الْكَلامِ إِلَى اللَّهِ أَرْبَعٌ: سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلا إِلَهَ إِلا اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، لا يَضُرُّكَ بِأَيِّهِنَّ بَدَأْتَ))

Imepokelewa kutoka kwa Samurah Bin Jundab kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Bora ya maneno kwa Allaah ni manne:



سُبْحَانَ اللهِ، والْحَمْدُ للهِ، وَلاَ إِلَهَ إَلاَّ اللهُ واللهُ أَكْبَرُ



Subhaana-Allaah, walhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar

Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa.



… si vibaya kuanza kwa lolote katika haya)) [Muslim (3/1685)]
 
www.alhidaaya.com



36-Kutamka Laa Ilaaha Illa-Allaah Wakati Wa Mafazaiko





عَنْ زَيْنَبَ بِنْتِ جَحْشٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم دَخَلَ عَلَيْهَا فَزِعًا يَقُولُ: ((لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَيْلٌ لِلْعَرَبِ مِنْ شَرٍّ قَدِ اقْتَرَبَ، فُتِحَ الْيَوْمَ مِنْ رَدْمِ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مِثْلُ هَذَا))‏ وَحَلَّقَ بِإِصْبَعِهِ وَبِالَّتِي تَلِيهَا، فَقَالَتْ زَيْنَبُ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ أَنَهْلِكُ وَفِينَا الصَّالِحُونَ؟ قَالَ: ((نَعَمْ، إِذَا كَثُرَ الْخَبَثُ))



Imepokelewa kutoka kwa Zaynba Bint Jahsh (رضي الله عنها) kwamba Nabiy alingia chumbani kwake akiwa katika hali ya kufazaika akasema:

‏ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ



((Laa ilaaha illa Allaah [hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah]



Ole kwa Waarabu kutokana na shari iliyokaribia. Leo limefunguka shimo katika boma la kizuzi cha Ya-ajuwj na Ma-ajuwj kama hivi!)) Akafanya kiduara kwa kufunga kidole chake cha gumba na cha shahada. Zaynab akasema: Kisha nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, hivi tutaangamia na hali tumo watu wema?”. Akasema: ((Ndio pindi maovu yakizidi)) [Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/181) [3346], Muslim (4/2208) [2880] na Riwaayah nyengine: “Aliamka usingizini akasema….
 
www.alhidaaya.com





37-Mema Yanayobakia Daima









عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((خُذُوا جُنَّتَكُمْ)) قُلْنَا يَا رَسُولَ اللهِ : مِنْ عَدُوٍّ قَدْ حَضَرَ ؟ ، قَالَ: ((لاَ، جُنَّتَكُمْ مِنَ النَّارِ، قُولُوا : سُبْحَانَ اللهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، فَإِنَّهَا يَأْتِينَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مُنْجِيَاتٍ، وَمُقَدَّمَاتٍ ، وَهُنَّ الْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ))



Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Jikingeni!)) Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah; Je adui ameshatufikia? Akasema: ((Hapana bali kinga yenu kutokana na moto. Semeni:





سُبْحَانَ اللهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ



Subhaana-Allaah, wal-HamduliLLaah, wa laa ilaaha illa-Allaah, wa Allaahu Akbar



Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa



Kwani yatakuja zitakuja hizo (Adhkaar) Siku ya Qiyaamah kama ni kinga na kitangulizi, nazo ni Mema yanayobakia daima)) [An-Nasaaiy fiy Sunan Al-Kubraa (10684), Atw-Twabaraniy fiy Al-Mu’jim Al-Awsatw (4027), na ameisahihisha Al-Abaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (3214), Swahiyh At-Targhiyb (1567), na kwa Riwaayah nyenginezo amesahihisha katika Swahiyh Al-Jaami’ (3264), (6/482)]
 
www.alhidaaya.com



38-Atakayesema AstaghfiruAllaahAlladhiy Laa Ilaaha Illa Huwa …. Atamghfuria Hata Kama Ana Makosa Ya Kukimbia Vitani







عن بِلاَلَ بْنَ يَسَارِ بْنِ زَيْدٍ، مَوْلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ سَمِعْتُ أَبِي يُحَدِّثُنِيهِ عَنْ جَدِّي أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: (( مَنْ قَالَ أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ الَّذِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَىُّ الْقَيُّومُ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ غُفِرَ لَهُ وَإِنْ كَانَ فَرَّ مِنَ الزَّحْفِ ))



Imepokelewa kutoka kwa Bilaal bin Yasaar bin Zayd mkombolewa wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba nimesikia baba yangu amenihadithia kutoka kwa babu yangu kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Atakayesema:

أَسْتَغْفِرُ اللهَ الْعَظِيمَ الَّذِي لَا إِلَهَ إلَّا هُوَ الحَيُّ القَيّوُمُ وأَتُوبُ إِلَيهِ

Astaghfiru-Allaahal-‘Adhwiyma Alladhiy laa ilaaha illaa Huwal-Hayyul-Qayyuwmu wa atuwbu Ilayhi



Namuomba maghfira kwa Allaah Mtukufu Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamizi wa kila kitu, na ninarejea kutubuia Kwake...



Allaah Atamghufuria kama ana makosa hata kama ya kukimbia vitani)) [Abu Daawuwd (2/85) [1517], At-Tirmidhiy (5/569) [3577], Al-Haakim na ameisahihisha na ameikubali Adh-Dhahaby (1/511) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله). Angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (3/182)]
 
www.alhidaaya.com



39-Du’aa Ya Swafaa Na Marwah Na Unaporudi Safarini





Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alisoma hivi mara tatu alipopanda jabali la Swafaa na baina yake akiomba du’aa, kisha akafanya alipokuwa Marwah kama alivyofanya alipokuwa Swafaa:



لا إِلهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ، لا إِلَهَ إلا اللهُ وَحْدَهُ أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ

Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahu mulku walahul Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu, Anjaza wa’dahu, Wa naswara ’abdahu, wa hazamal ahzaaba Wahdah

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala hana mshirika. Ni wake ufalme na Himdi Anastahiki Yeye, Naye juu ya kila kitu ni Muweza. Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake, Ametekeleza ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi Peke Yake. [Muslim (2/888) [1218]



Pia:



عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رضى الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا قَفَلَ مِنْ غَزْوٍ أَوْ حَجٍّ أَوْ عُمْرَةٍ يُكَبِّرُ عَلَى كُلِّ شَرَفٍ مِنَ الأَرْضِ ثَلاَثَ تَكْبِيرَاتٍ، ثُمَّ يَقُولُ: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ، وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ، آيِبُونَ تَائِبُونَ عَابِدُونَ سَاجِدُونَ لِرَبِّنَا حَامِدُونَ، صَدَقَ اللَّهُ وَعْدَهُ وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ ‏

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaporudi vitani au Hajj au ‘Umrah kila alipopanda mnyanyuko wa ardhi alileta Takbiyrah (Allaahu Akbar) mara tatu kisha akisema:



لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ، وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ، آيِبُونَ تَائِبُونَ عَابِدُونَ سَاجِدُونَ لِرَبِّنَا حَامِدُونَ، صَدَقَ اللَّهُ وَعْدَهُ وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ ‏

Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahu mulku walahul Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Aayibuwna, taaibuwna, ‘aabiduwnaa, saajiduwna, li-Rabbinaa haamiduwna. Swadaqa Allaahu Wa’dahu, wa-Naswara ’Abdahu wa-Hazama Al-Ahzaaba Wahdahu

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala hana mshirika. Ni wake ufalme na Himdi Anastahiki Yeye, Naye juu ya kila kitu ni Muweza. Tunarudi hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, tunasujudu na Rabb wetu tunamsifu. Amesadikisha ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi Peke Yake. [Al-Bukhaariy na wengineo]
 
www.alhidaaya.com



40-Du’aa Ya Kuogopa Ukandamizaji Na Dhulma Ya Mtawala: Allaahumma Rabbas-Samaawatis-Sab-’i wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwim...





عن عبدِ اللَّهِ بنِ مسعودٍ إذا كانَ على أحدِكم إمامٌ يخافُ تَغطرُسَهُ أو ظلمَهُ فليقلِ




Athar ya ‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: “Ikiwa kuna aliye na madaraka nawe ambaye unaogopa ukandamizaji wake na dhulma yake, basi aseme:



أللَّهُمَّ رَبَّ السَّمواتِ السَّبْعِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيم، كُنْ لِي جاَراً مِنْ (فُلانِ بْنِ فُلاَنٍ) وَأَحْزَابِهِ مِنْ خَلاَئِقِكَ أَنْ يَفْرُطَ عَلَيَّ أحَدٌ مِنْهُمْ أَوْ يَطْغَى، عَزَّ جاَرُكَ وَجَلَّ ثَناَؤُكَ، وَ لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ



Allaahumma Rabbas-samaawatis-sab-’i wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwim, kun liy jaaran min (fulani bin fulani) wa ahzaabihi min Khalaaiqika an yafrutwa ‘alayya ahadun minhum aw yatw-ghaa. ‘Azza Jaaruka, wa Jalla Thanaauka, walaa ilaaha illaa Anta



Ee Allaah, Rabb wa mbingu saba, na Rabb wa ‘Arshi Tukufu, kuwa Mlinzi wangu kutokana na (fulani bin fulani [taja mtu unayemkhofu]) na vikosi vyake miongoni mwa viumbe Vyako, kwa kunisaliti mmoja miongoni mwao, au kunifanyia uadui. Imeimarika madhubuti hifadhi Yako, na zimetukuka sifa Zako na hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe.

[Al-Bukhaariy Al-Adab Al-Mufrad [707] na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad [545, 546].
 
www.alhidaaya.com





41-Du’aa Ya Kumwogopa Mtawala Na Kukhofu Kushambuliwa: Allaahu Akbar, Allaahu A’azzu min Khalqihi jamiy’aa



عنِ ابنِ عبَّاسٍ قالَ إذا أتيتَ سلطانًا مَهيبًا تخافُ أن يسطوَ بِكَ فقلِ



Athar ya Ibn ’Abbaas (Radhwiya Allaahu ’anhumaa) ambaye amesema: Utakapokwenda kwa mtawala anayetisha ambaye utakhofia kuwa atakushambulia, basi sema:



الله أكْبَر، الله أعَزُّ مِنْ خَلْقِهِ جَمِيْعاً، الله أعَزُّ مِمَّا أخَافُ وَأحْذَر، أعُوذُ بِاللهِ الَّذِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ، الْمُمْسِكِ السَّمَوَا تِ السَّبْعِ أَنْ يَقَعْنَ عَلَى الأَرْضِ ِإلاَّ بِإِذْنِهِ، مِنْ شَرِّ عَبْدِكَ (فلان) وَجُنُوْدِهِ وَأَتْبَاعِهِ وَأَشْيَاعِهِ، مِنَ اْلجِنِّ والإِنْسِ، اَلَّلهُمَّ كُنْ لِيْ جَاراً مِنْ شَرِّهِمْ، جَلَّ ثَنَاؤُكَ وَعَزَّ جَارُكَ، وَتَبَارَكَ اسْمُكَ، وَلاَ إلَهَ غَيْرُكَ



Allaahu Akbar, Allaahu A’azzu min Khalqihi jamiy’aa. Allaahu A’azzu mimmaa akhaafu wa ahdharu. A’uwdhu biLLaahi Alladhiy laa ilaaha illaa Huwa. Al-Mumsikis-samawaatis-sab-’i an yaqa’-na ‘alal-ardhwi illaa biidhnihi, min sharri ‘abdika (fulani - mtaje mtu unayemhofu) wa junuwdihi, wa atbaa’ihi, wa ash-yaa’ihii minal jinni wal insi. Allaahumma kunliy jaaran min sharrihim, Jalla Thanaauka, wa ‘Azza Jaaruka, wa Tabaarakas-Smuka walaa ilaaha Ghayruka [mara 3]



Allaah ni Mkubwa, Allaah, ni Mwenye nguvu (Mshindi) kuliko viumbe Vyake vyote. Allaah ni Mwenye nguvu (Mshindi) kuliko kila nikiogopacho na kujihadhari. Najikinga kwa Allaah Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye tu Ambaye Ameshikilia mbingu saba ili zisiangukie ardhi ila kwa idhini Yake, kutokana na shari ya mja (fulani - mtaje mtu unayemhofu) na majeshi yake, na wanaomfuata, na wafuasi wake miongoni mwa majini na watu. Ee Allaah, kuwa Mlinzi wangu kutokana na shari yao. Zimetukuka sifa Zako na Umeheshimika ulinzi Wako na Limebarikika Jina Lako, na hapana mwabudiwa wa haki ghairi Yako.

[Al-Bukhaariy - Adabul-Mufrad [708] na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad [546], Swahiyh At-Targhiyb (2238)].
 
Skip to



www.alhidaaya.com



42-Amsaynaa Wa-amsal-Mulku LiLLaah WalhamduliLLaah Laa Ilaaha Illa-Allaah…

Miongoni Mwa Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni.



عَنْ عَبْدِ اللهِ بِنْ مَسْعُود رضي الله عنه، قَالَ: كَانَ نَبِيُّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا أَمْسَى قَالَ: ((أَمْسَيْنَا وَأَمْسَى الْمُلْكُ لِلَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ))‏ قَالَ: أُرَاهُ قَالَ فِيهِنَّ: (( لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ رَبِّ أَسْأَلُكَ خَيْرَ مَا فِي هَذِهِ اللَّيْلَةِ وَخَيْرَ مَا بَعْدَهَا وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا فِي هَذِهِ اللَّيْلَةِ وَشَرِّ مَا بَعْدَهَا رَبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْكَسَلِ وَسُوءِ الْكِبَرِ رَبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابٍ فِي النَّارِ وَعَذَابٍ فِي الْقَبْرِ))‏ وَإِذَا أَصْبَحَ قَالَ ذَلِكَ أَيْضًا: ((أَصْبَحْنَا وَأَصْبَحَ الْمُلْكُ لِلَّهِ ‏))



Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa pindi anapofika jioni akisema:



أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المـلكُ لله وَالحَمدُ لله، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ،

Amsaynaa wa amsal-Mulku liLLaah wal-HamduliLLaahi. Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu



Tumeingia wakati wa jioni na umekuwa Ufalme ni wa Allaah, na Himdi ni Zake Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali yakuwa Peke Yake, Hana mshirika (Msimuliaji akasema): Nadhani alisema pia:



لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هـذهِ اللَّـيْلَةِ وَخَـيرَ ما بَعْـدَهـا، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ ما في هـذهِ اللَّـيْلةِ وَشَرِّ ما بَعْـدَهـا، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ وَعَـذابٍ في القَـبْر



Lahul-Mulku walahul-Hamdu, wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr. Rabbi as-aluka khayra maa fiy haadhihil-laylati wakhayra maa ba’dahaa, wa a’uwdhu bika minsharri maa fiy haadhihil-laylati washarri maa ba’dahaa, Rabbi a’uwdhu bika minalkasli wasuw-il kibari, Rabbi a’uwdhu bika min ‘adhaabin finnaari wa ‘adhaabin filqabri



Ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi, na Yeye juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza). Rabb wangu, nakuomba khayr zilizomo katika usiku wa leo, na khayr za baada yake, na ninajikinga Kwako kutokana na shari zilizomo katika usiku wa leo na shari za baada yake. Rabb wangu, najikinga Kwako kutokana na uvivu, na ubaya wa uzee ubaya. Rabb wangu, najikinga Kwako kutokana na adhabu ya Moto na adhabu ya kaburi



Na alipoamka asubuhi pia alisema (kama hivyo kwa kutaja kuamka asubuhi):



أَصْـبَحْنا وَأَصْـبَحَ المـلكُ لله

Aswbahnaa wa aswbahal-Mulku liLLaah

Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Allaah…

[Muslim (4/2088) [2723]
 
www.alhidaaya.com



43-Jambo La Kwanza Kuwalingania Makafiri Kuingia Katika Uislamu

Liwe Ni Laa Ilaaha Illa-Allaah





عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا) أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) لَمَّا بَعَثَ مُعَاذًا إِلَى الْيَمَنِ: قَالَ لَهُ: ((إِنَّكَ تَأْتِي قَوْمًا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ، فَلْيَكُنْ أَوَّلَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ شَهَادَةَ أَن لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ)) وَفِي رِوَايَةٍ: ((إِلَى أَنْ يُوَحِّدُوا اَللَّهَ. فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوكَ لِذَلِك فَأَعْلِمْهُمْ أَنَّ اَللَّهَ اِفْتَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَوَاتٍ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ. فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوكَ لِذَلِكَ فَأَعْلِمْهُمْ أَنَّ اَللَّهَ اِفْتَرَضَ عَلَيْهِمْ صَدَقَةً تُؤْخَذُ مِنْ أَغْنِيَائِهِمْ فَتَرُدُّ عَلَى فُقَرَائِهِمْ. فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوكَ لِذَلِكَ فَإِيَّاكَ وَكَرَائِمَ أَمْوَالِهِمْ, وَاتَّقِ دَعْوَةَ الْمَظْلُومِ فَإِنَّهُ لَيْسَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ اَللَّهِ حِجَابٌ)) أَخْرَجَاهُ

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomtuma Mu’aadh Yemen alimwambia: ((Hakika wewe utakutana na watu miongoni mwa Ahlul-Kitaab, basi jambo la kwanza la kuwalingania liwe ni kushuhudia kwamba: Laa ilaaha illa-Allaah - hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah)). Na katika riwaayah nyingine: (([Walinganie] Kumpwekesha Allaah. Watakapokutii hilo, wajulishe kwamba Allaah Amewafaradhishia Swalaah tano usiku na mchana. Watakapokutii hilo, basi wajulishe kwamba Allaah Amewafaradhishia Zakaah ichukuliwe kutoka kwa matajiri wao na kupewa masikini wao. Watakapotii hilo, basi tahadhari kuchukua bora za mali zao [kama malipo ya Zakaah], na tahadhari na du’aa ya aliyedhulumiwa, kwani hakuna kizuizi baina yake na Allaah)) [Al-Bukhaariy (1395) Muslim (19)]
 
www.alhidaaya.com





44-Wasiya Wa Nabiy Nuwh:

Laa Ilaaha Illa-Allaah Ni Nzito Katika Mizani Kuliko Mbingu Saba Na Ardhi Saba





عن عبد الله بن عمرو: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ نبيَّ اللهِ نوحًا لما حضَرَتْه الوفاةُ قال لابنِه: إني قاصٌّ عليك الوصيَّةَ، آمرُك باثنتَينِ و أنهاك عن اثنتَينِ، آمرُك ب ( لاإله إلا اللهُ )، فإنَّ السمواتِ السبعَ والأرَضينَ السبعَ لو وُضِعَتْ في كِفَّةٍ، ووُضِعَتْ لا إلهَ إلا اللهُ في كِفَّةٍ، رجَحَتْ بهنَّ لا إلهَ إلا اللهُ، ولو أنَّ السمواتِ السبعَ والأرَضَينَ السبعَ كُنَّ حَلْقةً مُبهَمةً قصَمَتْهنَّ لا إلهَ إلا اللهُ، وسبحانَ اللهِ وبحمدِه فإنها صلاةُ كلِّ شيءٍ، وبها يُرزَقُ الخلقُ، و أنهاك عن الشركِ و الكِبر))ِ قال: قلتُ: أوْ قيل: يا رسولَ اللهِ هذا الشركُ قد عرفْناه فما الكِبْرُ؟ قال: أن يكون لأَحدِنا نعْلانِ حسَنتانِ لهما شِراكانِ حسنانِ؟ قال: ((لا)) قال: هو أن يكون لأحدِنا أصحابٌ يجلسون إليه؟ قال: ((لا)) قيل: يا رسولَ اللهِ فما الكِبْرُ؟ قال: ((سَفَهُ الحقِّ و غَمْصُ الناسِ)) السلسلة الصحيحة 134



Mauti yalipomfikia Nabiy wa Allaah (ambaye ni) Nuwh (‘Alayhis-Salaam) alimwambia mwanawe: Nakuhadithia wasiya wangu; Nakuamrisha mambo mawili na kukukataza mawili. Nakuamrisha Laa ilaaha illa Allaah (Hapana mwabudiwa wa haki illa Allaah) kwani ingelikuwa mbingu saba na ardhi saba zimewekwa katika mizani na Laa ilaaha illa Allaah imewekwa katika mizani ya pili basi Laa ilaaha illa Allaah ingelikuwa nzito.



Na kama ingelikuwa mbingu saba na ardhi saba zimefungwa katika mduara, basi Laa illa Allaah ingelivunja mduara huo.



La pili nakuamrisha Subhaana-Allaahi wa Bihamdihi (Ametakasika Allaah kwa Himdi Zake) kwani ni du'aa ya kila kitu na kwayo viumbe wanaruzukiwa.



Na nakukataza shirki na kiburi. (Msimuliaji akasema: Nikauliza au mtu akauliza) “Ee Rasuli wa Allaah! Shirki tunaifahamu, lakini je, nini kiburi? Je, ni vile mmoja wetu kuwa na viatu vyenye utepe mzuri?”



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hapana!))



Akauliza tena: Je, (kiburi ina maana) ni vile mmoja wetu kuwa ana marafiki wanaoketi naye?



Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Hapana!))



Mtu akauliza: Ee Rasuli wa Allaah! Basi ni nini kiburi?



Akasema: ((Ni kukataa haki na kudharau watu)) [As-Silsilah Asw-Swahiyhah (134)]
 
Mama Yake Muislamu, Baba Mkristo, Je Anaweza Kuoa Mwanamke Wa Kiislamu?
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI








Baada ya salamu. .naomba jibu tafadhali,nina rafiki yangu amekuja kupwoswa,lakini kijana aliyemposa mamake ni muislama na babake ni mkristo .lakini yeye kijana ni muislama sasa inamruhusu sheriya huyu msichana kuolewa na huyu kijana. .tunaongoja majibu

Wasalamu alaikum warahmatullahi wabarakatu

ndugu yenu mwislamu










JIBU:







Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Jibu ni kwamba inafaa kijana huyo kumuoa mwanamke wa Kiislamu, na hata ingelikuwa wazazi wake wote wawili sio Waislamu anaweza kuoa kwani inatosha yeye pekee kuwa Muislamu kuruhusiwa kuoa mwanamke wa Kiislamu. Isiyopasa ni mwanamke wa Kiislamu kuolewa na mwanamume asiyekuwa Muislamu.







Ni neema kwake huyo kijana kuwa yeye amefuata dini ya haki, hivyo inampasa amshukuru Mola wake kwa kumhidi katika haki. Mahusiano ya wazazi, ndugu, jamaa, hayamfai mtu siku ya Qiyaamah, kila mtu atakuwa pekee, atabeba madhambi yake na atahisabiwa pekee bila ya kunasibishwa na waliomhusu. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):













((إِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ فَلَا أَنسَابَ بَيْنَهُمْ يَوْمَئِذٍ وَلَا يَتَسَاءلُونَ)) ((فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ)) (( وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُوْلَئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ))




((Basi litapopulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana))




((Ama wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio wenye kufanikiwa))




((Na wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio waliozitia khasarani nafsi zao, na katika Jahannamu watadumu)) [Al-Muuminuun: 101-103 ]







Na Allaah Anajua zaidi
 
Mkiristo Anataka Kujua Mipaka Ya Kumuona Mwanamke Wakati Anataka Kuchumbiwa
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI:



Kuna mkiristo mmoja aliniuliza suali juu ya namna ya ukomo wa namna unavyoweza kumchunguza mchumba unayetarajia kumuo kimaumbile. mwanzoni nikiwa peke yangu nilimjibu taratibu kuwa unaenda kwa wazazi wake na kumuona kwake kabla ya kumuoa ni kama anavyostahiki kumuona mwanamke muislam wa kawaida na kwamba kabla ya kumuoa anpaswa kujiridhisha kwa umbile la nje na sikumuona sehemu ambazo zinakuwa ni uchi kwa mwanamke japo ni mchumba wake.

Siku nyingine mkristo huyo huyo alimuuliza muislam mwengine kutoka Nigeria naye alimwambia ikiwa kamchumbia anaruhusika kuona nywele zake na sehemu za viungo za mikono na miguu wakati akimjibu hayo nipo sikumpinga kwani sikuwa na elimu ya ufafanuzi wa hayo lakini bado nikawa nina wasiwasi juu ya hilo jibu hivyo naomba usahihi wa hili.












JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mipaka ya kumuoana mchumba wako.

Kumuona msichana kabla ya harusi au Nikaah ni agizo la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili kupatikane mapenzi baina ya wanandoa hao wawili. Agizo hili limepuuzwa sana na Waislamu wa jinsia zote mbili wakiona kuwa hilo litaleta kuondoa baadhi ya ada kwa Waislamu wanaoishi katika sehemu tofauti duniani.



Agizo hilo la Mtume wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) lilitolewa kwa ujumla wake na hivyo kupokewa na Jaabir bin ‘Abdillaahi, Mughiyrah bin Shu‘bah na wengineo (Radhiya Allaahu ‘anhum), na kufanya hivyo ni kuleta upendo wa kuvutiana katika maumbile ya mwili ili kuweza kuoana (an-Nasaa’iy na Ibn Maajah). Na katika Hadiyth ya Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhuma) ni ya kijumla sana kwa kiasi ambacho wanachuoni wamesema mengi kuhusu jinsi ya kumuona msichana au mwanamke unayetaka kumuoa.



Kwa muhtasari ni kuwa mwanamme anaweza kumtazama msichana uso na mikono.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Mume Aliyesilimu Hafanyi Bidii Kujifunza Kusoma Qur-aan Anasoma Tafsiyr Pekee
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina



SWALI:



Asalam aleykum warahmatulla, na mshukuru ALLAH SUBHANNA kwa kunionesha hii site. Swali langu ni kama ifuatavyo mimi nina mume ambaye aliyeingia dini kitambo lakini amejifundisha quraan kama surah nne, tano, na hatii bidii kujifunza surah zingine bali yeye husoma tafsiri peke yake akisema ni sawa kama kusoma quraan, swali langu ni sawa hivyo? Ama niaje tafadhali nahitaji majibu. Jazakaallah kheir ALLAH SUBHANNA atupe kheiri Inshallah.



JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mume asiyefanya bidii kusoma Qur-aan yenyewe kwa Kiarabu.

Hakika wengi hukosea katika mas-ala ya usomaji wakidhania kuwa kusoma tafsiri yake ni sawa na kusoma Qur-aan. Hili ni kosa na inafaa tujirekebishe ili tuwe ni wenye kupata thawabu zinazohitajika.



Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kila herufi ya Qur-aan ina thawabu kumi na wala sisemi kuwa Alif Laam Miym ni herufi bali Alif ni herufi, Laam ni herufi na Miym ni herufi”. Kwa hiyo, kwa kusoma Alif Laam Miym Muislamu anapata thawabu thelathini. Ukichukuwa mfano labda wa BismiLlaahi (Kwa jina la Allaah), kwa Kiarabu zipo herufi zifuatazo – Baa, Siyn, Miym, Alif, Laam, Laam na Haa, kwa ujumla hizi ni herufi saba ilhali ukiitafsiri katika Kiswahili utapata herufi za Kiswahili kumi na tano, yaani mara mbili ya asli yake.



Jambo lililo zuri ni Muislamu kufanya bidii kuweza kuisoma Qur-aan katika lugha yake ya asili na pia kujua maana kwani bila kujua maana huenda natija ya kufuata isiwe nzuri. Kwa kuwa anasoma tafsiri atakuwa mtu anapata thawabu ya kusoma mambo mema na mazuri. Hata hivyo, hahesabiwi kuwa amesoma Qur-aan.



Kwa hiyo, unatakiwa umueleze mume wako afanye bidii katika kujifunza kusoma ili apate kuweza kuisoma Qur-aan katika lugha yake ya asili na asome tafsiri ili aweze kujua maana na makusudio ili aweze kufuata maagizo yaliyo ndani na kuacha makatazo.




Bonyeza viungo vifautavyo upate maelezo zaidi:




Thawabu Kusoma Tafsiyr Au Kusoma Qur-aan Kwa Kiarabu?




Kusoma Qur-aan Kwa Maandishi Ya Kilatini Atapata Thawabu Sawa Na Mwenye Kusoma Qur-aan Kwa Kiarabu?



Na Allaah Anajua zaidi
 
Mwanamke Aliyesilimu Lazima Awe Na Walii? Ameoa Bila Ya Kuwajulisha Wazazi Wa Mke
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI




Assalam Alaykum? I would like to ask the following questions:- a) I have married a converted girl, before wedding she pronounced the shahada and she didn’t want her family to know either being a Muslim or getting married I was told that my marriage is not accepted because non of her family knows although she selected someone to be her Wali, from what I know is that walii cannot be a Christian and a single girl can not be married except from his decision, but I was told the family must know, if so do I have to remarry or I will be in the section of Quran where it says🙁ILLA MA QAD SALAF) EXEPT FOR WHAT HAS HAPPENED BEFFORE)?












JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako hilo kuhusu ndoa. Tufahamu kuwa ndoa ya Kiislamu kukubalika kisheria inafaa itimize masharti yafuatayo:



1. Kukubali kwa msichana anayeolewa.

2. Bwana harusi kukubali kwa ndoa hiyo.

3. Bibi harusi kupewa mahari yake.

4. Kuwepo kwa mashahidi wawili waadilifu.

5. Kuwepo na kupatikana idhini ya walii.



Kwa hiyo, Mkristo hawezi kuwa ni walii wa msichana aliye Muislamu. Sheria imeweka mipangilio madhubuti kuhusu binti kama huyo. Walii katika nikaha ya msichana aliyesilimu anakuwa ni Qadhi au Shaykh mcha Mungu au Muislamu muadilifu atakayesimama mahali pa baba yake. Kwa mujibu wa sheria ndoa hiyo iliyofungwa ni sahihi kabisa haina haja ya kufungwa tena.



Hata hivyo, kosa lililofanyika ni kutowajulisha wazazi wake. Hakika ni kuwa wazazi huwa na uchungu na watoto ambao wameuchukua kumlea mtoto wao mpaka akafika maksada ya kuolewa. Si ubinadamu, si Uislamu wala si utu kwa wewe kufanya hivyo. Je, wazazi wakijua kuwa binti yao ameolewa na Muislamu naye amekuwa Muislamu, mkeo huyo atarudi katika Ukristo.



Ni busara kwako kwenda kwa wazazi wa mke wako na kuwaeleza. Na msichana ikiwa ameingia Uislamu kwa sababu ya uzuri wake (yaani Uislamu) hataweza kushawishika lakini kama ameingia katika Uislamu kwa ajili yako huenda ukapata matatizo yatakayotoka kutoka wazazi wake. Hivyo jaribu utumie busara ili usalimishe ndoa yako.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Nani Ahlul-Kitaab Na Wanawake Gani Tumeruhusiwa Kuwaoa?
Nani Ahlul-Kitaab Na Wanawake Gani Tumeruhusiwa Kuwaoa?
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI:

asalaam alaykum,naitwa abdalah said heka ndugu zangu ktk uislamu mimi binafsi kabla ya swali langu nawashukuru kwa ujumbe wenu kwetu sisi waislamu kwani nimefaidika sana na mawaidha kupitia ALHIDAAYA ALLAH awafanyie wepesi ktk kuuwendeleza uislamu. shekhe swali langu la kwanza nataka kujua hawa ahlilkitab ni akina nani?na ivi sasa bado tunao.swali la 2 ni wanawake gani tulioruhusiwa kuwaoa sisi waislamu bila ya wao kusilimu? Asane



JIBU:

BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad:



Kwanza tunapenda na sisi kutoa shukurani kwa Du'aa zenu nzuri mnazotuombea nyote mnaotuma maswali yenu pamoja na wengineo wanaoingia AL HIDAAYA kutafuta faida mbali mbali. Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى Atutakabalie hizo Du'aa na Atuzidishie uwezo wa kuelimishana kwa kadiri Anavyotujaalia. Aamiyn





Nani Ahlul-Kitaab Na Wanawake Gani Muislamu Ameruhusiwa Kuoa?



Ahlul-Kitaab (Waliopewa vitabu, ni Manaswara (Wakristo) na Mayahudi).

Ibn Qudaamah رحمه الله alisema katika [Al-Mughniy 7/99]:

"Hakuna tofauti ya rai za maulamaa kuhusu kuruhusiwa kuwaoa wanawake wa Kitabu. Na miongoni mwa walio na rai hii ambayo ilisimuliwa kutoka kwao ni 'Umar, 'Uthmaan, Talhah, Hudhayfah, Salmaan, Jaabir na wengineo".

Ibn Al-Mundhir kasema:

"Hakuna usimulizi ulio sahihi kutoka kizazi cha mwanzo kusema kwamba hivyo ni haraam. Al-Khallaal amesimulia katika Isnaad yake kwamba Hudhayfah, Talhah, Al-Jaaruud ibn Al-Mu'alla na Udhaynah Al-'Abdi wote walioa wanawake wa Ahlul-Kitaab. Hii pia ilikuwa ni rai ya Maulamaa wengine wote".



Ushahidi mkuu kuhusu masuala haya ni Aayah ambayo Allaah سبحانه وتعالى Anasema (Na imefasiriwa kuwa na maana):

((الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلُّ لَّهُمْ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلاَ مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ وَمَن يَكْفُرْ بِالإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ))

((Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. (vitu vyote vilivyo halaal, katika chakula Allaah Alichokifanya halaal kama nyama iliyochinjwa, maziwa, mafuta, mboga, matunda) Na chakula (Wanyama waliochinjwa na wengine wanolika) cha waliopewa Kitabu (Mayahudi na Manaswara) ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa waliopewa Kitabu (Mayahudi na Manaswara) kabla yenu, mtakapowapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uasherati wala kuwaweka kinyumba. Na anayekataa kuamini (Tawhiyd ya Allaah na nguzo zote za Imani yaani kuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, Siku ya kufufuliwa, na Qadhaa na Qadar) bila shaka amali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara)) [Al-Maaidah: 5]





Masharti ya kuwaoa Ahlul-Kitaab



Sharti La Kwanza:



Lakini kuna sharti ya kuwaoa hao kama ilivyo katika Aayah kuwa: (wanawake wema miongoni mwa waliopewa Kitabu)



Abu Ja'afar Muhammad ibn Jariyr At-Twabariy ametoa maana ya 'muhswana' (mwema) katika Jaami' Al-Bayaan Ta-wiyl Aayatil-Qur-aan 8/165. "Muhswana ina maana kwamba ni mwanamke ambaye mwema aliyesitirika na msafi (kutokana na machafu ya zinaa) ambaye anajihifadhi sehemu zake za siri kutokana na kitendo cha Zinaa kama Aayah inavyosema:

((وَمَرْيَمَ ابْنَتَ عِمْرَانَ الَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا))

(Na Maryam binti wa 'Imraan, aliyelinda ubikira wake)) [At-Tahriym: 12]

Kwa maana kwamba amejilinda na kila kitendo chenye shaka na amejihifadhi na mwenendo wa uasherati.



Vile vile maana ya Muhswanaat (wanawake wema) ni wale ambao walio huru na walio katika stara. (Yaani katika heshima na aliye bikra, asiye mhuni) Ibn Kathiyr (Allaah Amrehemu) amesema katika Tafsiyr yake:

"Hii ni rai ya Maulamaa wengi wao na hii ndivyo inavyoelekea kuwa hali yenyewe. Asije kuwa dhimiyah (mwanamke asiye Muislam aliye katika hifadhi ya Kiislam) lakini pia asiyekuwa katika stara (heshima, bikra). Ikiwa atakuwa katika hali hii atakuwa amepotoka na mwenye ufisadi, na mumewe atamalizikia kuwa kama inavyoeleza katika methali: "Amenunua tende mbaya na amekhiniwa katika uzito na mizani pia".



Maana iliyo dhahiri katika aayah ni vile ilivyomaanisha "al-Muhswanah" (mwanamke mwenye stara, (aliyekuwa bikra, asiyekuwa mhuni) naye ni mwanamke aliyejiepusha na zinaa kama Allaah سبحانه وتعالى Anavyosema katika Aayah nyingine:

((مُحْصَنَاتٍ غَيْرَ مُسَافِحَاتٍ وَلاَ مُتَّخِذَاتِ أَخْدَانٍ))

((….wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara)) [An-Nisaa: 4:21]



Lakini tunasisitiza kuwa ni mwanamume pekee anayeweza kufunga ndoa na Ahlul-Kitaab, ama mwanamke wa Kiislamu haruhusiwi kuolewa na mwanamume wa Ahlul-Kitaab



Sharti Ya Pili:



Ni kwamba mwanamume awe ndiye mwenye mas-uliyah na nyumba na watoto, kwani kwa Hikma ya Allaah سبحانه وتعالى Amemfanya mume awe kiongozi wa nyumba kwa sababu itakuwa ni wepesi kwake kumuongoza mkewe. Na inabidi Muislamu anapooa Ahlul-Kitaab ajitahidi awezavyo kumuongoza katika dini ya Uislamu.



Sharti Ya Tatu:



Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amependekeza Muislamu aoe wanawake Waislamu walioshika dini. Kwa hiyo kwanza ni kufanya jitihada ya kuwaoa wanawake Waislamu walioshika dini kisha tena kama haikuwezekana ndio aelekee kwa Ahlul-Kitaab.

Na ifahamike kuwa ni bora na usalama kabisa kutokuoa wanawake wa Kitabu khaswa kwa siku hizi ila ikiwa atakubali kusilimu kisha atazamwe tabia yake na kama ataendeleza dini yake sawa sawa.



Ibn Qudaamah (Allaah Amerehemu) alisema: Kwa vile hali ni hii, ni bora kutokuoa mwanamke wa Kitabu kwa sababu 'Umar aliwaambia wale waliowaoa wanawake wa Kitabu "Waacheni (Wapeni talaka)" kwa hiyo wakawapa talaka isipokuwa Hudhayfah. 'Umar akamuambia: "Mpe talaka". (Hudhayfah) akasema: "Je, Unashuhudia kuwa yeye ni haraam?" Akasema: "Yeye ni mkaa wa moto wenye kuwaka, mpe talaka". Akasema: "Je, Unashuhudia kuwa yeye ni haraam?" Akasema: "Yeye ni mkaa wa moto wenye kuwaka". Akasema: "Najua kuwa yeye ni mkaa wa moto wenye kuwaka lakini yeye ni halali kwangu". Baada ya muda akampa talaka na akaulizwa "Kwa nini hukumpa talaka alipokuamrisha 'Umar?" Akasema: "Sikutaka watu wafikiri kuwa nimefanya kosa (kwa kumuoa)".

Labda alikuwa akimpenda au labda kwa sababu walipata mtoto pamoja kwa hiyo alimpenda". [Al-Mughniy 7/99]



Vile vile Hadiyth hii ifuatayo Sahiyh inasema:

((Ibn 'Umar alipokuwa akiulizwa kuhusu kumuoa mwanamke Mkiristo au Myahudi, alikuwa akisema: "Allaah Ameifanya kuwa ni Haraam kwa Muumini kuoa wanawake wanaomshirikisha Allaah katika ibada, na sijui lililo kubwa zaidi kuliko kumshirikisha Allaah katika ibada na kadhalika kama mwanamke kusema 'Iysaa ni Mungu ingawa yeye ni mja tu wa Allaah")) [Al-Bukhaariy]



Shaykh Ibn Baaz (Allaah Amrehemu) alisema: "Ikiwa mwanamke wa Kitabu anajulikana kuwa ni mwenye stara (sio muhuni) na kujiepusha na njia ambazo zinampeleka mtu katika uasherati, inaruhusiwa kwa sababu Allaah سبحانه وتعالى Ameruhusu hivyo na Ameturuhusu kuwaoa wanawake wao na kula nyama zao.



Lakini siku hizi kuna khofu kwamba wale wanaooa huenda wakakutana na uovu zaidi. Wanaweza kuwaita katika dini yao na wanaweza kuwalea watoto wao katika Ukristo. Kwa hiyo hatari ipo hakika na ni kubwa. Ili kuwa katika amani, Muumini ni bora asiwaoe. Na katika hali nyingi hakuna uhakika kama mwanamke hatofanya vitendo vya uasherati au hatowaleta watoto waliotoka katika uhusiano wa mwanzo. Lakini mwanamume akitaka kufanya hivyo basi hana dhambi kwake ili ajiweke katika stara na ainamishe macho yake kwa kumuoa. Ajitahidi kumuita katika Uislamu na awe na hadhari na uovu wake na hadhari ya kumruhusu asimvute yeye au watoto wake katika ukafiri". [Fataawa Islaamiyyah, 3/172]





Hivi Sasa Je, Tunao Ahlul-Kitaab?



Hivi sasa tunao Ahlul-Kitaab nao ni Wakristo na Mayahudi. Lakini wao wamekufuru na kumshirikisha Allah. Kwa hiyo ni makafiri na washirikina, kutokana na Qur-aan.



((اتَّخَذُواْ أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللّهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُواْ إِلاَّ لِيَعْبُدُواْ إِلَهًا وَاحِدًا لاَّ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ))

((Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Allaah, na pia Masiyh bin Maryam. Na wala hawakuamrishwa isipokuwa wamuabudu Mungu Mmoja, hapana mungu ila Yeye. Subhanahu, Ametakasika na hayo wanayomshirikisha nayo)) [At-Tawbah: 9:31]



Lakini wametolewa katika kuharamishwa kuolewa wanawake wao kwa sababu Allaah سبحانه وتعالى Anasema katika aayah yenye maana:

((وَلاَ تَنكِحُواْ الْمُشْرِكَاتِ حَتَّى يُؤْمِنَّ وَلأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ وَلاَ تُنكِحُواْ الْمُشِرِكِينَ حَتَّى يُؤْمِنُواْ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ أُوْلَئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ وَاللّهُ يَدْعُوَ إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ وَيُبَيِّنُ آيَاتِهِ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ))

((Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa mwanamume Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Hao wanawaitia kwenye Moto, na Allaah Anawaitia kwenye Pepo na maghafira kwa idhini Yake. Naye Huzibainisha Aayah zake kwa watu ili wapate kukumbuka)) [Al-Baqarah: 2:221]



Washirikina waliotajwa katika Aayah hii ni wale walio nje ya Ahlul-Kitaab mfano Baniani, Majusi, Mabudha na kadhalika.



Kwa hiyo 'Watu wa Vitabu' ni makafiri na washirikina, lakini Allaah سبحانه وتعالى Ameturuhusu kula nyama zao na kuwaoa wanawake wao ikiwa watakuwa wenye stara (wenye heshima sio wahuni). Hii imeruhusiwa kutokana na maana ya Aayah iliyo katika Suratul-Baqarah 2:221 (tulioitaja hapo juu).



Na Allaah Anajua Zaidi
 
Ndoa Na Aliyesilimu Asiyekuwa na Walii Inafaa
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI:

Asalaam alaikum!naomba kupata ufumbuzi wa suala hili kwani mimi nimeoa mwanamke ambaye amekubali kuwa muisilamu kwa kunifata mimi pia kukubali uisilamu,lakini wazazi wake ni wakiristo bado na katika ndoa yetu kulikua hakuna mtu wa upande wake mwanamke isipokua rafiki wa mbali tu,je vipi ndoa imekubalika?





JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu kwako ewe ndugu yetu kwa swali lako hilo zuri.

Alhamdulillaahi, Uislamu kwetu ni mfumo kamili wa maisha nao haukuacha chochote ila umetuelezea kinaganaga. Kila kitu katika Dini yetu kina masharti na kanuni zake ndoa ikiwa mojawapo. Miongoni mwa masharti ya ndoa ni lazima mwanamke awe na walii wake, kwani hakuna ndoa bila ya walii.



Asiyekuwa Muislamu anaposilimu wazazi wake hawawezi kuwa walii wake lakini hata hivyo ni vyema kuwajulisha kuhusu suala hilo la ndoa la binti yao na hata kuwaalika kuhudhuria harusi hiyo. Hiyo ni njia ya kuwavutia katika Uislamu. Uislamu umeweka kuwa msichana asiyekuwa na walii basi sultani au Qaadhi anakuwa walii wake. Na katika sehemu ambayo hakuna ma-Qaadhi basi kiongozi mmoja wa kidini kama Imaam anaweza kuchaguliwa akiwa ana maadili ya Kiislamu na muruwa kutekeleza jukumu kama hilo. Rafiki wa mbali hawezi kuwa walii wake katika suala nyeti kama hilo. Pia tuelewe kuwa Uislamu umekataza urafiki baina ya mwanamme na mwanamke. Ikiwa hakuna kabisa watu kama hao wanaoweza kuwa walii wake basi anaweza kumchagua yeyote katika Muislamu muadilifu kusimamia jambo hilo.



Hakika ni kuwa ndoa hiyo haina tatizo ikiwa masharti mengine yametimizwa kama kupatikana mashahidi wawili waadilifu, kuridhika kwa mwanamke mwenyewe na kumpatia mahari yake kamili mliyosikilizana.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Ndoa Ya Ahlul-Kitaab Inafungwa Msikitini Au Kanisani?
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina


SWALI:

Asalaam alaykum,

Nimesoma kwenye maswali na nimeona kuwa kuoa mwanamke wa Kitabu ni halali ingawa si halali nzuri, lakini pia ni kuwa mwanamke anayemshirikisha mwenyezi mungu na mabaye atakuwa mlezi wa watoto wako na watajifunza kumshirikisha mwenyezi mungu pia. Swali ni hili je mwanamke huyo unamuoa kwa ndoa ipi? Mnafungaje ndoa hapo, Mnafungia kanisani au msikitini au mnafunga ndoa ya serikali ambayo kila mtu anabaki na dini yake. Je ndoa ya serikali inaswihi, mimi kaka yangu amemuoa mwanamke wa kitabu kwa ndoa ya kiserikali je yuko sahihi? Au anazini tu kuna ndoa hapo?

Wasalaam alaykum






JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Qiyaamah.



Shukrani kwa swali lako hilo ambalo limekutia wewe katika wasiwasi na kuwa na dukuduku. Hakika ni kuwa ndoa ya Kiislamu inaweza kufanyika sehemu yoyote ambayo inakubaliwa katika Uislamu na si lazima ifanywe msikitini. Inaweza kufanywa Msikitini, nyumbani, kwenye ukumbi na kadhalika lakini haiwezi kufanyika katika Kanisa, Hekalu au Sinagogi kwa kuwa haijawahi kufanyika hivyo katika historia ya Kiislamu yote. Sehemu ya kufanyia si miongoni mwa masharti ya kukubalika kwa nikaah.

Masharti ya ndoa ya Kiislamu ni kama yafuatayo:

1. Kukubali bila ya kutenzwa nguvu kwa mume na mke.

2. Idhini ya walii k.m. baba, ndugu wa kiume, babu, n.k.

3. Mashahidi 2 waadilifu.

4. Mume kutoa mahari kumpatia mkewe.

5. Sigha (namna, maneno) ya kuozesha ni lazima iwe kwa njia ya kwamba mwenye kuozesha (walii au aliyepewa ruhusa naye kufanya hivyo) awe ni mwenye kusema: Nimekuozesha wewe Fulani binti Fulani kwa mahari yake kadhaa, na mume naye awe ni mwenye kujibu kuwa nimekubali kumuoa …..



Ikiwa Nikaah hiyo itafanywa serikalini mara nyingi masharti haya tuliyoyataja huwa hayakamiliki na hasa akiwa mke si Muislamu. Na ikiwa masharti hayatokamilika basi ndoa yenyewe itakuwa haijaswihi. Ikiwa mke mwenye kutaka kuolewa si Muislamu (Ahlul Kitaab), hata hivyo ndoa inafaa ifanywe Msikitini au nyumbani kwani mume ndiye mwenye majukumu na wala sio mke.

Na Allah Anajua zaidi
 
Nimemuoa Mwanamke Mbudhi (Budhist), Je Nimuache?
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI:



Asaalam Alekum Warhamutulah Taala Wabarakatu, natowa shukrani zangu kwa waisilam wa ALHIDAAYA. Swali langu ni kuhusu ndoa nimeowa mke Budist kutokana na uchache wa elimu ya dini yetu na nimeowa kwa shari’ah ya kidini na nimesoma si ruhusa kuowa Budist mpaka aamini na mke mpaka sasa hajabadili dini je nimuche? Au nifanye nini?



JIBU:


Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.


Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kumuoa mwanamke ambaye ni Mbudhi.

Hakika kama ulivyosema ndivyo Allaah Aliyetukuka Anavyotuambia:

“Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni” (al-Baqarah [2]: 221).


Kwa hiyo, huna budi isipokuwa umuache na utafute mwengine kwani mwanzo hakuna ndoa kishari’ah baina yako na yeye.


Isitoshe ndugu yetu, tusiwe na tabia ya kufanya mambo ambayo hatuyajui au hatuna uhakika nayo kasha ndio tunakuja kuuliza. Kufanya hivyo kutapelekea katika madhambi kwani ulikuwa unaweza kuuliza tokea mwanzo na hukufanya. Hii ni tabia waliyonayo Waislam wengi hivi sasa; hujiingiza kwenye matatizo, haraam, utata na kasha baadaye ndio wanauliza hukmu ya kishari’ah. Tusiwe hivyo Waislam na tumuogope Allaah katika mambo yetu yote.

Bonyeza kiungo kifutacho upate manufaa zaidi:


Ameoa Mwanamke Mshirikina Na Hataki Hadi Sasa Kubadili Dini Yake Nini Hukmu Ya Ndoa Yake?

Anaweza Kufunga Ndoa Na Mwanaume Mshirikina Bila Ya Kitendo Cha Ndoa Hadi Asilimu? Hapati Waume Wa Kiislamu Naye Anataka Sitara

Na Allaah Anajua zaidi
 
Wakristo Ni Ahlul-Kitaab Na Hali Wanaamini Waungu Watatu (Utatu Mtakatifu)?
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina


SWALI:

Assalaam Alaykum!

Nashukuru kwa ujumbe wa ijumaa ambao mara nyingi hutupa mafunzo hasa sie ambao pengine hatupati nafasi za kuhudhuria mawaidha masjid. Nimepitia ujumbe wa jana na kukuta mambo ya kuwaoa ahlul kitaab. Niliposoma kwa ndani zaidi naona pameelezwa kuwa wakristo nao pia ni Ahlil kitaab. Hapa ndio nilipo changanyikiwa.

Wajua sie watu wenye elimu ndogo mara nyingi twajifunza kwa kukariri na unapomsikia mtu anaeleza vingine unatatizika sana katika mambo haya ya "Shubhaat".

Ninavyo jua mimi wakristo hawa ndio ambao wana waungu watatu. Kwa imani zao wao wanadai kuwa kuna mungu mwana, mungu mama na mungu roho mtakatifu. Sina uhakika na wakriso wote duniani kuwa wana amini hivi lakini nilipo kuwa chuoni nilikutana na wakristo tokea karibu nchi 30 tofauti duniani na hawa wote waliamini kuwa na utatu katika uungu.

Ahlul kitaabi ninao wajua mimi ni wale walomfuata nabii Issa (Alayhis Salaam) na hawakuwahi kumshirikisha Allah (Subhaanahu Wataala). Wakati nabii Issa (Alayhis Salaam) anakaribia kukamilisha kipindi chake cha utume aliwaambia wafuasi wake kuwa kuna mtume anaeitwa Ahmad (SwallaAllahu Alayhi Wassallaam) ambae atashika hatamu za uongozi baada yake.

Sasa mimi naomba ufafanuzi hapa kuhusu hawa ahlul kitabi ambao pia ni wakristo sheikh wangu? Wanapatika nchi gani labda na wanafuata kitabu gani mana kama ni Taurati sidhani kama hawa waristo wa leo wanayo ikiwa kitabu chao cha biblia wanakibadilisha kila leo.

Nawatakia kila la kheri.




JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuwaoa Ahlul Kitaab. Awali ya yote ni kuwa taqriban wanazuoni wote wameafikiana kuwa Ahlul Kitaab wanajumuisha Mayahudi na Wakristo kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).



Hili ni suala lenye utata kidogo kwa sababu ya misimamo tofauti ya wanazuoni. Na utata mwengine unakuja kwa sababu ya kuchukua baadhi ya ibara na mistari ya Biblia ambayo kwa uhakika si kigezo chetu katika suala hilo na mengineyo. “Shubuhaat” ni jambo ambalo Muislamu hafai kulifanya kwani hilo ndilo alilotuambia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth ya an-Nu‘maan bin Bashiyr (Radhiya Allaahu ‘anhuma):

“Yeyote mwenye kuepuka ya Shubuhaat, ameihifadhi Dini na heshima yake. Na yeyote mwenye kuingia katika Shubuhaat ameingia katika haramu” (al-Bukhaariy na Muslim).



Hakika ni kuwa hata Wakristo waliokuwa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa wana waungu watatu. Na hao Wakristo walikuwa na Imani hiyo unayoizungumza na kwa ajili hiyo Allaah Aliyetukuka Akasema:

“Kwa hakika wamekufuru waliosema: Allaah ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja. Na ikiwa hawaachi hayo wanayoyasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanaokufuru” (5: 73).

Si hilo tu bali pia walikuwa wanamuabudu mama yake, ‘Iysa, yaani Maryam na Allaah Akawakataza kwa kauli Yake:

“Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume. Wamekwishapita Mitume kabla yake. Na mama yake ni mwanamke mkweli. Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia jinsi Tunavyowabainishia Aayah, kisha angalia vipi wanavyogeuzwa” (5: 75).

Kuelezewa kuwa wote wawili walikuwa wanakula chakula ni kuonyesha kuwa hao hawawezi kuwa wana sifa ya uungu. Kwa hiyo utatu huo ni madai batili nay a uovu, na madai hayo ya utatu yalikuwa hata kwa Wakristo waliokuwa katika enzi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).



Pia tufahamu kuwa si Wakriso wote duniani kuwa wanaamini hivyo kwani wapo wengine ambao hawaamini utatu mtakatifu. Na hao ambao hawaamini hivyo walikuwepo wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), mfano ni kina Najjaash, mfalme wa Uhabashi ambaye baada ya kusomewa Aayah za Surah Maryam na Ja‘far bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema tofauti yenu na yetu haizidi msitari huu (akachora msitari kwenye ardhi), na tunafahamu kuwa baadaye Najjaash huyo alifariki hali akiwa keshasilimu.

Hata hivyo, wale wenye kuamini utatu ni wengi kwa kiasi kikubwa sana.



Ama wale waliomfuata Nabii ‘Iysa (‘Alayhis Salaam) walikuwa ni Waislamu kwa mujibu wa Qur-aan. Allaah Aliyetukuka Anasema:

“‘Iysa alipohisi kuwa kati yao pana ukafiri alisema: Nani wasaidizi wangu kwa Allaah? Wanafunzi wake wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Allaah. Tumemuamini Allaah, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu” (3: 52).

Na zipo Aayah nyingine katika Qur-aan zinazotufahamisha hilo. Na kwa kuwa walikuwa ni Waislamu hawakuwahi kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala). Ukristo ulianza muda mwingi baada ya kuondoka duniani Nabii ‘Iysa (‘Alayhis Salaam).



Wapo wanazuoni wengine wanasema hawa Wakristo wa sasa si Ahlul Kitaab kwa kuwa Nabii ‘Iysa (‘Alayhis Salaam) alitumwa kwa kondoo waliopotea wa wana wa Israili. Na kwa kuwa hawa Wakristo wa sasa ni wana wa Israili hawawezi kuwa Ahlil Kitaab. Lakini muono huo wa wanazuoni hao hauna dalili yoyote bali kinyume chake ndio sahihi kabisa. Tunakuta kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipowatuma Maswahaba zake kwenda kulingania baadhi ya makabila ya Kiarabu yalioingia katika Ukristo alikuwa akiwausia kutowavamia au kuwaua watawa walio jitenga katika hekalu zao. Na kuwa hawa walikuwa wanachukuliwa kuwa ni Ahlul Kitaab na ndivyo walivyochukuliwa Wahabashi. Tunaona kuwa Waarabu wakati huo na Wahabashi hawakuwa ni wana wa Israili lakini walikuwa wanajulikana kama Ahlul Kitaab.



Kwa muhtasari wa maneno ni kuwa kila anayejiita kuwa yeye Mkristo basi anachukuliwa hivyo. Kwa jinsi hiyo watakuwa wanapatikana katika nchi zote hapa duniani. Na wao ikiwa ni Wakristo wanafuata Biblia ambacho ni mkusanyiko wa vitabu vingi ilhali Mayahudi wanafuata Agano la Kale peke yake katika hiyo Biblia. Na tufahamu ya kuwa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) tayari Biblia ilikuwepo ikitumika na Wakristo hata Waraqah bin Nawfal binamu ya Khadijah bint Khuwaylid (Radhiya Allaahu ‘anha), mkewe Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anazo nyaraka hizo kwa Kiarabu wakati Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anapewa Utume. Mbali ya kuwa Biblia hiyo imetiwa mikono ya waandishi kama inavyosema yenyewe katika kitabu cha Yeremia 8: 8.



Kubadilishwa kwa vitabu hivyo ni wazi kwani Allaah Aliyetukuka Hakutoa dhamana ya kuvihifadhi. Na kubadilishwa huko kulikuwepo kukifanywa na Mayahudi wakati wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mwenyewe. Kuhusu kubadilishwa huko tunaelezewa na Allaah Aliyetukuka:

“Basi ole wao wanaoandika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Allaah, ili wachumie kwacho pato dogo. Basi ole wao kwa yale iliyoandika mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma” (2: 79).



Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atuongoze katika njia nyoofu na Atuepushe na upotevu wa njia zote potofu.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…