Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب وجوب طاعة ولاة الأمر في غير معصية وتحريم طاعتهم في المعصية

080-Mlango Wa Wajibu wa Kuwatii Viongozi kwa Mambo Yasiyo ya Maasiya na Kukatazwa Kuwatii Katika Maasiya



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ ﴿٥٩﴾

Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi. [An-Nisaa: 59]





Hadiyth – 1

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( عَلَى المَرْءِ الْمُسْلِمِ السَّمْعُ والطَّاعَةُ فِيمَا أحَبَّ وكَرِهَ ، إِلاَّ أنْ يُؤْمَرَ بِمَعْصِيةٍ ، فَإذَا أُمِرَ بِمَعْصِيةٍ فَلاَ سَمْعَ وَلاَ طَاعَةَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kusikia na kutii ni wajibu kwa kila Muislamu katika alichokipenda na alicho kichukia, kwa muda ambao hakuamrishwa kufanya maasi. Kama ataamrishwa kufanya maasi basi hakuna kusikia wala kutii." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na An-Nasai].





Hadiyth – 2

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كُنَّا إِذَا بَايَعْنَا رسولَ الله صلى الله عليه وسلم عَلَى السَّمعِ والطَّاعَةِ ، يَقُولُ لَنَا : (( فِيمَا اسْتَطَعْتُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba amesema: Tulipokuwa tukimbai Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya kusikia na kutii alikuwa akituambia: "Kwa mnayo weza." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 3

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَنْ خَلَعَ يَداً مِنْ طَاعَةٍ لَقِيَ اللهَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلاَ حُجَّةَ لَهُ ، وَمَنْ مَاتَ وَلَيْسَ في عُنُقِهِ بَيْعَةٌ ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً )) رواه مسلم .

وفي رواية لَهُ : (( وَمَنْ مَاتَ وَهُوَ مُفَارِقٌ لِلجَمَاعَةِ ، فَإنَّهُ يَمُوتُ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً )) .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kuondosha mkono katika kutii atamkuta Allaah Siku ya Qiyaamah hana hoja. Na atakaye kufa na shingoni mwake hana bai'ah amekufa mauti ya kijahiliya. [Muslim]

Na katika riwaayah yake nyingine: "Na atakaye kufa naye amejitenga na jamaa (kikundi cha waislamu), hakika atakufa mauti ya ujahiliyyah."





Hadiyth – 4

وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( اسْمَعُوا وأطِيعُوا ، وَإنِ استُعْمِلَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حَبَشيٌّ ، كأنَّ رأْسَهُ زَبيبةٌ )) رواه البخاري .

Imepokewa kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Sikieni na mutii, japokuwa atachaguliwa juu yenu kama kiongozi mtumwa wa Habeshi (Ethiopia) kama kwamba kichwa chake kimefanana na zabibu." [Al-Bukhaariy]





Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( عَلَيْكَ السَّمْعُ وَالطَّاعَةُ في عُسْرِكَ وَيُسْرِكَ ، وَمَنْشَطِكَ وَمَكْرَهِكَ ، وَأثَرَةٍ عَلَيْكَ )) رواه مسلم .

Kutoka kwa abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ni juu yako kusikia na kutii katika utajiri wako na umasikini na uwe muaminifu." [Muslim]





Hadiyth – 6

وعن عبدِ اللهِ بن عمرو رضي الله عنهما ، قَالَ : كنا مَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم في سَفَرٍ ، فَنَزَلْنَا مَنْزِلاً ، فَمِنَّا مَنْ يُصْلِحُ خِبَاءهُ ، وَمِنّا مَنْ يَنْتَضِلُ ، وَمِنَّا مَنْ هُوَ في جَشَرِهِ ، إذْ نَادَى مُنَادِي رسولِ الله صلى الله عليه وسلم : الصَّلاةَ جَامِعَةً . فَاجْتَمَعْنَا إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : (( إنَّهُ لَمْ يَكُنْ نَبيٌّ قَبْلِي إِلاَّ كَانَ حَقّاً عَلَيْهِ أنْ يَدُلَّ أُمَّتَهُ عَلَى خَيْرِ مَا يَعْلَمُهُ لَهُمْ ، وَيُنْذِرَهُم شَرَّ مَا يَعْلَمُهُ لَهُمْ . وَإنَّ أُمَّتَكُمْ هذِهِ جُعِلَ عَافِيَتُهَا في أوَّلِهَا ، وَسَيُصيبُ آخِرَهَا بَلاَءٌ وَأمُورٌ تُنْكِرُونَهَا ، وَتَجِيءُ فِتنَةٌ يُرَقِّقُ بَعْضُهَا بَعْضاً ، وَتَجِيءُ الفتنَةُ فَيقُولُ المُؤْمِنُ : هذه مُهلكتي ، ثُمَّ تنكشفُ ، وتجيء الفتنةُ فيقولُ المؤمنُ : هذِهِ هذِهِ . فَمَنْ أحَبَّ أنْ يُزَحْزَحَ عَنِ النَّارِ، ويُدْخَلَ الجَنَّةَ، فَلْتَأتِهِ منيَّتُهُ وَهُوَ يُؤْمِنَ باللهِ واليَوْمِ الآخِرِ ، وَلْيَأتِ إِلَى النَّاسِ الَّذِي يُحِبُّ أنْ يُؤتَى إِلَيْهِ. وَمَنْ بَايَعَ إمَاماً فَأعْطَاهُ صَفْقَةَ يَدِهِ ، وَثَمَرَةَ قَلْبِهِ ، فَلْيُطِعْهُ إن استَطَاعَ ، فإنْ جَاءَ آخَرُ يُنَازِعُهُ فَاضْرِبُوا عُنْقَ الآخَرِ )) رواه مسلم .

Kutoka kwa 'Abdillah bin 'Amru (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) safarini, tukashuka mahali. Katika sisi kuna anaetengeneza hema lake, katika sisi kuna wanaoshindana, mwengine anailisha mifugo yake. Mwitaji wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Swalaah ya jamaa," Tukakusanyika mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akasema: "Hakika hakukuwa Nabiy kabla yangu ila ilikuwa ni haki yake kuonyesha Ummah wake kheri anayoijua kwa ajili yao, Na kuwaonya shari anayoijua kwa ajili yao. Hakika Umma wenu huu afya yake iko katika wa mwanzo wake, Na wa mwisho wake utapata balaa na mambo mnayo yakataa. Na itakuja fitna moja baada ya nyingine. Itakuja fitna Muumini atasema: 'Haya ni maangamivu yangu. Kisha itatoweka, na itakuja fitina muumini atasema: 'Ni haya haya Haya." Hivyo, anayependa kuepushwa na Moto na kuingizwa Peponi, Basi akutane na kifo chake akiwa anamuamini Allaah na Siku ya Mwisho, na awaletee watu ambao anapenda waletwe kwake. Na mwenye kumbai Imamu kwa kumpatia ahadi kwa mkono wake na tunda la moyo wake, Basi amtii anavyoweza. Akija mwingine kushindana naye, Basi ipigeni shingo ya yule Mwingine." [Muslim].





Hadiyth – 7

وعن أَبي هُنَيْدَةَ وَائِلِ بن حُجرٍ رضي الله عنه ، قَالَ : سَألَ سَلَمَةُ بن يَزيدَ الجُعفِيُّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : يَا نَبِيَّ الله ، أرأيتَ إنْ قامَت عَلَيْنَا أُمَرَاءُ يَسألُونَا حَقَّهُم ، وَيمْنَعُونَا حَقَّنَا ، فَمَا تَأْمُرُنَا ؟ فَأعْرَضَ عنه ، ثُمَّ سَألَهُ ، فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( اسْمَعْوا وَأَطِيعُوا ، فإنَّمَا عَلَيْهِمْ مَا حُمِّلُوا ، وَعَلَيْكُمْ مَا حملْتُمْ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hunaydah Waail bin Hujr (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Salamah bin Yaziyd Al-Ju'fiy alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kusema: "Ee Nabiy wa Allaah! Waonaje wakisimama juu yetu viongozi wakitaka haki zao na kukataa zetu, unatuamuru nini?" Nabiy alijiepusha na kujibu swalihilo. Kisha alimuuliza mara nyengine, hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Sikieni na mtii, hakika wao watabeba mzigo waliojitikwa nanyi mtabeba wenu." [Muslim]





Hadiyth – 8

وعن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّهَا سَتَكُونُ بَعْدِي أثَرَةٌ وَأُمُورٌ تُنْكِرُونَهَا ! )) قالوا : يَا رسول الله ، كَيْفَ تَأمُرُ مَنْ أدْرَكَ مِنَّا ذَلِكَ ؟ قَالَ : (( تُؤَدُّونَ الحَقَّ الَّذِي عَلَيْكُمْ ، وَتَسْأَلُونَ اللهَ الَّذِي لَكُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kutakuwa na ubinafsi na mambo msiyoyakubali." Wakauliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Unatuamuru nini kwa yule atakaye fikiwa na hayo?" Akajibu: "Tekelezeni wajibu wenu na mumuombe Allaah (Awapeni) ambalo ni haki yenu." [Al-Bukhaariy na Muslim]







Hadiyth – 9

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أطَاعَنِي فَقَدْ أطَاعَ اللهَ ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ عَصَى اللهَ ، وَمَنْ يُطِعِ الأَمِيرَ فَقَدْ أطَاعَنِي ، وَمَنْ يَعصِ الأميرَ فَقَدْ عَصَانِي )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kunitii mimi basi amemtii Allaah na mwenye kuniasi mimi basi amemuasi Allaah. Na mwenye kumtii amiri (kiongozi) basi amenitii mimi na mwenye kumuasi amiri basi ameniasi mimi." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 10

وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما : أن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ كَره مِنْ أمِيرِهِ شَيْئاً فَلْيَصْبِرْ ، فَإنَّهُ مَنْ خَرَجَ مِنَ السُّلطَانِ شِبْراً مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuchukia kwa amiri wake kitu basi asubiri, kwa sababu mwenye kutoka nje ya utawala wa amiri shubiri moja amekufa kifo cha kijahiliya (kikafiri)." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]





Hadiyth – 11

وعن أَبي بكرة رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَنْ أهانَ السُّلطَانَ أَهَانَهُ الله )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Bakrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Alaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Yeyote mwenye kumtweza kiongozi Allaah atamtweza." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
 
Maswali: Hukmu Za Swalah
Ibaadhi Hawaswali Nyuma Yetu; Je, Tuswali Nyuma Yao?



www.alhidaaya.com





SWALI:



Asalam Alaikium Warahmatullah wabarakatu, Tunawashukuru ndugu zetu kwa kazi mnayoifanya kwa kutuelimisha Inshaallah ALLAH Atawalipa kwa lililokuwa bora zaidi yeye ndio mlipaji wa kila kitu, Suala langu lipo kwenye masuala ya madhehebu ya ibadhi nilisoma kuhusu ibadhi humu alhidaaya lakini kuna kitu amabacho nintaka kukielewa zaidi kwani mimi ni sunni na ninaswali nyuma ya ibadhi kwenye misikiti yao suala langu lipo hawa ibadhi wanatuthamini vipi sisi kwani utakuta kama kuswali tunaswalisha sisi wao hawatufuati wao huwa wanasimamisha swala yao mbali na sisi mimi baada ya kufuatilia nimepata jawabu ya kuwa wao wanadai kuwa sisi tumetoka kwenye rehma ya ALLAH sasa nilikuwa ninataka kujua haya ni kweli na kama ni kweli sisi tunatakiwa tuwafuate kwa kuswali nao au tufanye kama wanavyofanya wao kwetu sisi ninaomba jawabu kwa kirefu Sukran





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Asli katika mas-alah ni kuwa Swalah nyuma ya kila Muislamu inasihi na inajuzu hata kama huyo Imaam ni katika wenye kufanya baadhi ya maasi, na hii ndio kauli iliyo sahihi zaidi katika kauli za Maulamaa. Hata hivyo Swalah nyuma ya aliyeshikamana na mafundisho ya Uislamu ni bora zaidi bila ya shaka yoyote ile.



Ama ikiwa Imaam ni katika wenye kufanya vijitendo vya ukafiri vyenye kumtoa mtu katika Uislamu basi Swalah nyuma ya Imaam kama huyo huwa haifai, kwani yeye mwenyewe huyo Imaam Swalah yake huwa si sahihi, kwani ametoka katika Uislamu na Swalah ya asiyekuwa Muislamu sio sahihi, na inapokuwa Swalah ya Imaam sio sahihi basi kumfuata Imaam huyo huwa hukufai.



Imaam At-Twahaawiy katika kitabu chake cha ‘Aqiydat Twahaawiyyah ameweka mlango wenye kusema: Tunaona Swalah nyuma ya kila mtenda wema na mtenda maovu miongoni mwa Ahlul Qiblah hata hivyo Hadiyth zenye kusema hivyo karibu zote ni dhaifu ila imethibiti kuwa baadhi ya Swahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) waliswali nyuma ya watu waovu kama Ibn Umar na Anas walikuwa wakiswali nyuma ya Hajjaaj bin Yusuf ambaye ni faasiq dhaalim.



Hata hivyo Imaam At-Twahaawiy amesema kuwa inajuzu kuswali nyuma ya asiyeeleweka uzushi wake -bid’ah zake- wala ufusqa wake, na si miongoni mwa shuruti za kumfuata Imaam kuelewa Maamuma itikadi ya Imaam anayemfuata au kumfanyia jaribio kwa kumuuliza maswali kuhusiana na itikadi yake; bali unatarajiwa kuswali nyuma ya Imaam huyo ambaye haeleweki hali yake.



Umesema hivi, ibadhi wanatuthamini vipi sisi kwani utakuta kama kuswali tunaswalisha sisi wao hawatufuati wao huwa wanasimamisha swala yao mbali na sisi





Swali kama hili liliulizwa kwa jopo la Wanachuoni wa kamati ya utafiti wa kielimu an utoaji Fatwa:

Swali: Je, Ibadhi ni kundi la Khaawarij linalohesabiwa kuwa ni potofu? Na je, inafaa kuswali nyuma yao?

Jibu: Ibaadhi ni kundi linalohesabika katika makundi potofu kwa sababu ya uhalifu wao na kumuasi Khalifah 'Uthmaan bin 'Iyfaan na 'Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu 'anhum), na haifai kuswali nyuma yao.

Na Allaah ni Mjuzi zaidi

Kamati ya Utafiti wa Kielimu na Utoaji Fatwa (mwisho wa kunukuu)



Unaweza vilevile kusoma makala hii muhimu Khawaarij



Umesema, wao wanadai kuwa sisi tumetoka kwenye rehma ya Allaah





Hayo kama ulivyosema ni madai yao, ama katika kanuni za Kiislam ni kuwa mwenye kuleta madai ya aina yoyote yale ni vyema alete dalili na ushahidi wa madai yake kama inavyotushauri Qur-aan kwa kusema:

“… Hayo ni matamanio yao. Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli.” Al-Baqarah: 111.



Ikiwa makafiri na washirikina katika huu uhai wote hawakutoka kwenye rehema za Allaah vipi atatoka kwenye rehma za Allaah mwenye kusema: Laa ilahaa illa Allaah? Aliyetoka kwenye rehma za Allaah kama inavyothibitisha Qur-aan ni Ibiliys, kwa kiburi chake cha kukataa amri ya Mola wake Mlezi, alimwambia: Basi toka kwenye kundi la watukufu walio juu, kwani wewe umekwishafukuzwa kutokana na rehema yangu! Qur-aan inasema:



“Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika. Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo”. Swaad: 77-78.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kasisimkwa Ndani Ya Swalaah Nini Hukumu Ya Swalaah Yake?
Maswali: Hukmu Za Swalah



ASsalamu alayka sheikh nauliza swali kama ifuatavyo Kuna kijana mmoja aliwahi kuniuliza SWALI: kuwa yeye aliswali swala ya faradhi, ghafla alijikuta misuli yake ya uume (dhakari) imesimama. Je kijana huyu alipaswa kuendelea na swala au swala yake imeharibika?





JIBU:






Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kusimika katika Swalah.







Hakika ni kuwa kusimama kwa misuli ya uume haivunji Swalah, hivyo kuendelea kwake katika kumaliza hiyo Swalah ndio sawa.

Hata hivyo, ikiwa ndani ya Swalah, ya faradhi au ya Sunnah atakuwa ni mwenye kufikiria kuhusu kitendo cha ndoa mpaka dhakari ikasimama Swalah yake itakuwa ni sahihi japokuwa thawabu za Swalah hiyo zitapungua.



Swalah itaharibika tu ikiwa kwa kusimama kwa dhakari atatokwa na maji. Yakiwa ni madhii au manii. Bila shaka ikiwa ni madhii itabidi avunje Swalah akaoshe sehemu ya nguo ambayo imeingia maji hayo pamoja na kuosha dhakari yake.

Na yakiwa ni manii yaliyomtoka itabidi aende akaoge ndio kisha arejee kuiswali tena Swalah hiyo.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Je, Imethibiti Khatwiyb Kukamata Fimbo Katika Khutbah Ya Ijumaa Akiwa Kwenye Minbar?



www.alhidaaya.com





SWALI:



Nini hukmu ya Khatibu kutegemea/kukamatia fimbo/gongo?





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Suala hili la kubeba au kushikilia fimbo au upinde au upanga wakati Khatwiyb wa Ijumaa anatoa khutbah wamekhitalifiana Wanachuoni. Na ikhtilaaf imekuja kwa sababu Ahaadiyth zilizokuja kuhusu suala hilo, wametofautiana usahihi wake. Wengi wanakubali kuwa Ahaadiyth zake hazijathibiti. Wanaoona inafaa jambo hilo, wamesema Ahaadiyth zake zimetiliwa nguvu na zingine hadi kukubalika.



Kuna wanaoona kuwa ni jambo lenye kupendeza, nao ni Wanachuoni wa ki-Maalik, ki-Shaafi'y na ki-Hanbaliy. Na Wanachuoni wa ki-Hanafiy wanaoona ni jambo lenye kuchukiza.



Nao wanaounga mkono wametoa dalili ya Hadiyth ifuatayo:

Kutoka kwa Al-Hakam bin Hazn kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisimama siku ya Ijumaa (kwenye Minbar) akiegemea fimbo au upinde, na kisha akamhimidi Allaah na kumsifu..."

[Abuu Daawuwd. Amesema An-Nawawiy katika "Al-Majmuw'" kuwa ni Hadiyth Hasan, na vilevile kasema hivyo hivyo Al-Albaaniy kwenye "Swahiyh Abiy Daawuwd", lakini Wanachuoni wengine wameidhoofisha na kusema ni Hadiyth dhaifu, na Ibn Kathiyr katika "Irshaad Al-Faqiyh" kasema isnaad yake haina nguvu.]



Anasema Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah):

"Alikuwa hachukui mkononi mwake upanga wala kisicho hicho, bali alikuwa akiegemea upinde au fimbo kabla hajaingia kwenye Minbar. Na alikuwa vitani akiegemea upinde. Na katika Ijumaa akiegemea fimbo, na hakuna kilichohifadhiwa kutoka kwake kuwa akiegemea upanga, na wanayodhania baadhi ya wajinga kuwa alikuwa daima akiegemea upanga, na kwamba hiyo ni ishara kuwa Dini ilisimama kwa upanga. Huo ni ujahili uliopindukia (kwa anayedhania hivyo.

Na hakujahifadhiwa kutoka kwake kuwa baada ya kutoka Minbarini, alikuwa akipanda kwa kutegemea upanga au upinde, au chochote kingine, na wala kabla ya kupanda Minbarini hakuwa akichukua upanga katu. Bali alikuwa akiegemea juu ya fimbo au upinde (katika nyakati zingine)."

[Zaadu Al-Ma'aad, mj. 1, uk. 429]



Katika maneno ya Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah), anaonyesha kuwa haukuwa mwenendo wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuegemea juu ya fimbo au chochote kwenye Khutbah ya Ijumaa akiwa Minbarini.





Na amesema Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) akisherehesha:

"Kauli yake: "Akiegemea juu ya upanga au upinde au fimbo", maana yake: inasuniwa kuegemea wakati wa Khutbah juu ya upanga au upinde au fimbo. Na wakatolea dalili ya Hadiyth inayosimuliwa kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo usahihi wake una walakini. Na tukikadiria usahihi wake, amesema Ibn Al-Qayyim: Hakujahifadhiwa kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kupanda kwake Minbar kuwa alikuwa akiegemea juu ya chochote.

Na katika wajihi wa hilo, kwamba kuegemea kunakuwa kwa ajili ya mahitajio; ikiwa Khatwiyb atahitajia kuegemea juu ya kitu, mfano ni mtu dhaifu anahitaji fimbo kuegemea juu yake, basi itakuwa ni Sunnah, kwa sababu hiyo inamsaidia yeye kusimama ambako huko kusimama ni Sunnah. Na kinachosaidia katika Sunnah nacho ni Sunnah.

Ama ikiwa hakuna mahitajio ya hilo, basi hakuna haja ya kubeba fimbo."

[Ash-Sharh Al-Mumti', mj. 5, uk. 62-63]



Na ameliunga mkono Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) maneno ya Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah), na amekataa kuwa kumethibiti katika Ahaadiyth lenye kujulisha kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akikhutubu juu ya Minbar alikuwa akiegemea upinde au fimbo. Kayaeleza hayo kwenye "As-Silsilatu Al-Ahaadiyth Adhw-Dhwa'iyfah, Hadiyth namba 964]





Kadhalika katika Fatwa nyingine ya Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

"Akihitaji kufanya hivyo kutokana na kuwa yeye ni dhaifu (anahitaji kitu cha kuegemea) basi ni Sunnah kwa sababu kusimama ni Sunnah kwani kinachosaidia Sunnah basi ni Sunnah. Ama ikiwa hakuna haja ya kukamata fimbo basi hakuna haja ya kukamata."

[Majmuw’ Fataawa wa Rasaail, Al-Mujallad 16, Baabu Swalaatil-Jumu’ah]





Na Allaah ni Mjuzi zaidi.
 
Khushuu (Unyenyekevu) Katika Swalah
Maswali: Hukmu Za Swalah
SWALI:

Je, Swalah yako inapungua daraja mfano ukiwa unawaza kuhusu mambo mengine kwenye Swalah, na hata kama unijitahidi usiwaze chochote isipokuwa kuweka akili yako kwenye Swalah?







JIBU

Utajitahidi vile unayoweza kuweka mawazo yako yote katika Swalah ili upate "khushuu" (unyenyekevu) wa Swalah ambao ni muhimu sana. Kwa hiyo utaanza kwa kumlaani ibliys kusema A'udhu Billahi Mina Shaytaanir-Rajiym. Swala yako itakubaliwa hata kama baadhi ya wakati mawazo yako yalikuwa kwengine. Lakini kila ukiweka mawazo yako kwenye Swalah ndio Swalah inakuwa na thawabu zaidi na inahesabika zaidi kuwa ni Swalah nzuri yenye kumridhisha Allaah سبحانه وتعالى. kama alivyotaja kuwa ni miongoni mwa sifa za watu watakorithi Jannah ya Firdaws.

قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ ﴿1﴾ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ ﴿2﴾

1. HAKIKA wamefanikiwa Waumini

2. Ambao ni wanyenyekevu katika Sala zao

Al-Mu'minuun

Ikiwa Kama unapoteza kabisa mawazo wakati wa Swalah nzima basi ni bora kuirudia Swalah, lakini isiwe mazoea kwani itakuwa ni shetani anakuchezea.
 
Kijana Kaunga Swalaah Pembeni Ya Mwanamke Kwenye Chumba Wakiwa Wawili Peke Yao
Maswali: Hukmu Za Swalah
SWALI:
Naombeni kuuliza wiki iliyopita nilikuwa sehemu ambayo ina chumba kimoja cha sala kwa wanawake na wanaume. Kwahiyo wakiwahi wanawake wanaume wanasubiri. Mie wakati naswali akaja kijana mmoja labda alikuwa na haraka akaingia na kusimama safwu moja na mie akaswali. Mie alinikuta katikati ya swala khiyo sikuweza kuikata. Je hapo swala zetu ziliswihi?



Ufafanuzi:
Muulizaji ni mwanamke. Na inavyoonekana, siyo kwamba aliunga swala ya mwanamke, bali alikuja akasimama usawa mmoja na mwanamke



JIBU:
Kwa hali hiyo kama ulivyofafanua hilo swali, jambo hilo halifai kishariy'ah,
Ni haraam mwanamke kuwa faragha na mwanamme asiye Mahram (Maharimu) yake. Na kinyume chake vilevile mwanamme haifai kuwa faragha na mwanamke asiye Mahram wake. Iwe kwenye Swalaah au kwenye mazingira mengine.
Wanachuoni wanaeleza kanuni kuwa, kile kinachopelekea kwenye haraam nacho ni haraam.



Ziko Ahaadith nyingi zenye kuharamisha faragha baina ya jinsiya mbili zisizo na mahusiano ya damu au mke na mume, kuwa faragha.



Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



'Mwenye kumuamini Allaah na siku ya mwisho basi asikae peke yake na mwanamke asiyekuwa na maharimu wake pamoja naye, kwani watatu wao ni Shaytwaan' [Ahmad]



“Hakai mwanamme na mwanamke peke yao (faragha) ila watatu wao ni Shaytwaan”. [At-Tirmidhiy]



Na akasema tena:
“Shaytwaan hutembea kwenye mwili wa binaadamu kama damu (inavyotembea kwenye mishipa)”.



Na akasema tena:
"Asikae faragha mmoja wenu na mwanamke isipokuwa awe pamoja na maharimu wake." [Al-Bukhaariy na Muslim]



Na akasema tena:
"Tahadharini na kuingia kwa wanawake'. Akasema mmoja katika Answaar, 'Ee Mtume wa Allaah, unaonaje jamaa zake mume (shemeji)?' Akajibu: 'shemeji ni mauti." [Al-Bukhaariy na Muslim]



Na akasema tena akiwa kwenye Minbari siku moja:
"Baada ya leo, hapaswi mwanamme yeyote kuingia kwa siri kwa mwanamke ambaye mume wake hayupo, ila isipokuwa awepo mwanamme mwengine au wanaume wawili pamoja naye." [Muslim]



Makusudio hapo, ni kuwa, mwanamme asiingine nyumba ya mwanamke yeyote ambaye ni mke wa mtu, au yule mwanamke ambaye hajaolewa lakini si Mahram yake, ila kuwepo na watu wengine pamoja naye au pamoja na huyo mwanamke. Vilevile mwanamme asiingie mahali wako wanawake watupu ambao si Mahram zake.



Kwa dalili zote hizo, kunaonesha ubaya na uharamu wa mwanamme na mwanamke kuwa faragha peke yao kwenye eneo lolote lile na hata kwenye Swalaah.



Maimaam na Wanachuoni wametoa ufafanuzi zaidi kuhusu hilo, kwa kueleza kuwa, ikiwa wanawake watakuwa wengi na mwanamme ndiye mwenye kuongoza Swalaah, hilo linawezekana lakini ni makruuh. Linawezekana kwa sababu wanaona uwezekano wa kuwepo fitnah wakiwa wengi, si mkubwa kama ilivyo wawili peke yao. Na wanaona makatazo na uharamu ni pale wanapokuwa wawili faragha. Lakini wakiwa wengi, na mwanamme mwenye kuongoza Swalaah ni mtu mwenye kuaminika, basi inakubalika japo kuna karaha ndani yake. Likiepukika pia hilo, basi ni bora zaidi ili kufunga milango na penyo zote za fitnah.



Ama tukirejea kwenye qadhwiyyah hiyo ya muulizaji, ni kuwa kitendo kile kilikuwa hakifai kishariy'ah na wanapaswa wafanye tawbah kwa hilo na kama walikuwa hawajui hukmu basi wajihadhari mbeleni na huyo kijana aelimishwe kwani anaonekana ni Jaahil wa shariy'ah za Dini.



Na Allaah ni Mjuzi zaidi.
 
Kiza Kinaingia Mapema Mno Msimu Wa Baridi Aswali Vipi Magharibi Na Ishaa
Maswali: Hukmu Za Swalah




SWALI:



Asalam Aleykum! Ndugu zetu waislamu, Mwenyezimungu awajaze na awape subra na muendele kutusaidia na maswali yetu. Inshallah.


Swali langu la pili, mimi naishi ujerumani kwa sasa, na wakati umebadilika, kwa mfano, saa kumi na nusu kumekuwa usiku yaani giza limetanda, je nitaswali magharibi saa ngapi na ishaa saa ngapi?.



Tafadhali ningependa munijibu maswali yangu



ASANTENI SANA NA JAZA YENU IKO KWA MWENYEEZI MUNGU:







JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani kwa maswali yako, na hapa tunakupatia majibu yako.





Swalah zote zimewekewa wakati maalumu na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo inatakiwa popote ulipo ufuate mwongozo huo. Swalah ya Magharibi inaingia wakati jua linapozama, hivyo likiwa linazama saa kumi na nusu inabidi uswali wakati huo wala usiwe unangojea ifike wakati ambao watu wa Afrika Mashariki wanaswali.



Nchi nyingi ambazo zina mabadiliko ya masika, wakati wa Swalah unabadilika sana. Wakati wa baridi Swalah ya Magharibi inakuwa mapema kama wakati huo uliotaja lakini wakati wa joto mchana unakuwa mrefu na inawezekana mukawa mnaswali magharibi huko hata saa mbili au tatu usiku.



Na Allah Anajua zaidi
 
Kuchelewesha Swalaah Ya Alfajiri Mpaka Atakapoamka Kwenda Shule inajuzu?
Maswali: Hukmu Za Swalah
SWALI:




Assalam Aleikum ndungu zangu in islam. swali langu linahusu salah. ninaishi na mtoto wa dada yangu ana miaka kumi na mbili na anaswali ALHAMDULLILAH. Salah ya fajr huku kwetu ni saa tisa na dakika hamsini na sunrise saa kumi na moja na dakika hamsini na moja anawesa kuswali saa kumi na mbili saa ya kuenda shule??? JAZAAKA ALLAH KHEYRAN] ASSLAM ALEIKUM] REHMA YA ALLAH SUBHAANA WATA'ALA EWE JUU YENU NDUGU ZANGU IN ISLAM]





JIBU:




Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Swalah na wakati wake. Ni jambo linalofahamika kuwa kila Dini au ideolojia hapa ina kanuni zake ambazo zinafaa kufahamika na kufuatwa na wafuasi wake.




Uislamu kama Dini ina kanuni zake ambazo ni za kipekee katika kila nyanja. Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wameweka kanuni na masharti katika kila Ibadah ili iweze kukubaliwa na kupatiwa thawabu. Swalah si tofauti na Ibadah nyingine. Katika masharti ya kukubaliwa Ibadah yoyote ile ni:




Kuwa na Ikhlaasw na nia njema.
Kufuata kama ilivyofundishwa au kufanywa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).



Na hasa katika Swalah, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia:

"Swalini kama mlivyoniona nikiswali" (al-Bukhaariy).




Katika sharti la kukubaliwa Swalah ni kuiswali kwa wakati wake makhsusi. Ndio kwa ajili hiyo, Allaah Aliyetukuka Amesema:

"Kwa hakika Swalah kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalumu" (4: 103).




Na wenye kuitoa katika wakati wake basi wanangojewa na adhabu kali kama Alivyosema Aliyetukuka:

"Basi adhabu itawathubutikia wanaoswali. Ambao wanapuuza Swalah zao" (107: 4 – 5).




Hivyo, haifai kabisa kwa Muislamu kuitoa katika wakati wake makhsusi uliowekewa. Swalah ya Alfajiri ni kabla ya kuchomoza jua hivyo hata kama ni saa tisa inabidi umuamshe aswali na azoee hivyo kwani huenda kijana huyo wako amebalighi au karibu kubaleghe. Kumuachia hivyo atazoea na ataona kuwa hakuna tatizo lolote la kuchelewesha Swalah hata kama hakuna udhuru wa kisheria. Malezi ya kumzoeza mtoto njia njema na bora ndio yatakayomuweka yeye katika maadili mema na mazuri.




Hatuoni kama itakuwa mashaka makubwa ukimuamsha nusu saa kabla ya hapo, ambayo ni saa kumi na moja na nusu akaswali na kisha akafanya mengine kama kusoma Qur-aan na kujiandaa kwa shule, na kisha akirudi jioni baada ya kula na kuswali akapumzika kidogo.




Kwa hiyo tunakunasihi uwe unamzoeza katika mafunzo hayo ili awe mtoto mzuri zaidi. Na kuswaliwa mapema huko inaonekana muko katika masika ya joto ambamo mchana unakuwa mrefu na hatudhani ya kuwa mwaka mzima wakati unakuwa ni huo. Na hata kama utakuwa huo hatuna budi ila kufuata maagizo ya Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili tupate kuongoka duniani na Akhera.




Allaah Atamwezesha kijana wako kufanya hilo na zaidi ya hilo.




Na Allaah Anajua zaidi
 
Kudhihirisha Kisomo Cha Baadhi Ya Aayah Kwa Sauti Kwenye Swalaah Zisizo Za Sauti
Maswali: Hukmu Za Swalah
SWALI:



Nimeshuhudia Imaamu kwenye Swalaa ya Adhuhuri na Al-'Asri akidhihirisha kisomo cha Aayaat kama mbili hivi, katika Rak'ah mbili za mwanzo.

Nini hukmu ya jambo hili Baaraka Allaahu fiykum.



JIBU:



بسم الله الرحمن الرحيم

Sifa zote njema na za ukamilifu zinamstahiki Allaah Rabb wa walimwengu wote, Swalaah na Salaam zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) Na waliowafuata hao kwa wema mpaka siku ya mwisho.



Bila ya shaka inafaa katika Shariy'ah Imaam kuwasikilizisha Maamuma Aayah moja au mbili au sehemu ya Aayah katika baadhi ya nyakati katika Swalaah ya Adhuhuri na Al-'Asr kutokana na mapokezi yaliyothibiti juu ya hilo kupitia Hadiyth aliyoipokea Al-Imaam Al-Bukhaariy na Muslim katika Swahiyh zao mbili kutoka kwa Swahaba Abuu Qataadah Al-Haarith bin Rib'iy (Radhiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema:

“Alikuwa Nabii wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa 'alaa aalihi wa sallam) akisoma katika Rakaa mbili za mwanzo katika Swalaah ya Adhuhuri na Al-‘Asr Suwrat Al-Faatihah na Suwrah nyinginezo na alikuwa akitusikilizisha Aayah mara nyingine. [Swahiyh Al-Bukhariy (762) na Muslim (451).]



Kuhusu Neno (alikuwa akitusikilizisha Aayah mara nyingine), amesema Al-Imaam Mulla 'Aliy Al-Qaariy (Rahimahu Allaah):

“Amesema At-Twiybiy maana yake alikuwa akiinua sauti yake kwa kuyasoma baadhi ya maneno katika Suwrat Al-Faatihah na Suwrah nyingine kiasi kwamba anasikika kwa hicho akisomacho mpaka hufahamika ni Suwrah gani anaisoma.”

[Mirqaatul-Mafaatiyh, Juz. 2 uk. 688]





Amesema Ibn Hajar (Rahimahu Allaah):

“Kusikika katika baadhi ya maneno kwenye Rakaa mbili za mwanzo katika Swalaah ya Adhuhuri na Al-'Asr kumetokana na wingi wa mazingatio yake wakati anapoisoma Qur-aan akiwa katika Swalaah hadi anafikia kudhirisha baadhi ya maneno au Aayah bila kukusudia, au anafanya hivyo ili apate kubainisha kuwa inafaa kudhihirisha Aayah au baadhi ya maneno katika usomaji ndani ya rakaa hizo. Au anafanya hivyo ili awafahamishe watu kuwa huwa anasoma Suwrat Al-Faatihah na Suwrah nyingine katika Rakaa mbili hizo za mwanzo katika Adhuhuri na Al-'Asr pia kuwasikilizisha baadhi ya maneno na Aayah ili watu wamuige katika hilo.”

Mwisho wa kunukuu.



Amesema Al-Imaam Ibn Al-Jawziy (Rahimahu Allaah) akiizungumzia kauli (Na alikuwa akitusikilizisha Aayah mara nyingine):

“Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa 'alaa aalihi wa sallam) akifanya hivyo katika baadhi ya nyakati kwa kuwa ili iwe kufanya hivyo hakuitoi Swalaah katika asili yake kuwa ni ya siri na si ya Jahri.”

[Kashful-Mushkil, Juz. 2, uk. 142]



Aliulizwa Al-Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah):



Swali:

Hivi inafaa nikadhihirisha kisomo katika Swalaah isiyokuwa ya kudhihirisha?



Jibu:

Sunnah ni kusoma siri katika Swalaah ya siri lakini lau akidhirisha baadhi ya Aayaat si vibaya kwani alikuwa Mtume akiwasikilizisha Maswahaba Aayah baadhi ya nyakati katika Swalaah ya Adhuhuri na Al-‘Asr lakini bora katika Adhuhuri na Al-'Asr ni kusoma kwa siri na katika Swalaah za usiku ni kusoma kwa kudhihitisha na katika Swalaah ya Alfajiri pia.

[Fataawa Nuurun 'Alaa Ad-Darb, Juz. 8, uk. 224-225]





Na amesema Al-Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) akielezea hikmah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa 'alaa aalihi wa sallam) kuwasikilizisha Swahaba baadhi ya maneno au Aayah katika Swalaah ya Adhuhuri na Al-‘Asr ima ili awafahamishe kuwa alikuwa akisoma Qur-aan baada ya Suwrat Al-Faatihah, au awazindue kwa kwa namna fulani kwa sababu Imaam anapodhihirisha kisomo katika Swalaah ya siri basi watu huzinduka.

[Liqaau Al-Baabi Al-Maftuwh, juz. 6, uk. 101]



Tunatumai kwa Tawfiyq ya Allaah hapo tutakuwa tumejaribu kulijibu Swali lako.
 
Kuelekea Wapi Kuswali Ikiwa Hujui Qiblah Kiko Wapi?
Maswali: Hukmu Za Swalah

SWALI:

Ukiwa umehamia mahali ugenini na hujui kibla unaelekea wapi? NI jinsi gani unaweza kujua kibla kilipo kwa kuangalia jua linapochomoza au linapozama???




JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Ni muhimu kwa Muislamu anaposafiri sehemu ya ugenini angalau ajue jiografia fupi ya sehemu kama hiyo ili asipate shida katika ibadah zake za Swalah anapofika huko. Al-Ka‘bah ndiyo tunayoelekea wakati wa Swalah na Alhamdullillahi kwa sasa ipo miswala ambayo ina dira (‘compass’) pamoja na kijitabu kidogo kinacho kufahamisha namba ya kuelekeza ukiwa katika miji tofauti ulimwenguni. Hii ni njia moja rahisi ya kukutoa katika usumbufu aina yoyote.

Ikiwa huna mswala kama huo basi ni muhimu ujue jiografia japokuwa kidogo. Ikiwa upo Afrika Mashariki, kawaida Qiblah ni kaskazini, hivyo mkono wako wa kuume ukielekea kunapochomoza jua na mkono wa kushoto kunapotua jua basi uso wako utakuwa umeelekea Makkah. Kukusaidia zaidi ni mpaka tujue uko wapi.

Na Allaah Anajua zaidi
 
Masharti Ya لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ مُحَمد رَسُول الله

(Hapana Mwabudiwa Wa Haki Isipokuwa Allaah, Muhammad Ni Rasulu Wa Allaah)



Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (حفظه الله)

Kutoka Kitaab ‘Aqiydah At-Tawhiyd



Alhidaaya.com





Hakika Himdi Anastahiki Allaah, Tunamshukuru na kumuomba msaada, na tunamtaka maghfirah, na tunajilinda kwake kutokana na shari za nafsi zetu, na makossa ya ‘amali zetu, atakaemuongoza Allaah hakuna wa kumpoteza, na atakaempoteza hakuna wa kumuongoza, na ninashuhudilia ya kwamba hakuna apasae kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allaah Peke Yake Hana mshirika, na ninashuhudilia yakuwa Muhammad ni mja wake na ni Rasuli wake (صلى الله عليه وآله وسلم)





Ammaa baad. Hii ni sherehe kwa muhtasari ya Masharti ya



لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ

Laa Ilaaha Illa Allaah (hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah), yaliyoandikwa na Shaykh: Swaalih Fawzaan(حفظه الله) kwenye kitabu chake cha: ‘Aqiydah At-Tawhiyd. Tunamuomba Allaah (عز وجل) Anufaishe kwa kitabu hicho.





Masharti Ya لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ





Ni lazima katika Shahaadah ya لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ yapatikane masharti saba, na hatoweza kunufaika mtamkaji wa shahada hiyo mpaka zikusanyike kwake sharti zote.



Hizo sharti kwa ujumla ni:





Sharti Ya Kwanza: 'Ilmu (Elimu, Maarifa, Ujuzi, Utambuzi), inayo ondosha ujinga.





Sharti Ya Pili: Yaqini, inayoondosha shaka.





Sharti Ya Tatu: Kukubali, kunakozuia kupinga.





Sharti Ya Nne: Kunyenyekea, kunakopinga kuacha.





Sharti Ya Tano: Ikhlaasw, inayopinga kumshirikisha.





Sharti Ya Sita: Ukweli, unaopinga kukadhibisha.





Sharti Ya Saba: Kupenda, kunako pinga chuki.





Ama tafsili ya masharti haya ni kama ifuatavyo:





Sharti Ya Kwanza: 'Ilmu (Elimu, Maarifa, Ujuzi, Utambuzi).





Anakusudia 'Ilmu kwa maana yake inayokusudiwa, maana inayopinga na inayothibitisha, Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):



إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ﴿٨٦﴾

Na wala wale wanaowaomba badala Yake hawana uwezo wa kumiliki uombezi isipokuwa yule aliyeshuhudia kwa haki nao wanajua. [Az-Zukhruf: 86]



Ameshuhudia kwa لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ilihali wanajuwa kwa nyoyo zao, kile kilichoshuhudiwa na ndimi zao, na lau mtu akitamka bila kujua maana yake, hiyo Shahaada haitamnufaisha, kwa sababu hajaizingatia ile maana inayo julishwa na لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ.







Sharti Ya Pili: Yaqini:



Nayo ni kuwa aliyeitamka ana yaqini na maana inayojulishwa na tamko hilo, na kama atatia shaka kwenye maana ya لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ basi neno hilo halitamsaidia na hatopata manufaa yake, anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ لَمْ يَرْتَابُوا

Hakika Waumini ni wale waliomwamini Allaah na Rasuli Wake, kisha wakawa si wenye shaka [Al-Hujuraat: 15]



Akiwa mwenye mashaka mtu huyo huwa ni mnafiki. Na katika Hadiyth:



وقال النبي صلى الله عليه وسلم مَنْ لَقِيتَ مِنْ وَرَاء هَذَا الْحَائِطِ يَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاّ اللّهُ مُسْتَيْقِنا بِهَا قَلُبُهُ فَبَشّرْهُ بِالْجَنّةِ))

((Ee Abaa Hurayrah (akanipa viatu vyake) Nenda na viatu vyangu hivi, utakayemkuta nyuma ya ukuta huu akiwa anakiri moyoni na anashuhudia kwamba: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ )laa ilaaha illa Allaah( hapana muabudiwa wa haki ila Allaah akiwa amethibitika nayo moyoni, mbashirie Jannah)) [Muslim]



Yeyote ataekosakuwa na yaqiini kwenye moyo wake hatostahiki kuingia Jannah.






Sharti Ya Tatu: Kukubali



Kile kinachopelekea (kumaanisha) kwenye hili neno, ambayo ni kumwabudu Allaah Pekee, na kuacha kila aina ya ‘ibaadah isiyokuwa ya Allaah (عز وجل), atakayetamka bila kukubali moyo wake, na bila kulazimiana na neno hilo, huyo atakuwa kwenye kundi ambalo amesema Allaah (سبحانه وتعالى) kuhusu hao:



إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ يَسْتَكْبِرُونَ ﴿٣٥﴾ وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ ﴿٣٦﴾



Hakika wao walipokuwa wakiambiwa: Laa ilaaha illa Allaah, Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hutakabari. Na wanasema: Je, sisi kweli tuache waabudiwa wetu kwa ajili ya mshairi majnuni?! [Asw-Swaffaat: 35 – 36]



Na ndio kama hivi, hali ya waabudia makaburi, kwani wao wanatamka لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ na wala hawaachi kuabudia makaburi, hawa wanakuwa hawajakubali bado maana ya لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ.







Sharti Ya Nne: Kunyenyekea.



Kwa kile kilichojulishwa. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):



وَمَن يُسْلِمْ وَجْهَهُ إِلَى اللَّـهِ وَهُوَ مُحْسِنٌ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ

Na anayeusalimisha uso wake kwa Allaah, naye akawa ni mtenda ihsaan, basi kwa yakini ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika. [Luqmaan: 22]



العُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ



Kishikio madhubuti ni: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ



Na maana ya

يُسْلِمْ وَجْهَهُ



anayeusalimisha uso wake ni: Kunyenyekea kwa Allaah kwa Ikhlaasw.







Sharti Ya Tano: Ukweli.



Mtu anatakiwa atamke neno la لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ kwa moyo wake ukiwa unasadikisha kile kinachotamkwa na ulimi wake, kama atatamka kwa ulimi ilihali moyo hausadikishi hilo, mtu huyu anakuwa ni mnafiki, anasema Allaah (سبحانه وتعالى):



وَمِنَ النَّاسِ مَن يَقُولُ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَبِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَمَا هُم بِمُؤْمِنِينَ ﴿٨﴾ يُخَادِعُونَ اللَّـهَ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَمَا يَخْدَعُونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ ﴿١٠﴾

Na miongoni mwa watu wako wasemao: Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho hali ya kuwa si wenye kuamini. (Wanadhani) Wanamhadaa Allaah na wale walioamini lakini hawahadai ila nafsi zao na wala hawahisi. Ndani ya nyoyo zao mna maradhi na Allaah Akawazidishia maradhi, na watapata adhabu iumizayo kwa waliyokuwa wakiyakadhibisha. [Al-Baqarah: 8 – 10]







Sharti Ya Sita: Ikhlaasw:



Nako kusafisha ‘amali kutokana na takataka za ushirikina, asikusudie kwa kauli yake tamaa fulani katika tamaa za kidunia, wala Riyaa (kujionyesha kwa watu), wala kutaka umaarufu kwa watu, imekuja katika Hadiyth:



عن عِتْبَانَ بْن مَالِكٍ الْأَنْصارِيَّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ قَدْ حَرَّمَ عَلَى النَّارِ مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ يَبْتَغِي بِذَلِكَ وَجْهَ اللَّهِ ))



Imepokelewa kutoka kwa ‘Itbaan bin Maalik Al-Answaariyy Radhhwiyaa1 kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Ameharamisha An-Naar (Moto) kwa anayesema: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ (laa ilaaha illa Allaah) akitafuta Wajihi wa Allaah.” [Al-Bukhaariy (425), Muslim (33)]







Sharti Ya Saba: Kupenda:



Nako ni kulipenda Neno la لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ pamoja na maana yake na kuwapenda wanaolifanyia kazi Neno hilo, kwa mujibu wa maana yake, Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):



وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ

Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah na kuwafanya kuwa ni wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. [Al-Baqarah: 165]





Watu wa لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ wanampenda Allaah mapenzi yenye Ikhlaasw, na watu washirikina wanampenda Allaah na wanapenda vitu vingine na hivi huwa vinapinga maana na malengo yake.





Masharti Ya Shahaadah مُحَمد رَسُول الله





Masharti ni kama yafuatayo:





Sharti Ya Kwanza:



Kukiri (kukubali) Risala yake na kuiitakidi (kuuamini) katika moyo.





Sharti Ya Pili:



Kutamka na kukiri kwa dhahiri (kutamka) kwa ulimi.





Sharti Ya Tatu:



Kumfuata Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kukifanyia kazi alichokuja nacho, ambayo ni haki, na kuacha aliyoyakataza ambayo ni baatil.





Sharti Ya Nne:



Kumsadikisha kwa yale aliyoyaelezea, katika mambo ya ghaib (yaliyo jificha), yaliyopita na yajayo.





Sharti Ya Tano:



Kumpenda yeye zaidi ya kuipenda nafsi mali, watoto wazazi na watu wote.





Sharti Ya Sita:



Kuitanguliza kauli yake kabla ya kauli ya mtu yoyote yule, na kuzifanyia kazi Sunnah zake.




Tafsiyr ya Imaam As-Sa’diy (رحمه الله) kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):



فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ﴿١٩﴾

Basi jua kwamba: hapana muabudiwa wa haki ila Allaah, na omba maghfirah kwa dhambi zako na kwa ajili ya Waumini wa kiume na Waumini wa kike. Na Allaah Anajua harakati zenu huku na kule na pahala penu pa kupumzikia. [Muhammad (47:19)]





Yanayopelekea Kutambua Ujuzi Wa Laa Ilaaha Illa-Allaah:





Kulijua ipasavyo neno “Laa Ilaaha Illa Allaah” kunahitajia moyo kulikiri na kulijua, kwa maana kwamba Rasuli (pamoja na sisi) anatakiwa alijue neno hilo inavyotakikana, halafu akamilishe ujuzi huo kwa kutenda kwa mujibu wa vipengele vyake.



Ilimu hiyo ambayo Allaah (سبحانه وتعالى) Ameiamuru - ambayo ni ilimu ya Tawhiyd (Kumpwekesha Allaah) ni fardhw ‘ayn (faradhi kwa kila mtu binafsi), kwa kila mwanaadam, na haisamehewi kwa yeyote yule, na haijalishi yeye ni nani. Bali kila mtu amewajibika kuijua. Na njia ya kujua kwamba hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye (Allaah عزّ وجلّ) ni kwa haya yafuatayo:





(i) Ya kwanza bali iliyo kuu kabisa ni kuzingatia Majina Yake (Allaah عزّ وجلّ) na Sifa Zake na Matendo Yake yanayodalilisha Ukamilifu Wake, na U’adhwama Wake, na Ujalali Wake, kwani yanampelekea mtu kufanya jitihada ya kujisabilia Kwake, na kumwamudu Rabb Anayemiliki Majina Mazuri Kabisa Na Sifa, na Ambaye Himdi zote ni Zake, Utukufu, Ujalali na Uzuri.





(ii) Kujua kwamba Yeye (Allaah عزّ وجلّ) Ndiye Muumbaji Pekee na Msimamizi. Hivyo basi mtu atambue kuwa Yeye (Allaah عزّ وجلّ) Ndiye Pekee Mwenye Kustahiki kuabudiwa.





(iii) Kujua kwamba Yeye (Allaah عزّ وجلّ) Ndiye Pekee Mwenye Neema za dhahiri (zinazoonekana) na za siri (zisizoonekana) za kidini na za kidunia. Kujua hilo kunaulazimisha moyo kushikamana Naye na Kumpenda na kujisabilia Kwake Yeye Pekee, Asiye na mshirika.





(iv) Yale tunayoyaona na kuyasikia juu ya malipo kwa mawalii Wake waliosimamisha Tawhiyd Yake (Allaah عزّ وجلّ), kama vile ushindi na neema za haraka za hapa duniani, pamoja na adhabu zake kwa maadui Zake wanaomshirikisha, hayo yote ni chachu ya kujua kwamba Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Ndiye Pekee Anayestahiki kuelekezewa ibaada zote.





(v) Kujua hali halisi ya masanamu na mizimu na wanaolinganishwa sawa na Allaah (سبحانه وتعالى) ambao wanaabudiwa pamoja na Allaah, na kufanywa ni waabudiwa, na kwamba hao ni wenye upungufu kwa kila upande, ni madhaifu wa dhati, hawana uwezo wa kujinufaisha au kujidhuru nafsi zao wala kwa wanaowaabudia, wala hawana uwezo wa kufisha, wala kuhuisha, wala kufufua, wala hawawezi kuwanusuru wanaowaabudia, wala hawawezi kuwanufaisha hata kwa uzito wa chembe ya atomu kwa kuleta kheri au kukinga shari. Basi kwa kujua hayo, kunawajibisha kujua kwamba hapana Mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba miungu inayoabudiwa badala Yake (Allaah عزّ وجلّ) ni ya uongo.





(vi) Vitabu vya Allaah vyote vimeafikiana juu ya hilo (Neno la Tawhiyd; laa ilaaha illa-Allaah) na vyote kimoja baada ya kingine vimeelezea hilo.





(vii) Viumbe bora kabisa ambao wamekamilika katika khulqa (tabia) njema, akili, busara, fikira sahihi, hikma, na ilimu, yaani Rusuli wa Allaah na Manabii na ‘Ulamaa wenye taqwa, wameshuhudia hayo (kwamba laa ilaaha illa-Allaah).





(viii) Ishara za kilimwengu na za kinafsi (namna tulivyoumbwa) Alizozisimamisha Allaah na ambazo zinaonyesha kwamba Yeye Ni Mmoja Asiye na mshirika, ndizo dalili kubwa kuliko zote. Dalili hizi kwa namna Alivyoziumba kwa uzuri wa ajabu, kwa umadhubuti usiyo na kombo, na kwa uumbaji wa ajabu, zote zinamtangaza Allaah kwa jinsi zilivyo kwa namna ya kipekee kabisa isiyo na ruwaza. Ishara hizi ambazo Allaah Amekithirisha kwazo kuwazindusha viumbe, Akiwajulisha kwamba hakuna mwingine wa kuabudiwa isipokuwa Yeye, Akazieleza katika Kitabu Chake na Akazitawanya kote kote, ikiwa mtu atataamuli kwa kina baadhi yake tu, basi ni lazima atapata yakini na ujuzi wa kweli wa maana ya kumpwekesha Allaah (Tawhiyd). Sasa hali itakuwa vipi ikiwa dalili zote zitakusanyika pamoja, zikaoana, zikakubaliana na zikasimama toka pande zote?! Hapa ndipo pale iymaan na ujuzi wa hilo vinapojikita na kutuama ndani ya moyo wa mja na kuwa mithili ya mlima mrefu usiyoweza kutikiswa na shubha au dhana hewa, bali huzidi nguvu na ustawi kila mtu anapokutana na upotoshaji na propaganda chafuzi. Mwisho wa yote, unabakia mlango mkubwa na mpana zaidi wa kumwezesha mtu kuijua Tawhiyd kwa mapana yake na marefu yake. Mlango huu ni kuizingatia Qur-aan Tukufu na kuzitafakari Aayaat zake, na hili halipatikani toka chanzo kingine chochote isipokuwa humo.

[Tafsiyr As-Sa’diy]
 
أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Sifa Zake



Alhidaaya.com



000-Utangulizi





بِسْمِ الله الرَّحْمنِ الرَّحِيم

الْحمْدُ لِلَّه وَالصَّلاةُ وَالسِّلامُ عَلى خَاتم الأنْبِيَاء وَالْمُرْسَلِين، الْمَبْعُوثُ رَحْمَةً لِلْعَالَمِين، مُحَمَّد وَعَلى آلِه وَأصْحابِه أجْمَعِين وَمَنْ تَبِعَهُمْ بِإِحْسَانٍ إِلَى يَوْمِ الدِّينِ.



Himdi zote Anastahiki Allaah, Swalaah na Salaam ziwe juu ya Nabiy na Rasuli wa mwisho, aliyetumwa awe rahmah kwa walimwengu, Muhammad, pamoja na ahli zake na Maswahaba zake wote, na wanaowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Malipo.



Al-Asmaaul-Husnaa imetajwa mara nne katika Qur-aan katika kauli zifuatazo za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ

Sema; “Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah). Vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. [Al-Israa 17: 110]



Na pia:

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ﴿٨﴾

Allaah, hapana ilaaha (muabudiwa wa haki) ila Yeye. Anayo Majina Mazuri kabisa.[Twaahaa 20: 7-8]

Na:

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa katika Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-A’raaf 7: 180]



Na pia:



هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٤﴾

Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa, kinamsabbih Pekee viliyoko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Hashr (59:22-24)]




Kumpwekesha Allaah Katika Majina Yake Na Kuthibitisha Sifa Za Allaah (سبحانه وتعالى) Na Ndio Aqiydah Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah (سبحانه وتعالى) Na Sifa Zake:




Aqiydah ya Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah kuhusiana na Majina Mazuri kabisa ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Sifa Zake ni Tawqiyfiyyah; Yanathibitishwa Aliyoyathibitisha Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى) katika Qur-aan na Sunnah bila kuzifanyia Ta'twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala Tamthiyl (kumithilisha, kufafanisha, kulinganisha), wala Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah), wala Tahriyf (kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutoa maana isiyo sahihi).




Hivyo basi, Allaah (سبحانه وتعالى) Anaposema kuwa Ana Qudra (Uwezo), na sisi tunaamini kuwa Anao Uwezo. Anaposema Yeye ni Qawiyy (Mwenye Nguvu), na sisi tunaamini kuwa Ana nguvu. Anaposema kuwa Anaona, na sisi tunaamini kuwa Anaona. Anaposema kuwa Anasikia, na sisi tunaamini kuwa Anasikia. Lakini Sifa hizo za Uwezo Wake, au Nguvu Zake, au Kuona Kwake au Kusikia Kwake hazifanani kabisa na kiumbe chochote kile! Na Anaposema kuwa Anayo Macho, na sisi tunaamini kuwa Anayo Macho. Na Anaposema kuwa Anayo Mikono na sisi tunaamini kuwa Anayo Mikono, na Anaposema kuwa Anao Wajihi, na sisi tunaamini kuwa Anao Wajihi. Lakini Macho Yake au Masikio Yake au Wajihi Wake, hakuna kabisa mfano Wake kwa kiumbe chochote kile kama Anavyosema (سبحانه وتعالى):


لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١١﴾

Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ndiye Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote. [Ash-Shuwraa 42: 11]



Kwa hiyo Anapotujulisha kuwa Yeye ni Al-‘Aliym (Mjuzi wa yote daima), hatuwezi kusema hivyo kwa bin Aadam. Na kadhalika hatuwezi pia kufananisha Sifa Zake nyinginezo kwa kiumbe chochote kile wala kumfananisha au kumlinganisha, au kumshabihisha Yeye kwa dhati Yake au Sifa Zake na yeyote yule Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):



فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٧٤﴾

Basi msimpigie mifano Allaah! Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui. [An-Nahl 16: 74]



Kutokuzithibitisha sifa ambazo Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amejipa ni kuzigeuza na kuzipotoa; Anaonya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):



وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopotoa katika Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-A’raaf 7: 180]



Hiyo ndiyo ‘Aqiydah sahihi kabisa waliyoitakidi Salaf wa ummah na ndivyo ipasavyo kuzikubali Sifa zote za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) bila ya kukisia kwa akili zetu namna yake au mfano wake, wala kuogopa kuzithibitisha zilivyo kwa kukhofia kufananisha na viumbe. Kuzithibitisha vile vile zilivyokuja kutoka katika Kitabu Chake kama Alivyoziita Mwenyewe (‘Azza wa Jalla) na Alivyotaka Yeye, hiyo ndio salama kwetu. Tujisalimishe na Alivyojithibitishia Mwenyewe na alivyothibitisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwani akili zetu haziwezi kufikia upeo wa utambuzi na ujuzi wa Sifa Zake (‘Azza wa Jalla).



Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:



وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَـٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا ﴿٣٦﴾

Na wala usiyafuate (kusema au kushuhudia) yale usiyokuwa nayo elimu. Hakika masikio na macho na moyo; vyote hivyo vitakuwa vya kuulizwa (Siku ya Qiyaamah). [Al-Israa 17:36]



Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا ﴿١١٠﴾

Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawawezi kuzunguka elimu Yake. [Twaahaa 20: 110]





Umuhimu wa kuyajua na kujifunza Majina Mazuri kabisa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na Sifa Zake:





1-’Ilmu kuhusu Majina ya Allaah na Sifa Zake ni kumtambua Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na kutambua Utukufu Wake.



Unapotaka kutaamali na mtu, hakuna shaka kuwa utataka kujua jina lake, kun-yah yake na kuulizia khabari zake upate ufahamu bayana kumhusu yeye hata uridhike unapotaamali naye. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ametuumba na Ndiye Anayeturuzuku kila kitu na tunakhofia ghadhabu Zake na tunataraji rahmah Zake Atughufurie madhambi yetu Asituadhibu. Kwa hiyo, hakuna budi kutambua yanayomridhia ili Naye Aridhike na sisi, na pia kutambua yanayomghadhibisha ili tujiepushe nayo. Kama vile ambavyo huwezi kumpenda usiyemjua, hali kadhaalika huwezi kumkhofu na kumpenda Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa haki apasayo kukhofiwa na kupendwa isipokuwa kwa kumtambua Utukufu Wake, na njia mojawapo ni kutambua Majina Yake Mazuri kabisa na Sifa Zake. Usipomtambua ukampenda, Naye Hatokutambua wala kukujali.



Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):



وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّـهَ فَأَنسَاهُمْ أَنفُسَهُمْ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ﴿١٩﴾

Na wala msiwe kama wale waliomsahau Allaah, Naye (Allaah) Akawasahaulisha nafsi zao, hao ndio mafasiki. [Al-Hashr 59: 19]



Hivyo, kumtambua Allaah kunapelekea katika kumpenda, na kumkhofu, na kutawakali Kwake, na kumsafishia niyyah (ikhlaasw) katika matendo na kutaraji rahmah Yake.





2-’Ilmu Ya Majina ya Allaah na Sifa Zake ni ’Ilmu ya asasi.



’Ilmu kuhusu Majina ya Allaah na Sifa Zake ni’ilmu ya asasi, kwani ni aina ya tatu ya Tawhiyd. Na tawhiyd ndio jambo kuu walilokuja nalo Rusuli wote katika ulinganiaji wao. Na ni ’ilmu bora na tukufu kabisa kuitambua. Na ndio lengo kuu na kuumbwa kwa kumpwekesha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) katika ’ibaadah.





3-’Ilmu ya Majina ya Allaah na Sifa Zake Inazidisha Iymaan.



’Ilmu kuhusu Majina ya Allaah na Sifa Zake ni sababu ya kuzidisha iymaan kama alivyosema Imaam As-Sa’dy (Rahimahu Allaah): “Hakika kuamini Asmaa Allaah Al-Husnaa na utambuzi wake, inajumuisha aina tatu za tawhiyd; Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah, Tawhiyd Al-Uluwhiyyah (’Ibaadah) na Tawhiyd Asmaa wasw-Swifaat. Na aina hizi ndio roho ya iymaan na ndio furaha halisi na kitulizo cha dhiki za moyo, na ndio asili yake na lengo lake. Basi kila mja anapozidi kutambua maarifa ya Asmaa Allaah na Sifa Zake ndipo inapozidi iymaan yake na kuthibitika yakini yake. [At-Tawdhiwyh Wal-Bayaan Lishajaratil-Iymaan Lis-Sa’dy, uk. 41]





4-’Ilmu kuhusu Majina ya Allaah na Sifa Zake ni sababu ya kupata Jannah:



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّ لِلَّهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ اسْمًا مِائَةً إِلا وَاحِدًا مَنْ أَحْصَاهَا دَخَلَ الْجَنَّةَ))

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ’anhu) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hakika Allaah Ana Majina tisini na tisa, atakayejifunza moyoni ataingia Jannah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Ahswaahaa imekusudiwa: Kuyafahamu maana Zake, kuyahifadhi, kufanyia kazi, kuomba du’aa kuyatumia kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. [Al-A’raaf 7: 180]



Imaam Ibn ’Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema: Ahswaahaa haimaanishi kuwa ni kuyaandika Majina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwenye karatasi na kuyakariri mpaka mtu aweze kuyahifadhi bali inamaanisha:

Kujifunza kuyatamka.
Kufahamu maana Zake.
Kumwabudu Allaah kwayo, kwa njia mbili:


Kwanza: Kumuomba du’aa kwayo kwa sababu Allaah Anasema:

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. [Al-A’raaf 7: 180]



Kwa hivyo, uyafanye kuwa ni wasiylah (kurubisho) ya du’aa yako, hivyo utachagua Jina linalowafikiana na haja yako. Unapotaka kuomba maghfirah useme: ”Yaa Ghafuwru nighufurie.” Na si kusema: ”Yaa Shadiyd Al-’Iqaab Ighfir-liy (Ee Mkali wa kuakibu nighufurie!)” kwani hii inakuwa kama ni istihzaa. Linalopasa (ikiwa utamwita Allaah hivyo) useme ”Ee Mkali wa kuakibu, Niepushe na ikabu Yako.”





Pili: Katika ’ibaadah zako, vitendo viashirie Majina Yake. Kama Ar-Rahiym (Mwenye kurehemu) kusudio lake ni rahmah, basi fanya vitendo vyema vitakavyosababisha kupata rahmah ya Allaah.





Hiyo ndio maana ya ahswaahaa. Basi itakapotekelezwa hayo ndipo itakapostahiki kuingizwa Jannah.” [Majmuw’ Fataawa wa Rasaail Ibn ’Uthaymiyn (1/74)]

’Ulamaa wamekubaliana kwamba Majina ya Allaah si tisini na tisa pekee bali yako zaidi ya hayo kwa dalili ya Hadiyth:





عن عَبْدِ اللَّهِ بن مسعود قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا أَصَابَ أَحَدًا قَطُّ هَمٌّ وَلا حَزَنٌ فَقَالَ: اللَّهُمَّ إِنِّي عَبْدُكَ، وَابْنُ عَبْدِكَ، وَابْنُ أَمَتِكَ، نَاصِيَتِي بِيَدِكَ، مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤُكَ، أَسْأَلُكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّيْتَ بِهِ نَفْسَكَ، أَوْ عَلَّمْتَهُ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ، أَوْ أَنْزَلْتَهُ فِي كِتَابِكَ، أَوْ اسْتَأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الْغَيْبِ عِنْدَكَ، أَنْ تَجْعَلَ الْقُرْآنَ رَبِيعَ قَلْبِي، وَنُورَ صَدْرِي، وَجَلَاءَ حُزْنِي، وَذَهَابَ هَمِّي، إِلا أَذْهَبَ اللَّهُ هَمَّهُ وَحُزْنَهُ وَأَبْدَلَهُ مَكَانَهُ فَرَجًا)) فَقِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَلا نَتَعَلَّمُهَا؟ فَقَالَ: ((بَلَى يَنْبَغِي لِمَنْ سَمِعَهَا أَنْ يَتَعَلَّمَهَا)) صححه الألباني في السلسلة الصحيحة (199)



Ibn Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yeyote atakayefikiwa na dhiki na huzuni kisha akasema:



Allaahumma inniy ‘abduka, ibnu-‘abdika, ibnu-amatika, naaswiyatiy Biyadika, maadhwin fiyya hukmuka, ‘adlun fiyya qadhwaauka, as-aluka bikullismin huwa Laka, sammayta bihi Nafsaka aw Anzaltahu fiy Kitaabika, aw ‘Allamtahu ahadan min Khalqika, awis-staa-tharta bihi fiy ‘ilmil-ghaybi ‘In-daka, an Taj-’alal-Qur-aana rabiy’a qalbiy, wanuwra swadriy, wajalaa-a huzniy, wa dhahaaba hammiy.



Ee Allaah hakika mimi ni mtumwa Wako, mtoto wa mtumwa Wako, mtoto wa kijakazi Chako, utosi wangu uko Mikononi Mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako, ni usawa kwangu kunihukumu Kwako, nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako Ulilojiita Mwenyewe au Uliloliteremsha katika Kitabu Chako, au Ulilomfundisha yeyote yule kati ya viumbe Vyako, au Ulilolihifadhi Wewe mwenyewe (na kujihusisha kulijua) katika ’ilmu ya ghayb Kwako, nakuomba Ujaalie Qur-aan kuwa ni rabiy' (uhuisho, raha, furaha na ustawisho) wa moyo wangu na nuru ya kifua changu, na ufumbuzi wa huzuni yangu, na sababu ya kuondoka wahka wangu. - Akisema hivyo hakuna isipokuwa Allaah Atamuondoshea dhiki na huzuni na Atambadilisha badala yake faraja.” Ikasemwa: Ee Rasuli wa Allaah! Je tujifunze? Akasema: ”Ndio, inampasa kwa mwenye kuisikia kujifunza.” [Ameipokea Ahmad (1/391) [452], Al-Haakim (1/509) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (199) na Al-Kalimi Atw-Twayyib (124)]





Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:



“Hii (du’aa katika Hadiyth hiyo) ni dalili kwamba Allaah Ana Majina zaidi ya tisini na tisa.” [Majmu’w Al-Fataawa (6/374)]





Na Imaam Ibn ’Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema alipoulizwa kuhusu idadi ya Majina ya Allaah:



“Majina ya Allaah hayana idadi maalumu. Na dalili ni kauli ya (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh:



((Ee Allaah hakika mimi ni mtumwa Wako, mtoto wa mtumwa Wako, mtoto wa kijakazi Chako, utosi wangu uko Mikononi Mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako, ni usawa kwangu kunihukumu Kwako, nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako Ulilojiita Kwako Mwenyewe au Uliloliteremsha katika Kitabu Chako, au Ulilomfundisha yeyote yule kati ya viumbe Vyako, au Ulilolihifadhi Wewe mwenyewe (na kujihusisha kulijua) katika ’ilmu ya ghayb Kwako)).





Basi ambayo Aliyoyahifadhi Allaah katika ’ilmu ya ghayb hayawezi kujulikana, na ambayo hayajulikani hayawezi kuhesabika. Ama kauli ya (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

”Hakika Allaah Ana Majina tisini na tisa, atakayejifunza moyoni ataingia Jannah.”





Haimaanishi kuwa Hana isipokuwa Majina haya tu. Lakini inayokusudiwa ni kwamba atakayehifadhi Majina haya tisini na tisa basi ataingia Jannah. Kauli yake: Man Ahswaahaa (atakayejifunza kwa moyo) ni kamilisho la sentensi ya mwanzo na si kiendelezo kilichojitenga, ni kama vile Waarabu wanaposema: “Nina farasi mia ambao nimewaandaa kwa jihaad kwa ajili ya Allaah”; Hii haimaanishi kwamba msemaji ana farasi mia tu bali hawa mia ndio aliowaandaa kwa ajili ya jambo hili.” [Majmuw’ Fataawa Ibn ‘Uthaymiyn (1/122)]





Kazi hii ya ku-tarjam na kuelezea Majina ya Allaah na Sifa Zake tuliyoyakusanya humu hakika ni mukhtasari tu kwa sababu ’ilmu yake ni pana mno haiwezekani kuijumuisha kwa makala fupi kama hizi. Lakini tunatumai kuwa mukhtasari huu utatoa maarifa ya kumtoshelezea kiasi msomaji kutambua maana za msingi za Majina ya Allaah na Sifa Zake.





Haya ndio Ambayo Allaah Ametuwezesha kwa tawfiyq Yake, huku tukimuomba Ajaalie kazi hii iwe yenye ikhlaasw Kwake na ilete manufaa kwa jamii na Atutakabalie. Aamiyn.





Alhidaaya.com
 
أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Sifa Zake



Alhidaaya.com



الله

001-ALLAAH









Allaah: Mwenye Uluwhiyyah (Anayestahiki kuabudiwa Pekee bila kumshirikisha) na Al-‘Ubuwdiyyah (Unyenyekevu, mapenzi, khofu ya adhabu za Allaah na kutaraji rahma za Allaah, utiifu na udhalili kwa Allaah Aliyetukuka, na kutovuka mipaka Yake, na kutekeleza maamrisho Yake na kujizuia na makatazo Yake, kwa kujikurubisha kwa Allaah na kutaka thawabu Zake na kujihadhari na ghadhabu na ikabu Zake)





Mwenye kustahiki kupwekeshwa katika kuabudiwa kwa Alivyojisifu kwa Sifa za Uwluwhiyyah nazo ni Sifa za ukamilifu.



Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Mwenye Kustahiki kurejewa kwa mapenzi, kwa unyeyenyekevu, kwa khofu, matumaini, matarajio, kuadhimishwa na kutiiwa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):



اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kuzunguka chochote katika elimu Yake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye Uluwa, Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa. [Al-Baqarah 2: 255]



Maana ya Allaah kilugha: Allaah; Asili yake ni Al-Ilaah, na Al-Ilaah katika lugha ya Kiarabu ina maana nne:



Kwanza: Al-Ma’buwd: Mwenye kuabudiwa. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ ۚ

Na Yeye Ndiye Muabudiwa wa haki mbinguni na ardhini [Az-Zukhruf 43: 84]



Pili: Mwenye kukimbiliwa katika hali ya khofu:



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ ﴿٧٤﴾

Na wamejichukulia badala ya Allaah miungu (ya uongo) ili (wakitumaini) watawanusuru! [Yaasiyn 36: 74]



Yaani; Wanategemea wawanusuru dhidi ya maadui wao, Waarabu wakawa wanaelekea miungu yao kuomba nusra.



Tatu: Al-Mahbuwb Al-Mu’adhwam – Mpendwa Mtukuzwa.



Waarabu wakawa wanapenda masanamu yao waliyokuwa wakiyaabudu na wakayatukuza Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):



وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ

Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah na kuwafanya kuwa ni wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah. [Al-Baqarah 2: 165]



Nne: Ambaye kwayo akili zinakanganyika



Yaani: zinakanganya nyoyo zinapotafakari utukufu Wake (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kisha zikashindwa kufikia ufahamu wa dhati ya Ujalali Wake na Utukufu Wake (‘Azza wa Jalla).

Jina hili ni Jina tukufu kabisa kuliko yote miongoni mwa Asmaul-Husnaa, na ni lilotukuka zaidi na lililojumuisha maana za Majina Yake yote. Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Amejipwekesha Kwalo kutokana na walimwengu wote. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Akazitia khofu nyoyo za majahili na ndimi zao zikatamka bila kipingamizi wala taradadi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ

Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” bila shaka watasema: “Allaah.” [Luqmaan 31: 21]



Jina hili ni Ambalo linalokusanya Majina Mazuri yote na Sifa tukufu za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Mja anapoomba husema “Allaahumma” hivyo atakuwa ameomba kwa kila Majina Mazuri na Sifa Zake tukufu [Madaarij As-Saalikiyn (1/32)] Ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anaongezea Jina hili Tukufu katika Al-Asmaaul-Husnaa yote mfano kauli Yake:

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo [Al-A’raaf 7: 180]



Na ndio maana pia baadhi ya ‘Ulamaa wakaona kuwa Jina hili la Allaah Ndilo Jina tukufu kabisa ambalo likiombwa kwalo du’aa hutakabaliwa.

Na husemwa Ar-Rahmaan na Ar-Rahiym, Al-Qudduws, As-Salaam, Al-‘Aziyz, Al-Hakiym kuwa ni miongoni mwa Asmaaul-Husnaa wala haisemwi “Allaah” ni miongoni mwa Majina ya Ar-Rahmaan wala miongoni mwa Majina ya Al-‘Aziyz n.k, na ndipo Anaposema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿٢٢﴾

Yeye ni Allaah, Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Mjuzi wa ghayb na ya dhahiri, Yeye Ndiye Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu.



هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ ۚ سُبْحَانَ اللَّـهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٢٣﴾

Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye kusalimisha, Amesalimika na kasoro zote, Mwenye kusadikisha ahadi, Mwenye kuaminisha, Mwenye kutawalia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Jabari, Asiyeshindwa kufanya Atakalo, Mwenye kutakabari dhidi ya dhulma nk, Yuko juu ya viumbe, Utakasifu ni wa Allaah! kutokana na ambayo wanamshirikisha.



هُوَ اللَّـهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٤﴾

Yeye Ndiye Allaah, Muumbaji, Mwanzishi viumbe bila kasoro, Muundaji sura na umbile, Ana Majina Mazuri kabisa, kinamsabbih Pekee kila kilichokuweko katika mbingu na ardhi, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Hashr 59: 22-24]



Jina hili ndio asili ya Majina ya Majina ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na yanayofuatia mengine yote yamejumuika ndani Yake.



Jina la Allaah linamhusu Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا ﴿٦٥﴾

Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake; basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika ‘ibaadah Yake. Je, unamjua mwenye Jina kama Lake (Allaah)? [Maryam 19: 65]
 
أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Sifa Zake



Alhidaaya.com



إله

002-ILAAH







Ilaah: Muabudiwa Wa Haki





Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾

Na Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rasuli yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana Muabudiwa wa haki ila Mimi; basi Niabuduni.” [Al-Anbiyaa 21: 25]



Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

“Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu.” [Al-Baqarah: 2: 163]



Ilaah ni mwenye kustahiki kuabudiwa na Mwenye kuabudiwa kwa mapenzi, kwa kujidhalilisha Kwake, kwa kumkhofu, kwa kutaraji, kwa kumtukuza kwa utiifu kwa sababu Yeye Ndiye Anayeabudiwa.



Hivyo kila chenye kuabudiwa chini ya ‘Arshi Yake hadi ardhini ni batili; Amesema Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: “Laa Ilaaha Illa Anta” (Hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe) ndani yake kuna kuthibitisha upweke Wake, Uungu Wake, na Uungu unathibitisha wema Wake kwa waja Wake. Ilaah Ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa, na kwa sababu Anastahiki kuabudiwa, Yeye ni kama Alivyojisifu kwa Sifa Zake ambazo zinalazimu apendwe mapenzi yote, kilele cha mapenzi, na kunyenyekewa Kwake kilele cha kumnyenyekea, na ‘ibaadah inakusanya kilele cha mapenzi, kwa lengo la kunyenyekewa. [Daqaaiq At-Tafsyir (2/364)]



Na jina la Ilaah linatofautiana maana yake na Ar-Rabb katika maeneo mengi, miongoni mwazo ni: Kuwa Ar-Rabb maana yake inarejea kwenye kupwekeka katika kuumba na uendeshaji. Ama Ilaah, Ambaye Anastahiki kuabudiwa na ambaye nyoyo zinamtukuza na wananyenyekea Kwake kwa mapenzi na kumtukuza, Mwenye kustahiki kuabudiwa kwa kila aina zake na kuenea kwake.



Ama tofauti kati ya Allaah na Ilaah ni kuwa Ilaah ni wasifu ambao washirikina walimshirikisha kwao Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) kwa kuabudu miongoni mwao; jua, mwezi na sayari, na hawakufanya hivyo kwa kutumia jina la Allaah, na hawakujiita kwayo yeyote. [Al-Asmaa ya Al-Qurtubiy (uk. 368)]



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

فَلَوْلَا نَصَرَهُمُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ قُرْبَانًا آلِهَةً ۖ بَلْ ضَلُّوا عَنْهُمْ ۚ وَذَٰلِكَ إِفْكُهُمْ وَمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٨﴾

Basi kwa nini wasiwanusuru wale waliowafanya badala ya Allaah kuwa ni miungu ya kikurubisho (Kwake)? Bali wamewapotea, na huo ndio uongo wao na yale waliyokuwa wakiyatunga [Al-Ahqaaf 46 :28]
 
أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Sifa Zake



Alhidaaya.com





الرَّبّ

003-AR-RABB







Ar-Rabb: Rabb: Al-Maalik (Mfalme), Ar-Razzaaq (Mwenye kuruzuku), Al-Murabbi (Mlezi), Al-Khaaliq (Muumbaji), Al-Mudabbir (Mwendeshaji na Mpangaji)





Ni Rabb wa walimwengu na Anaundesha ulimwengu wote. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾

Himidi zote Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu. [Al-Faatihah (1: 2)]



Na pia Ar-Rabb inamaanisha kama alivyosema Ibn Al-Mandhdwur: “Ar-Rabb katika lugha ni Al-Maalik (Mfalme), As-Sayyid (Bwana), Al-Mudabbir (Mwendeshaji na Mpangaji), Al-Murabbi (Mlezi), Al-Qayyim (Msimamiaji), Al-Mun’im (Mwenye kuneemesha).” [Lisaan Al-‘Arab (1/399)]



Ar-Rabb inajumuisha pia Mwenye kuabudiwa kwa dalili ya kuwa swali mojawapo la kaburini ni “Man Rabbuka” (Nani Rabb wako)” yaani; nani Muabudiwa wako”.



Na Ar-Rabb katika asili ni katika ulezi: yaani Yule anayelea na kukuza kidogo kidogo hadi anakamilika, wala haisemwi kwa yeyote Ar-Rabb isipokuwa kwa Allaah Pekee na huongezwa kwa kusema: “Rabbul ‘Aalamiyn”. Au kwa asiyekuwa Allaah kwa kuongezewa kitu mbele yake kama vile kusema: Rabb Ad-Daar (bwana au mwenye nyumba), Rabb Al-Faras (bwana au mwenye farasi) au ngamia kwa anayemiliki hivyo [Angalia ‘An-Nihaayah fiy Gharyib al-Hadiyth (338) na Mufradaat Alfaadhw Qur-an (336) na Al-Asmaa (1/394)]



Jina hili tukufu linakusanya sifa nyingi za kimatendo, “Bali linaweza kuunganishwa na majina mengine matukufu ya kiutendaji na sifa zake tukufu. [Fiqh Al-Asmaa Al-Husnaa Dr. Abdur-Razzzaq Al-Badr (79)] Hivyo Ar-Rabb kuingia katika: Al-Qaadir, Al-Khaaliq, Al-Baariu, Al-Muswawwir, Al-Hayyu, Al-Qayyuwm, Ar-Rahmaan na mengineyo. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

سَلَامٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ ﴿٥٨﴾

“Salaamun”; kauli kutoka kwa Rabb Mwenye kurehemu) [Yaasiyn (36: 58)]



Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Ambaye ni Rabb wa viumbe wote, kila kilichoko mbinguni na ardhini ni mja Kwake na katika udhibiti Wake. Yeye ndiye Aliyelea viumbe vyote kwa neema Zake, kisha Akakipa kila kitu umbo lake linalolaiki, kisha Akakiongoza kama ilivyothibiti katika Qur-aan:

قَالَ فَمَن رَّبُّكُمَا يَا مُوسَىٰ ﴿٤٩﴾

(Fir’awn) Akasema: “Basi nani (huyo) Rabb wenu ewe Muwsaa?”



قَالَ رَبُّنَا الَّذِي أَعْطَىٰ كُلَّ شَيْءٍ خَلْقَهُ ثُمَّ هَدَىٰ ﴿٥٠﴾

(Muwsaa) Akasema: “Rabb wetu ni Yule Aliyekipa kila kitu umbo lake, kisha Akakiongoza.” [Twaahaa (20: 49-50)]



Akawaenezea viumbe Vyake neema kubwa kubwa ambazo lau watazikosa hawatoweza kuishi. Akawakuza, Akawapa malisho, Akawalea kwa malezi kamilifu. Basi hakuna neema isipokuwa neema Yake. Ndipo Jina hili likawa tukufu, lenye umuhimu mkubwa na azizi katika nafsi na nyoyo za Manabii, na vipenzi vya Allaah, na ndipo ikawa aghlabu ya du’aa za Qur-aan na Sunnah ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Salaf zinaanzia na “Rabbanaa” au “Rabbi” kama du’aa ya Nabiy Aadam ('Alayhis-Salaam):



قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٢٣﴾

“Rabb wetu! Tumedhulumu nafsi zetu, na basi Usipotughufuria na Ukaturehemu; bila shaka tutakuwa miongoni mwa waliokhasirika.” [Al-A’raaf (7: 23)]



Na du’aa ya Khaliylur-Rahmaan Nabiy Ibraahiym ('Alayhis-Salaam):



رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ ﴿٤١﴾

“Rabb wetu! Nighufurie na wazazi wangu wawili na Waumini Siku itakayosimama hesabu.” [Ibraahiym (14: 41)]



Na Du’aa ya Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ ﴿٩٧﴾ وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ ﴿٩٨﴾

Na sema: “Rabb wangu! Najikinga Kwako kutokana na uchochezi (na wasiwasi) wa mashaytwaan.” “Na najikinga Kwako Rabb wasinihudhurie.” [Al-Muuminuwn (23: 97-98)]





Na du’aa za wenye ‘ilmu:



رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴿٨﴾

“Rabb wetu, Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kutuongoza na Tutunukie kutoka kwako rahmah. Hakika Wewe ni Mwingi wa kutunuku na kuneemesha.” [Aal-‘Imraan (3: 8)]





Na du’aa za ‘Ibaadur-Rahmaan (waja wa Mwingi wa Rahmah):



رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا ﴿٧٤﴾

“Rabb wetu! Tutunukie katika wake zetu na dhuria wetu viburudisho vya macho yetu, na Tujaalie kuwa waongozi kwa wenye taqwa [Al-Furqaan (25: 74)]



Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema kuhusu Rabb kuwa mja anakuwa karibu Naye wakati wa kusujudu na ndipo ikawa kusujudu ni sababu moja wapo ya wasiylah (kujikurubisha) kwa Ar-Rabb katika kuomba du’aa:



أقربُ ما يكُونُ الرَّبُّ مِنَ العبدِ في جوفِ اللَّيلِ الآخِرِ، فإنِ استطعتَ أن تكونَ ممّن يذكُرُ اللهَ في تِلكَ الساعةِ ، فكُن

“Wakati Rabb Anakuwa karibu kabisa na mja, ni wakati wa mwisho wa usiku, kwa hiyo ukiweza kuwa miongoni mwa wanaomdhukuru Allaah katika saa hiyo basi uwe.” [Swahiyh At-Tirmidhiy (3578)]
 
أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Sifa Zake



Alhidaaya.com





الرَّحْمن

004-AR-RAHMAAN







Ar-Rahmaan: Mwingi Wa Rahmah



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

الرَّحْمَـٰنُ ﴿١﴾ عَلَّمَ الْقُرْآنَ ﴿٢﴾

Ar-Rahmaan; Mwingi wa rahmah. Amefundisha Qur-aan [Ar-Rahmaan: 1-2]



Jina hili ni pana zaidi na lenye kuenea zaidi kuliko Ar-Rahiym (Mwenye kurehemu). Hili linakusanya maana zote za rahmah, huruma n.k. Allaah Ndiye Mwenye rahmah iliyokusanya kila kitu, iliyoenea kwa viumbe Vyake vyote duniani, bin Aadam kwa majini, Waumini kwa makafiri, wanyama, mimea, hakuna yeyote au chochote katika kuwepo kwake ila rahmah Yake imemuenea, na ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ الرَّحْمَـٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا ﴿٥٩﴾

Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah), Ar-Rahmaan; Mwingi wa Rahmah, basi ulizia kuhusu Yeye, (kwani Yeye) ni Mjuzi wa yaliyodhahiri na yaliyofichikana. [Al-Furqaan: 59]



Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

Ar-Rahmaan; Mwingi wa Rahmah juu ya ‘Arshi Istawaa (Yuko juu kwa namna inayolingana na Utukufu Wake Yeye Mwenyewe Allaah) [Twaahaa 5]



Istawaa katika ‘Arshi kwa jina la Ar-Rahmaan, kwa sababu ‘Arshi imezungukwa na viumbe na ina wasaa kwao, na rahmah imewazunguka waja Wake, ina wasaa kwao kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ

Na rahmah Yangu imeenea kila kitu [Al-A’raaf: 156]



Istawaa katika kilicho kipana zaidi katika Alivyoviumba, nayo ni ‘Arsh Yake na kwa sifa iliyo pana zaidi nayo ni rahmah Yake. Na kwa ajili hiyo rahmah Yake imeenea katika kila kitu.



Ar-Rahmaan ni jina Analoitwa Allaah Peke Yake. Ama athari ya jina hili ni kwa wote; kwa watu wema na waovu. Na ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amelitaja zaidi Jina hili katika Suwrah ziloteremshwa Makkah, khasa katika Suwrat Maryam ambayo imetajwa mara nyingi zaidi ya Suwrah nyinginezo.



Kipindi hicho cha Makkah ni kipindi cha mwanzo cha Uislamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akawadhihirishia makafiri Sifa Yake hiyo kwamba Yeye ni Mwingi wa rahmah juu ya kuwa wanamshirikisha.



Na katika Sunnah zimethibiti Hadiyth kadhaa kuhusu rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) wanayorehemeana viumbe ardhini:



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((إِنَّ اللَّهَ خَلَقَ الرَّحْمَةَ يَوْمَ خَلَقَهَا مِائَةَ رَحْمَةٍ، فَأَمْسَكَ عِنْدَهُ تِسْعًا وَتِسْعِينَ رَحْمَةً، وَأَرْسَلَ فِي خَلْقِهِ كُلِّهِمْ رَحْمَةً وَاحِدَةً، فَلَوْ يَعْلَمُ الْكَافِرُ بِكُلِّ الَّذِي عِنْدَ اللَّهِ مِنَ الرَّحْمَةِ لَمْ يَيْأَسْ مِنَ الْجَنَّةِ، وَلَوْ يَعْلَمُ الْمُؤْمِنُ بِكُلِّ الَّذِي عِنْدَ اللَّهِ مِنَ الْعَذَابِ لَمْ يَأْمَنْ مِنَ النَّارِ)) البخاري في الأدب، باب جعل الله الرحمة في مائة جزء

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Hakika Allaah Ameumba rahmah. Siku Aliyoumba Alizifanya rahmah mia (100) Akazuia Kwake rahmah tisini na tisa (99) Akateremsha rahmah moja kwa viumbe Vyake vyote. Lau kafiri angelijua kuhusu rahmah zilizokuweko kwa Allaah, basi asingekata tamaa kuingia Jannah. Na lau Muumini angejua adhabu zilizoko kwa Allaah, basi asingejiaminisha na moto)) [Al-Bukhaariy fiy Ar-Riqaab Baab Ar-Rajaa ma’al-khawf]



وعن أبي هريرة رضي الله عنه أنه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((جَعَلَ الله الرَّحْمَةَ مِائَةَ جُزْءٍ، فَأَمْسَكَ عِنْدَهُ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ جُزْءًا وَأَنْزَلَ فِي الأَرْضِ جُزْءًا وَاحِدًا، فَمِنْ ذَلِكَ الْجُزْءِ يَتَرَاحَمُ الْخَلْقُ حَتَّى تَرْفَعَ الْفَرَسُ حَافِرَهَا عَنْ وَلَدِهَا خَشْيَةَ أَنْ تُصِيبَهُ)) البخاري في الأدب، باب جعل الله الرحمة في مائة جزء

Na pia amepokea Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Allaah Amejaalia rahmah mia, Akazuia Kwake rahmah tisini na tisa, Akateremsha moja tu ardhini. Basi kutokana na hiyo ndio wanayorehemeana viumbe hadi kwamba farasi huinua makwato yake kukhofia asimkanyage mtoto wake)) [Al-Bukhaariy Baab Ja’ala Allaahu Ar-Rahmah fiy miat juz’]



عَنْ عَطَاءٍ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((إِنَّ لِلَّهِ مِائَةَ رَحْمَةٍ أَنْزَلَ مِنْهَا رَحْمَةً وَاحِدَةً بَيْنَ الْجِنِّ وَالإِنْسِ وَالْبَهَائِمِ وَالْهَوَامِّ فَبِهَا يَتَعَاطَفُونَ وَبِهَا يَتَرَاحَمُونَ وَبِهَا تَعْطِفُ الْوَحْشُ عَلَى وَلَدِهَا وَأَخَّرَ اللَّهُ تِسْعًا وَتِسْعِينَ رَحْمَةً يَرْحَمُ بِهَا عِبَادَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ))

Na pia imepokelewa kutoka kwa ‘Atwaa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Ana rahmah mia, Ameiteresha moja kati ya majini na wana Aadam na wanyama na wadudu, ambao wanaoneana huruma na wanarehemeana, na hiyo hiyo mpaka mnyama mwitu anamhurumia mwanawe. Akazuia Allaah rahmah tisini na tisa Atawarehemu kwazo waja Wake Siku ya Qiyaamah)) [Muslim (6/98), Ahmad (2/434), Ibn Maajah (4293)]



Sifa hii ya Rahmah ni ya dhati Yake Allaah ambayo haiwezi kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Makafiri wa Makkah hawakupenda Jina hili la Ar-Rahmaan wakakataa kuliandika katika mkataba wa Hudaybiyah pale Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomuamrisha mwandishi wa mkataba andike “BismiLLaah (Kwa Jina la Allaah) Ar-Rahmaan (Mwingi wa rahmah) Ar-Rahiym (Mwenye kurehemu).” Wakasema: “Andika: Biismika-Allaahumma.”

Hapo Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akateremsha:



قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ

Sema; “Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan; Mwingi wa rahmah, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. [Al-Israa: 110]

[Tafsiyr Ibn Kathiyr]



Na ndio maana Suwrah za Qur-aan zinaanza na BismiLLaah inayotaja Majina Yake Mawili ya Ar-Rahmaan na Ar-Rahiym, na pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametanguliza katika ufunguzi wa Suwrat Al-Faatihah Akaanza na Ar-Rahmaan (Mwingi wa rahmah) na Ar-Rahiym (Mwenye kurehemu).



Vipi Uweze kupata rahmah ya Allaah?



1. Njia ya kwanza kuweza kupata Rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni yale yote yenye uhusiano wa mtu na Rabb Wake kama vile:



Kujipuesha na yote yaliyoharamishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sababu baadhi ya yaliyoharamishwa yanamsababisha mtu kupata laana ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) inayomaanisha ni kuwekwa mbali na rahmah Zake.

Pia katika njia ya kupata rahmah ya Allaah, ni kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٣٢﴾

Na mtiini Allaah na Rasuli mpate kurehemewa. [Aal-‘Imraan: 132]



Na pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametaja sifa za waja Wake ambao amehusisha na Jina na Sifa Yake hii ya Ar-Rahmaan Anawaita: ‘Ibaadur-Rahmaan (Waja wa Rahmaan).” Pindi atakapotekeleza mtu hayo yaliyotajwa katika Suwratul-Furqaan Aayah 63 mpaka Aayah 76 basi atastahiki kuwa ni miongoni mwa ‘Ibaadur-Rahmaan.



وَعِبَادُ الرَّحْمَـٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا ﴿٦٣﴾

Na waja wa Ar-Rahmaan Mwingi wa Rahmah ni wale wanaotembea katika ardhi kwa unyenyekevu na upole, na majahili wanapowasemesha, wao husema: Salaam!



وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا ﴿٦٤﴾

Na wale wanaokesha (baadhi ya) usiku kwa ajili ya Rabb wao wakisujudu na kusimama….. [Al-Furqaan: 63-76]



Hali kadhaalika kuzidisha ‘ibaadah kwa wingi, Swalaah za usiku (tahajjud), kuomba du’aa, kuisikiliza kwa makini na kuisoma Qur-aan, kuzingatia maana zake, kuwa na taqwa, kusimamisha Swalaah na kutoa Zakaah, kufanya jihaad katika njia ya Allaah, kuvuta subira katika mitihani na misiba, kuomba maghfirah, na kwa ujumla ni kumwamini Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).



Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَاكْتُبْ لَنَا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الْآخِرَةِ إِنَّا هُدْنَا إِلَيْكَ ۚ قَالَ عَذَابِي أُصِيبُ بِهِ مَنْ أَشَاءُ ۖ وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ ﴿١٥٦﴾

“Na Tuandikie katika dunia hii mazuri na katika Aakhirah. Hakika sisi tumerudi kutubu Kwako.” (Allaah) Akasema: “Adhabu Yangu Nitamsibu nayo Nimtakaye. Na rahmah Yangu imeenea kila kitu. Basi Nitawaandikia wale wenye taqwa na wanaotoa Zakaah na ambao wao wanaziamini Aayaat (na hoja, dalili) Zetu.” [Al-A’raaf: 156]



Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Aayah zifuatazo:



وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٥٦﴾

Na simamisheni Swalaah, na toeni Zakaah, na mtiini Rasuli ili mpate kurehemewa. [An-Nuwr: 56]



وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٢٠٤﴾

Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na bakieni kimya (mzingatie) ili mpate kurehemewa. [Al-A’raaf: 204]



وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٥٥﴾

Na hiki Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha kilichobarikiwa, basi kifuateni na muwe na taqwa mpate kurehemewa. [Al-An’aam: 155]





قَالَ يَا قَوْمِ لِمَ تَسْتَعْجِلُونَ بِالسَّيِّئَةِ قَبْلَ الْحَسَنَةِ ۖ لَوْلَا تَسْتَغْفِرُونَ اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٤٦﴾

(Swaalih) Akasema: “Enyi kaumu yangu! Kwa nini mnahimiza uovu kabla ya mema; kwa nini msimwombe Allaah maghfirah huenda mkarehemewa?” [An-Naml: 46]



وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ ﴿١٥٥﴾

Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri.



الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ﴿١٥٦﴾

Wale ambao unapowafika msiba husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.”



أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ ﴿١٥٧﴾

Hao zitakuwa juu yao barakah kutoka kwa Rabb wao na rahmah, na hao ndio wenye kuongoka. [Al-Baqarah: 155-157]



إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢١٨﴾

Hakika wale walioamini na wale waliohajiri na wakapigana jihaad katika njia ya Allaah, hao wanataraji rahmah ya Allaah, na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Baqarah: 218]



Na kuomba du’aa ni ambazo zimethibiti katika Sunnah za kumwomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) rahmah Yake mifano ya du’aa mbili miongoni mwa du’aa nyingi ni:



اللّهُـمَّ رَحْمَتَـكَ أَرْجـو فَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـيْن، وَأَصْلِـحْ لي شَأْنـي كُلَّـه لَا إِلَهَ إِلَّا أنْـت



Allaahumma Rahmatika arjuw falaa takilniy ilaa nafsiy twarfata ‘aynin, wa aswlih liy sha-aniy kullahu, laa ilaaha illaa Anta



Ee Allaah, nataraji rahmah Zako, usinitegemeze kwenye nafsi yangu japo kwa muda wa upepesa jicho, na Unitengenezee mambo yangu yote, hapana Muabudiwa wa haki ila Wewe [Hadiyth ya Abu Bakr Nafiy’ bin Haarith Ath-Thaqafiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) - Abu Daawuwd (4/324) [5090], Ahmad (5/42), ameipa daraja ya Hasan Al-Albaaniy katika Swahiyh Abi Daawuwd (3/959) ]



اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مُوجِبَاتِ رَحْمَتِكَ، وَعَزَائِمَ مَغْفِرَتِكَ، وَالسَّلامَةَ مِنْ كُلِّ إِثْمٍ، وَالْغَنِيمَةَ مِنْ كُلِّ بِرّ، وَالْفَوْزَ بِالْجَنَّةِ، وَالنَّجَاةَ مِنَ النَّاَرِ.

Allaahumma inniy as-aluka muwjibaati Rahmatik wa 'azaaim maghfiratik was-salaamata min kulli ithm, wal ghaniymata minkulli birr, wal fawza bil Jannati, wan najaata minan-naari



Ee Allaah hakika mimi nakuomba azima za rahmah Yako, azimio la maghfirah Yako, na amani katika kila dhambi, na ghanima katika kila jema, na kufuzu katika Jannah na kuokoka na moto [Al-Haakim (1/525) na ameipa daraja ya Swahiyh na ameiwafiki Adh-Dhahabiy]





2. Njia ya pili ya kuweza kupata Rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni yale yote yenye uhusiano wa bin Aadam na viumbe vinginevyo.



Imaam As-Sa’dy (Rahimahu Allaah) amesema: “Rahmah ya mja kwa viumbe ni sababu kuu inayomfikisha mtu kupata rahmah ya Allaah ambayo taathira yake ni kupata khayraat za dunia na khayraat za Aakhirah, na kukosa kwake ni kukatwa na kuzuilika kupata rahmah ya Allaah. Na mja anahitaji kwa dharura rahmah ya Allaah, asiikose hata kidogo kadiri ya muda wa upepeso wa jicho. Na kila kilichopo chenye neema na kukimbiza balaa, ni katika rahmah ya Allaah.



Basi anapotaka kubakia katika rahmah ya Allaah na kuzidi kuipata na afanye yote yanayosababisha kupata rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Yote yanajumuika katika kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

إِنَّ رَحْمَتَ اللَّـهِ قَرِيبٌ مِّنَ الْمُحْسِنِينَ ﴿٥٦﴾

Hakika rahmah ya Allaah iko karibu na wafanyao ihsaan. [Al-A’raaf: 56]

[Bahjatu Quluwb Al-Abraar, uk. 197-198]



Hadiyth nyingi za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zimethibiti kuhusu kupata rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kufanya ihsaan na wema. Baadhi ya Hadiyth ni kama zifuatazo:



عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو يَبْلُغُ بِهِ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الرَّاحِمُونَ يَرْحَمُهُمْ الرَّحْمَنُ ارْحَمُوا مَنْ فِي الْأَرْضِ يَرْحَمْكُمْ مَنْ فِي السَّمَاءِ

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba amesema: ((Ar-Rahmaan Atawarehemu wenye kurehemu. Mrehemuni aliyeko ardhini Atakurehemuni Aliyeko mbinguni)) [Sunan At-Tirmidhiy (1924) Ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy, Swahiyh Abiy Daawuwd (4941), Swahiyh At-Targhiyb (2256)]



قال رسول الله - صلى الله عليه وسلّم: ((مَنْ لاَ يَرْحَمِ النَّاسَ لاَ يَرْحَمْهُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ‏)) رواه البخاري (6013) ومسلم (2319)

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Asiyerehemu watu hatorehemewa na Allaah Aliyetukuka na Aliye Jalali)) [Al-Bukhaariy (6013) Muslim (2319)]



Kusulihisha waliokhasimikiana:



إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٠﴾

Hakika Waumini ni ndugu, basi suluhisheni baina ya ndugu zenu. Na mcheni Allaah ili mpate kurehemewa. [Al-Hujuraat: 10]



Na Sifa hii ya rahmah imehusiana na Ar-Rahm (fuko la uzazi) ambalo kwalo ndugu na jamaa hurehemeana na likawa jambo la kukata undugu ni dhambi kubwa mno inayosababisha laana za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na ghadhabu Zake kama ilivyotajwa katika Qur-aan. [Muhammad: 47: 22-23] Na pia Akasisitiza mno katika Qur-aan [Al-Baqarah: 27, Ar-Ra’d: 20-21]. Na pia Hadiyth kadhaa zimethibiti makemeo na khatari ya kukata undugu hadi kwamba inamharamisha Muislamu kuingia Jannah. Na katika Hadiyth zifuatazo zimehusisha sifa hiyo ya rahmah na undugu:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال: ((إِنَّ الرَّحِمَ شَجْنَةٌ مِنْ الرَّحْمَنِ، فَقَالَ اللَّهُ: مَنْ وَصَلَكِ وَصَلْتُهُ وَمَنْ قَطَعَكِ قَطَعْتُهُ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Ar-Rahm [fuko la uzazi] linatokana na Jina la Ar-Rahmaan; Basi Allaah Amesema: Atakayekuunga Nami Nitamuunga na Atakayekukata Nami Nitamkata)) [Al-Bukhaariy 5988]



Na pia:

عنْ عَائِشَةَ (رضي الله عنها) قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((الرَّحِمُ مُعَلَّقَةٌ بِالْعَرْشِ، تَقُولُ مَنْ وَصَلَنِي وَصَلَهُ اللَّهُ وَمَنْ قَطَعَنِي قَطَعَهُ اللَّهُ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ar-Rahm [fuko la uzazi] limetundikwa katika ‘Arshi, linasema: Anayeniunga Allaah Atamuunga, na anayenikata Allaah Atamkata)) [Al-Bukhaariy na Muslim]



Na katika kuwarehemu wanyama:



Mwanamke kahaba aliyemnywesha mbwa maji alighufuriwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ غُفِرَ لِامْرَأَةٍ مُومِسَةٍ مَرَّتْ بِكَلْبٍ عَلَى رَأْسِ رَكِيٍّ يَلْهَثُ قَالَ كَادَ يَقْتُلُهُ الْعَطَشُ فَنَزَعَتْ خُفَّهَا فَأَوْثَقَتْهُ بِخِمَارِهَا فَنَزَعَتْ لَهُ مِنْ الْمَاءِ فَغُفِرَ لَهَا بِذَلِكَ

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ameghufuriwa mwanamke kahaba. Alimpitia mbwa akihaha (kwa kiu) karibu na kisima. Alipoona anakaribia kufa kwa kiu, alivua kiatu chake akakifunga kwenye shungi lake akamchotea maji. Allaah Akamghufuria kwa kufanya hivyo)) [Al-Bukhaariy (3143) Muslim (2245)]



Mwanamke aliyemuadhibu paka aliingizwa motoni:



عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((عُذِّبَتْ امْرَأَةٌ فِي هِرَّةٍ حَبَسَتْهَا حَتَّى مَاتَتْ جُوعًا فَدَخَلَتْ فِيهَا النَّارَ, لاَ هِيَ أَطْعَمْتِهَا وَسَقَيْتِهَا إِذْ هِيَ حَبَسْتِيهَا وَلاَهِيَ تَرَكَتْها تَأكُلُ مِنْ خَشَاشِ الأرْضِ)) متفق

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mwanamke fulani aliadhibiwa kwa sababu ya paka aliyemfungia mpaka akafa kwa njaa, akaingia motoni [kwa sababu] alipomfungia hakumpa chakula wala hakumnywesha maji wala hakumwacha aende akale vidudu ardhini. [Al-Bukhaariy na
 
أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Sifa Zake



Alhidaaya.com



الرَّحِيم



005-AR-RAHIYM







Ar-Rahiym Mwenye Kurehemu



Sifa mbili za Rahmaan na Rahiym zinatokana na herufi tatu za asili na hivyo maana zake ni moja, isipokuwa tu kama ilivyobainishwa katika Sifa ya Rahmaan kwamba maana yake ni pana na inaenea zaidi kwa viumbe wote; Waumini kwa makafiri, watu wema kwa watu waovu. Ama Rahiym ni Sifa khaswa kwa ajili ya Waumini pekee kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا ﴿٤٣﴾

Naye kwa Waumini daima ni Mwenye kurehemu. [Al-Ahzaab: 43]



Na Anasema kuhusu waja Wake:

نَبِّئْ عِبَادِي أَنِّي أَنَا الْغَفُورُ الرَّحِيمُ ﴿٤٩﴾

(Ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Wajulishe waja Wangu, kwamba: Hakika Mimi ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Hijr: 49]



Na pia kuhusu Maswahaba waliorudi kutubia:



لَّقَد تَّابَ اللَّـهُ عَلَى النَّبِيِّ وَالْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ الَّذِينَ اتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ الْعُسْرَةِ مِن بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ ۚ إِنَّهُ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١١٧﴾

Kwa yakini Allaah Amepokea tawbah ya Nabiy na Muhajirina na Answaar ambao wamemfuata (Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم) katika saa ya dhiki (vita vya Tabuwk) baada ya nyoyo za kundi miongoni mwao zilikaribia kuelemea mbali na haki (Allaah) Akapokea tawbah yao. Hakika Yeye kwao ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu. [At-Tawabah: 117]



Na Waumini watakapoingia Jannah:

إِنَّ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ الْيَوْمَ فِي شُغُلٍ فَاكِهُونَ ﴿٥٥﴾

Hakika watu wa Jannah leo wamo katika kushughulika wakifurahi.



هُمْ وَأَزْوَاجُهُمْ فِي ظِلَالٍ عَلَى الْأَرَائِكِ مُتَّكِئُونَ ﴿٥٦﴾

Wao na wake zao, wakiwa katika vivuli, juu ya makochi ya fakhari wakiegemea.



لَهُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ ﴿٥٧﴾

Watapata humo kila aina ya matunda, na watapata wanavyoomba.



سَلَامٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ ﴿٥٨﴾

“Salaamun”; kauli kutoka kwa Rabb Mwenye kurehemu. [Yaasiyn: 55-58]



Na pia katika hali nyingine ya Waumini wanapofishwa na kubashiriwa Jannah:



إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ ﴿٣٠﴾

30. Hakika wale waliosema: “Rabb wetu ni Allaah.” Kisha wakathibitika imara; Malaika huwateremkia: (wanapofishwa kuwaambia): “Msikhofu, na wala msihuzunike, na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa.”



نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ ﴿٣١﴾

31. “Sisi ni marafiki walinzi wenu katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Na mtapata humo yale yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale mtakayoomba.



نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ ﴿٣٢﴾

32. “Ni takrima kutoka kwa Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu.” [Fusw-Swilat: 30-32]



Na katika du’aa, Anas bin Maalik amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Mu’aadh bin Jabal:




"أَلا أُعَلِّمُكَ دُعَاءً تَدْعُو بِهِ لَوْ كَانَ عَلَيْكَ مِثْلُ جَبَلٍ دَيْنًا لأَدَّى اللهُ عَنْكَ؟ قُلْ يَا مُعَاذُ: اللَّهُمَّ مَالِكُ الْمُلْكِ، تُؤْتِي الْمُلْكَ مَنْ تَشَاءُ، وَتَنْزِعُ الْمُلْكَ مِمَّنْ تَشَاءُ، وَتُعِزُّ مَنْ تَشَاءُ، وَتُذِلُّ مَنْ تَشَاءُ، بِيَدِكَ الْخَيْرِ إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، رَحْمَانُ الدُّنْيَا وَالآخِرَةِ، تُعْطِيهُمَا مَنْ تَشَاءُ، وَتَمْنَعُ مِنْهُمَا مَنْ تَشَاءُ، ارْحَمْنِي رَحْمَةً تُغْنِينِي بِهَا عَنْ رَحْمَةِ مَنْ سِوَاكَ"


((Je, nikufundishe duaa ambayo ukiiomba basi ikiwa una deni mfano wa mlima wa Uhud, Allaah Atakukidhia. Sema ya Mu’aadh: “Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, khayr imo Mkononi Mwako. Hakika Wewe juu ya kila kitu ni Muweza. Mwingi wa rahmah duniani na Aakhirah Mwenye kurehemu, Unampa rahmah mbili hizo Umtakaye na Unamnyima Umtakaye. Nirehemu rahmah itakayonitosheleza kwayo rahmah isiyotoka kwa mwengine isipokuwa Wewe.)) [Hadiyth Hasan - Swahiyh At-Targhiyb (1821)]



Na pia Akaihusisha sifa hiyo kwa mja Wake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢٨﴾

Kwa yakini amekujieni Rasuli anayetokana na nyinyi wenyewe, ni yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini (muongoke) mwenye huruma kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rahmah. [At-Tawbah: 128]



Hivyo Waumini ni wenye neema na jina hili la Ar-Rahiym na lile la Ar-Rahman kama ilivyo katika Hadiyth: ((…Atakamilisha rahmah mia moja kwa mawalii Wake siku ya Qiyaamah)) [Hadiyth Swahiyh kwa sharti la Shaykhaan; Al-Bukhaariy na Muslim - angalia ‘Zawaaid Al-Muwatwaa na Al-Musnad 1/53].



Na Sifa au Majina haya mawili yametajwa katika Qur-aan kwa pamoja katika Aayah kadhaa mfano:

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

163. “Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu.” [Al-Baqarah: 163]



حم ﴿١﴾

Haa Miym.





تَنزِيلٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٢﴾

Ni uteremsho kutoka kwa Mwingi wa Rahmah, Mwenye kurehemu. [Fusw-Swilat: 1-2]



هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۖ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿٢٢﴾

Yeye ni Allaah, Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye. Mjuzi wa ghayb na ya dhahiri, Yeye Ndiye Mwingi wa rahmah, Mwenye kurehemu. [Al-Hashr: 22]



Ama Sifa ya Rahiym imetajwa pamoja na Sifa au Majina Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) mbali mbali khaswa pamoja na Al-Ghafuwr (Mwingi wa kufughuria) na Al-‘Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika). Mifano michache:

قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Aal-‘Imraan: 31]



وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ وَأَنَّ اللَّـهَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ ﴿٢٠﴾

Na lau si fadhila ya Allaah juu yenu na rahmah Yake, na kwamba Allaah ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu. [An-Nuwr: 20]



وَاسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٌ وَدُودٌ ﴿٩٠﴾

“Na ombeni maghfirah kwa Rabb wenu, kisha tubieni Kwake. Hakika Rabb wangu ni Mwenye kurehemu, Mwenye upendo khalisi.” [Huwd: 20]



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ ۖ وَلَا تَجَسَّسُوا وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا فَكَرِهْتُمُوهُ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ تَوَّابٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢﴾

Enyi mlioamini! Jieupusheni sana na dhana kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi. Na wala msifanyiane ujasusi, na wala wasisengenyane baadhi yenu wengineo. Je, anapenda mmoja wenu kwamba ale nyama ya nduguye aliyekufa? Basi mmelichukia hilo! Na mcheni Allaah! Hakika Allaah ni Mwingi wa kupokea tawbah, Mwenye kurehemu. [Al-Hujuraat: 12]



بِنَصْرِ اللَّـهِ ۚ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٥﴾

Kwa nusura ya Allaah. Anamnusuru Amtakaye, Naye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye kurehemu. [Ar-Ruwm: 5]



إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ ﴿٢٨﴾

Hakika sisi tulikuwa kabla Tunamuomba Yeye Pekee, hakika yeye Ndiye Mwingi wa huruma na fadhila, Mwenye kurehemu.” [Atw-Twuwr: 28]
 
Maswali: Maasi


Alikuwa Akifanya ‘Ibaadah Sana Kabla Ya Kumuoa, Kisha Baada

Ya Ndoa Mume Haswali Tena Afanyeje



Alhidaaya.com





Swali:



Asalaam aleykum



Napenda kuwapongeza kwa kazi nzuri ya kutuelimisha sisi Waislamu In shaa Allaah Allaah awalipe malipo mema na siku ya mwisho tukutane wote katika pepo Aamiin.



Mimi ni mwanamke niliyeolewa, na hakika mume huyu nilimpenda kutokana na muonekano wake wa kuwa mwenye kufanya ibada sana na ni mtu mwema, anapenda kusaidia watu wenye matatizo n.k, tulikutana tulipokuwa masomoni na alikuwa ni kiongozi wetu katika kikundi cha dini katka hiyo shule, ukweli mashallah Dini ameisoma na anaelewa vizuri sana.



lakini kinachonikwaza kwa mume wangu huyu amekuwa hasimamishi swala, na kila ninapomkumbusha huwa anasema sawa mke wangu ninasali sasa kwa kuwa kila mmoja anashughuli zake tunaachana pale asubuhi na kuonana jioni lkn muda wa magharibi, Ishaa na subhi simuoni mwenzangu kusali, najitahidi kumkumbusha lakini hadi inafikia kipindi amani inatoweka ndani ya nyumba sababu ni kumwambia kila mara bwana muda wa sala huo umefika, na Allaah ametujaalia nyumba yetu inatizamana na msikiti. Ukweli ninasikitika sana nashindwa nifanye nini kwani Nilimuomba Allaah anipe mume mwema lkn mwenzangu anamapungufu hayo tu katika swalah. Naomba mnisaidie nifanye nini ili aweze kusimamisha swala kama inavyotakiwa.



Nawatakia kazi njema wabillah Tawfiq.





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Hakika dunia ina mitihani mingi sana na wakati mwengine sisi wanaadam hushindwa kukabiliana na mitihani hiyo kwa sababu moja au nyingine.



Ndio kwa minajili hiyo tunatakiwa kila wakati tuwe ni wenye kumuomba Muumba wetu, Allaah Aliyetukuka Atupatie hatima njema na tusife ila katika Imani na Uislamu. Kwa njia hii kwa kuwa Uislamu ni muongozo wa maisha yetu hapa duniani umetupatia ufumbuzi wa kila jambo na tatizo linalo mkabili mwanaadamu katika huu ulimwengu.



Kwa ajili hiyo, mwanzo inatakiwa wewe umlilie Rabb wako kwa tatizo unalokabiliana nalo kwa kuishi na mume ambaye haswali. Swalah ndio tofauti baina yetu sisi na makafiri, mwenye kuiacha amekuwa kafiri. Mlilie Rabb wako Amuongoze mume wako na arudi kama alivyokuwa hapo awali na zaidi ndio maombi yetu ya dhati.



Pili, inatakiwa umnasihi mumeo kwani wewe ndio unaomjua yeye kwa kiasi kikubwa sana. Jaribu kuangalia wakati unaofaa na uzungumze naye kwa njia nzuri na upole, kwani Allaah Aliyetukuka Anatuambia:

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ

"Lingania katika njia ya Rabb wako kwa hikmah na mawaidha mazuri. Na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi". [An-Nahl: 125].



Usizungumze naye kwa ghadhabu wala hasira. Jaribu kumkumbusha yaliyopita alivyokuwa mstari wa mbele shuleni katika mas-ala ya Dini na mjulishe hiyo ndio sababu kubwa iliyokufanya wewe kuvutika kuwa mume wako, na mengineyo mazuri yaliyowakaribisha na Allaah Aliyetukuka. Katika nasaha, inawezekana kumpatia vijitabu au kanda zinazozungumzia kuhusu uzuri na fadhila ya Swalah na adhabu ya asiyeswali. Kuna mawaidha mengi ndani ya Alhidaaya yanayoeleea mas-ala ya Swalah na hukmu ya Taarikus Swalaah.



Ikiwa hakuna mabadiliko yoyote yale itakuwa vyema sasa ushirikishe familia yako na yake katika kusuluhisha tatizo hilo kubwa sana katika Dini. Allaah Aliyetukuka Anasema:



وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُوا حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَا إِن يُرِيدَا إِصْلَاحًا يُوَفِّقِ اللَّـهُ بَيْنَهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًا ﴿٣٥﴾

Na mkikhofu mafarikiano baina yao wawili, basi pelekeni mwamuzi kutoka watu wa mume na mwamuzi kutoka watu mke. Wakitaka sulhu Allaah Atawawafikisha baina yao. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [An-Nisaa: 35].



Wakati wa mkutano huo inatakiwa ueleze dhahiri yanayoendelea katika ndoa yenu na mabadiliko ya mumeo katika mas-ala ya msingi ya Dini.



Ikiwa katika mkutano huo hakukupatikana ufumbuzi itabidi uende ukapeleke kesi yako kwa Qaadhi kama wapo katika mji unaoishi au Shaykh anayejulikana kwa uchaji wa Allaah, Dini na uadilifu. Ikiwa baada ya mzunguko wote huo wa kutafuta suluhisho haukupatikana itabidi ufanye Istaakhaarah kumtaka Allaah Akujulishe kama mume huyo unaweza kuendelea kuishi naye au hapana. Lakini kwa kifupi mume asiyeswali si mume anayefaa katika maisha ya Muislamu.



Twakutakia kila la kheri na tunamuomba Allaah Aliyetukuka mumeo huyo abadilike na kurudia katika hali yake ya zamani.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Amekula Vidonge Kutoa Mimba Nini Hukmu Yake?



Alhidaaya.com





Swali:



Assalam Alaekum wa Rahmatu llahi wa Barakatul, Suala langu linahusu Juu Mwanamke aliyekula Vidonge Kwa ajili ya kutoa mimba Nini hukumu yake ifahamike kuwa mwanamke ana akili timamu ila pengine aliafanya haya kuvunja alakati na Baba watoto wake aliemuacha, Ahsanteni sana wa Jazakumu Allaahu Kheir.





Jibu:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Haifai kwa mwanamke katika Uislamu kutoa mimba kwani kufanya hivyo ni kuua kiumbe cha Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), ambacho kimekatazwa kishari’ah kuuliwa ila kwa sababu inayokubalika Kiislamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:



وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَمَن قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلَا يُسْرِف فِّي الْقَتْلِ ۖ إِنَّهُ كَانَ مَنصُورًا ﴿٣٣﴾

Na wala msiue nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha (kuiua) isipokuwa kwa haki. Na atakayeuliwa kwa kudhulumiwa, basi Tumemfanya mrithi wake awe na mamlaka. Lakini asipindukie mipaka katika kuua. Hakika yeye atasaidiwa (kwa shariy’ah). [Al-Israa: 33].



Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kuondoshwa (kuhalikishwa) kwa dunia mbele ya Allaah ni sahali zaidi kuliko kuuliwa kwa Muislamu" (at-Tirmidhiy, an-Nasaa'iy na Ibn Maajah).



Uchukivu wa mke kwa aliyekuwa mume wake usimfanye kufanya dhambi kubwa kama la kutoa mimba. Na huko akidhani anamkomoa mume wake wa zamani au kuvunja mahusiano yoyote baina yao, hajui kuwa amejikomoa mwenyewe kwa kuidhulumu nafsi yake na kujiweka pabaya mbele ya Allaah Mtukufu.



Na kwa kuwa tayari ashatoa mimba bila dharura yoyote inayokubaliwa na Shari’ah, anachotakiwa hivi sasa ni arudi kwa Allaah kwa kuomba msamaha wa kikweli kweli. Awe atatimiza masharti haya yafuatayo:



1. Kujiondoa katika maasiya hayo.

2. Ajute sana katika kufanya kosa hilo.

3. Aazimie kutolirudia tena kosa hilo.





Bonyeza kiungo kifautacho upate maelezo zaidi:



Kutoa Mimba - Hukmu Na Kafara Yake





Na Allaah Anajua zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…