08-Swalaah Ya Ijumaa: Wajibu Kwa Imaam Kuwasalimia Maamuma Baada Ya Kupanda Minbari

Wajibu Kwa Imaam Kuwasalimia Maamuma Baada Ya Kupanda Minbari



Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Ni Sunnah kwa Khatwiyb (wa Ijumaa) kuwasalimia maamuma anapopanda minbari kabla ya kukaa kitako (kusubiri Adhana).





[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/234)]
 
09-Swalaah Ya Ijumaa: Kuzungumza Wakati Khutbah Inapotolewa Ni Haramu

Kuzungumza Wakati Khutbah Inapotolewa Ni Haramu



Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Maongezi ya watu wakati Imaam anatoa khutbah siku ya Ijumaa ni haramu.





[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/240)]
 
10-Swalaah Ya Ijumaa: Hukmu Ya Kumuombea Rahmah Anayepiga Chafya Au Kurudisha Salaam Wakati Imaam Anakhutubia



Hukmu Ya Kumuombea Rahmah Anayepiga Chafya

Au Kurudisha Salaam Wakati Imaam Anakhutubia



Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Kauli iliyo sahihi ya ‘Ulamaa ni kwamba, haijuzu kumuombea rahmah anayepiga chafya wala kurudisha salaam wakati Imaam (Khatwiyb) anakhutubia.





[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/242)]
 
11-Swalaah Ya Ijumaa: Hakuna Sunnah Rawaatib Katika Swalaah Ya Ijumaa



Hakuna Sunnah Rawaatib Katika Swalaah Ya Ijumaa



Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Hakuna Sunnah za Rawaatib za qabliyyah (kabla ya Swalaah) katika Swalaah ya Ijumaa. Lakini anaweza kuswali Sunnah atakazo kabla ya kuingia Imaam.





[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/249)]
 
12-Swalaah Ya Ijumaa: Suwrah Za Kusomwa Katika Swalaah Ya Ijumaa



Suwrah Za Kusomwa Katika Swalaah Ya Ijumaa



Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Iliyo katika Shariy’ah kusomwa katika Swalaah ya Ijumaa ni Suwrat “Al-A’laa” na “Al-Ghaashiyah” au “Al-Jumu’ah” na “Al-Munaafiquwn”, au “Al-Jumu’ah” na “Al-Ghaashiyah”.





[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/279)]
 
13-Swalaah Ya Ijumaa: Hukmu Ya Anayeswalisha Ahli Zake Nyumbani Swalaah Ya Ijumaa



Hukmu Ya Anayeswalisha Ahli Zake Nyumbani Swalaah Ya Ijumaa



Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Atakayeswalisha ahli zake Swalaah ya Ijumaa nyumbani, anapaswa airudie kwa kuiswali Swalaah ya Adhuhuri, wala Swalaah (hiyo) ya Ijumaa (walioiswali nyumbani) haisihi kwao.





[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/196)]
 
Elimu Ya Hadiyth: Maana Ya Idadi Fulani Ya Imaam Wa Hadiyth



Alhidaaya.com











Inaposemwa Hadiyth (fulani) imesimuliwa na As-Sab’ah (watu saba), basi ina maana wanaokusudiwa hapo ni:



1- Al-Bukhaariy

2- Muslim

3- At-Tirmidhiy

4- An-Nasaaiy

5- Abuu Daawuwd

6- Ibn Maajah

7- Ahmad









Inaposemwa Hadiyth (fulani) imesimuliwa na As-Sittah (watu sita), basi ina maana wanaokusudiwa hapo ni:





1-Al-Bukhaariy

2-Muslim

3-At-Tirmidhiy

4-An-Nasaaiy

5-Abuu Daawuwd

6- Ibn Maajah







Inaposemwa Hadiyth (fulani) imesimuliwa na Al-Khamsah (watu watano) basi ina maana wanaokusudiwa hapo ni:



1- At-Tirmidhiy

2- An-Nasaaiy

3-Abuu Daawuwd

4- Ibn Maajah

5- Ahmad







Inaposemwa Hadiyth (fulani) imesimuliwa na Al-Arba’ah (watu wanne), basi ina maana wanaokusudiwa hapo ni:



1- At-Tirmidhiy

2- An-Nasaaiy

3- Abuu Daawuwd

4- Ibn Maajah









Inaposemwa Hadiyth (fulani) imesimuliwa na Ath-Thalaathah (watu watatu), basi ina maana wanaokusudiwa hapo ni:



1- At-Tirmidhiy

2- An-Nasaaiy

3-Abuu Daawuwd







Inaposemwa Hadiyth (fulani) imesimuliwa na Ash-Shaykhaan (Mashaykh wawili) au Asw-Swahiyhayn (Swahiyh Mbili) au Muttafaqun 'alayhi (Wameafikiana juu yake), basi wanaokusudiwa hapo ni:



1- Al-Bukhaariy

2- Muslim
 
01-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Dhikri Bora Kabisa



Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Ila Allaah



01-Dhikri Bora Kabisa Ni Laa Ilaaha Illa Allaah








عَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((أَفْضَلُ الذِّكْرِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَأَفْضَلُ الدُّعَاءِ الحَمْدُ لِلَّهِ)) رواه الترمذي وقال: حديث حسن

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) amesema: Nimemsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Dhikri bora kabisa ni Laa ilaaha illa Allaah na du'aa bora kabisa ni Alhamdulillah)) [At-Tirmidhiy amesema: Hadiyth Hasan, Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaaniy: Swahiyh Al-Jaami’ (1104), Swahiyh Ibn Maajah (3080) Swahiyh At-Tirmidhiy (3383)]
 
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



02-Laa Ilaaha Illa Allaah: Iko Daraja Ya Juu Kabisa



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((الإيمَانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ)) أَوْ ((بِضْعٌ وَسِتُّونَ شُعْبَةً، فَأَفْضَلُهَا قَوْلُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى عَنْ الطَّرِيقِ، وَالْحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنْ الإِيمَانِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Iymaan ni sabiini na kitu)) au alisema ((Tanzu sitiini na kitu. Ilio bora kabisa ni kauli ya ‘Laa ilaaha illa-Allaah’, na ya chini kabisa ni kuondosha taka njiani. Na kuona hayaa ni utanzu katika tanzu za Iymaan)). [Al-Bukhaariy na Muslim]



Faida: Bidhw’ ni idadi baina ya tatu na tisa.
 
03-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayefariki Akiwa Anajua Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah Ataingia Jannah

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Ila Allaah





03-Atakayefariki Akiwa Anajua Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah Ataingia Jannah





عَنْ عُثْمَانَ بِنْ عَفَّان رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَعْلَمُ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّةَ))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Uthmaan bin ‘Afaan (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayefariki akiwa anajua kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah ataingia Jannah)). [Muslim]
 
04-Atakayeshuhudia Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah … Allaah Atamuingiza Jannah Kwa ‘Amali Zozote Alizonazo:





عن عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللّهِ صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ شَهِدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ وَالْجَنَّةُ حَقٌّ وَالنَّارُ حَقٌّ أَدْخَلَهُ اللَّهُ الْجَنَّةَ عَلَى مَا كَانَ مِنْ الْعَمَلِ))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Ubaadah Bin Swaamit (رضي الله عنه) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayeshuhudia kwa kuamini na kukiri moyoni kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na kwamba ‘Iysaa ni mja wa Allaah na Rasuli Wake, na neno Lake Alilompelekea Maryam na Ruwh kutoka Kwake, na kwamba Jannah ni haki, na Moto ni haki, Allaah Atamuingiza Jannah kwa ‘amali zozote alizonazo)) [Al-Bukhaariy (3/1267) (3252), Muslim (1/57) (28) Ahmad (5/313) (22727), Ibn Hibbaan (1/431) (202), An-Nasaaiy (6/331) (11132)].
 
05-Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Akakanusha Wanaoabudiwa Asiyekuwa Allaah Italindwa Mali Yake Na Uhai Wake Na Hesabu Yake Itakuwa Kwa Allaah







عَنْ أَبِي مَالِكٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَكَفَرَ بِمَا يُعْبَدُ مِنْ دُونِ اللَّهِ حَرُمَ مَالُهُ وَدَمُهُ وَحِسَابُهُ عَلَى اللَّهِ)) مسلم‏

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Maalik kutoka kwa baba yake amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Atakayesema “Laa ilaaha illa Allaah” na akakanusha wanaoabudiwa wasio Allaah italindwa (itakuwa haramu mtu kuchukua) mali yake na damu yake (uhai wake) na hesabu yake iko kwa Allaah)) [Muslim]
 
06-Abashiriwe Jannah Mwenye Kushuhudia Akiwa Na Yakini Moyoni

Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah.







Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwita:



((يَا أَبَا هُرَيْرَةَ (وَأَعْطَانِي نَعْلَيْهِ) قَالَ: اذْهَبْ بِنَعْلَيّ هَاتَينِ فَمَنْ لَقِيتَ مِنْ وَرَاء هَذَا الْحَائِطِ يَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاّ اللّهُ مُسْتَيْقِنا بِهَا قَلُبُهُ فَبَشّرْهُ بِالْجَنّةِ))

((Ee Abaa Hurayrah (akanipa viatu vyake) Nenda na viatu vyangu hivi, utakayemkuta nyuma ya ukuta huu akiwa anakiri moyoni na anashuhudia kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki ila Allaah akiwa amethibitika nayo moyoni, mbashirie Jannah)) [Muslim]
 
07-Atatoka Motoni Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Akiwa Moyoni Mwake Kuna Khayr (Iymaan) Kiasi Cha Uzani Wa Shairi Au Mbegu Au Punje





عَنْ أَنَسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((يَخْرُجُ مِنَ النَّارِ مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ شَعِيرَةٍ مِنْ خَيْرٍ، وَيَخْرُجُ مِنَ النَّارِ مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ بُرَّةٍ مِنْ خَيْرٍ، وَيَخْرُجُ مِنَ النَّارِ مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ ذَرَّةٍ مِنْ خَيْرٍ)) الْبخاري ومسلم



Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atatoka motoni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah (hakuna muabudiwa wa haki ila Allaah)) akiwa moyoni mwake kuna khayr (iymaan) kiasi cha uzani wa shairi. Na Atatoka motoni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah akiwa moyoni mwake kuna khayr (iymaan) kiasi cha mbegu moja. Na atatoka motoni anayesema: laa ilaaha illa Allaah akiwa moyoni mwake kuna khayr (iymaan) kiasi cha uzani wa punje)). [Al-Bukhaariy (44) Muslim (193)]
 
08-Laa Ilaaha Illa Allaah Ni Kauli Thabiti Ya Uhai Wa Dunia Na Aakhirah





عَنْ الْبَرَاء بْن عَازِب رَضِيَ اللَّه عَنْهُ أَنَّ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((الْمُسْلِم إِذَا سُئِلَ فِي الْقَبْر شَهِدَ أَنْ لاَ إِلَه إِلاَّ اللَّه وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُول اللَّه فَذَلِكَ قَوْله (يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ))) البخاري وَرَوَاهُ مُسْلِم أَيْضًا وَبَقِيَّة الْجَمَاعَة

Imepokelewa kutoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muislamu akiulizwa katika kaburi, atashuhudia kwamba: "Laa ilaaha illa-Allaah wa anna Muhammadar-Rasuwlu-Allaah" [Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli wa Allaah] hiyo ndiyo maana ya kauli ya Allaah: “Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah”)). [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]
 
09-Atakayefurahika Zaidi Kwa Shafaa Ya Nabiy Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Kwa Niyyah Safi Moyoni Au Nafsini Mwake







عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللهِ مَنْ أَسْعَدُ النَّاسِ بِشَفَاعَتِكَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ؟ قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلى اللهُ عليهِ وَسَلَّمَ: ((لَقَدْ ظَنَنْتُ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ أَنْ لا يَسْأَلَني عَنْ هذَا الْحَدِيِثِ أَحَدٌ أَوَّلَ مِنْكَ لِما رَأَيْتُ مِنْ حِرْصِكَ عَلَى الْحَدِيثِ أَسْعَدُ النَّاسِ بِشَفَاعَتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَنْ قَالَ: لا إِلهَ إِلاَّ اللهُ خَالِصَاً مِنْ قَلْبِهِ أَوْ نَفْسِهِ))



Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: “Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Nani atakayefurahika kabisa kwa Shafaa’ah (uombezi) wako Siku ya Qiyaamah: Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Nlidhani ee Abaa Hurayrayh kwamba hakuna yeyote asiyekuwa wewe atakayeniuliza maelezo haya kwa vile jinsi nilivyoona himma yako juu ya jambo hili. Atakayefurahika zaidi kati ya watu kwa Shafaa’ah yangu Siku ya Qiyaamah ni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, kwa niyyah safi moyoni mwake au nafsi yake)). [Al-Bukhaariy]
 
10-Allaah Ameharamisha Moto Anayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Akitafuta Kwayo Wajihi Wa Allaah





عن عِتْبَانَ بْن مَالِكٍ الْأَنْصارِيَّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ قَدْ حَرَّمَ عَلَى النَّارِ مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ يَبْتَغِي بِذَلِكَ وَجْهَ اللَّهِ ))



Imepokelewa kutoka kwa ‘Itbaan bin Maalik Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Ameharamisha An-Naar kwa anayesema: laa ilaaha illa Allaah akitafuta Wajihi wa Allaah)). [Al-Bukhaariy (425), Muslim (33)]
 
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



www.alhidaaya.com



11-Atakayekiri Na Kushuhudia Laa Ilaaha Illa Allaah Akiyasadikisha Moyoni Ataharamishwa Na Moto.





عَنْ أنَس بِن مالِك رضي الله عنه عن النَّبِيّ صلى الله عليه وسلم قال: (( مَا مِنْ أَحَدٍ يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ صِدْقًا مِنْ قَلْبِهِ إِلَّا حَرَّمَهُ اللَّهُ عَلَى النَّارِ))

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna mtu atakayekiri na kushuhudia kwa kusadikisha moyoni mwake kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, isipokuwa Allaah Atamharamisha na Moto)). [Al-Bukhaariy (128) Muslim (32)]
 
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



www.alhidaaya.com



12-Miongoni Mwa Mambo Matano Yatakayokuwa Mazito Katika Mizani Siku Ya Qiyaamah





عن ثوبان رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((بَخٍ بَخٍ لِخمسٍ ما أثقلَهُنَّ في الميزانِ : لا إلهَ إلَّا اللهُ، وسبحانَ اللهِ، والحمدُ للهِ ، واللهُ أكبرُ، والولَدُ الصالِحُ يُتوَفَّى للمرْءِ المسلِمِ فيَحتَسِبُهُ)) النسائي وابن حبان والحاكم ، وأحمد ، وصححه الألباني في صحيح الترغيب والجامع



Imetoka kwa Thuwbaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Heko heko kwa vitu vitano, uzito gani vitakavyokuwa katika Mizani; Laa Ilaah Illa Allaah, Wa-Allaahu Akbar, Wa Subhaanah-Allaah, Wa-AlhamduliLLah, na mtoto mwema atakayekufa na wazazi wake wanatarajia thawabu kutoka kwa Allaah)) [An-Nasaaiy, Ibn Hibbaan, Al-Haakim, Ahmad, na kaisahihisha Al-Albaaniy katika: Swahiyh At-Targhiyb (1557), Swahiyh Al-Jaami'(2817)]
 
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



www.alhidaaya.com



13- Moto Hautamgusa Atakayeruzukiwa Kauli Hiyo Katika Mauti Yake





عن أَبِي هُرَيْرَةَ، وَأَبِي سَعِيدٍ، أَنَّهُمَا شَهِدَا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِذَا قَالَ الْعَبْدُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ. يَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَأَنَا أَكْبَرُ. وَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ . قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا وَحْدِي .وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ لَا شَرِيكَ لَهُ. قَالَ : صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَلَا شَرِيكَ لِي .وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، لِي الْمُلْكُ، وَلِيَ الْحَمْدُ . وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ . قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِي. ثم قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: مَنْ رُزِقَهُنَّ عِنْدَ مَوْتِهِ لَمْ تَمَسَّهُ النَّارُ))



Kutoka kwa Abuu Hurayrah na Abuu Sa’iyd (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) wameshuhudia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



((Mja akisema: “laa ilaaha illa Allaah wa Allaahu Akbar – hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Allaah ni Mkubwa.” Allaah ‘Azza wa Jalla Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi Nami ni Mkubwa.” Akisema mja: “Laa ilaaha illa Allaah Wahdahu – hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Pekee.” Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi Pekee.” Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaahu laa shariyka Lahu - hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah hana mshirika.” Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi sina Mshirika.”.Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu – hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, ufalme na Himdi ni Zake.” Husema: Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi, Ufalme na Himdi ni Zangu.” Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaahu, walaa hawla walaa quwwata illa biLLaah – hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Allaah.” Husema: Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka Kwangu.” Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Atakayeruzukiwa [kauli] hiyo wakati wa mauti yake, An-Naar [Moto] hautomgusa)). [Ibn Maajah (3794) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (713)]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…