Rais Samia Suluhu Hassan: Serikali kufanya mazungumzo kuendeleza mradi wa bandari ya Bagamoyo

Mbona hamkudai mkataba wa manunuzi ya ndege na Bei halisi??!

Tulitamani pia kujua ila Mwendazake hakutuvumilia wadadisi na wakosoaji. Uzuri mama ameturuhusu tukosoe.

Ila hili la Bandari ya Bagamoyo linafikirisha sana, kwanini tujenge bandari mpya ndani ya only 50km kutoka Existing Port ya Dar? Kwanini badala ya kujenga mpya tusiboreshe ya Tanga ikahudumia Kaskazini na ile ya Mtwara ikahudumia Kusini na Nchi za Zambia, Malawi ambazo zitakuwa karibu zaidi na Mtwara kuliko Bagamoyo?

Why Bagamoyo mkuu, naomba unieleweshe zaidi kama hutajali.
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa serikali ipo katika mazungumzo ili kuweza kuendeleza mradi wa bandari ya Bagamoyo. Hayo ameyasema leo Tarehe 26, 06. 2021 wakati wa hotuba yake katika mkutano wa 12 wa baraza la biashara.

Rais Samia amesema pia hiyo itakwenda sambamba na mradi wa Mchumchuma na Linganga kuwa nao mazungumzo yanaendelea ili waone mwekezaji atatoa ngapi na Serikali ngapi ili kuweza kuendeleza mradi huo. Akaongeza kuwa chuma imepanda bei duniani hivyo ni wakatk sahihi wa Tanzania kuchamka.

View attachment 1830564

Pia soma:
Bila Environmental and Social Impact assessment hii miradi itatuumiza huko mbeleni. Na terms za Mchina mara nyingi sio rafiki.

Amandla...
 
Bila Environmental and Social Impact assessment hii miradi itatuumiza huko mbeleni. Na terms za Mchina mara nyingi sio rafiki.

Amandla...
Hili la bandari ya Bagamoyo lilikuwa ni suala la muda tu na haijalishi kama mradi utatuumiza au una faida. Hata haya mazungumzo ni suala la formality tu, uamuzi umeshatolewa. Wakati ndiyo utaamua ila mama anaingizwa kingi mbaya sana na atakuja kubeba lawama za vizazi vijavyo.
 
Ndio maana nimeuliza. Umekaa mno kimaghumashi. Na ni kweli atabebeshwa lawama.

Amandla...
 
Kuuliza sio ujinga. Aliyekuwa Rais (JPM) na Makamu wa Rais SSH wakati ule waliukataa huu mradi. Miezi mitatu baada ya kifo Cha JPM , aliyekuwa Makamu wa Rais Kawa Rais anaukubali tena huo mradi. Je hawa viongozi wawili wakati wa uongozi wao walikuwa wanafanya maamuzi kwa kushirikiana?
I wish Magu angefufuka tu...
 
Tuna imani na serikali yetu adhimu ya BI MKUBWA kuwa itazingatia maslahi ya taifa, penye mapungufu itarekebisha penye maslahi itashadadia
Nimesoma taarifa kamili ya Rais nimeona ametumia maneno " kwa maslahi ya taifa "ila unisamehe tu, kwangu kiongozi yeyote wa CCM akitamka hayo maneno nakuwa mgumu kumuamini sababu wanapenda sana 10% na usiri kwenye mikataba.
 
Muda ndio utasema yote. Tukae kwa kutulia.
Au yeye anaogopa kufa kwa ajili ya wengine. Anaona bora liende.

Inasikitisha hii. I wish na Mbeya tupate raisi tukaneemeke.
 
Ila hata mimi I dont trust these Chinese, najua mama anani njema ila kama kandarasi ya huu Mradi akipewa nchi nyengine kama za ulaya kutakuwa na unafuu kidogo
 
Ukisoma comments vizuri, utagundua kuwa watu hawataki kabisa kutafakari kwa undani ishu ya hii bandari badala yake wanakubali tu kisa itamkomoa magufuli.
Hi ni ajabu sana hii nchi tuna kazi ngumu sana.
 
Kwa hili nitasimama na Magufuli kila siku
 
Ukisoma comments vizuri, utagundua kuwa watu hawataki kabisa kutafakari kwa undani ishu ya hii bandari badala yake wanakubali tu kisa itamkomoa magufuli.
Hi ni ajabu sana hii nchi tuna kazi ngumu sana.
Binafsi naona maoni ya watu ni 50/50, coz swali la mkataba mpaka leo limekosa majibu.
 
Back
Top Bottom